Cheza na number ya Kahaba Nabii Mke EGW
Pili, abishe kwamba gematria
E L L E N G O U L D W H I T E
0+50+50+0+0 + 0+ 0+5+50+500+10+0+1+0+0 = 666 si hesabu sawa.
Leo nataka uelewe biblia inasema nini kuhusu namba 666 na maana yake kulingana na Biblia takatifu.
*Ufunuo 13:16-18*
Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake. Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kabisa damu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.
Kabla hatujahesabu hesabu ya mnyama huyu,
hebu na tuone sifa za alama ya mnyama huyo
*SIFA ZA ALAMA YA MNYAMA*
1. Jina la mnyama huyo.
Ufunuo 13:16
2. Hesabu ya jina lake.
Ufunuo 13:16
3. Ni jina la makufuru.
Ufunuo 17:5
4.Mnyama amekaliwa na mwanamke. Ufunuo 17:18
5. Mnyama ni mamlaka ya kidini. Daniel 7:17
6.Mnyama aliwatesa watakatifu wa Mungu. Ufunuo 18:24 &
Daniel 7:25
7.Mnyama alimtukana Mungu na wote wakaao Mbinguni.
Ufunuo 13:6
8.Mnyama aliazimu kubadili majira na sheria. Daniel 7:25
9.Mnyama aliazimu kuenenda kinyume chake aliye juu.
*Je ni mamlaka gani iliyo na sifa tajwa hapo juu?*
Mnyama aliwatesa watakatifu wa Mungu.
Rumi ilifanya mauaji ya kutisha katika kipindi cha mfalme Nero na Constantine, pia UPAPA uliongoza mauaji ya kikatili yasiyoweza kuelezeka kuanzia mwaka 538 hadi Mwaka 1798. Ikiwa ni jumla ya kipindi cha miaka 1260 watakatifu wa Mungu waliuawa kikatili wale wote ambao walikuwa waaminifu na watunzaji wa amri za Mungu pamoja na neno lake. Mauaji hayo yalifanywa chini ya Kiongozi wa kanisa katoliki St. Bartholomew na yalijulikana kama BARTHOLOMEW MASSACRE.
Mnyama amekaliwa na Mwanamke Kahaba.
Mpaka sasa hakuna kanisa lolote duniani linalomiliki nchi yake isipokuwa Catholic Church ambapo inamiliki nchi ya VATICAN na raisi wake ni Kiongozi wa juu kabisa wa kanisa hilo yaani PAPA.
Aliazimu kubadili majira na sheria.
Kanisa katoliki ndilo lililobadili kalenda na nyakati mpaka sasa inatumika ulimwenguni kote. Mamlaka ya kipapa yalibadili siku 30 za kila mwezi kama mpango wa Mungu na kuweka mpango wa mwezi kuwa na siku 28,29,30,31 Ikiwa ni kuendesha ibada za miungu na hata majina ya miezi asili yake ni majina ya miungu mfano JANUARY (ni muungu JANUS) n.k
Pia mwanzo wa siku ulibadilishwa kulingana na Mpango wa Mungu siku huanza jioni na kuisha jioni lakini sasa majira yamebadilishwa wanadamu tumepigwa upofu na kudhan ya kuwa siku huanza saa sita kamili usiku ndio maana leo hii watu wengi inapokaribia tarehe moja mwezi wa kwanza kila mwaka husubiri mpaka saa sita usiku na kushangilia. Huo sio mpango wa Mungu
Pia walibadili pumziko takatifu la sabato ya siku ya saba na kupeleka siku ya kwanza ya juma yaani Jumapili.
"Jumapili ni alama yetu ya madaraka.......
.... kanisa liko juu ya Biblia, na huku kuhamisha kwa utunzaji wa sabato ni kizibiti cha ukweli huo. "
*Catholic Record, September 1,1923*
"Papa ana Mamlaka ya kubadilisha nyakati, kubadili sheria, na kutupilia mbali vitu vyote, hata mafundisho ya Kristo."
*Decretal De Translat*
*Espiscop. Cap.*
"Labda jambo la kijasiri la mabadiliko yaliyofanywa na kanisa yalitokea katika karne ya kwanza. Siku takatifu. Sabato, zilibadilishwa kutoka jumamosi kwenda jumapili............ sio kwa maagizo yoyote yaliyoandikwa katika Biblia, lakini kwa kanisa kujisikia lina mamlaka............. Watu wanaofikiri kwamba Biblia ndiyo mamlaka pekee, inabidi wawe wasabato, watunze jumamosi. "
*Saint Catherine Catholic Church, sentinel, May 21, 1995.*
Ana jina la makufuru.
Cheo cha papa hujulikana kama Vicarius Filii Dei (Vicar of Christ-Badala ya Mungu duniani) kwa hiyo basi papa hufananishwa na Mungu aliye juu na kufanya kazi ambao ni Mungu pekee awezaye na anayestahili kuzifanya kama vile *Kusamehe Dhambi* Hii ni kufuru kuu kwa Mungu aliye juu *Marko 2:7*
Soma pia *1Timotheo 2:5*
Hebu sasa na tuhesabu hesabu ya Cheo chake
VICARIUS FILII DEI ni lugha ya kilatini ambayo ndio lugha haswa ya kanisa hilo pamoja na serikali ya Vatican.
Biblia inatuambia ni hesabu ya kibinadamu
Na tuanze kuihesabu
V=5
I=1
C=100
A=0
R=0
I=1
U=5
S=0
F=0
I=1
L=50
I=1
I=1
D=500
E=0
I=1
JUMLA NI *666*
*USIDANGANYIKE UKADHANI NI KITU FULANI AMBACHO HUWEZI KUKIFAHAMU*
Lakini yawezekana ujumbe huu ukawa kama moto nafsini mwako usishangae Omba Mungu azidi kukufunulia Nuru yake.
YHWH IS GOOD