,
Ili kukusaidia kukurekebisha bandiko lako naomba nikusaidie kurekebisha tafsiri ya huu unabii wako ili usiwachukulie kuwa shambulia watu wa dhehebu fulani moja kwa moja. Vita hii si ya kanisa katoliki pekee bali ni Watu wote mnaofanya ibada ya kumuabudu ibilisi wakiwemo waadventista wasabato.
Nitaanza na tafsiri ya Babeli ni nani na kwa nini biblia inatoa wito kwa watu wote watoke Babeli kama ilivyoandikwa kwenye hicho kitabu cha ufunuo.
Ufunuo 18:2
" Akalia kwa sauti kuu akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu, umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza; kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo wa ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanyabiashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake."
Na baada ya hapo wito sasa unatolewa
Ufunuo 18:4
.....Tokeni kwake, enyi watu wangu,msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake........
Unabii wa Ufunuo umetumia neno Babeli, Mnyama na Mwanamke. Nitaanza kutolea maelekezo ya kila neno hapo ili kupata picha kubwa ya maana nzima ya kinachoendelea katika tafsiri ya unabii huo.
BABELI:[soma mwenyewe Mwanzo 10:8]
Kitabu cha Ufunuo kimetaja neno Babeli, huu ulikuwa ni mji wa kale ambao ulianzishwa na Nimrodi, kumbuka Nimrodi alikuwa ni mtoto wa Kushi, ambaye Kushi ni mtoto wa Kanaani . Kanaani ni mtoto wa Nuhu ambaye alilaaniwa na baba yake kwa vile alimchungulia uchi wake alipokuwa amelewa. Pia kumbuka wana wa Israeli waliambiwa wasioe au kuchangamana na watu wa Kanaani na vile vile waliambiwa wakati wanatoka utumwani Misri, wawaue wote baadhi ya miji ya wakaanani, yale mataifa ya wahiti, wayebusi, wamoabu, nk [mataifa saba].
Kwa nini Mungu aliwaambia hivyo, kwa kuwa Vizazi vile [offspring] ilikuwa imechangamana na mashetani. Rejea kitabu cha Mwanzo 6:2 “wana wa Mungu waliwaona hao binti za binadamu kuwa ni wazuri, wakajitwalia wake wowote waliowachagua”
Mwanzo 6:4 “Nao Wanefili walikuwapo duniani siku zile, tena baada ya hayo, wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu, wakazaa wana; hao ndio waliokuwa watu HODARI zamani, WATU WENYE SIFA”
Kumbuka Nimrodi alijulikana ni mtu Hodari, kwa vile kizazi chake kilikuwa ni cha “wana wa Mungu waliozaa na wanadamu”.
Hawa “wana wa Mungu” ni wale malaika waovu walioamua kujigeuza na kuamua kuzaa na wanadamu, na hivyo kuzaliwa watoto walio na jamii isiyo na asili ya ubinadamu, ambao walikuwa na sifa za ukubwa wa maumbile, akili nyingi sana, walikuwa baadhi wana vidole sita, kama Mfalme Ogu, Goliati na wengineo. Kizazi hiki cha watu wenye Sifa [Genious] kilifanya mapinduzi makubwa ya kuleta ujuzi mbalimbali hapa Duniani. Dunia ilijaa uovu mkubwa kutokana na kuleta ujuzi wa kubadilisha viumbe kwa kufanya Cross breeding ya wanyama, mimea kuibadilisha, yaani kile ambacho Mungu alikiumba na kusema ni chema sana, wao walivibadilisha. Hata leo hii ujuzi huo unaendelea umetoka kwao. Mungu akaona uovu huo duniani na kwamba kila kiumbe kilikuwa kimeathirika na uchakchuliwaji huo wa binadamu. Isipokuwa Nuhu na watoto wake walionekana hawana kasoro za ki genetic. Mungu akawahifadhi kwa ajili ya kizazi kijacho. Hivyo kizazi kile cha Majitu au Wanefili kikaangamizwa na gharika.
Unaweza kujiuliza tena hawa watu wa ajabu walitoka wapi baada ya gharika? Jibu ni kwamba katika wale wanawake wa watoto wa Nuhu ambao hawajatajwamajina yao kwenye Biblia yawezekana wakawa wamezaliwa kutoka kwenye Kizazi kile cha “wana wa Mungu” ndo maana Kanaani kizazi chake kilikuwa na laana ya kuwa na offspring isiyo ya kibinaadamu. Ukumbuke pia Ibrahimu alimzaa Ishmaeli ambaye mama yake alikuwa ni Hajiri Mmisri, ambao pia ni watoto wa Kanaani kizazi cha “wana wa Mungu waliozaa na binadamu”
Esau pia ambaye ni mtoto wa Isaka wa Ibrahimu aliamua kwenda na njia isiyo sahihi na kwenda kuoa wana wa Kanaani kizazi ambacho Mungu alikilaani kwa vile hakikuwa na asili ya binadamu.
Kumbuka kizazi hiki kilikuwa kinafanya ritual za kipagani au kwa lugha nyingine walikuwa wanafanya Ibada za kumuabudu Shetani kwa vile ndio baba yao. Kizazi hiki kilifundishwa maarifa na baba zao [wale malaika wana wa Mungu walioamua kuzaa na binadamu] maarifa haya yalikuwa ni siri ya Mungu kwa binadamu kufahamu. Walifundishwa Uchawi na kuuzindua [sorcery, hallucination, incantation], walifundishwa kutengeneza silaha, walifundishwa Unajimu [ astronomy], walifundishwa elimu ya chuma [metallugy] na elimu nyingi za juu. Leo hii elimu hizo utazipata kama utajiunga na makundi ya Freemasonry, Illuminatti na baadhi ya secret society kama Skull and Born, Mafia, na baadhi ya makundi yenye elimu na utaalamu katika Pharmaceutical Industry, utengenezaji wa drugs za kulevya nk.
Ndo maana baadhi ya elimu leo huwezi kuzipata chuoni hata usome vipi, lazima uwe mwana jumuiya Fulani ili ufundishwe.
Miaka ilivyozidi kwenda mbele Utawala rasmi uliotawala kisiasa duniani ulianzishwa ambao ni utawala wa Babeli chini ya Nebukadneza. Utawala huu ulienea dunia nzima, ulitengeneza sheria na taratibu za kufuata kwa walimwengu, elimu ya kichawi ilitawala sana katika utawala ule. Kutokana na elimu iliyotolewa Babeli na utaalamu mbalimbali, Bustani inayoelea ya Babeli iliingia katika maajabu saba ya dunia miaka ya zamani.
Utawala wa Babeli ulikuwa utawala tajiri na wenye nguvu, baada yake ulirithiwa na Utawala wa Kiarabu ya Kiajemi [Midiani na Persia] hawa baadaye wakarithiwa na Wagiriki ambao walikuwa wataalamu wa elimu ya Chemistry [pharmakeia enzi hizo] na Biolojia.
Baada ya wagiriki wakaja Warumi [Roman Empire] ambayo utawala huu wa Kirumi unaendelea hadi leo kwa namna ambayo watu wengi hawaelewi. Kwa vile Rumi ya kisiasa ilipotea karne ya tatu [3 A.D] ikaja Rumi ya Kidini iliyoongozwa na Askofu wa Kanisa la Roma.[Papacy]
Upapa uliendelea kutawala Dunia ambapo Karne ya sita [6 A.D] upapa ulikusudia kuhamisha maskani yake kuipeleka Yerusalemu hivyo kuanzisha Kwa siri dini ya Uislamu, ambayo lengo lake hasa ni kuwaangamiza Waebrania waliokuwa wanatumia kalenda yao kama ndo msingi wa kuendesha tamaduni zao za Kiibada kama Sabato ya siku ya Saba, sikuu za mwaka kama Pasaka n.k
Dini hiyo ya kiislamu ililengwa hasa kwa wana wa Ishmaeli ambao ni kizazi cha waarabu ambao kwa asili walikuwa na Chuki [antagonism] na Wayahudi. Wakati dini hiyo inaanzishwa, waliambiwa wawauwe watu wote ambao hawakubali kuwa Waislamu [kazi inayofanywa na waislamu wa ki sunni leo] na kuwaacha watawa [monks wa kikatoliki walioishi kwenye majumba ya kidini].
Kwa vile watawala wa Kirumi ambao ni mapapa walijua fika kuwa Ukweli wa Ibada sahihi ya kweli kwa Muumba walikuwa wanayo wayahudi. Hivyo ilipaswa kizazi hiki kiangamizwe duniani. [nadhani ndo chanzo cha wayahudi wengi kusambaa duniani na kubadilisha ID zao na pia yale mauaji ya Kinazi ya Holocoust kipindi cha Hitler].
Siri hii ya kuanzisha dini hii walikuwa wanaijua Hadija[ambaye alikuwa mke wa mtume Muhamad, ambaye alipewa kazi ya kumtafuta kijana ambaye ni intelligent, ili baadaye atangazwe kuwa ni Nabii ajaye] na Muhamed ambaye baadaye alipewa manifesto kama andiko pekee la dini ya kiislamu iliyojulikana kama Korani.
Wapiganaji wa kiislamu wenye kueneza dini hiyo kwa nguvu ya upanga, hawakufahamu isipokuwa waliambiwa wapigane kuuleta Uislamu duniani kwa masharti waliyopewa na viongozi wao wa juu. Viongozi wajuu wa Uislamu waliambiwa wakimaliza kazi ya kuwaangamiza Wayahudi wale wautwae Jerusalamu wamkabidhi Kiongozi wa Kirumi [Papa] ili ahamishe Headquoter ya ufalme wake iliyopo Roma, Italia na kuipeleka Jerusalemu [Kumbuka pia Jerusalemu ilitakiwa kuwa kitovu cha dini zote za Kipagani{dini za watoto wa kikaanani} pamoja na Ukristo{ule uliochakachuliwa wa kifarisayo na kisadukayo, huu ni ukristo wote wa ki orthodox, nk}]
Sasa baada ya wale makamanda wa kiislamu kuona wanashinda kila sehemu wanayoenda [Bila kufahamu mfadhili wao ni Mtawala wa Kirumi wa Roma] wakajianzishia Utawala wao wa Ottoman.
Na pale kwenye mji wa Jerusalemu wakajenga msikiti mkubwa wa Al Aqsa sambamba na hekalu la kiyahudi Top of the Dome
Ndio maana mgogoro wa Kipalestina na Kiyahudi unaendelea hadi kesho kwa vile Wapalestina wanataka Yerusalemu iwe mji wao na Wayahudi wa Kiisraeli hawataki kuuachilia mji huo kwa vile ni wao.
[Tambua pia taifa la Israeli lilianzishwa na Illuminatti mwaka 1948 kwa lengo la kuendeleza mgogoro pale Middle East kama adhabu kwa waarabu wa kiislamu ambao walipewa mchongo wa kumpatia Mtawala wa kirumi mji wa Yerusalemu]
Nitaendele kuchambua ili tuweje kuijua Babeli vizuri,
Kumbuka kwamba huyu mtawala wa Kirumi amerithi empire yake toka utawala wa Kibabeli, mfano wa alichokirithi ni Kalenda, kalenda hii ambayo tunaitumia leo inaitwa Babylon kalenda,ambayo katika karne ya 16 Papa Gregory alii modify na kuiboresha kidogo na hivyo kujulikana kama Gregorian Calendar kama jina lake lilivyo leo. Kalenda hii inatumia mzunguko wa jua tu wa siku 366. Tofauti na kalenda ya kiebrania ambayo inatumia mzunguko wa mwezi ili kupata namba za siku, majuma, miezi na miaka [Rejea Mwanzo 1:14].
Katika karne ya 15 watawala wa Kirumi walikuwa katika hatari ya kupoteza empire yao kwa vile kulikuwa kumeibuka wimbi la wanaharakati wa kimageuzi ya kidini ambapo baada ya mashine za uchapaji kugunduliwa Biblia ilikuwa inatafsiriwa na kusomwa na wengi, na hivyo watu wakawa wanasoma wenyewe badala ya kufundishwa kanisani pekee.
Baada ya watawala wa kirumi kuona hatari hiyo ya watu kiijua Biblia, kukaanzishwa ndani ya Vyumba vya watawala wa Kiroma, taasisi ijulikanayo kama Jesuits, hawa lengo lao ni moja, kwa kiapo chao waliapa kutetea maslahi ya watawala wao kwa gharama yoyote ile. Hawa Jesuits walijulikana kama jumuiya ya Yesu kwa jina lakini kazi zake za ndani zilikuwa ni za kiibilisi kabisa. Waliwaua waprotestant wa kijerumani kwa usiku mmoja zaidi ya 80000, kwa vile tu walipingana na Papa kwa kuwa hata Kiongozi wao wa kijerumani naye alikataa kumtii kiongozi wakirumi., mwisho wa siku wakaanzisha chuo chao cha ma Jesuits, kilichoko Ingolstadt, Bavaria.
Misheni za Jesuits ziliendelea bara la ulaya lote, walihakikisha kila Mfalme wa Ulaya anamtii kiongozi wa Kirumi. Katika karne ya 17 mwishoni Jesuits walijulikana misheni yao, wakaanza kufukuzwa katika majumba ya wafalme wa Ulaya nao baada ya kuona wameshitukiwa wakamua kutoka Ulaya na kuhamia Marekani, wakati huo huo Marekani imechipuka na kuanza kuwa taifa huru la kidini na kiuchumi, taifa ambalo sasa litakwenda kuhatarisha maslahi ya Jesuits duniani.
Wakanzisha kundi Fulani lenye agenda ile ile ya Jesuits ya Ulaya wakajiita ILLUMINATTI na hivyo Jesuits ikahamia Marekani na kuweka Headquoter yao Chicago., ikaja kwa sura nzuri kwa kuanzisha Shule, Vyuo vikuu, Hospitali nk. Hapa kwetu Bongo, jumuia zao ni zile za Capuchins, San Fransarians, na vyuo vyao ni kama St,Joseph na seminaries nyingi sana za kikiristo na za Kiislamu, agenda ni ile ile kupika na kutafuta watu wa kuweza kufanya kazi zao na agenda zao za kuhakikisha utawala wao unarudi kwa Kiongozi wa kirumi.
Illuminatti walivyokuwa Marekani wao waliamua ku deal na mifumo ya kiuchumi na kisiasa, walianzisha makampuni ya chuma, reli , meli , mifumo ya nishati, usafiri wa unga, Unajimu, teknolojia, Madawa[pharmaceutical industry], mifumo ya fedha na benk. Walihakikisha mifumo yote ya kiuchumi ipo chini yao, na kwa hilo wamefanikiwa kuitawala dunia kwa kuanzisha Benki Kuu za nchi[Central Banks] na hivyo ku control fedha za nchi husika na kufanya manipulation za kiuchumi, wanaendesha mifumo ya kisiasa wanavyotaka wao, wakaanzisha Umoja wa mataifa kwa lengo la kuwavuta nchi zote ndani ya paa moja ili wawatawale, nk
Hivyo kitabu cha ufunuo kinapozungumza habari ya Babeli tunamaanisha Mfumo wa uendeshaji wa kidini wenye mfumo wa kalenda iliyoanzishwa na wa Babeli. Kwa kuwa kwa kalenda yao dunia nzima imetawaliwa, na hata dini kuu za Ulimwengu, ambazo ni Christianity, Islam, Judaism nk zote zinaendesha Ibada zao kuitegemea kalenda hiyo ya ki Babeli, yaani wote hao wana Pay Homage to the same Deity!! Yaani wote wanamuabudu Ibilisi aliye muanzilishi wa kalenda yao wanayoitumia yaani Ijumaa, Jumamosi na Jumapili.
Muanzilishi wa kalenda ya kweli ya kiebrania, ambaye anataka hesabu ya siku ipatikane kwa kufuata movement za heavenly bodies ambazo hazibadilishi sequency ya mzunguko wake, ambaye anataka viumbe wote waje wamuabudu katika siku yake ya Saba ambayo ni Sabato na sio Jumamosi.
Huyu Ibilisi kupitia agent wake hapa duniani anataka kuchukua Ibada halisi impasayo Mungu na kuielekeza kwake., kama ilivyoandikwa nia yake kwenye kitabu cha Isaya 14:13,14 inasema “ Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu, Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini, Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na Aliye juu”
Shetani amekusudia kufanana na Mungu ili apate ibada, na kwa kufanya hivyo amekaa juu ya mlima wa mkutano maana yake katika mikusanyiko ya ibada yote inayofanyika duniani ikifuata kalenda ya kipagani ya Gregorian yeye yupo juu na watu wapo chini wakimuabudu kwa vile lengo lake ni kufanana na Mungu muumbaji aliye juu. Hiyo ndio Babeli! Ndo Ufunuo inawaita watu watoke huko Babeli, haitaji kanisa Fulani ndo Babeli.
Ili kumalizia maelezo yangu, nitafafanua kidogo kwa maelezo mafupi juu ya;
MNYAMA.
Katika vitabu vya unabii kama Danieli, Falme mbali mbali katika zama za historia ya Dunia walikuwa wakiwakilishwa na wanyama mbali mbali., hivyo katika kitabu cha Ufunuo hasa kuanzia sura ya 13 japo contest ya Story nzima inaanzia sura ya 12 ya kitabu hicho. Wanyama wa aina mbili wamezungumzwa. Mnyama wa kwanza akiibuka kutoka katika Bahari, kwa tafsiri ya Danieli na Ufunuo(soma unabii huo unajitafsiri wenyewe, sio kila kitu niandike hapa), bahari ni junction ya mataifa au watu wengi, ambapo kutokana na sifa za Ufalme (mnyama) huu ni Utawala wa Kirumi ulio chini ya mapapa) ambapo ulikuwa na sifa ya Kubadilisha kalenda [Danieli 7:25], kubadilisha kawaida ya saa, kutesa watu wanaopinga utawala wake pamoja pamoja na kubadili Sheria ya Mungu mfano Sabato ya siku ya Saba na kuifanya Jumamosi, na Ibaya kuabudu sanamu nk. Utawala huu wa Rumi ya kidini chini ya mapapa uliendelea hadi Karne ya 17 mwishoni, ambapo Papa wa wakati huo alikamatwa na Napoleon na kupelekwa Ufaransa na kufia huko. Enzi ya Mtawala wa Kirumi ya kidini iliishia hapo kwa vile mamlaka yake ilisimamiwa kutokea Ufaransa. Na hii ilitokana na Jesuits kuanza kupingwa kila kona katika nchi za Ulaya Hapo ikabidi mfalme huyu kuwa Kifungoni [ufunuo 17:3 inasema “akanichukua katika roho hata jangwani, nikaona mwanamke ameketi juu ya mnyama mwekundu sana…..” Nitaifafanua hapo mbele]
Kwa hiyo kitendo cha utawala wa kirumi ya kidini kuondolewa na kujifungia ndani ya Majengo yao ambayo kulingana na “lateran accord” ili kutatua mgogoro wa “Roman Question” [unaweza ukajifunza zaidi kupitia google, lateran accord/ au the roman question] Watawala wa Rumi ya kidini wakapewa nchi ya Vatican hapo mwaka 1929, Musolin na papa wa wakati Huo waliposaini mkataba rasmi wa Kuwaondoa maaskofu hao kifungoni, sasa Watawala hao wa Kirumi wakaibuka wakiwa hawana nguvu za Kisiasa ila wana nguvu za kiuchumi tu. Hivyo Illuminatti ambao ni Jesuits waliojificha wakajitokeza sana na kueiendelea kuitawala Dunia si kwa nguvu lakini kwa namna iliyojificha kama inavyoonekana leo, ufanyaji wake wa kazi ni SIRI [kitabu cha ufunuo 17:5 inasema” Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri{Mystery}, Babeli Mkuu, Mama wa Mkahaba na machukizo ya nchi”]. Kama leo hii agenda yao ya kuipeleka dunia kwenye Mfumo mpya wa dunia ambao wenyewe wanauita A new world order ambapo watu wanashangaa ufanyaji kazi wa Isis na Ugaidi mwingine, watu wanawezaje kupitisha silaha na kupambana na nchi wakati Serikali Imara za dunia zipo, hiyo ni kazi ya Illuminatti. Hivyo mnyama huyu anayezungumzwa ni Mfumo wa Jesuits au Illuminatti ya Watawala wa Kirumi ambyo headquater yao ipoVatican kwa Jesuits Master Mind wao ni Black Pope.
Mnyama wa pili wa kitabu hiki cha ufunuo anaibuka katika nchi na ana pembe mbili..
Maana yake taifa linaibuka katika sehemu tulivu ya Dunia na kuwa taifa kubwa, hili taifa lenye pembe mbili ni USA, na hizo pembe mbili ni Uhuru wa kisiasa na kidini lililoanza navyo.
Yaani hata sarafu yao na Mnara wao wa Liberty unatangaza uhuru wa kisiasa na msemo wao In God we Trust ni tangazo taifa hili ni la uhuru wa kidini. Ndo maana asilimia kubwa ya dini zetu za leo zina makao makuu kule USA. Japo kitabu cha ufunuo kinasema Ufunuo13:11”……….akanena kama joka ” Pamoja na Uhuru huo wa kidini, taifa la Marekani limeingiliwa na Illuminatti toka karne ya 18,na wamefaikiwa kuibadilisha katiba ya Marekani iliyotangaza uhuru wa kisiasa na kidini.Uhuru wa mtu umeanza kuondolewa kwa kubadilisha vipengere vya katiba vyenye kuleta uhuru.
Walifanikiwa kuivunja vunja Marekani kwa kuleta vita ya wenyewe kwe yenyewe iliyosababisha hiyo nchi kuwa na majimbo ambayo ni nchi zenye sheria zake na maaumuzi yake yanayojitegemea, ndo maana inaitwa United States of America, hii imepunguza uimara na Umoja wa nchi.
Taifa hilo limeingiliwa na hao Illuminatti kwa kuhakikisha Rais yeyote anayeingia madarakani lazima awe mwanachama wa makundi hayo ya Illuminatti na anayepinga basi anaondolewa kwa kutengenezewa kashfa au Sumu au Risasi, lengo ni kuhakikisha agenda za Illuminatti zinatimia. Kwa vile Taifa hili lipo chini ya Illuminati, limekopeshwa pesa nyingi na hawa Illuminatti na kuwa taifa kubwa lenye deni kubwa ambapo sasa hivi mtikisiko wa kiuchumi duniani utasababishwa na deni hilo kushindwa kulipika. Hiyo ni mbinu ya hawa jamaa kuzinunua nchi za dunia na kuzitawala kwa malengo yao.
MWANAMKE.
Katika kitabu cha Ufunuo neno mwanamke linawakilisha Kanisa kwa maana ya watu wenye kuabudu Mungu/mungu [nadhani imeeleweka] ambapo biblia inafananisha watu wanoabudu Mungu kama wanawake, mtoa mada umefafanua.
Mwanamke huyu ameonekana jangwani akiwa amempanda Mnyama[Illuminatti/Jesuits] mwekundu mwenye majina ya makufuru.[maelezo yametolewa,
Maana yake kanisa hili linaongoza Illuminatti/Jesuits kwa kuwa mtu aliyempanda mnyama maana yake mtu huyo ana m control mnyama, kama mwendesha farasi.
Hivyo kutokana na maelezo mengi niliyotoa Kanisa la Kirumi lina control dunia kwa upande wa kisiasa na kiuchumi kutokana na utajiri wake mkubwa unaotokana na kukamata kila kitu kwenye uchumi wa dunia kupitia mifumo yao ya Illuminatti na makundi mengine ya siri yanyotokana na kundi kubwa la Illuminatti Na Jesuits.. Hivyo Babeli si kanisa la Roma Bali ni mfumo pekee wa Ibada ya Sanamu yenye kumuabudu ibilisi, ikiongozwa Kisirisiri na Vatican.
Ili nisiwachoshe sana na haya, kitabu cha Ufunuo 17 kimeeleza vizuri kurudi kwa Mfumo huu wa kipagani kujaribu kulazimisha watu wamuabudu shetani, na kufanya mwisho wa Dunia na Yesu kurudi.
Mambo mengine yatafafanuliwa kulingana na wachangiaji.