Uongo upi....?mbona hoja zenu zote zimejibiwa.
Kuhusu kuabudu Sanamu mulijibiwa vzuri sana kwenye thread zilizopita japo hamukutaka kuelewa.
Kuhusu Sabato mmejibiwa pia japo hamtaki kuelewa.
Kuhusu kuombea wafu au wafu kutuombea(Watakatifu) mlijibiwa kwa hoja za nguvu.
Kuhusu kumuomba mama Bikira Maria kutuombe,mlijibiwa vzuri sana.
Na hili la sasa la 666/616 bado mnajibiwa japo mnarukaruka hamujibu maswali mnayoulizwa na Benchecs/Sala na Kazi/Otorong'ong'o.
Namkumbuka Mzee mmoja alikuwa rafiki yangu sana alikuwa msabato toleo la kwanza, alishatangulia mbele ya haki alikuwa ni mwenyeji wa Tarime(Mjaluo),cha kwanza alichokuwa anakipinga ni Yesu kuwa mwana wa Mungu/Utatu Mtakatifu aking'ang'ania kwamba hayo ni mapokeo ya kibinadamu bila kutambua hata biblia tunayoisoma leo ni mapokeo ya kibinadamu.
Plz Kitaja me naomba ugusie Great Disappointment, Je unaitambuaje hii dhahama....?Kama huitambui nakushauri rudi Kanisani au tafuta Padri upate kuungama.
Sent from my TECNO-W3 using JamiiForums mobile app
Ukitaka kujua kuhusu Great Dissapointment iloyotokea mwaka 1884 sharti uweke chini mihemko na mvinyo ya uroma ili uwe tayari kupokea nuru ya kweli.
Iko hivi, kipindi hicho wana matengenezo ( Reformers) wa wakati huo wakiongozwa na William Miller aliyekuwa wa madhehebu ya Baptist, walitafakari Neno la Mungu na kuona kuwa katika kitabu cha Daniel 8:14 kuna tukio kubwa ambalo lingetokea. "Akamwambia, Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa". Hivyo walianza kuchunguza maana ya unabii huu ambapo walipata ufafnuzi katika sura ya 9. Daniel 9:24-27 "Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha makosa, na kuishiliza dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na kuleta haki ya milele, na kutia muhuri maono na unabii, na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu. Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu. Na baada ya yale majuma sitini na mawili, masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu; na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika, na hata mwisho ule vita vitakuwapo; ukiwa umekwisha kukusudiwa. Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu;
na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.
Huu unabii unaeleza tangu kuwekwa amri ya kuujenga upya Yerusalemu mwaka 457 BC ndipo majuma 70 au miaka 490 zinaanzia. Unabii unaelezea meengi kutokea kama kuzaliwa kwa Yesu, maisha yake na kifo chake. lakini unabii huo unahitimishwa baada ya siku 2300 yaani miaka 2300. kwa hesabu za kibiblia, siku hizo huishia mwaka 1884. Kipindi hicho unabii unasema "patakatifu patakaswa" maana palikuwa pamechafuliwa mno na lile chukizo la uharibifu. ambalo hata Yesu alilitaja katika
Mathayo 24:15. "Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu)" Hapa Bwana Yesu hutuweka wazi kuwa awezaye kufahamu ni yule asomaye tu.
Kwa kuufuatilia unabii huu watu wa Mungu hawa, waliongozwa kuwa tukio la kutakaswa kwa patakatifu ni ujio wa Yesu Kristo kuja duniani kuchukua wateule wake na kuifanya dunia upya kama ahadi yake ilivyo. Tukio hili lilikuwa la furaha kubwa sana na lilipata mwitikio mkubwa na ndipo likapatikana kundi kubwa lilifahamika kama "Adventsists" yaani wanaotazamia marejeo ya Yesu mara ya pili. Lakini ulipofika mwaka 1884 Yesu haukurudi kama walivyotarajia. watu wengi wakakata tamaa na ndiyo maana ikaitwa Great Dissapointment. Jambo hili linenwa na Yohana pia katika Ufunuo 10:9-11 "Nikamwendea malaika yule nikamwambia kwamba anipe kile kitabu kidogo. Akaniambia, Kitwae, ukile, nacho k
itakutia uchungu tumboni mwako, bali katika kinywa chako kitakuwa kitamu kama asali. Nikakitwaa kile kitabu kidogo katika mkono wa malaika yule, nikakila; nacho kikawa kitamu kama asali kinywani mwangu, na nilipokwisha kukila tumbo langu likatiwa uchungu. Wakaniambia, Imekupasa kutoa unabii tena juu ya watu na taifa na lugha na wafalme wengi". habari za kurudi kwa Yesu zilikuwa tamu sana kutamka kinywani, lakini baadaye zikawa chungu. Na ndipo Malaika nasema "
Yakupasa kutoa unabii tena".
Baada ya great disappointment, imani ya wengi ilivunjika na ukristo wa wengi ulikufa rasmi wakarudia matendo yao ya kidunia. Ndipo kukatokea kundi dogo la wanamarejeo hawa, wakakaa na kutafakari kosa lao likuwa wapi hasa. Katika kuyachunguza maandiko, wakafunuliwa kuwa, hawakukosea katika muda bali tukio walilodhani litatokea duniani linaendelea katika Hekalu la Mbinguni ambalo Musa alionyeshwa, hata Nabii Yohana aliliona. ufunuo 11:19. "K
isha Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua ya mawe nyingi sana". Katika Hekalu la duniani kulikuwa na vymba viwili vya patakatifu. Kulikuwa na chumba cha patakatifu mabapo makuhani na watu wa kawaida walileta sadaka zao za kuteketezwa kama ilivyoagizwa.Lakini kuilikuwa na chumba cha pili, patakatifu mno.
Huko aliingia Kuhani Mkuu Pekee akiwa na damu ya wanyama ili kufanya upatanisho wa nafsi yake na kisha wa watu.
Waebrania 9:1-3."Basi hata agano la kwanza lilikuwa na kawaida za ibada, na patakatifu pake, pa kidunia. Maana hema ilitengenezwa, ile ya kwanza, mlimokuwa na kinara cha taa, na meza, na mikate ya Wonyesho; ndipo palipoitwa, Patakatifu. Na nyuma ya pazia la pili, ile hema iitwayo Patakatifu pa patakatifu".
Sasa Yesu aliingia chumba hiki huko Mbinguni.
Waebrania 9:11-12 "Lakini Kristo akiisha kuja, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo, kwa hema iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu, wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele.
Kwa hiyo Yesu hakupotea njia kama wengine wanavyodhihaki, ila alikuwa akiendelza kazi ya kuwaombea watakatifu huko Mbinguni kama tulivyoona.Biblia husema yeye pekee ndiye mwombezi wetu katika hekalu la Mbinguni.
Waebrania 9:24-26. "Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu; wala si kwamba ajitoe mara nyingi, kama vile kuhani mkuu aingiavyo katika patakatifu kila mwaka kwa damu isiyo yake; kama ni hivyo, ingalimpasa kuteswa mara nyingi tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu; lakini sasa, mara moja tu, katika utimilifu wa nyakati, amefunuliwa, azitangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake. Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu; kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu".
Hivyo Yesu Kristo yupo katika hekalu la mbinguni akituombea, akitoka hapo anarejea duniani kuchukua wateule wake walimpokea. Hatujui siku wala saa ila dalili zinaonyesha mwisho u karibu. Maana chukizo la uharibifu limeanza ile kazi yake ( asomaye afahamu).