Mfahamu Double Agent wa CIA na EIJ aliyemfundisha OSAMA mbinu za kigaidi na vita

Mfahamu Double Agent wa CIA na EIJ aliyemfundisha OSAMA mbinu za kigaidi na vita

Kweli kabisa, inabidi tubadilike nasi kwani miaka hii siyo ya kipindi kile cha 60's na 70's.
Uko sawa lakini ujasusi ndio roho ya dola!!!!!
Sasa iko hivi,kuimarisha ujasusi ni kuondoa watu wenye hila na siasa bila hila ni kitendawili hapo!!!

Umejiuliza kwa nini mataifa yenye nguvu yanathamini sana hii kitu????!!!!
 
Ni Ali Mohamed alikuwa double agent wa CIA na EIJ( Egyptian islamic jihad) ambayo ndio ilipelekea kuundwa kwa ALQAEDA huku yeye akiwa mwendesha mafunzo wa mbinu za kivita na kijasusi wa kwanza kwenye kambi zao kwa ajili ya kuwaandaa na mapambano dhidi ya utawala wa kisovieti nchini Afghanistan miaka ya 90. yeye ndiye mwalimu wa kwanza wa Osama bin Laden na Ayman Zawahiry( kiongozi wa sasa wa Alqaeda)

Ali anaelezwa kuwa mtu mwenye uzito wa kilo 90, urefu futi 6 huku akielezwa mtu aliye fiti kimwili, aliyebobea kwenye sanaa za mapigano( martial art),mwenye ufahasa mzuri wa lugha za kiingereza,kifaransa,kiyunani na kiarabu. alikuwa mwenye nidhamu ya juu, mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri, mwenye kujichanganya na watu na uwezo wa kupata marafiki kwa urahisi.

Uhusiano wake na CIA kwa mara ya kwanza aliingia marekani kama mkalimani wa Ayman Zawahiry( kiongozi wa sasa wa alqaeda) wakati alipoenda kuchangisha michango kusaidia wana mgambo katika harakati za kuutoa utawala wa wasovieti Aghanistan.kwa maelezo inasemekana Zawahiri akamshauri a-infiltrate marekani, mwaka 1984. Ali anaelezwa aliweza kuingia kwenya kitio cha CIA Egypt kwa urahisi na kuweza kuongea na mkuu wa kituo kuhusu ofa yake ya kufanya nao kazi na akawa recruited kama junior intelligence officer. kazi ya kwanza alipewa ni kupenya ndani ya msikiti mmoja mjini hamburg ujerumani ulisemekana kuwa na mahusiano na wanamgambo wa Hizbollah wa nchini Lebanon lakini cha ajabu akawataarifu viongozi kuwa yeye ni jasusi wa CIA ametumwa kuchukua taarifa, kwa kuwa katika ule mkusanyiko alikuwepo jasusi mwingine wa CIA, taarifa juu ya alichokifanya Ali Mohamed zikawafikia mabosi CIA. Kwa mujibu wa mwandishi maarfu wa jarida la New Yorkers na mshirika wa kituo cha sheria na usalama New York University of Law ni kwamba ulitumwa ujumbe wa limawasiliano kutoka CIA ukitaarifu kuwa sio mwaminifu na ameshadhibitiwa, lakini mda huo taarifa inatumwa tayari Ali mohamed alikuwa mjini Carlifonia kushiriki program maalum ya kuwapatia ruhusa ya kuingia marekani bila kuwa na visa kwa ‘Valuable assets' waliolifanyia taifa la Marekani utumishi wa hali ya juu, program ambayo yenyewe pia ilikuwa ikifadhiliwa na CIA. Ali akafanikiwa kuoa mmarekani Linda Sanchez na akachukuliwa kwenye special forces na akapangwa katika kambi kubwa ya Fort bragg kama drill commander( sijui kwa kiswahili wanaitwaje, yani wale ambao wanawapokea makuruta na kuwafundisha maisha ya jeshini, taratibu na nidhamu)

Mnamo mwaka 1988 Ali aliwataarifu wakuu wake jeshini kuwa anachukua likizo fupi kwa ijili ya kwenda afghanistan kupambana na wasovieti( huko ndio akawa anatoa mafunzo kwa wanamgambo waanzilishi wa Alqaaeda). Huku nyuma afisa mwandamizi wa Ali, Lt. Col Robert Anderson aliandika ripoti ya kina ikilenga kutaka idara ya ujasusi ya jeshi kumchunguza Ali Mohamed na kumfungulia mashtaka lakini taarifa yake hiyo ilipuuzwa. anaeleza kuwa " Kuwa na mwanajeshi mmisri, aliyehusika na mauji ya rais wa zamani wa misri Saadat, alafu akapata visa ya kuja kuishi marekani na akachukuliwa kwenye vikosi maalum vya jeshi(special forces) inashangaza, haya mambo hayatokei tu hivi hivi" anaendelea kueleza kuwa ilikuwa ni vigumu kuamini kuwa mwanajeshi wa kawaida wa Marekani kupigana vita katika jeshi la nje bila kuadhibiwa. akaendelea kusema anaamini atakuwa anafadhiliwa na shirika la kijasusi la kimarekani.



Ali mohamed aliendelea kutoa mafunzo kwa wana mgambo wa kiislamu wa Maktab al-Khidamat (iliyoanzishwa na Abdullah Azzam ambayo baadae alijiunga Osama, wakagombana hatimae Osama akaigeuza kuwa ALQAEDA baada ya ku-win popularity over Azzam)nchini marekani kupitia Kambi ya Al Kifah iliyokuwepo mjini brooklyn iliyokuwa akisapotiwa na Marekani kwa ajili ya kuwawaezesha kuutoa utawala wa kisovieti nchini Afghanistan

Miaka ya 90 akarudi tena Afganistani ambako alitoa mafunzo ya kijasusi ikiwemo, kuteka watu, kuteka ndege, jinsi ya kuua n.k na inasemekana katika wanafunzi wake wa kwanza kabisa ni Osama bin laden, Ayman Zawahiry(kiongaozi wa sasa wa Alqaeda) na viongozi wengine wa Alqaeda kwa mijibu wa FBI special agent Jack Cloonan

Mwaka 1993 akiwa ndani ya Alqaeda akawa informant wa FBI, na mmoja wa wapigaji wa ALQAEDA Mohamed Atyf aliyepewa jukumu la kufanya survey katika ubalozi wa marekani nchini kenya(uliolipuliwa mwaka 1998) alikataa kumtajia Ali Mohamed passport namba yake kwa kuwa alikuwa na mashaka kuwa Ali alikuwa ni mshirika wa Marekani

Wiki mbili baada ya balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania kulipuliwa, FBI walisachi makao ya Ali na kukuta nyaraka mbalimbali zenye ushahidi juu ya kuhusika kwa na milipuko nchini Kenya na Tanzania na kukamatwa. Ali alikubali makosa ya kigaidi na akaeleza mwanza mwisho kuhusu ushiriki wake katika kundi la Al qaeda, akakiri makosa ili apate kifungo cha maisha jela bila msamaha wowote ule

Mwaka 2001 gazeti la Raleigh News and Observer lilitaarifu kuwa Ali anatoa ushirikiano kwa serikali ya marekani, naeleza kamanda mstaafu wa Delta force katika kitabu chake cha The Mission,The Men and Me:Lessons from former Delta Force Commander Pete Blaber "Mawakili wa utetezi wanaamini kuwa Ali hajahukumiwa na anasirikiana na serikali japo serikali haijathibitisha hilo,akihukumiwa anaweza akahukumia kidogo, kama miaka 25 kwa mujibu wa makubaliano yao"

Mwaka 2006, mke wa Ali Linda Sanchez alisema kuwa mumwe bado hajahukumiwa na haruhusiwi kuzungumza na yeyote "yani wamemshikilia kiusiri sana ni kama vile amepotelea kwenye hewa"

By Wikileaks01 Spy
 
Ujasusi ni kitu kingine ndio maana hata hapa bongo wanasiasa wanaodhani wameweka mfukoni idara za ujasusi hawajui kuwa wao ndio wamewekwa mfukoni!!
Ukiona jinsi FBI na CIA wanavyoshiriki kwenye uchafu lakini wakiwa na projection za matunda bora baadae kwa Marekani ndio hapo unapoheshimu movement za kijasusi kama nguzo za taifa lolote.
Tuwape TISS mradi wa gesi bana wakue kama CIA (msinitoe macho).

Mkuu umeongea vizuri wamekusikia
 
Urafiki wenu haukuwa wa bahati ila planned chunguza mienenndo yenu utajua kupitia wewe kakutana na watu au kafika maeneo mengi tu "orientation and/ raport"
Ali expose hiyo historia as past ili wewe usijue current mission na kukuweka karibu ni kukisimulia hayo uliyopenda kuyasikia!!!!!
Katika urafiki wenu wewe ulikuwa ukiongea naye nini??!!!

Man [emoji119][emoji119][emoji119][emoji122][emoji122] upo Vizuri sana Maana unavyofikiria ndo hivyo hivyo nilikuwa nafikiria,hawa watu wa CIA hawakoseagi Maana kila kitu kinakuwa tayari kishapangwa kabisa
 
Kama ndo alikuwa mwalimu wa Osama Bin Laden basi, inawezekana yeye ndie alietoa maagizo ya kumuita mwanafunzi wake, ili wakae wote, waimalishe CIA na FBI kwa masirahi ya USA
 
mmeisahau mossad ya Israel? Hiyo ndo noma sasa,majasusi wa mossad wametapakaa dunia nzima na huwezi kuwajua hata kidogo,kuna wengine wanajifanya ma padre ma sister,wapo ktk taasisi za kimataifa kama UNHCR,UNICEF,UN na nk,tena wengi wao wakitumia paspot za mataifa mengine,ili kuficha utaifa wao,hata hapa TZ tunao wengi,mwaka 2007 nikiwa nafanya bulyanhulu gold mine,nilishangaa kumuona mzungu mmoja akiwa anajua kiswahili vyema ana uraia wa canada ila cha ajabu anaijua mno israel na kuizungumzia mara nyingi kuliko canada,nataka niwaeleze kuwa,hawa mabalozi wa marekani ktk nchi mbalimbali ni majasusi namba 1 wa CIA,nyie huwa mnadhani hao ni diplomats,marekani na Israel si mataifa ya kawaida ktk medani za kijasusi,ni hatari sana.
Sisi huku tunawapeleka makada na wakurugenzi waliofeli mipango kuwa mabalozi
 
Sisi huku tunawapeleka makada na wakurugenzi waliofeli mipango kuwa mabalozi
Ni shida, halafu unaweza sikia kabajeti ka TIS kanafanana na ka wizara ka Afrika mashariki. Inawezekana pia hata east Afrika yetu hatujaikava vyema kijasusi. TIS ilitakiwa taasisi huru kabisa hata kifedha ijitengenezee yenyewe kijasusi, ituchagulie raisi na akizingua imtoe kijasusi, ingekuwa poa sana. Afrika tunalishwa ujinga eti demokrasia, taifa gani duniani ni la kidemokrasia bana.
 
Back
Top Bottom