Mfahamu Carlos the Jackal: Gaidi tishio zaidi kuwahi kutokea duniani

Hivi vikundi ni noma sana...bila kusahau black September..
 
ukifuatilia sana hawa magaidi sijui alqaeda, boko haram, ISIS connections na mashirika ya kijasusi CIA, KGB etc haipingiki. kwa mtazamo wangu naona ugaidi ni kama njia moja wapo ya utawala duniani kama wanavyosema wenyewe "out of chaos comes order"
Hawa watu wanatumika na CIA na KGB kupigana na mwingine kwa kupewa information na silaha. Uko sahihi sana
 
Nini chanzo cha jina lake ,Carlos the jackel
 
Safi sana...nimeipenda sana...mm nilisoma novel ya the Jackal 1984 nikiwa Mazengo...kule waliandika alipokua Patrice Lumumba Usoviet ya zamani alikutana na Mohamed Boudia ktk party,alikua anapiga gitaa akamrushia...Carlos akapiga kama Boudia alivyokua anapiga...lkn kabla ya hapo girl friend wa Boudia aliwachanganya na ndie aliyewaunganisha ktk party...niliipenda sana novel ile kwani co sawa na James Hadley Chase kwani Chase ni matukio ya kufikirika....asante kunikumbusha mbali 💪💪
 
Carlos the Jackal ni jina alilopewa na vyombo vya habar baada ya mwandishi wa vitabu vya riwaya, Frederick Forsyth kumwandika ktk kitabu chake cha mwaka 1967 kinachoitwa "the day of the jackal".

Carlos ambaye sasa anatumikia kifungo cha maisha nchini ufaransa baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya makachero wa nchi hiyo mwaka 1975, alizaliwa jumatano ya oktoba 12,1949 ktk mji wa Michelena jimbo la Tachira nchini Venezuela.

Jumapili ya disemba 30,1973 alimpiga risasi na kumjeruhi Joseph Edward Sieff,aliyekuwa mfanyabiashara wa uingereza na rais wa kampuni ya marks and Spencer mwenye asili ya Kiyahud. Ingawaje Sieff hakufa lkn alijeruhiwa sana,alimfyatulia risas iliyopenya shavu moja na kutokea shavu la pil ikivunja meno kadhaa,Sieff alipoanguka chini Carlos aligeuka haraka na kukimbia akiamin tayari ameshamuua.

Jumatat ya January 13,1975 Carlos alifanya jaribio la kulipua ndege ya Israel ambayo ilikua ktk sekunde za mwisho kupaa angani ikielekea new York marekani ikiwa na abiria139 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa orly jijini Paris, Ufaransa.

Kombora la kwanza halikuipata ndege hiyo badala yake likapiga ndege ya Yugoslavia, YugoslavDC-9 iliyokuwa imetua uwanjan hapo.Aliporusha kombora la pili lilipiga na kuharibu sehemu ya jengo na yy na wenzake kufanikiwa kutoroka.

Siku sita baadaye kwa mujibu wa kitabu cha"The Sage Encyclopedia of terrorism ,second edition"kilichohaririwa na Gus Martin, Carlos na Wapalestina watatu walirud uwanjani hapo, safar hii walifanikiwa kufanya shambulio moja kabla ya kukabiliwa na makachero wa ufaransa lkn walifanikiwa kutoroka na walirud wiki moja baadae na kurusha mabom ya mkono kwenye eneo LA kupumzikia abiria na kujeruhi watu zaid ya 25.

Mmoja wa washirika wake siku hiyo ni Michel Moukharbal ambaye alikamatwa baadae. Baada ya kukamatwa Moukharbal alitoa habar za washirika wake na akakubali kuwapeleka makachero watat wa ufaransa kwa mmoja wa wapenz wa kike wa Carlos.

Usiku wa ijumaa ya juni 27 Moukharbal na makachero watat wa ufaransa waliwasili ktk jengo alimokuwamo Carlos kwa nia ya kumhoji. Baada ya mahojiano ya muda mfupi na maofisa hao Carlos aliwaambia anataka kwenda kujisaidia atarud kwa mahojiano zaid.
Aliporejea baadae alikua amebeba bastola baada ya sekunde chache akawa amewaua Moukharbal pamoja na makachero wawili wa ufaransa mmoja alifanikiwa kutoroka.

Haya ni machache kati ya mengi yanayozungumzwa kuhusu huyu mwamba mnaweza mkaelezea na mengineyo.
 
Kama yapi?!
Sina uthibitisho nayo lkn ktk hali ya kawaida hakuna mtu anayefanya mabaya tuuuu asiwe na jema hata chembe, firaun licha ya mabaya yote lkn alimuhudumia musa ndani ya nyumba yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…