Mfahamu kahaba mkuu wa Ufunuo 17

Rudia kusoma mwanzo vzr ,
 
Wewe naona ulishachanganyikiwa, taja iman yako kwanza

Wenzio tunaweka nukuu, wewe unabwabwaja

Nahis wewe ni kund lile'linalodai Hakuna Mungu ,

Hapa hapakufai

YHWH IS GOOD
 
Malaika wa pili alimfuata huyo wa kwanza akisema, Ameanguka! Naam, Babuloni mkuu ameanguka! Babuloni ambaye aliwapa mataifa yote wainywe divai yake divai kali ya uzinzi wake" Ufunuo 14:8

Ameaguka, Babuloni Ameaguka

Ni nani "Babuloni", "Babuloni Mkuu" na "Kahaba"?

Katika Ufunuo sura ya 17, "kahaba" ameelezwa. Anazo sifa nyingi zilizoelezwa, hivyo itakuwa ni rahisi kumtambua. Usikiapo jambo hili mara ya kwanza, huenda ukaichukulia hii kuwa ni lugha kali, lakini hata hivyo: alama zote za kutambulisha katika Biblia zaingiana na Kanisa Katoliki. Bila shaka kunao washiriki wengi wa kanisa hili ambao ni wazuri, wasio na hatia, na si kusudi letu kuwanasa. Lakini twajihisi kuwa tunao mwito wa kuwaonya wao, pamoja na wengineo dhidi ya mfumo huo, hali kadhalika mafundisho ambayo mfumo umejengwa juu yake. Usuli ya onyo hili ni amri ya Biblia, na pia ya kwamba hatuwezi, hali kadhalika kwa sababu ishara na alama za kumtambua yule "Kahaba" kwa mujibu wa biblia zaingiana na utawala huu (Ufunuo 17:5).

Mojawapo ya ishara hizi ni:

Alikuwa ameandikwa juu ya paji la uso wake jina la fumbo: "Babuloni mkuu, mama wa wazinzi na wa mambo yote ya kuchukiza sana duniani"(Ufunuo 17:5)

Kanisa katoliki hujiita mama wamakanisa. Katika barua waliotumiwa maaskofu wote wa ulimwengu, Cardinal Joseph Ratzinger aliandika hivi:

"Yapasa izidi kueleweka waziwazi ya kwamba kanisa moja lilio takatifu, la kikatoliki na la mitume linalozaa dunia nzima, hilo sio dada bali ni mama wa makanisa yote" (Daily telegraph,September 4, 2000).

Matangazo ya aina hii huchangia kuhakikisha ya kwamba kanisa katoliki ndilo linalo utimiza unabii wa Ufunuo 17:5.

HUYU Cardinal Joseph Ratzinger ALIKUJA KUWA PAPA BAADAE

LAKINI KUNA WATU WATAKUJA HAPA KUPINGA HUKU WAKIJIITA NI WAKATOLIKI





YHWH IS GOOD
 
ADHABU KALI KWA WATAKAONDELEA KUBAKI ROMAN CATHOLIC


MUNGU MWENYEZ ANASEMA

yeyote anayemwabudu yule mnyama na sanamu yake na kukubali kutiwa alama yake juu ya pajila uso wake au juu ya mkono wake, yeye mwenyewe atakunywa divai ya ghadhabu ya Mungu ambayo imeminwa katika kikombe cha ghadhabu yake bila kuchanganywa na maji."(ufunuo 14 : 910)

YHWH IS GOOD
 
ADHABU KALI KWA WATAKAONDELEA KUBAKI ROMAN CATHOLIC

kweli kwa hiyo statement yako hapo juu..............
NIMEGUNDUA UPO KWA MALENGO MAALUMU.....................

wnzako walitafuta wafuasi, kwa wao wenyewe kujitoa maisha yao na hata kumwaga damu..................
wewe unatafuta wafuasi kwa njia ya vitisho.............

kazana mbingu ipo karibu
 
Wewe naona ulishachanganyikiwa, taja iman yako kwanza

Wenzio tunaweka nukuu, wewe unabwabwaja

Nahis wewe ni kund lile'linalodai Hakuna Mungu ,

Hapa hapakufai

YHWH IS GOOD
Mbona una swali la kijinga, unataka nikwambie imani yangu, unaweza kuiona, swali linarudi kwako, Hivi Yesu alikuwa na imani gani? Ukinijibu nitakujibu..
 
RC NDIO MAMA WA LAANA DUNIANI

ISAYA 24:4-6 Dunia inaomboleza,
inazimia; ulimwengu unadhoofika,
unazimia; watu wakuu wa dunia
wanadhoofika. Tena dunia imetiwa
unajisi kwa watu wanaoikaa; kwa
maana wameziasi sheria,
wameibadili amri, wamelivunja
agano la milele. Ndiyo sababu laana
imeila dunia hii, na hao wanaoikaa
wameonekana kuwa na hatia, ndiyo
sababu watu wanaoikaa dunia
wameteketea, watu waliosalia
wakawa wachache tu.
SABABU YA KWANZA –WAMEZIASI
SHERIA ZA MUNGU
KATIKA KIPENGELE HIKI TUTATUMIA
USHAHIDI WA BIBLIA NA, KITABU
CHA KATEKISIMU NDOGO YA
KANISA KATOLIKI UK 56, ILI
KUDHIBITISHA;
A. Amri kumi katika biblia KUTOKA
20:1-17 na Amri kumi katika
katekisimu ndogo ya kanisa katoliki;
I. AMRI YA KWANZA KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:1-3
Mimi ni Bwana, Mungu wako,
niliyekutoa katika nchi ya Misri,
katika nyumba ya utumwa.Usiwe na
miungu mingine ila mimi
AMRI YA KWANZA KATIKA
KATEKISIMU
Ndimi Bwana Mungu wako,
usiabudu miungu wengine
II. AMRI YA PILI KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:4-6
Usijifanyie sanamu ya kuchonga,
wala mfano wa kitu cho chote
kilicho juu mbinguni, wala kilicho
chini duniani, wala kilicho majini
chini ya dunia.Usivisujudie wala
kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana,
Mungu wako, ni Mungu mwenye
wivu; nawapatiliza wana maovu ya
baba zao, hata kizazi cha tatu na
cha nne cha wanichukiao, nami
nawarehemu maelfu elfu
wanipendao, na kuzishika amri
zangu
AMRI YA PILI KATIKA KATEKISIMU
Usilitaje bure jina la Mungu wako
III. AMRI YA TATU KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:7
Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu
wako, maana Bwana hatamhesabia
kuwa hana hatia mtu alitajaye jina
lake Bure
AMRI YA TATU KATIKA KATEKISIMU
Shika kitakatifu siku ya Mungu
IV. AMRI YA NNE KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:8-11
Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
Siku sita fanya kazi, utende mambo
yako yote; lakini siku ya saba ni
Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku
hiyo usifanye kazi yo yote, wewe,
wala mwana wako, wala binti yako,
wala mtumwa wako, wala mjakazi
wako, wala mnyama wako wa
kufuga, wala mgeni aliye ndani ya
malango yako. Maana, kwa siku sita
Bwana alifanya mbingu, na nchi, na
bahari, na vyote vilivyomo,
akastarehe siku ya saba; kwa hiyo
Bwana akaibarikia siku ya Sabato
akaitakasa.
AMRI YA NNE KATIKA KATEKISIMU
Waheshimu Baba na Mama, upate
miaka mingi na heri Duniani
V. AMRI YA TANO KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:12
Waheshimu baba yako na mama
yako; siku zako zipate kuwa nyingi
katika nchi upewayo na Bwana,
Mungu wako.
AMRI YA TANO KATIKA KATEKISIMU-
Usiue
VI. AMRI YA SITA KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:13
Usiue.
AMRI YA SITA KATIKA KATEKISIMU
Usizini
VII. AMRI YA SABA KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:14
Usizini
AMRI YA SABA KATIKA KATEKISIMU-
Usiibe
VIII. AMRI YA NANE KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:15
Usiibe
AMRI YA NANE KATIKA KATEKISIMU
Usiseme uongo
IX. AMRI YA TISA KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:16
Usimshuhudie jirani yako uongo
AMRI YA TISA KATIKA KATEKISIMU
Usitamani mwanamke asiye mke
wako
X. AMRI YA KUMI KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:17
Usiitamani nyumba ya jirani yako,
usimtamani mke wa jirani yako; wala
mtumwa wake, wala mjakazi wake,
wala ng'ombe wake, wala punda
wake, wala cho chote alicho nacho
jirani yako
AMRI YA KUMI KATIKA KATEKISIMU
Usitamani mali ya mtu mwingine
MAELEZO MAFUPI
Angalia hizo amri utaona ujanja
uliofanyika amri ya pili imeondolewa
kabisa kwa mjibu wa biblia na amri
ya kumi imegawanywa zikawa mbili
ilikusudi ijaze nafasi ya amri
iliyoondolewa ilimradi tu ziwe kumi


YHWH IS GOOD
 
ROMAN CATHOLIC, ACHENI KUMSAIDIA JOKA KAZI

"Ndipo yule Joka [Ibilisi] akamkasirikia sana yule mwanamke [Kanisa la Mungu], akaenda zake afanye vita dhidi ya wazao wake waliosalia - wale wanaozitii amri za Mungu na kuwa na ushuhuda wa Yesu." - (Ufunuo 12:17).

Unabii huu unalenga katika siku zetu hizi. Shetani amekasirika sana; anafanya vita dhidi ya wazao wa mwanamke waliosalia" - yaani, dhidi ya watu wa Mungu wa siku hizi. Angalia alama zao zinazowatambulisha:
(1)Waumini hao wa siku za mwisho wanao "ushuhuda wa Yesu." Kwa uaminifu wakiyang'ang'ania mafundisho safi ya Neno la Mungu, wanamshuhudia Yesu kwa njia ya maisha yao yenye nguvu nyingi ya Kikristo.

(2) Wakristo hao wa siku za mwisho ni watu wa unabii. Kuupokea ule "ushuhuda wa Yesu Kristo" kulimwezesha Yohana kukiandika kitabu kile cha Ufunuo (Ufunuo 1:1-3). Kundi hilo la mwisho la waumini linapokea karama ile ile: yaani, ushuhuda wa moja kwa moja toka kwa Mungu kupitia kwa mjumbe wa kibinadamu. Karama yao ya unabii inalenga juu ya ufunuo wa Mungu kuhusu utume wao na mwisho wao.

(3) Wakristo hao wa siku hizi za mwisho wanatambulikana pia kama "wale wanaozitii Amri [kumi] za Mungu." Hawatetei tu ukamilifu wa hizo Amri Kumi, bali wanazitii pia. Upendo wa Mugu ulio mioyoni mwao unawaletea utii unaotolewa kwa moyo wa furaha (Warumi 5:5; 13:8-10).

Wakristo hao wa siku hizi za mwisho wanakifuata kielelezo cha Kristo na cha kanisa lile la kwanza kwa kuzitii amri [kumi] za Mungu. Jambo hilo linamkasirisha vibaya sana yule Joka - yaani, yule Ibilisi. Naye anapigana vita dhidi ya "wazao" wa mwanamke "waliosalia" kwa sababu wanatoa ushuhuda kwamba upendo wao kwa Mungu unawafanya wafuasi wake hao kuwa watii. Kama vile Kristo alivyoagiza, aliposema:
"Mkinipenda, mtazishika amri zangu" - Yohana 14:15.

Maisha ya Wakristo hao wa siku hizi za mwisho yanaonyesha kwamba uwezekano upo wa kumpenda Mungu kwa mioyo yetu yote na kuwapenda wenzetu kama sisi tunavyojipenda wenyewe. Kulingana na maneno ya Yesu, sifa hizo za tabia, yaani, upendo kwa Mungu na upendo kwa watu, hufanya muhtasari wa Amri kumi za Mungu (Mathayo 22:35-40).

Ya nne katika hizo amri inatutaka sisi kuitunza Jumamosi, siku ya saba ya juma, kama Sabato. Kwa kuwa upendo wao kwa Yesu umezitia ndani ya mioyo yao amri zote kumi [Ebr. 8:10; Kut. 20:3-17; Yak. 2:10-12], basi, Wakristo hao wa siku hizi za mwisho ni Wasabato.

Sabato ndicho kiini cha ujumbe wa mwisho wa Mungu kwa watu wake katika kitabu cha Ufunuo, sura ya 12 na 14:6-15. Nguvu zote za mbinguni zinajipanga nyuma ya Wakristo hao wa siku hizi za mwisho walioelezwa katika sura hizo. Mwokozi wao aliye hai ndiye rafiki yao daima, na Roho Mtakatifu anafanya kazi yake "kuwafanya imara kwa nguvu katika utu wao wa ndani." Ahadi yake ni ya hakika. WATAmshinda Shetani "kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao" (Ufunuo 12:11).

Je! unataka kuwa mmoja wa Wakristo hao wa siku hizi za mwisho ambao "wanazitii amri [kumi] za Mungu" tena wa"na ushuhuda wa Yesu"? Kwa nini usikate shauri sasa hivi?



YHWH IS GOOD
 
NAMBA 666 AU 616 ILIYOANDIKWA KWENYE UFU 13:18 HAIMHUSU PAPA ISIPOKUWA ELLEN GOULD WHITE
Imbeni pamoja nami ALLELUYA! Kwa nini? Kwa sababu Mungu amenitendea makuu. Amenisaidia kukitegua kitendawili cha karibu karne mbili sasa, yaani kitendawili cha namba 666. Kwa muda mrefu tangu enzi za akina ELLEN GOULD WHITE, yaani miaka ile ya 1846, namba 666 ya katika Ufu 13:18 imekuwa ikielekezwa kwa majungu na matusi kwa Baba Mtakatifu. Ndugu zanguni, tulikuwa tunazugwa tu. Kumbe, siri ni kwamba ilikuwa inamwelekea mwenyewe aliyekuwa anaelekeza mashambulizi na matusi kwa Baba Mtakatifu, yaani ELLEN GOULD WHITE.
Nina furaha kubwa sana. Nawaalikeni mfurahi pamoja nami. Binafsi, nilikuwa napata taabu sana kujaribu kufumbua kitendawili hicho. Lakini, wakati huo huo, nilikuwa najiuliza kwa nini mashambulizi kwa Baba Mtakatifu ni makali hivyo? Kumbe, sasa tumefumbuliwa. Yote yalikuwa ni mbinu ya kutupoteza watu “maboya” tusijue kwamba namba inamwelekea mwenyewe anayetukana. Kumbe, ilikuwa ni mbinu ile ile ya mwizi kupiga kelele za “Mwizi, mwizi, mwizi huyo!” kusudi watu wamfukuze mtu mwingine na siyo yeye mwenyewe.
Acheni niwakumbusheni mambo. Nadhani nyote mna habari na mashtaka maarufu sana dhidi ya Wakatoliki kwamba namba 666 au 616 inamhusu kiongozi wetu mkuu yaani Papa au Baba Mtakatifu na kwamba namba hiyo imeandikwa kwenye mavazi yake na kofia yake. Zaidi ya hapo kuna madai kwamba namba hii ipo pia katika kompyuta na satelite. Leo nataka niwafunulieni mambo yalivyo.

Hii ni Mada ya Lugha na Hesabu Kidogo
Vijana wangu msishtuke na kuhangaika. Mada hii itahusisha herufi za Kiebrania na Kigiriki lakini zitakuwa chache tu nanyi mtaelewa yote nitakayoandika kwani ni masuala rahisi kuyafuatilia. (Kwa bahati mbaya herufi za Kigiriki zinakataa humu). Papo hapo, kutakuwa na hesabu. Hata hizo hazitawahangaisheni kwani ni hesabu za kujumlisha tu. Leo kumbukeni pia hesabu za Shule ya Msingi tulipokuwa tunatumia tarakimu za Kilatini, kwa mfano, I = 1, V = 5, X= 10, L = 50, C= 100, D = 500 na M = 1000.
Ili tuelewane, nitaanza na historia, kishapo nitakwenda nje ya Biblia ilikohamishiwa namba 666.

Mama ni Historia
Hebu nianze na jibu fupi linalolingana na historia. Wayahudi hujumlisha thamani ya kitarakimu majina ya watu na maneno mbalimbali na kuzaa namba mbalimbali. Kuhesabu kwa namna hii huitwa gematria nako kumetumika katika Ufu 13:18 na kuzaa namba 666 au katika nakala zingine za Biblia namba 616. Swali kubwa ni je, namba hiyo inamhusu nani? Ukweli ni kwamba namba 666 au 616 haimhusu Papa au Baba Mtakatifu hata kidogo. Tena haikuandikwa katika mavazi ya Papa na wala haimo katika kompyuta ama satelite.
Ukweli, kibiblia na kihistoria, ni kwamba namba hiyo ilimhusu na bado inamhusu kiongozi wa dola ya Kirumi zamani zile, yaani Kaisari Nero. Basi, namba 666 au 616 ndiyo hesabu ya jina la Nero aliyekuwa akiwadhulumu Wakristo katika karne ya kwanza ya Ukristo. Hesabu hiyo inapatikana kwa kukokotoa kigematria maneno NERON KAISAR (kwa Kiebrania - נרון קסר) au NERO KAISAR (kwa Kiebrania - נרו קסר) na KAISAR THEOS (kwa Kigiriki).

Jibu refu: Hakuna mahali po pote katika Biblia ambapo msomaji ameombwa kutumia akili isipokuwa hapa. Kwa kuwa ili kuipata hesabu hii kulihitaji kupiga hesabu, wasomaji wote wa kifungu kile walialikwa kupiga hesabu, gematria. Ndipo imeandikwa “Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili na aihesabu hesabu” (Ufu 13:18). Kumbe, kinyume na matumizi ya akili, hapa ndipo mahala wasomaji kadha wa kadha wasipotumia akili yoyote katika kusoma isipokuwa majungu na usingiziaji.
Ndugu yangu, wapo watu chungu nzima wanaoeneza tafsiri kwamba namba 666 au 616 inamhusu Baba Mtakatifu na imeandikwa kwenye mavazi yake kama nilivyosema hapo juu (rejea Ufu 13:18, 15:2). Je, mafundisho hayo yana ukweli? Najijibu mwenyewe: si ya kweli.
Tusisahau, kitabu cha Ufunuo wa Yohane kina mazingira yake ya kihistoria ambayo ni muhimu katika kuielewa sura ya 13. Mazingira hayo ni ya historia ya Dola ya Kirumi. Wakristo walipokuwa wakidhulumiwa na dola hiyo, mwandishi wa kitabu cha Ufunuo alichukua kalamu na kuandika ili kuwaliwaza ndugu zake aliokuwa akiteseka pamoja nao (rejea Ufu 1:9). Basi, katika kuandika akatumia lugha ya mafumbo ili watesi wasifahamu wanayosemwa. Ndicho kisa, basi, joka kuu lenye pembe na kadhalika linamaanisha Dola ya Kirumi. Mkubwa wa dola hiyo naye akapewa jina la kupanga au jina la kifumbo kwa mtindo wa kucheza na namba za jina lake (gematria).
Ukitaka kupata picha kidogo ya haya, chukulia mfano wa vitabu vya marehemu Shaban Robert. Yeye aliandika mashairi mengi ya kuwatia watu hamasa wapiganie uhuru. Katika mashairi hayo, wananchi anawaita, mathalani, siafu na wakoloni nyoka. Hao siafu wanakazana kumdhuru nyoka. Aidha, kitabu chake cha Kusadikika ni kitabu cha fumbo kinachofumbia hali ya mambo katika hewa ya kikoloni. Kwa hakika wakoloni hawakuambulia lolote katika mashairi na fasihi ya Shaban Robert. Kinyume chao, wananchi walielewa mada husika na “kuwaacha kwenye mataa” wakoloni. Ndivyo inavyotokea shuleni, mwalimu mbaya kupangwa jina ambalo mwenyewe halijui hata kama litatajwa mbele yake.
Upangaji wa jina la mtu kwa kutumia hesabu ya herufi za jina lake mwenyewe ulikuwa mtindo maarufu wa marabi na ulijulikana kama gematria. Ufu 13:18, si mahali pa kwanza kutumia gematria hata namba kumi na nne ya vizazi vilivyotajwa katika Mt 1:17 ni gematria ya jina Daudi (דוד) kwani d + w + d ni 6 + 4 + 6 = 14. Sasa ni nani katika karne ya kwanza aliyekuwa adui wa Wakristo na jina lake kigematria lilizaa namba 666 au 616? Hili ndilo swali la kuulizana. Alikuwa KAISARI NERO.
Tukitafsiri Biblia kwa usahihi huu, mtesi wa walengwa wa kitabu, aliyekuwa akifumbiwa katika 13:18 kwa kuhesabu jina lake kigematria, hawezi kuwa mtu wa karne ya tano au ya ishirini na moja. Walengwa walikuwa ni Wakristo wa karne ya kwanza na adui yao alikuwa akiishi nao kwa wakati huo huo. Basi, nani alikuwa mtesi maarufu katika mazingira ya karne ya kwanza? Wakati ule alikuwa Kaisari Nero ama Kaisari fulani aliyejidai kuwa Mungu na huyo ndiye kigematria jina lake linazaa namba 666 au 616.
Basi, gematria ikitumika kwa konsonanti za Kiebrania: נרון קסר - NERON KAISAR (yaani Kaisari Neron) au kwa maneno ya Kigiriki: KAISAR THEOS (yaani Kaisari Mungu) tunapata pasipo kuzunguka zunguka namba 666 au 616. Tazama hesabu zenyewe zinavyofanyika. (נרון קסר) r s q n w r n = 200 + 60 + 100 + 50 + 6 + 200 + 50 = 666.
k a i s a r th e o s = 20 + 1 + 10 + 200 + 1 + 100 + 9 + 5 + 70 + 200 = 616.
Angalia vyema. Hii tafsiri ya ‘KAISAR THEOS’ yaani ‘Mungu Kaisari’ ndiyo inayorejewa kwenye Biblia zenye kuandika jumla ya namba 616. Lakini vile vile 616 iliweza kupatikana kwa kuondoa “n” ya mwisho kwenye jina נרון (n w r n) katika Kiebrania. Kwa Wakristo, namba 666 ilipomtaja Neron ilisema pia kwamba ni MPINGA KRISTO kwani alikuwa kinyume cha utimilifu. Kinambari, utimilifu ni namba 777. Kumbe, yeye Kaisari Nero ni upungufu kwani hesabu yake ni 666 ambayo ni 777 kutoa 111.
Basi, kwa kuzingatia mazingira ya kitabu cha Ufunuo namba 666 au 616 haiwezi kusimama kwa ajili ya jina lingine kama Baba Mtakatifu, Mtume Mohamed au Mussolini. Haya ni baadhi ya majina wanayolazimisha watu yafanye hesabu ya 666. Na, kwa hakika, namba hiyo haimo katika mavazi wala kofia (mitra) ya Baba Mtakatifu. Hakuna mtu yeyote anayeweza kuonesha vazi hilo au kofia hiyo kwa ushahidi. Kwani ni vazi gani au kofia ipi? Basi, kama tunautafuta uzima wa milele, aheri tuache majungu na uongo kama huu. Kama ni maandishi, ni mitra yake tu yenye herufi mbili A na W yaani alpha na omega (rejea Ufu 1:8,17).
Acha tuendelee. Wanaombambikizia Baba Mtakatifu namba 666 hudai kuikokotoa nambari hiyo katika majina matatu tofauti: jina la Kilatini VICARIUS FILII DEI (Kaimu wa Mwana wa Mungu), jina la Kigiriki LATEINOS (Mlatini) na jina la Kiebrania ROMIITH (רמיית - Mrumi). Majina hayo huhesabiwa na wanaombambikizia Baba Mtakatifu namba hiyo kama ifuatavyo:
VICARIUS FILII DEI = 5 + 1 + 100 + 0 + 0 + 1 + 5 + 0 + 0 + 1 + 50 + 1 + 1 + 500 + 0 + 1 = 666.
LATEINOS = 30 + 1 + 300 +5 + 10 + 50 + 70 + 200 = 666.
ROMIITH yaani th y y m w r = 400 + 10 + 10 + 40 + 6 + 200 = 666.
Ndugu zangu, kwa misingi halali ya kusoma Biblia hatuwezi kuyapokea majina haya bila kuyafanyia tahakiki ya kihistoria. Bila kurefusha mjadala, majina haya hayajapata kutumiwa na Baba Mtakatifu yeyote, katika historia ya Kanisa sembuse wakati wa karne ya kwanza Baada ya Kristo wakati ambao hata upapa wenyewe ulikuwa haujakua. Mapapa wa karne zile hawakuwa hatari kwa mtu yeyote. Na watu wasio hatari watapewaje majina ya kupanga na ya siri? Wale wasomaji wa kitabu cha Ufunuo wangelielewaje aya ngumu inayotaja kitu kisichojulikana kwa jina hilo? Wangelifanyaje gematria kwa kutumia majina wasiyoyajua?
Aya 13:18 ilizungumzia jina ambalo wasomaji walikuwa wakilijua kama jina la adui yao aliyekuwa akiwadhulumu na si majina ya ndoto au majungu ya karne ya 20 na 21 B.K. Zaidi ya hayo majina mengine yamelazimishwa kihesabu ili jumla ya kiherufi iwe 666. Kwa ushuhuda tazama U ilivyolazimishwa imaanishe tarakimu 5. Katika Kilatini 5 ni V na wala siyo U. Zaidi ya hayo, jina “MLATINI” kama lingelitumika wakati huo, wasomaji wangelielewa kuwataja wakoloni au askari wa kirumi ambao walikuwa wakitawala ulimwengu wa wakati ule.
Hali kadhalika, kama jina “MRUMI” lingelitumika wakati huo, wasomaji wangelielewa kuwataja wakoloni au askari wa kirumi ambao walikuwa wakitawala ulimwengu wa wakati ule. Kwa hoja hizi, majina hayo ya majungu ni ya tangu karne ya 16, Kanisa Katoliki lilipoanza kupingwa kwa ari mpya na uongozi wake kukataliwa.
Nadhani hadi hapa kila mwenye kutaka kujua anajua kwamba majina waliyobuni Wasabato hayatumiwi na Baba Mtakatifu yeyote. Na zaidi ya hayo ni majina ambayo mwandishi wa kitabu cha Ufunuo hakuwa hata na habari nayo katika karne ile ya kwanza B.K. kwa vile alivyokiandika kitabu chake kwa Kigiriki na wala si kwa Kiebrania au Kilatini. Kumbe, kwa kufanya hivyo Wasabato huwa wanainyonga historia na kukizungumzia kitabu cha Ufunuo nje ya muktadha wake wa kihistoria. Hili ni kosa la kusiganisha nyakati za kikalenda (kwa Kiingereza “anachronism”).
Basi, kwa heshima ya Maandiko Matakatifu, tutafsiri namba 666 au 616 kwa gematria asilia na tukomee hapo hapo. Tusiihamishe namba hiyo na kuwapachika watu wasio na hatia. Kufanya hivyo ni kujitowelesha majungu na ni dhambi isiyo na maana yo yote. Lakini, basi namba 666 imetolewa nje ya mazingira ya Biblia na ndipo ilipowekwa sasa. Nami nimefika hapo hapo.

Namba 666 Imehamishiwa Nje ya Biblia
Ni kituko lakini ndivyo ilivyo. Watu wengine hudai kwamba namba hiyo imeandikwa shingoni kwenye nguo za Papa. Huo ndio uongo na usingiziaji usio na aibu kwa sababu nguo hizo hakuna anayeweza kutuonesha wenziwe. Siku moja niliwahi kuambiwa na wainjilisti wawili kwamba namba 666 ipo kwenye bidhaa za siku hizi, yaani kwenye kifungashio, pale inapochorwa mistari mingi mifupi na mirefu na kuandikwa namba kwa chini, na kwa namna hiyo ipo pia kwenye satelite. Siku hiyo niliwakamata kutokujua nilipowadai wanioneshe mfano. Basi, wakaleta baadhi ya bidhaa za kisasa, wakaniambia niangalie ile mistari iliyochorwa katika kifungashio cha kila bidhaa. Hapo walionesha pia mistari miwili miwili inayojitokeza zaidi kwa chini (jambo ambalo si kweli kwa kila bidhaa). Basi, hapo ndipo walipodai kuna namba 666.
Kumbe, huu ulikuwa ujinga wao mkubwa. Ndugu yangu, mistari hiyo, ndiyo bei ya bidhaa hasa kwa zile zinazouzwa „“supermarket. Katika nchi zilizoendelea watu hawaandiki bei shilingi fulani au fulani wakabandika kwenye bidhaa. Badala yake ndiyo hiyo mistari, kadiri ilivyochorwa ndivyo mashine ya kupigia hesabu inavyotambua na kutofautisha bei za bidhaa ambazo mnunuzi amezifikisha kwenye “kaunta” ya kulipia manunuzi. Na tena bei hizo hazikuingizwa katika satelite; zilivyo nyingi hazihusishwi na satelite yoyote.
Basi, niliwaonya wainjilisti wale wasiwadanganye watu kwa kutumia ujinga wao wakati wenyewe pia hawajui mambo ya kisasa. Hatimaye, niliwaambia, kwa uongo wa namna ile, wao si wainjilisti kwani Injili ni Habari Njema ya ukombozi wetu uliotufikia kwa kifo na ufufuko wa Yesu Kristo na wala siyo namba 666 inayodaiwa kuandikwa kwenye nguo za Papa na kuingizwa kwenye satelite kwa njia ya michoro ya bidhaa za kisasa. Kwa kweli niliwaambia kwa kueneza uongo na kuwatia watu hofu kwa kuwatinga, hawakuwa mbali sana na moto wa milele kwa vile wanamtumikia Shetani aliye baba wa uongo. Hapo nikapata mwanya wa kuwaalika watubu kwa haraka. Lakini, badala ya kupokea mafundisho yangu walisema sina Roho Mtakatifu na kuondoka. Waliondoka na hawakurudi tena kwangu. Kumbe, niliwafuma katika kutokujua kwao, yaani ujinga wao. Samahani kwa simulizi hili; majadiliano yetu yaliacha kuwa ya Kikristo.

Safari Ndefu ya Kutegua Kitendawili cha Kale
Kwa vile madai ya kwamba namba 666 inamhusu Baba Mtakatifu yametutoa sote kutoka kwenye Biblia na kutupa kazi ya kumtafuta nani mwingine anaweza kuwa anatajwa na namba hiyo, nilichukua kalamu na kuanza kuchunguza maneno ya wanaotukana kama hayahusiki vile vile. Utafutaji wangu ulizaa matunda mwaka ule ule 1998. Nikategua kitendawili kwa kugundua kwamba kauli za Wasabato wenyewe zilikuwa ndiyo namba 666.

Nilifanyaje? Nilichukua kauli tatu: PONYA SIKU MUHIMU YA SABA (kwa Kiingereza CURE VITAL SEVENTH DAY, kwa Kilatini CURATUS VITALE SABBATA DIES) na WOKOVU, PONYA SIKU YA SABA (kwa Kiingereza SALVATION, CURE SEVENTH DAY, kwa Kilatini SALVUS, CURARE SABBATA DIES) na VUNJA, CHUKIA UPAPA (kwa Kiingereza DEAL AXE, VIE PAPACY). Nilistaajabu sana kuona ndiyo inakuja 666 ndipo mara moja nikaingiza ugunduzi wangu katika kitabu changu KISA CHA IMANI namba 1.

Ni kweli. Kauli mbiu za Wasabato ni namba hiyo hiyo 666. Angalia gematria inavyokwenda:
CURE VITAL SEVENTH DAY = 100 + 5 + 0 + 0 + 5 + 1+ 0 + 0 + 50 + 0 + 0 + 5 + 0 + 0 + 0 + 0 + 500 + 0 + 0 = 666
CURATUS VITALE SABBATA DIES = 100 + 5 + 0 + 0 + 0 + 5 + 0 + 5 + 1 + 0 + 0 + 50 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 500 + 1 + 0 + 0 = 666
SALVATION, CURE SEVENTH DAY = 0 + 0 + 50 + 5 + 0 + 0 + 1 + 0 + 0 + 100 + 5 + 0 + 0 + 0 + 0 + 5 + 0 + 0 + 0 + 0 + 500 + 0 + 0 = 666
SALVUS, CURARE SABBATA DIES = 0 + 0 + 50 + 5 + 5 + 0 + 100 + 5 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 500 + 1 + 0 + 0 = 666
DEAL AXE VIE PAPACY = 500 + 0 + 0 + 50 + 0 + 1 0 + 0 + 5 + 1 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 100 + 0 = 666

Kuendelea Kutafuta
Basi, kwa kuwa nilikuwa namtafuta nani mwingine anayesemwa na namba 666 au 616, nikagundua kumbe ni hao hao wanaotukana. Lakini, sikukomea hapo mwaka huu 2017 macho yangu yakasaidiwa kuona zaidi. Nilichukua jina la mwasisi wa matusi mwenyewe ELLEN GOULD WHITE ndipo nikashtuka kabisa kumbe ni namba 666. Kwa kisa hiki, leo nawaomba tuimbe alleluya pamoja.

ALLELUYA! KUMBE NAMBA 666 NI ELLEN GOULD WHITE MWENYEWE
Sasa nawapeni habari njema kabisa. Tusi la namba 666 limefumbua macho yangu kwa namna ya ajabu na sasa nawatangazia wote nilichokigundua ili kiwafumbue macho ninyi pia. Kifupi, nimefikishwa kwenye ugunduzi huo kwa kupitia tahadhari ya wahenga. Wao walisema, “Unapokula na kipofu, usimguse kipofu mkono!” Msidanganyike tena, namba 666 ni ELLEN GOULD WHITE mwenyewe.

Nawasimulieni. Kwa kuzidi kutukana, niliwatazama watukanaji nione kama matusi hayawahusu wenyewe. Nikagundua kumbe ndiyo hivyo hivyo. Kumbe, wakati mwingine heri utukanwe maana waweza kufunguliwa mlango kwa jambo jema fulani. Basi, natangaza kadamnasi kwamba tusi la namba 666 limekuwa tusi la neema na heri sana kwetu Wakatoliki, tulionyanyasika kwalo kwa muda mrefu. Linawahusu wanaotutukana hao hao. Kumbe, walikuwa wanapiga kelele za “Mwizi, mwizi!“ ili kutupoteza maboya tu. Wezi ni wenyewe.

Tuamke. Jamani, Bi Ellen Gould White alikuwa anapiga kelele na kutukana kusudi tusishughulike na jina lake. Wafuasi wake wakadakia mbinu hiyo hiyo. Kumbe, Wasabato hukazania namba 666 imwelekee Baba Mtakatifu kwa sababu walitaka tusijue kwamba namba 666 inamwelekea “nabii” wao ELLEN GOULD WHITE! Walitaka tukamsake sungura katika kichaka kingine. Kumbe, Ufu 13:18 inamtaja Bi Ellen White moja kwa moja kama mnyama ambaye jina lake ukilikokotoa linakuja moja kwa moja kwenye namba 666. Yaani linakuja 666 taslimu!
Je, unaniuliza kwa vipi? Ni hivi ifuatavyo. Ukiliandika jina la Bi ELLEN WHITE pamoja na jina la asili yake GOULD unakuja kwenye namba 666 juu ya alama. Nifuatilie vyema hapa kusudi tukokotoe tarakimu pamoja. Lakini, angalia vyema, jambo lile la kuhitajika hekima, linahusisha pia kuirudisha “W” ya WHITE kwenye uasilia wake yaani V maradufu (kwa Kiingereza “double v”). Kwa taarifa yako, tangu kale “W” ni “V” mbili na ni kwa sababu ya asili hiyo Wajerumani huitamka “W” kama “V”. Umeshanielewa uzuri? Kama umeshanielewa, sasa tazama “gematria“ inavyokubali:
E L L E N G O U L D W H I T E
0+ 50 + 50 + 0 + 0 + 0 + 0 + 5 + 50 + 500+ 10+0+1+0+0 = 666

Je, unaona jinsi jina la Bi Ellen White linavyokubali kama jina la mnyama yule? Yaani sawa sawa pasipo kuacha mashaka yoyote. Kinyume chake, jiulize ni Baba Mtakatifu gani mwenye jina kama hilo? Maskini, Wasabato walisahau jambo hili la kimahesabu! Lakini nadhani wanalifahamu na ndiyo maana hufanya juhudi kubwa kulikoneshea tusi la namba 666 kwa Baba Mtakatifu. Ni janja yao lakini sasa ipo hadharani.
Narudia. Wanachofanya Wasabato ni mbinu ya kawaida tu, yaani kwamba ukitaka watu wasikuangalie wewe elekeza umakini wao kwa mtu mwingine au kitu tofauti. Ndipo, badala ya watu kuelekeza umakini kwenye jina “ELLEN GOULD WHITE” huzugwa waelekeze kwenye majina ya kubuni ya “VICARIUS FILII DEI”, “LATEINOS” na “ROMIITH”, majina yasiyo na maana yoyote kihistoria na muktadha wa kitabu cha Ufunuo.
Je, umeona eh! Kumbe, mambo yako kwenye majina “ELLEN GOULD WHITE”. Namba 666 inakubali taslimu kabisa. Chukua hii!

germve himself
 
Hao Seventh Day ndio akina nani ?
Na huyo Ellen G White ndio nani ?

Mi siwaoni kwenye Biblia.
Nawaona Waisraeli, Warumi, Wafilipi nk.

Pia nawaona watumishi kama Musa Eliya Paulo nk.

Hebu tufafanulie kwanza umewatoa wapi hao unaowaita,

Seventh Day na huyo Ellen White ?
 
 

Hizi ni nondo barikiwa mtumishi.
 

Naomba asiyejua vizuri mafundisho ya Kisabato asome hapo chini

Waadventista wasabato huipokea Biblia kama kanuni yao pekee na hushika baadhi ya
misingi ya imani kuwa ndiyo mafundisho ya mabadiliko matakatifu. Imani hizi, kama
zilivyoorodheshwa hapa, hufanya welekevu wa kanisa na udhihirisho wa mafundisho ya
mabadiliko. Masahihisho ya kauli hizi yanaweza kutegemewa katika kikao cha Halmashauri
kuu wakati kanisa likiongozwa na Roho Mtakatifu kwenye ufahamu ulio kamili zaidi ya
ukweli wa Biblia au linapopata lugha iliyo bora zaidi ya kuelezea mafundisho ya Neno
Takatifu la Mungu.
1.Maandiliko Matakatifu
Maandiko Matakatifu, yaani Agano la kale na Jipya ndiyo Neno la Mungu lililoandikwa,
likatolewa kwa uvuvio wa Mungu, kupitia kwa watu watakatifu walionena na kuandika kama
walivyoagizwa na Roho Mtakatifu. Ndani ya neno hili, Mungu amemkabidhi mwanadamu
maarifa yaliyo lazima kwa ajili ya wokovu. Maandiko matakatifu ni ufunuo usioweza kukosa
wa mapenzi yake. Ndiyo upeo wa tabia, kipimo cha uzoefu, ufunuo thabiti wenye mamlaka
wa mafundisho ya imani, na kumbukumbu aminifu ya matendo ya mungu katika historia.
(2Petro 1:20,21. 2Timotheo 3:16,17. Zaburi 119: 105. Mithal 30: 5,6. Isaya 8:20. Yoh
17:17. 1Wathe 2:13. Waeb4:12.)
2.Utatu Mtakatifu
Kuna Mungu mmoja: Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, umoja wa nafsi tatu za milele.
Mungu hapatikani na mauti, mwenye nguvu zote, ajuaye yote, zaidi ya yote, na aliyeko
daima. Yeye hana mwisho na ni zaidi ya ufahamu wa kibinadamu, hata hivyo anafahamika
kupitia kujifunua kwake binafsi. Milele zote yu astahili kuabudiwa, kusujudiwa, kutumikiwa
na viumbe vyote. (kumb 6:4. Mith 28:19. 2kor 13:14. Waef 4:4-6. 1Petr 1:2 1Tim 1:17
Ufunuo 14:7)
3.Baba
Mungu Baba wa milele ndiye muumbaji, Chimbuko, Mtengenezaji, na Mfalme wa viumbe
wote. Ni mwenye haki na Mtakatifu, Mwingi wa rehema,, mwenye fadhili, si mwepesi wa
hasira, na mwingi wa uthabiti wa upendo na uaminifu. Tabia na uwezo vilivyodhihirishwa
ndani ya Mwana na Roho Mtakatifu pia ni ufunuo wa Baba. (Mwanzo 1:1 Ufu 4:11.
1wakor 15:28. Yoh 3:16. 1Yoh 4:8. 1Tim 1:17. Kut 34:6,7. Yoh 14:9).
4.Mwana
Mungu Mwana wa milele alifanya mwili katika Yesu Kristo. Kupitia kwake vitu vyote
viliumbwa, tabia ya mungu imefunuliwa, wokovu wa wanadamu unakaribishwa na
ulimwengu unahukumiwa. Milele zote Mungu kweli, Alifanyika mwanadamu kweli, Yesu
aliye kristo. Alichukuliwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na kuzaliwa na bikira
Mariamu. Akaishi na kupitia uzoefu majaribu kama mwanadamu, lakini kwa ukamilifu
alioonyesha kwa mfano wa haki na u[endo wa Mungu. Kwa miujiza yake alidhihirisha
uwezo wa Mungu na alithibitishwa kama Masihi aliyeahidiwa. Aliteseka na kufa kwa hiari
msalabani kwa ajili ya dhambi zetu, na kama mbadala wetu, Alifufuliwa kutoka kwa wafu,
na akapaa kuhudumu katika hekalu la mbinguni kwa niaba yetu. Atakuja tena katika
utukufukwa ajili ya ukombozi wa mwisho wa watu wake na urejeshwaji wa vitu vyote. (Yoh 1: 1-3,14. Wakol 1: 15-19,. Wafil 2:5-11. Yoh 10:30, 14:9 Warum 6:23. 2Wakor 5:17-19.
Yoh 5:22. 1Wakor 15:3,4. Luka 1:35. Yoh 14:1-3)
5.Roho Mtakatifu
Mungu Roho wa milele alikuwa mtendaji pamoja na Baba na Mwana katika uumbaji,
kufanyika mwili, na katika ukombozi. Aliwavuvia waandishi wa mabadiliko matakatifu.
Alijaza maisha ya kristo na uwezo. Huwavuta na kuwasadikisha wanadamu, na wale
wanaoitikia huwafanya upya na kuwabadilisha katika sura ya Mungu. Akipelekwa na Baba
na Mwana ili kuwa siku zote pamoja na watoto wake, hutoa karama za kiroho kwa kanisa,
huliwezesha kumshuhudia kristo, na kwa upatano wa maandiko uliongoza kwenye ukweli
wote. (Mwa 1,2. Luka 1:35, 4:18. Mdo 10:38. 2Petr 1:21. 2Wakor 3:18. Yoh 14:16-18,26,
15:26,27, 16:7-13)
6.Uumbaji
Mungu ni muumba wa vitu vyote, na amefunua katika maandiko uhalisi wa tukio la
shughuli zake za uumbaji. Katika siku sita Bwana alizifanya “Mbingu na Nchi” na vitu vyote
vilivyoko hai juu ya nchi, akastarehe siku ya saba ya juma lile la kwanza. Na hivyo
akaanzisha sabato kama kumbukumbu ya milele ya kukamilika kwa kazi yake ya uumbaji.
Mwanaume na Mwanamke wa kwanza walifanywa kwa mfano wa Mungu kama upeo wa
kazi yake ya Uumbaji, wakapewa utawala juu ya ulimwengu, na wakaagizwa kuajibika na
utunzaji wake. Wakati ulimwengu ulipomalizika kila kitu kilikuwa “ni chema sana”
ukitangaza utukufu wa Mungu. (Mwa 1,2. Kut20:8-11. Zab 19:1-6, 33:6-9, 104. Waebr
11:3)
7.Asili ya Mwanadamu
Mwanaume na Mwanamke walifanyawa kwa mfano wa Munguwakiwa kila mmoja na nafsi
yake, uwezo na uhuru wa kufikirina kutenda. Ingawa waliumbwa viumbe huru, kila mmoja
ni umoja wa nafsi isiyogawanyika ya mwili, akili na roho, akimtegemea Mungu kwa uhai na
pumzi na mengine yote. Wakati wazazi wetu wa kwanza walipomwasi Mungu, walikana
utegemezi wao kwa Mungu na wakaanguka kutoka hadhi yao ya juuchini ya Mungu. Sura
ya Mungu iliyopo ndani yao ikaharibika na wakawa chini ya mauti. Wazao wao hushiriki
asili hii ya kuanguka na matokeo yake. Wanazaliwa wakiwa na udhaifu na mivuto ya
kuelekea kwenye uovu. Lakini Mungu katika kristo aliupatanisha ulimwengu na nafsi yake,
na kwa Roho wake hurejesha ndani ya mwanadamuwatubuo sura ya muumba wao.
Wakiwa wameumbwa kwa ajili ya utukufu wa Mungu, wanaitwa kumpenda na kupendana
wao kwa wao na kutunza mazingira yao.(Mwa 1:26-28, 2:7. Zab 8:4-8. Mdo 17:24-28. Mwa
3. Zab 51:5 War 5:12:17. 1Yoh 4:7,8,11,20. Mwa 2:15
8.Pambano kuu
Jamii yote ya wanadamu sasa inahusika katika pambano kuu baina ya kristo na shetani
kuhusu tabia ya Mungu, sheria yake, na utawala wake juu ya ulimwengu. Ugomvi huu
ulianza mbinguni wakati kiumbe aliyeumbwa na kutunukiwa uhuru wa kuchagua, katika
kujiinua akawa shetani, mpinzani wa Mungu, na kupelekea sehemu ya Malaika kwenye uasi. Akaiagiza Roho ya uasi katika ulimwengu huu pale alipowaongoza Adamu na Hawa
kingia dhambini. Dhambi hii ya mwanadamu ilileta matokeo ya upotoshaji ya sura ya
Mungukatika wanadamu, Uvurugaji wa ulimwengu ulioumbwa, na mwishowe kuteketea
wakati wa gharika iliyokumba ulimwengu wote. Ukitazamwa na viumbe wote ulimwengu
huu ukawa uwanja wa vita ya ulimwengu, ambao kutokana nao Mungu wa upendo
hatimaye akathibitika kuwa mwenye haki. Katika kuwasaidia watu wake katika pambano
hili, kristo anamtuma Roho Mtakatifu na malaika watiifu kuongoza, kulinda, na
kutegemeza katika njia ya wokovu. (Ufu 12:4-9, Isa 14:12-14, Eze 28:12-18, War 1:19-32,
5:12-21, 8:19-22, 1Wakor 4:9, Waeb 1:14)
9.Maisha, Mauti na Ufufuo wa kristo
Katika maisha ya kristo ya utii mtakatifu kwa mapenzi ya Mungu, mateso yake, mauti na
ufufuo, Mungu alitoa njia pekee ya kafara kwa ajili ya dhambi ya mwanadamu, ili kwamba
wale ambao kwa imani wanapokea upatanisho huu waweza kuwa na uzima wa milele, na
ulimwengu wote uweze kuelewa vizuri upendo mtakatifu usio na kikomo wa muumba.
Kafara hii kamilifu huthibitisha haki ya sheria ya mungu na fadhili za tabia yake, kwa
sababu hufanya vyote viwili kuhukumu dhambi zetu na kutupatia msamaha. Kifo cha kristo
ni cha badala na cha kulipia, kupatanisha na chenye kubadilisha. Ufufuo wa Yesu kristo
hutangaza ushindi wa Mungu dhidi ya nguvu za uovu, na kwa wale wanaopokea kafara
huakikisha ushindi wao wa mwisho dhidi ya dhambi na mauti. Kinatangaza ukuu wa Yesu
Kristo, ambaye mbele zake kila goti mbinguni na duniani litapigwa.(Yoh3:16, Isa13:1,
1Petr 2:21, 22,1Wakor 15:3, 4, 20-22, 2Wakor 5:14, 19-21. War1:4, 3:25, 4:25, 8:3, 4,
Wafil2:6-11)
10.Uzoefu wa Wokovu
Katika upendo usio na mwisho na rehema zake Mungu alimfanya Kristo, asiyejua dhamdi
kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili kwambakatika yeye tuweze kufanywa haki ya Mungu.
Tukiongozwa na Roho mtakatifu tunatambua hitaji letu, tunakili hali yetu ya kuwa wenye
dhambi, tunatubu maasi yetu, na kuonyesha imani katika Yesu kama Bwana na Kristo,
kama mbadala na kielelezo. Imani hii inayopokea wokovu huja kupitia katika uwezo wa
kimbingu wan a ni karama ya neema ya Mungu. Kupitia kwa kristo tunahesabiwa haki,
tunafanywa kuwa wana wa binti za Mungu, na kukomesabiwa haki kutoka katika hali ya
kuwa chini ya dhambi. Kupitia kwa Roho tunazaliwa upyana kutakaswa, Roho hufanywa
upya nia zetu, huandika sheria ya Mungu ya upendo katika mioyo yetu, na tunapewa uwezo
wa kuishi maisha matakatifu. Tukikaa ndani yake tunakuwa washiriki wa asili ya uungu na
tuna hakika ya wokovu sasa na katika hukumu. (2Wakor 5:17-21, Yoh3:16, Wag1: 4, 4:4-
7, Tito3:3-7, Yoh16:8, Wag3:13,14. 1Petr 2:21,22. Warumi10:17, 3:21-26, 8:14-17, 12:2.
Warumi8:1-4,5:6-10, 2Petr 1:3,4)
11.Kukua katika kristo
Kwa kifo chake msalabani Yesu alizishinda nguvu za uovu. Yeye aliyewatiisha pepo
wachafu wakati wa huduma yake hapa duniani amezivunja nguvu zao na kuthibitisha
mwisho wao ni uangamivu usioepukika. Ushindi wa Yesu utupatia ushindi dhidi ya nguvu
za uovu ambazo bado zinatafuta kututawala, tunapo tembea naye kwa amani, fyraha, na
uhakika wa upendo wake.Sasa Roho Mtakatifu anakaa ndani yetu na kututia nguvu.
Tukidumu kujikabidhi kwa Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yetu tunawekwa
huru kutoka katika mzigo wa matendo yetu yaliyopita. Hatuishi tena gizani, katika hofu ya
nguvu za uovu, ujinga, na katika kukosa maana kwa namna ya maisha yetu ya awali,. Katika
uhuru huu mpya ndani ya kristo, tumeitwa kukua katika kufanana na tabia yake, tukiongea
naye kila siku katika sala, na kujilisha neno lake kikamilifu, tukikusanyika pamoja kwa ajili
ya ibada, na kushiriki katika utume wa kanisa. Tukijitoa katika kuwahudumia kwa upendo
wale wanaotuzunguka na kuwashuhudia wokovu wake, kuwepo kwake nasi daima kwa njia
ya Roho hugeuza kila wasaa na kazi kuwa uzoefu wa kiroho. (Zab.1:1,2. 23:4, 77:11,12,
Kol1:13-14, 2:6, 14-15, Luka10:17-20, Efe5:19-20, 6:12-18, 1Theo 5:23, 2Petr 2:9, 3:18.
Fil3:7-14, Math20:25-28, Yoh20:21, Gal5:22-25, Rum8: 38-39, 1Yoh4:4, Ebr10
12.Kanisa
Kanisa ni jamii ya waumini wanaomkiri Yesu kristo kuwa bwana na mwokozi katika
mfululizo wa kufungamana na watu wa Mungu katika nyakati za agano la kale, tunaitwa
kutoka katika ulimwengu, na tunajiunga pamoja kwa ajili ya ibada, kwa ajili ya ushirika, kwa
ajili ya mafundisho katika neno, na kwa ajili ya maadhimisho ya meza ya bwana, kwa ajili ya
huduma kwa wanadamu wote, na kwa ajili ya tangazo la injili ulimwenguni kote, kanisa
linapata mamlaka yake kutoka kwa kristo, aliye neno lililofanyika mwili, na kutoka katika
maandiko, ambayo ndiyo neno lililoandikwa. Kanisa ni jamaa ya Mungu, waliofanywa nay
eye kuwa watoto wake, washiriki wake huishi katika misingi ya agano jipya. Kanisa ni mwili
wa Kristo, jamii ya weny imani ambayo kristo mwenyewe ndiye kichwa. Kanisa ni bibi arusi
ambaye kwa ajili yake kristo apate kulisafisha na kulitakasa.Wakati wa kurudi kwake kwa
ushindi, ataliwasilisha kwake mwenyewew kanisa lenye utukufu, waaminifu wa karne zote,
walionunuliwa kwa damu yake, lisilo na waa au kunyanzi, lakini takatifu na lisilo na
ila.(Mwa12:3, Mdo:7:38, Waef4:11-15, 3:8-11, Math28:19,20, 16:13-20, 18:18,
Waef19:22,23, 5:23-27, Wakol1:17-18).
13.Masalio na Utume Wake
Kanisa la ulimwengu lijumuisha wale wote ambao kwa kweli wanamwamini kristo, lakini
katika siku za mwisho, kipindi cha kuenea kwa ukengeufu, masalio wameitwa kuzishika
amri za Mungu na imani ya Yesu kristo. Masalio hawa hutangaza kuwadia kwa saa ya
hukumu, hutangaza wokovu kupitia kristo, na hupiga mbiu ya kukarinia kwa marejeo yake.
Tangazo hili huwakilishwa katika mfano wa malaika watatu wa ufunuo 14, juambatana na
kazi ya hukumu mbinguni na kuwa na matokeo ya kazi ya toba na matengenezo duniani.
Kila muumini anatakiwa kuwa na sehemu binafsi katika ushuhuda huu wa ulimwenguni
kote. (Ufu12:17, 14:6-12, 18:1-4, 2Wakor 5:10, Yuda3,14, 1Petro1:16-19, 3:10-14,
Ufu21:1-14)
14.Umoja katika Mwili wa Kristo
Kanisa ni mwili mmoja ulio na washiriki wengi, walioitwa kutoka katika taifa, kabila, lugha,
na watu. Katika kristo tu viumbe wapya, ubainishi wa rangi, tamaduni, elimu, na taifa, na tofauti kati ya tabaka ya juu nay a chini, tajiri na maskini, mwanaume na
mwanamke,havipaswi kuleta mgawanyiko miongoni mwetu.Sote tu sawa katika kristo,
ambaye kwa roho mmoja ametufunga katika ushirika mmoja pamoja nay eye na sisi
wenyewe kwa wenyewe, tunapaswa kutumika na kutumikiwa pasipo kupendelea au kusita.
Kupitia kwa Yesu kristo katika maandiko tunashiriki imani na tumaini moja, na tunawafikia
wote kwa ushuhuda mmoja. Umoja huu una chimbuko lake katika umoja wa Mungu
mmoja mwenye nafsi tatu, ambaye ametufanya sisi tu watoto wake.(War12:4,5,
1Wakor12:12-14, Math28:19,20, Zabr133:1, 2Wakor5:16,17, Mdo17:26,27, Waef4:14-16,
4:1-6, Yoh17:20-23)
15.Ubatizo
Kwa njia ya ubatizo tunakiri imani yetu katika kifo na ufufuo wa Yesu kristo, na
kushuhudia kufia kwetu dhambi na kusudi letu la kuenenda katika upya wa maisha. Hivyo
tunamkubali kristo kuwa Bwana na Mwokozi, tunakuwa watu wake, na tunapokelewa kama
washiriki wa kanisa lake. Ubatizo ni mfano wa muungano wetu na kristo, msamaha wa
dhambi zetu na kupokea kwetu Roho Mtakatifu. Ni kwa kuzamishwa najini na unategemea
uthibitisho wa imani katika yesu na ushindi wa toba ya dhambi. Unafuata mafunzo katika
maandiko matakatifu na ukubali wa mafundisho yake. (Warum6:1-6, Wakol2:12,13,
Mdo16:30-33, 22:16, 2:38,Math28:19-20)
16.Meza ya Bwana
Meza ya Bwana ni ushiriki katika mfano wa mwili na damu ya Yesu kama udhihirisho wa
imani katika yeye, Bwana na mwokozi wetu. Katika ushirika huu kristo anakuwepo
kukutana na kuwaimarisha watu wake. Kadri tunavyoshiriki, kwa furaha tunatangaza mauti
ya Bwana mpaka arudipo tena. Maandalizi kwa ajili ya meza ya Bwana hujumuisha kujihoji
nafsi, toba na ungamo. Bwana aliamua huduma ya kutawadhana miguu kumaanisha
kutakaswa upya, kuonyesha nia ya kutumiana wenyewe kwa wenyewe katika unyenyekevu
ufananao na wa kristo, na kuungana mioyo yetu katika upendo. Huduma ya Meza ya
Bwana wazi kwa waumini wote wakristo. (1Wakor10:16,17. 11:23-30, Math 26:17-30,
Ufu3:20, Yoh6:48-63, 13:1-17)
17.Karamu za Roho na Huduma
Mungu huwakirimia washiriki wote wa kanisa lake katika kila kizazi karama za kiroho
ambazo kila mshiriki atatumia katika huduma ya upendo kwa ajili ya mema ya kawaida ya
kanisa na wanadamu. Zikitolewa kwa wakala wa Roho Mtakatifu, ambaye humgawia kila
mshiriki kama apendavyo yeye, karama hizo hutoa uwezo wote na huduma zinazohitajiwa
na kanisa katika kuytekeleza shughuli zake zilizoamuriwa na Mungu. Kulingana na
maandiko huduma hizi hujumuisha huduma kama: Imani, uponyaji, unabii, mahubiri,
mafundisho, utawala, upatanisho, huruma, na huduma ya kujinyima na ufadhili kwa ajili ya
msaada na faraja kwa watu. Baadhi ya washiriki huitwa na mungu na kukirimiwa na Roho
kwa ajili ya shughuli zinazotambuliwa na kanisa katika uchungaji, uinjilisti, na utume, na
huduma za kufundisha zinahitajika hasa katika kuwapatia zana washiriki kwa ajili ya
huduma kulijenga kanisa hadi ukomavu wa kiroho, na kukuza umoja wa imani na maarifa
ya Mungu. Pale washiriki wanapozitumia karama hizi za kiroho kama mawakili waaminifu wa neema mbalimbali za Mungu, kanisa hulindwa dhidi ya mivuto miharibifu ya
mafundisho ya uwongo, na hukua kwa ukuaji unaotoka kwa Mungu, nakujengeka imara
katika imani na upendo.(Warumi12:4-8, 1Wakor12:9-11, 27,28. Waef4:8,11, Mdo6:1-7,
1Petr4:10-11)
18.Karama ya Unabii
Mojawapo ya karama za Roho Mtakatifu ni unabii, karama hii ni alama-kitambulisho cha
kanisa la masalio na ilidhihirishwa katika huduma ya Ellen G. White. Kama mjumbe wa
Bwana, maandishi yake ni chanzo kiendelezi na yenye mamlaka ya ukweli yanayolipatia
kanisa faraja, uongozi, mafundisho, na maonyo. Pia yanaweka wazi kuwa Biblia ndiyo
kanuni ambayo kwa hayo mafundisho yote na uzoefu lazima vipimwe. (Yoeli2:28,29,
Mdo2:14-21, Waeb1:1-3, Ufu12:17, 19:10)
19.Sheria ya Mungu
Kanuni kuu za sheria ya Mungu zimetiwa pamoja katika Amri kumi na mfano wake
ulidhihirishwa katika maisha ya kristo,. Nazo zinadhihirisha upendo wa Mungu, mapenzi
yake, na makusudi yake kuhusu mwenendo wa binadamu na mahusiano nazo ni sharti kwa
watu wote katika kila kizazi. Amri hizi ndiyo msingi wa agano la Mungu na watu wake na
kanuni katika hukumu ya Mungu. Kupitia uwakala wa Roho Mtakatifu zinasonda dhambi
na kuhamsha hisia za hitaji la mwokozi. Wokovu wote ni katika neema, na si kwa matendo,
lakini tunda lake ni utii wa amri kumi. Hutii huu hukuza tabia ya kikristo na huwa na
matokeo ya ustawi. Ni ushuhuda wa upendo wetu kwa Bwana na wajibu kwa ajili ya
wanadamu wenzetu. Utii wa imani udhihirisha uwezo wa kristokubadilisha maisha, na
hivyo huimarisha ushuhuda wa kristo. (Kut 20:1-17, Zab40:7,8 Math22:36-40 Kumb28:1-
14 Math5:17-20, War8:3,4 Zab 19:7-14)
20.Sabato
Muumbaji mkarimu, baada ya siku sita za uumbaji, alipumzika siku ya saba na kuanzisha
sabato kwa ajili ya watu wote kama kumbukumbu ya uumbaji. Amri ya nne ya sheria za
Mungu zisizobadilika inaagiza adhimisho la sabato hii ya siku ya saba kama siku ya
mapumziko, ibada, na huduma kulingana na mafundisho na uzoefu wa Yesu, Bwana wa
sabato. Sabato ni siku ya mawasiliano yenye furaha pamoja na Mungu na sisi kwa sisi. Ni
mfano wa ukombozi wetu katika kristo, ishara ya utakaso wetu, ishara ya utii wetu, na
mwonjo wa umilele wetu wa siku zijazo katika ufalme wa Mungu. Sabato na ishara ya daima
ya mungu ya agano la milele la Mungu kati yake na watu wake. Utunzaji wa furaha wa
wakati huu mtakatifu toka jioni hadi jioni, jua kuchwa hadi jua kuchwa, ni adhimishola
matendoya Mungu ya uumbaji na ukombozi. (Mwa 2:1-3, Kut20:8-11, Luka4:16, Isay56:5-
6, 58:13-14, Math12:1-12, Ezek20:12-20, Kumb5:12-15, Wal23:32, Marko1:32).
21.Uwakili
Sisi tu mawakili wa Mungu, tuliokabidhiwa nay eye wakati na fursa, uwezo na mali, na
mibaraka ya dunia na raslikamali zake. Tunawajibika kwake kwa matumizi yake sahihi.
Tunakiri umilikaji wa Mungu kwa huduma ya uaminifu kwake na kwa wanadamu wenzetu, na kwa kurudisha Dhaka na kutoa sadaka kwa ajili ya utangazaji wa injili yake na kwa
utegemezaji na ukuaji wa kanisa lake. Uwakili ni fursa iliyotolewa kwetu na Mungu kwa ajili
ya malezi katika upendo na ushindi dhidi yao choyo na tama. Wakili kufurahia mibaraka
inayowajia wengine kama matokeo ya uaminifu wake.(Mwa1:26-28, 2:15, 1Nyak29:14,
Hagai 1:3-11, Malak3:8-12, 1Wakor 9:9-14, Math23:23, 2Wakor8:1-15 Warumi15:26-27.).
22. Mwenendo wa kikristo
Tumeitwa kuwa watauwa wanaofikiri, kujisikia, na kutenda kutenda kulingana na kanuni za
mbinguni. Ili Roho aumba ndani upya ndini yetu tabia ya Bwana wetu tunajihusisha tu
katika mambo yale ambayo yatazaa katika maisha yetu usafi unaofanana na kristo, afya, na
furaha katika maisha yetu. Hii inamaanisha kwamba maraha na maburudisho yetu
yanapaswa kufikia viwango vikuu vya maonji na uzuri wa kikristo. Huku tukitambua tofauti
za kitamaduni, mavazi yetu yanapaswa yawe ya kawaida, si ya anasa, na safi, yanayostahili
wale ambao uzuri wao wa asili yake si mapambo ya nje, bali asili yake ni mapambo
yasiyoharibika, yenye roho ya upole na utulivu. Pia inamaanisha kwamba kwa kuwa miili
yetu ni maekalu ya Roho mtakatifu, tunapaswa kuitunza kwa akili. Pamoja na mazoezi
tosha na mapumziko, yatupasa kuchagua lishe yenye afya sana kadiri inavyowezekana na
kuepuka vyakula visivyo najisi, vilivyotajwa katika maandiko matakatifu. Kwa vile vinywaji
vya vileo, tumbaku na matumizi mabaya ya madawa hudhuru miili yetu, yatupasa
kuepukana nayo pia. Badala yake yatupasa kujishughulisha na chochote kile kitakacholeta
mawazo yetu na miili yetu yawe katika nidhamu ya kistro, ambaye hutamani uzima wetu,
furaha, na wema. (Warumi 12:1-2, 1Yoh 2:6, Waef5:1;21, Wafil 4:8, 2Wakor 10:5, 6:14,
7:1, 1Pet3:1-4, Walawi 11:1-47, 3Yoh. 2)
23. Ndoa na Familia
Ndoa ilianzishwa Edeni na Mungu na ikasibitishwa na Yesu kuwa muungano wa maisha
yote kati ya mwanaume na mwanamke katika wenzi wenye upendo. Kwa mkristo kifungo
cha ndoa ni kwa Mungu na pia kwa mwenzi, na kishirikiwe tu na wenzi wenye imani moja.
Upendo wa hiari, heshma, staha, na uwajibikaji ndizo fito za {kujenga}uhusiano huu,
ambao utaakisi upendo, utakatifu, ukaribu, uthabiti wa uhusiano kati ya kristo na kanisa
lake. Kuhusu talaka, Yesu alifundisha kwamba mtu anayemwacha mwenza, isipokuwa kwa
sababu ya uasherati, na akaoa {au kuolewa} na mwingine azini. Ingawa baadhi ya
mahusiano ya kifamilia huenda yakashindwa kufikia lengo, wenzi katika ndoa ambazo
wamejitoa kikamilifu kila mmoja kwa mwenzake katika kristo wanaweza kufaulu kufikilia
katika umoja wenye upendo kupitia uongozi wa Roho na malezi ya kanisa. Mungu hubariki
familia na anakusaidia kwamba washirika wake watasaidiana wao kwa wao kufikia upevu
kamili. Wazazi wawalee watoto wao katika kumpendeza na kumtii Bwana. Kwa kielelezo
chao na maneno yao wawafundishe kwamba kristo ni mtiishaji mwenye upendo, daima
mpole na mwenye kujali, anayetaka wawe kiungo katika mwili wake, familia ya Mungu.
Kukuza ukaribu wa mahusiano wa kifamilia ni moja wapo ya alama{ya kujulisha}ujumbe wa
mwisho wa injil. (Mwa 2:18-25, Math 19:3-9, Yoh 2:1-11, 2Wakor6:14, Waef5:21-33, Luka
16:18, 1Wakor7:10-11, Kut20:12, Kumb6:5-9, Mith22:6, Mal 4:5-6)
24. Huduma ya Kristo katika Hekalu la Mbinguni
Kuna hekalu mbinguni, hema la kweli lililosimamishwa na Bwana na siyo mwanadamu.
Ndani yake kristo anahudumu kwa niaba yetu, akiwezesha kupatikana kwa ajili ya waumini
fanaka za kafara yake ya upatanisho iliyotolewa mara moja msalabani kwa ajili ya wote.
Alizinduliwa kuwa kuhani wetu mkuu na akaanza huduma yake ya uombezi wakati wa
kupaa kwake mbinguni. Mnamo mwaka 1884, mwishoni mwa kipindi cha unabii wa siku
2300, aliingia katika awamu ya pili nay a mwisho katika huduma yake ya upatanisho. Ni
kazi ya hukumu ya upelelezi ambaya ni sehemu ya mwisho ambayo hatimaye itakomesha
dhambi yote, iliyokuwa mfano wa kutakaswa kwa hekalu la kale la waebrania katika siku ya
upatanisho. Katika huduma hiyo kielelezo hekalu lilitakaswa kwa damu ya wanyama wa
kafara, likini mambo ya mbinguni hutakaswa kwa kafara kamilifu ya damu ya Yesu.
Hukumu ya upelelezi kufunua kwa viumbe wa mbinguni ni nani miongoni mwa wafu
wamelala katika kristo na hivyo, katika yeye wanahesabiwa kustahili kuwa na sehemu katika
ufunuo wa kwanza. Pia inadhihirisha zazi ni nani miongoni mwa walio hai wanakaa ndani
ya kristo, wakishika amri za Mungu na imani ya Yesu, na katika yeye, hivyo basi, wako
tayari kwa ajili ya kuhamasishwa kuingia katika ufalme wa milele. Hukumu hii huthibitisha
haki ya Mungu, katika kuwokoa wale wanaomwamini Yesu. Hutangaza kwamba wale
waliohudumu kuwa watiifu kwa Mungu watapokea ufalme. Hitimisho ya huduma hii ya
kristo itakuwa ndiyo mwisho wa kufunga mlango wa rehema ya mwanadamu kabla ya
marejeo ya Yesu. (Waebr 8:1-5, 4:14-16, 9:11-28, 10:19-22, 1:3, 2:16-17. Dan 7:9-27, 8:13-
14, 9:24-27. Hes 14:34. Ezekl 4:6 Ufu 14:6-7, 20:12, 14:12, 22:12. )
25. Kuja kwa Kristo mara ya pili
Kuja kwa kristo mara ya pili ndilo tumaini lenye baraka la kanisa, hitimisho kuu la injili.
Kuja kwa mwokozi kutakuwa halisi, binafsi, kutaonekana kwa dunia mzima. Atakaporudi
wenye haki waliokufa watafufuliwa na pamoja na wenye haki walio hai watavikwa utukufu
na kuchukuliwa kwenda mbinguni, lakini waovu watakufa. Kutimizwa karibu kabisa kwa
sehemu nyingi za unabii, pamoja na hakli ya sasa ya ulimwengu, huonyeshe kwamba kuja
kwa kristo ku karibu sana. Wakati wa tukio hilo hakukufunuliwa, na hivyo basi
tunahimizwa kuwa tayari kwa nyakati zote. .(Tito 2:13, Math 24, Mdo1:9-11, Math24:14,
Ufu1:7, 14:14-20, Math24:43-43, Wakor15:51-50, 1Wathes1:7, 4:13-18, 5:1-6, Marko 13,
Luka 21:2, Tim 3:1-5).
26. Mauti na Ufunuo
Mshahara wa dhambi ni mauti. Lakini Mungu, ambaye peke yakehapatwi na mauti,
atawapa uzima wa milelewaliokombolewa wake. Mpaka siku hiyo mauti ni hali ya
kutokuwa na fahamukwa watu wote. Wakati kristo, aliye uzima wetu, atakapotokea, wenye
haki waliofufuliwa na walio hai watafikwa utukufu na kunyakuliwa juu ili kumlaki Bwana
wao. Ufufuo wa pili ambao ni ufufuo wa waovu, utatokea miaka elfu moja baadaye.
(Warum 6:23,1Tim 6:15-16, Mhu 9:5-6, Zab 149:3-4, Yoh 11:11-14, 1Wakor 15:51-54,
1Wathes 4:13-17, Ufu 20:1-10)
.
27. Milenia {Miaka Elfu} na Mwisho wa Dhambi
Milenia ni miaka elfu moja ya utawala wa kristo pamoja na watakatifu wake mbinguni kati
ya ufufuo wa kwanza na pili. Wakati huo waovu waliokufa watahukumiwa, dunia itakuwa
ukiwa na utupu, bila wanadamu wakazi walio hai, lakini ikikaliwa na shetani na malaika
zake. Mwishowe kristo na watakatifu wake na Mji Mtakatifu watashuka kutoka Mbinguni.
Ndipo waovu waliokufa watafufuliwa, nao pamoja na shetani na malika zake watauzingira
mji, Lakini moto kutoka mbinguni utawateketeza ili kuitakasa dunia. Na hivyo ulimwengu
utakuwa huru bila dhambi na wenye dhambi milele. (Ufu 20, 1Wakor 6:2-3, Yer 4:23-26,
Ufu 21:1-5,Mal 4:1, Ezekl 28:18-19)
28. Dunia Mpya
Katika dunia mpya, ambamo haki hukaa,Mungu ataweka tayari makao ya milele
waliokombolewa na mazingira makamilifu kwa maisha ya milele, upendo, furaha na
kujifunza mbele zake. Kwa hapa Mungu mwenyewe atakaa pamoja na watu wake, na taabu
na mauti vitakuwa vimepita. Pambano kuu litakuwa limemalizika, na dhambi haitakuwepo
tena. Vitu vyote vyenye uhai na visivyo na uhai vitatangaza kwamba Mungu ni pendo, naye
atatawala milele. Amina. (2Pet 3:13, Isa 35, 65:17-25, Math 5:5, Ufu 21 :1-7, 22:1-5, 11:5).
 
Makahaba wengi tu kwenye biblia. Kuna visa huwezi kusoma kwa sauti mbele ya yeyote. Ona hawa wanangonoka na baba yao.

Mwanzo 19:
30 Lutu akapanda kutoka Soari akakaa mlimani, na binti zake wawili pamoja naye, kwa sababu aliogopa kukaa katika Soari. Akakaa katika pango, yeye na binti zake wawili.
31 Yule mkubwa akamwambia mdogo, Baba yetu ni mzee, wala hakuna mtu mume katika nchi atuingilie kama ilivyo desturi ya dunia yote.
32 Haya, na tumnyweshe baba yetu mvinyo, tukalale naye, ili tumhifadhie baba yetu uzao.
33 Wakamnywesha baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka huyo mkubwa akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka.
34 Ikawa siku ya pili, mkubwa akamwambia mdogo, Tazama, nimelala jana na baba yangu, tumnyweshe mvinyo tena usiku huu, ukaingie ukalale naye.
35 Wakamnywesha tena baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka mdogo akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka.
36 Basi hao binti wote wawili wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao.
37 Yule mkubwa akazaa mwana, akamwita jina lake Moabu; huyo ndiye baba wa Wamoabi, hata leo.
38 Na yule mdogo naye akazaa mwana akamwita jina lake Benami; huyo ndiye baba wa Waamoni hata leo.
 

Naomba ufafanuzi hapo namba 24. Wasabato mlifikiaje huo mwaka 1884? Ni mahesabu ya mwanzilishi wenu Milller au ni Ellen G. White aliyekokotoa na kufikia huo mwaka?

Mafundisho yote katika namba 24 hayana misingi ya Kibiblia na yamebakia kuwa doa mojawapo kuu katika Usabato. Yesu Alimaliza kazi yote msalabani na hakuna cha hukumu ya upelelezi wala nini. Watheolojia wengi wanaamini kuwa, baada ya kuachana na mafundisho mengi ya Miller (mf. Kiherehere cha kuweka tarehe na mwaka wa kurudi kwa Yesu kulingana na mahesabu katika vitabu vua Daniel, Ufunuo; na kwingineko), Usabato sasa umefanikiwa kuachana na makandokando mengi ya waanzilishi wake na kuwa dhehebu la kweli linalofuata misingi ya Biblia. Doa kubwa linalotajwa sana ni hicho kipengele # 24.

Halafu nanyi mnakubaliana na Jehovah's Witness kuwa mbinguni wataenda watu 144, 000 tu na wengine tutaishi hapa hapa duniani milele na milele baada ya dunia kutakaswa?
 
Faiza. Stori kama hizi hazimo kwenye Korani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…