Mfahamu Dimitri Polyakov, MOLE wa CIA ndani ya KGB aliyechomeshwa na Afisa wa CIA Aldrich Ames

mcTobby

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2018
Posts
7,894
Reaction score
22,679
Ngoja nikupe mfano kwa kitu nachotaka ku share nawe hapa. Chukulia wewe ni mfanyakazi ambaye tuseme ni msaidizi wa CEO wa kampuni ya AB. Kila kitu kuhusu AB ,mipango ,waajiri pamoja na shughuli zote(safi na chafu) unazijua. Ikatokea kwamba kampuni ya AB unayoifanyia kazi imeajiri kwa siri watu ndani ya kampuni ya CD ili kutoa siri za kampuni ya CD na kuiuzia AB. Lakini tuseme wewe kwa vile upo broke,kampuni yako ya AB pamoja na boss wako hawakuzingatii sana, na mbaya zaidi mshahara hautoshi unaanza namna ya kutengeneza hela kwa kuvujisha siri za AB kwa CD. Unaanza kuropoka kwamba AB imeajiri watu ndani ya CD wanaovujisha siri za kampuni na kuiuzia AB. Kutokana na siri ulizovujisha kwa CD wanakupa hela kisha kampuni ya CD inaamua "kuwapoteza" wale wote uliowataja wanaovujisha siri kwenda AB.



anyway huu ni mfano .

Twende kwenye mada .
Siku ijumaa ya tarehe 4 mwezi wa 7 mwaka 1986,yupo mzee mmoja mstaafu akiwa nyumbani kwake ,alipata ujumbe kwamba aripoti makao makuu ya idara aliyokuwa akiifanyia kazi siku ya jumatatu saa nne kamili asubuhi kwa ajili ya "presentation". Mzee huyo hakuwa mwingine bali ni jenerali mstaafu wa jeshi la Urusi ambaye alikuwa akifanya kazi kwe kitengo cha maswala ya ujasusi wa kijeshi kilichokuwa kikijulikana kama GRU bwana Dimitri Polyakov.


Dimitri Polyakov akiwa kwenye sare ya kijeshi , GRU.

Mzee huyu hakuambiwa sababu ni nini haswa aliitwa ghafla hivyo, alichoambiwa ni kwamba atatumiwa gari na dereva lije kumchukua kwenye makazi yake hadi makao makuu alipokuwa akihitajika. Huyu bwana kwakuwa hakujua ni nini aliitiwa, alijua tu hii itakuwa ni surprise, labda kuna mzee mwenzake amestaafu anaagwa au kuna birthday party ya mmoja wa wastaafu.

Hakutilia mashaka sana. Sasa jioni ilipofika huyu mzee alikuwa na kijana wake mkubwa anayeitwa Peter alifika hapo nyumbani baada ya kutoka misele yake. Sasa ujio wa kijana wa huyu mzee Polyakov ulimualert jambo fulani. Kwa mbali aliona magari 2 ya ambulance yamepark pembezoni mwa barabara uelekeo wa nyumba ya huyu mzee. Kengele ya hatari ikagonga kichwani kwa huyu mzee Polyakov.


Dimitri akiwa kizuizini jela

Ikumbukwe huyu ni jasusi mstaafu wakijeshi. Akajiuliza maswali kadhaa ndani ya sekunde ,hizi ambulance kutoka moscow mjini zinafanyaje sahizi huku nje ya mji usiku? Pia kwa mji ulio karibu na makazi yake haujawahi kuwa na ambulance imekuwaje zipo mbili mida hii huku uchochoroni? Kwa kuwa peter naye alifuata nyayo za baba yake kwa kujiunga na GRU, walikuwa wanafahamu kwamba kuna muda KGB na kikosi cha Alpha Team walikuwa wanatumia hizi ambulance katika kuteka ama kumkamata mtu au mhalifu wanayemhitaji iwe kama cover up kwa sababu gari za polisi zinatoa alert na ni rahisi kushtukiwa haraka sana kuliko ambulance. Ni sawa na kule kaskazini mashariki mwa Nicaragua ,polisi au kikosi kazi wa hiyo nchi kutumia magari yasiyo na plate number au plate number fake kukamata walengwa wanaowahitaji.najua umenielewa😎😎😎.

Huyu bwana mdogo Peter naye alimweleza mzee wake naye ameambiwa aripoti siku ya jumatatu makao makuu saa nne kamili asubuhi kama tu mdingi alivyoambiwa. Kumbuka hii ilikuwa ni siku ya jumapili ambapo alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kufikisha miaka 60. Hivyo alikuwa amewaalika watoto wake pamoja na majirani kwa ajili ya tukio hilo. Sasa Polyakov alimwambia kijana wake asimweleze mtu yoyote ndani ya familia kwamba kesho yake jumatatu wanahitajika makao makuu.. ilikuwa ni siri yao. Huyu mzee alianza kuchezwa na machale. Machale ya huyu mzee yalimcheza baada ya kuuunganisha baadhi ya matukio ya nyuma. Kwa mfano mwaka 1980 akiwa new delhi india kikazi ,aliitwa ghafla nyumbani moscow kisha akaambiwa kazi ya huko India imekuwa aborted hivyo atafanya kazi za kiofisi hapo makao makuu. Sababu za huyu mzee kuitwa nyumbani ghafla , ni kwamba baadhi ya wenzake walianza kupenyeza minong'ono kwamba huenda ni jasusi anyetumiwa na Marekani.

Basi Polyakov akaamua kukaa hapo makao makuu na baadaye minong'ono na umbea ulipozidi akaamua kustaafu ili kuwapisha washindani wake waliokuwa wakiitaka hiyo nafasi. Sasa baada ya kustaafu ndio hivyo tena ghafla ameitwa makao makuu.

Kwa kifupi wenzake hawakuwa wanamtilia mashaka kwa bahati mbaya. Alikuwa ni jasusi wa urusi akiifanyia kazi CIA kwa takribani miaka 18 kuanzia miaka ya 1960s kipindi akiwa New York kikazi. Na jasusi huyu Polyakov alikuwa akivujisha classified documents kuhusiana na jeshi la Russia. Nyaraka za siri hizi ziliwasaidia CIA na marekani kwa ujumla na alipendwa haswa. Moja ya nyaraka za kijeshi za siri alizovujisha ni kuhusiana na jeshi la Vietnam pamoja na uwezo wake ambao uliwasaidia marekani kwa kiasi fulani katika vita ile ya Vietnam 1960-1970s.

Okay... na kweli ilipofika jumatatu asubuhi mzee huyu alijiandaa vizuri akiwa amevalia sare rasmi za jeshi kitengo cha GRU kwa ajili ya kuripoti yeye pamoja na kijana wake. Na ikumbukwe hakuna aliyempa maagizo kwamba akiripoti awe amevalia sare za kazi...what a joke.


Pichani ni Dimitri Polyakov akisomewa makosa yake kwenye mahakama ya kijeshi kwa tuhuma za ujasusi .

Na kweli alipofika tu makao makuu ya KGB pasipo hata kukaribishwa wala kupumzika alidakwa na kuwekwa chini ya ulinzi mkali akituhumiwa kwamba ni jasusi. Kufupisha hii stori ni kwamba huyu mzee aliwekwa rumande na kuzuiliwa kwa miezi kadhaa kwa ajili ya mahojiano ya kina na aliyekuwa akimhoji ni mwenyekiti wa KGB wakati huo bwana Chebrikov. Mkewe na watoto wake waliruhusiwa kumtembelea akiwa jela. Mkewe alijua tu kinachoenda kumpata mumewe siku si nyingi baada ya kumaliza kuhojiwa. Kilichomtokea Ni RISASI MOJA TU YA KISOGONI NA BRATISKAYA MOGILA. stori ya huyu mzee Dimitri Polyakov ikawa imeisha hivyo.

Huyu mzee ni mmoja tu wa wahanga au victims wa Aldrich Ames afisa wa ngazi za juu wa CIA aliyeamua kuuza mchongo(siri) kwa KGB ili apate pesa za kutanua maisha na mchepuko wake aliyeitwa Rosario Casas Dupuy. Kisa cha Ames nimekielezea humu JamiiForums hivyo sitamchimba sana huyu msaliti wa CIA .


Picha hii hapa juu Aldrich Ames akiwa kwenye tabasamu mwanana na mrembo Rosario.

Kwa kifupi huyu bwana Ames ambaye mchepuko wake Rosa alikuwa akipenda kumuita Rick Ames alikuwa anauza taarifa za CIA kwa KGB, na moja siri alizotoa ni kuhusiana na maafisa wa ngazi za juu wa jeshi la Russia waliokuwa wamepandikizwa ili kuvujisha kwa marekani. Mmoja wa maafisa hao ni huyu jenerali mstaafu bwana Dimitri Polyakov nilyetangulia kukuelezea. Na kweli huyu bwana AMES alipiga pesa ndefu sana kutoka kwa Russia ikikadiriwa kufikia dola milioni 1.2.

Ames na mpenzi wake Rosario Casas Dupuy walikuwa wanafanya matanuzi kila walikoenda kikazi. Kwa mfano Ames na mpenziwe walinunua nguo za gharama wakiwa huko Italia kiasi kwamba kila mmoja yaani wafanyakazi wenzake wakawa wanajiuliza huyu mwenzao pesa anatoa wapi? PESA ANATOA WAPI?


Nafikiri hiyo picha hapo juu inajieleza kuhusiana na Ames.😍😍😎😎

Pichani ni Ames akiwa na Rosario mchepuko wake kwenye moja ya fukwe huko Mexico wakila bata kwa pesa ya usaliti kutoka russia taratibu..maisha yanataka nini?😎😎🤣🤣🤭


Ames enzi za ujana wake miaka 1960s.🤪🤪🤪🥸🥸


Ames alianza kutiliwa mashaka na FBI hatimaye naye alidakwa na mkewe baada ya kufuatiliwa nyendo zake kwa muda. Na ikabainika kumbe naye ni TRAITOR aliyewachoma wenzake. Ames alipokuja kuhojiwa baadaye akiwa ameshahukumiwa kifungo cha maisha jela kwanini alifanya aliyoyafanya kuisaliti CIA alisema tu. "I DID IT FOR MONEY".

Ames hapa akiwa kwenye viunga vya mahakama baada ya kupigwa mvua ya jela maisha kwa makosa ya ujasusi.


Ames aka rick ames .. waandishi wa habari walikuwa mubashara kama unavyowaona wakiripoti tukio la msaliti Ames ndani ya CIA. Hapa akisindikizwa chini ya ulinzi mkali mahakamani.


Nadhani maelezo ya hii picha yanajitosheleza . Ushahidi ambao ulizidi kumpigilia msumari bwana Ames kwenye vyombo vya sheria kwamba ni jasusi . Hichi kikaratasi kilikutwa kwenye trashbin ,makazi yake yalipopekuliwa.


Hii ni summary ya bank statement ya account ya pesa ya rick Ames ikitoa maelezo ya miamala ya fedha alizokuwa akitumia na kupokea kwenye vyanzo mbalimbali allivyovijua yeye.💲💲💲🚫🚫⚠️

Naweza kumaliza kwa nukuu inayosema "MONEY , THE GREASE THAT OILS THE WHEELS OF SO MUCH ESPIONAGE" sijajua hii nukuu ni ya nani.
 

Picha hii ni ya maafisa Kadhaa wa CIA waliohusika kumnasa Msaliti Aldrich Ames. Kuanzia Wa kwanza kushoto ni mwanamama Sand y Grimes, Paul redmond, Jeanne Vertefeuille, Diana Worthen na Dan Payne.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…