Acha kupaniki
Kama umeahindwa kung'amua jambo dogo tu ,sabato ni siku ipi ,
Utaweza kujadiliana na mimi kweli?
Mada ya sabato ni lini ,hiyo nitakuletea mwanangu akufundishe
YHWH IS GOOD
Ngoja sasa nikueleweshe kuhusu sabato ya kweli ya siku ya saba ewe ndugu.
Mwanzo 1:14 inasema "Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndio dalili na majira na siku na miaka."
Mungu aliumba Jua na mwezi ili kupata hesabu ya siku, juma, mwezi na mwaka. Sabato ni siku ya Saba ya Juma, hivyo lazima kutumia kalenda ambayo inatumia mwezi na jua ili kukamilisha mzunguko. Ni kalenda ya kiebrania peke yake yenye sifa hizo. Huwezi kupata sabato ya siku ya saba kwa kuangalia kalenda ya ukutani, lazima ufuate kalenda ambayo inaongozwa na moving bodies angani, yaani jua na mwezi.
Utaratibu huo umetumika tangu mwanzo wa kuumbwa kwa binadamu na utaratibu huo utaendelea kipindi cha nchi mpya na mbingu mpya. Isaya 66:23 inasema "Na itakuwa , mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu " [hapa biblia haisemi jumamosi hata jumamosi]
Waebrania walikuwa wana desturi ya kutunza sabato kufuatana na mwandamo wa mwezi, mwezi unapoandama ndio mwanzo wa kupata siku, juma na hatimaye mwezi. Mwezi huanza na kumalizika, vibyo hivyo huwezi kupata sabato bila kutambua mwezi.
Ushahidi upo mwingi kwenye biblia nakupa fungu la Amosi 8:5
inasema " .mkisema, Mwezi mpya utaondoka lini, tupate kuuza nafaka? na sabato nayo, tupate kuandika ngano?...."
Hapa wengi hamfahamu namna gani tunaweza kupata haya majuma na masiku kwa kufuta kalenda hiyo ya kiebrania, iko hivi; mwezi ukiandama leo, kesho inaitwa siku ya mwandamo wa mwezi, waebrania waliambiwa wasifanye kazi siku hiyo japo sio sabato, then baada ya pumziko hilo la mwandamo wa mwezi siku inayofuata inakuwa tarehe 2 ya mwezi huo na sequence hiyo inaendelea hadi mwezi uishe. Hivyo basi kama tarehe 2 ni siku ya kwanza ya juma siku ya saba inakuwa tarehe 8 ambayo ni sabato, tarehe 15 ni sabato, tarehe 22 ni sabato na tarehe 29 inakuwa sabato ya mwisho ya mwezi huo. Kalenda hiyo haibadiliki kila mwezi kila mwaka. Ndio maana wayahudi waliambiwa waadhimishe pasaka kila mwaka siku ya maandalio ambayo ni tarehe 14 mwezi wa kwanza kila mwaka [Soma Kutoka 12:18 " Mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne, wakati wa jioni, mtakula mikate isiyochachwa........."
Kutoka 13:10 inasema "Kwa hiyo utaitunza amri hii kwa wakati wake mwaka baada ya mwaka "]
Bila shaka Yesu alikufa siku ya maandalio ambayo ni tarehe 14 ya mwezi wa kwanza na kufufuka tarehe 16 mwezi wa kwanza, kwa vile tarehe 15 ilikuwa ni sabato.
Wapagani wa kiroma, ili kuonekana hawawafuati waebrania na kalenda yao ya kidini, wali jaribu kuiga na kuichomeka pasaka yao ambayo imeshindwa kuwa fixed na kalenda yao. Haiwezekani kuadhimisha pasaka kwa tarehe ile ile na siku ile ile kila mwaka. Ndo maana kila mwaka wa kalenda ya kipagani ya gregorian pasaka huadhimishwa kwa tarehe tofauti kila mwaka badala ya tarehe iliyoagizwa na Mungu. wamebakisha siku tu ya Ijumaa na Jumapili ili kuendelea kuukazia uongo wao kuwa jumamosi ni siku ya saba, hivyo ni sabato.
Hivyo kwa kuhakikisha true sabbath inapotea lazima uhakikishe calenda ya kiebrania inapotea kabisa na kuingiza kalenda ya bandia ya gregorian, na kuipa majina ya miungu yao , na kusema Sunday ni siku ya kwanza, Monday the second day....nk na saturday the seventh day. Hivyo wamefanikiwa sana warumi kuudanganya ulimwengu kama andiko la unabii la Danieli 7:25 kwamba " .....naye ataazimu kubadili majira(times) na sheria (laws)" hii kalenda ilibadilishwa na saa zikabadilishwa yaani siku hizi saa inaanza saa sita usiku, japo wasabato wanaanza siku jioni na kuadhimisha kwa masaa 24 kinyume na waebrania ambapo siku inaadhimishwa kwa masaa 12 tu [angalia Yohana 11:9 " Yesu akajibu, Je saa za mchana si kumi na mbili?"] Yaani waebrania waliadhimisha sabato jua linapochomoza na kuisha jua linapozama, siku imeisha.
Ili nisiwachoshe, zipo evidence za kutosha katika biblia zinazoonyeha waebrania wale hawakuabudu sabato siku ya jumamosi au kwa kutumia kalenda ya gregorian bali walitumia kalenda yao ambayo inatumia mwezi na jua. na wasomaji wazuri wa unabii wa biblia wanajua kuwa mwaka wa biblia una siku 360 na mwezi una siku 30. Yaani unachukua average ya siku 354 ya mwezi[siku 29.5 mzunguko wa mwezi] na siku 366[mzunguko wa jua] ya jua unapata 360.
Warumi kwa vile ibilisi ndo anawatumia kuendesha empire yake amehakikisha kalenda hii haifahamiki ili kuwapotosha binadamu wasimfahamu muumba wao, kwa vile sabato inawasogeza binadamu kwa muumba wao waeze kumwabudu.
Itaendelea.