Messenger RNA
JF-Expert Member
- Jul 24, 2022
- 1,411
- 3,712
Kumbe ni mtu kabisa,nilikuwa najua ni sanamu,asante mleta mada.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dada wa Nike kuna kitu alipata baadae ukiacha malipo ya dola 35 za mwanzoAlipata hela kidogo sana na sio mtu famous wa kujionyesha. Ni kama dada wa tiki ya Nike (swoosh) aliyeiuza dola 35 akiwa designer chuo. Kwa sasa ile logo pekee ina thamani zaidi ya $20 billion
Alipata hela kidogo sana na sio mtu famous wa kujionyesha. Ni kama dada wa tiki ya Nike (swoosh) aliyeiuza dola 35 akiwa designer chuo. Kwa sasa ile logo pekee ina thamani zaidi ya $20 billion
Wakati wa Majira ya Kiangazi mwaka 1991 huko nchini Marekani, Kampuni kongwe ya filamu ya Columbia Pictures iliyopo chini ya kampuni mama ya SONY ilikuwa imepata wazo la kubadilisha logo yake ya mwaka 1923 na kuweka mpya ili kujiongezea mvuto wa kibiashara.
Basi akatafutwa mbunifu wa masuala ya Logo, ndugu Michael Deas na kupewa jukumu hilo la kubuni logo mpya.
Michael Deas akamtafuta swahiba wake ambaye anafanya modeling Kathy Anderson ili awe model katika upigaji wa picha itakayotumika kama logo ya Columbia Pictures.
Siku ya tukio ikapangwa na ikafanyika nyumbani kwa Kathy Anderson huko New Orleans akitumia moja ya apartments zake kwa zoezi hilo.
Sasa katika zoezi hilo alikuwepo pia Jenny Joseph aliyekuwa na miaka 30 kwa wakati huo. Huyu alikuwa ni rafiki wa Kathy Anderson ila huyu Jenny hakuwa model.
Basi zoezi la upigaji picha likaanza, zikapigwa picha nyingi baada ya hapo, wakati watu wakiwa wamechoka, Michael Deas akamtania Kathy Anderson, mwambie rafiki yako nae avae mavazi ya tukio husika walau tumpige picha mbili tatu. Wakati huo Jenny alikuwa amekaa zake pembeni akikodoa zoezi la upigaji wa picha.
Basi Jenny Joseph akabadili mavazi na kuanza kupigwa picha kadhaa kisha zoezi likaisha. Ikabaki kazi ya Michael Deas kwenda kufanya editing kabla ya kuwasilisha kazi aliyopewa kwa kampuni ya Columbia Pictures.
Kinyume na matarajio ya wengi, zile picha za Jenny Joseph zilivutia wengi kuliko hata picha za Model halisi aliyeandaliwa, na ikumbukwe Jenny hakuwahi kufanya shughuli za modelling.
Basi baada ya miezi miwili ya kuedit picha na kuunganisha na logo, Michael akamtaarifu Kathy Anderson kuwa wameamua kutumia ile picha ya rafiki yake badala ya yeye. Kathy aliunga mkono jambo hilo na hakuwa na kinyongo.
Ikawa rasmi, picha ya Jenny Joseph ndio ikaanza kutumika kama logo pale filamu yoyote iliyotengenezwa na kampuni ya Columbia Picture inapoanza. Jenny akapewa mshiko wake akapita hivi.
Jenny hakuwahi kufanya modelling ya kupiga picha kabla ya dili la Columbia Pictures na hakuwahi kufanya tena baada ya dili hilo. Yaani ni kama ilitokea ngekewa tu.View attachment 2572315
Kwasasa ni mama wa watoto wawili na anaishi zake huko Houston, Texas nchini Marekani.View attachment 2572316
Lions gate ni balaaNazikubali movies zao na wale dream line, Lions gate
Free mason ni Idea tu, na itapotea....kama ilivyokua tales za Dragons, Zombie n.kHii picha itakuwa na maana iliyojificha na bila shaka ni mambo ya free mason haya.
Acha utani aisee! Wamuweke Simba kisha sauti ya Tiger! Ili iweje!? Yule ni Mfalme wa Mwitu na ile ndiyo Ngurumo yake. Tiger hana jeuri ya kuwa na sauti hiyo.Metro Goldwyn Mayer. Ila sauti inayotumika ni ya tiger, simba ana sauti mbaya na haitoi kiholela
Sauti ya simba huijui na wala sauti ya tiger huijui kama ndio hivyo. Kwanini ubishe kitu huna ufahamu nacho.Acha utani aisee! Wamuweke Simba kisha sauti ya Tiger! Ili iweje!? Yule ni Mfalme wa Mwitu na ile ndiyo Ngurumo yake. Tiger hana jeuri ya kuwa na sauti hiyo.
Wewe unazijua au na wewe umesoma kama sio kuhadithiwa!?Sauti ya simba huijui na wala sauti ya tiger huijui kama ndio hivyo. Kwanini ubishe kitu huna ufahamu nacho.
Hollywood scenes za simba nyingi sana wanatumia mlio wa tiger, hata Lion King walitumia zaidi mlio wa tiger. Ile ni biashara na sauti ya tiger inalipa zaidi kuliko ya simba. Sauti ya simba haitishi kuliko ya tiger na kibiashara hailipi zaidi.
Swali la kitoto, nizijue mara ngapi.Wewe unazijua au na wewe umesoma kama sio kuhadithiwa!?
Nibishe wakati sauti ya Simba inajulikana. By the way inaweza kuwa hata sauti ya paka pori iliyochezewa studio. Hiyo kwamba ni sauti ya tiger wewe umehadithiwa tu. Endelea Kubisha.Swali la kitoto, nizijue mara ngapi.
Hata kwa kuhadithiwa au kusoma ulishindwa? Ulibisha kitu hujui
MGM - Metro Goldw