Teko Modise
JF-Expert Member
- May 20, 2017
- 2,331
- 7,733
Wakati wa Majira ya Kiangazi mwaka 1991 huko nchini Marekani, Kampuni kongwe ya filamu ya Columbia Pictures iliyopo chini ya kampuni mama ya SONY ilikuwa imepata wazo la kubadilisha logo yake ya mwaka 1923 na kuweka mpya ili kujiongezea mvuto wa kibiashara.
Basi akatafutwa mbunifu wa masuala ya Logo, ndugu Michael Deas na kupewa jukumu hilo la kubuni logo mpya.
Michael Deas akamtafuta swahiba wake ambaye anafanya modeling Kathy Anderson ili awe model katika upigaji wa picha itakayotumika kama logo ya Columbia Pictures.
Siku ya tukio ikapangwa na ikafanyika nyumbani kwa Kathy Anderson huko New Orleans akitumia moja ya apartments zake kwa zoezi hilo.
Sasa katika zoezi hilo alikuwepo pia Jenny Joseph aliyekuwa na miaka 30 kwa wakati huo. Huyu alikuwa ni rafiki wa Kathy Anderson ila huyu Jenny hakuwa model.
Basi zoezi la upigaji picha likaanza, zikapigwa picha nyingi baada ya hapo, wakati watu wakiwa wamechoka, Michael Deas akamtania Kathy Anderson, mwambie rafiki yako nae avae mavazi ya tukio husika walau tumpige picha mbili tatu. Wakati huo Jenny alikuwa amekaa zake pembeni akikodoa zoezi la upigaji wa picha.
Basi Jenny Joseph akabadili mavazi na kuanza kupigwa picha kadhaa kisha zoezi likaisha. Ikabaki kazi ya Michael Deas kwenda kufanya editing kabla ya kuwasilisha kazi aliyopewa kwa kampuni ya Columbia Pictures.
Kinyume na matarajio ya wengi, zile picha za Jenny Joseph zilivutia wengi kuliko hata picha za Model halisi aliyeandaliwa, na ikumbukwe Jenny hakuwahi kufanya shughuli za modelling.
Basi baada ya miezi miwili ya kuedit picha na kuunganisha na logo, Michael akamtaarifu Kathy Anderson kuwa wameamua kutumia ile picha ya rafiki yake badala ya yeye. Kathy aliunga mkono jambo hilo na hakuwa na kinyongo.
Ikawa rasmi, picha ya Jenny Joseph ndio ikaanza kutumika kama logo pale filamu yoyote iliyotengenezwa na kampuni ya Columbia Picture inapoanza. Jenny akapewa mshiko wake akapita hivi.
Jenny hakuwahi kufanya modelling ya kupiga picha kabla ya dili la Columbia Pictures na hakuwahi kufanya tena baada ya dili hilo. Yaani ni kama ilitokea ngekewa tu.
Kwasasa ni mama wa watoto wawili na anaishi zake huko Houston, Texas nchini Marekani.