Mfahamu kahaba mkuu wa Ufunuo 17

Mfahamu kahaba mkuu wa Ufunuo 17

Biblia wataisoma saa ngapi?mafundisho kama ni j2 somo moja linafundishwa dunia nzima,kama leo wanasoma kifungu cha biblia kimoja,kifungu hicho hicho watakachosoma hapa tz,hivo hivo watakisoma waliopo kenya,vietnam,marekani,na viongozi wa dini wajanja hawataki wafuasi wajue ukweli wa kuichambua biblia.wakianza kuhoji watajua jinsi wanavodanganywa.
VICARIUS FILII DEI=666 is papacy symbol

Huo ndo utaratibu unaowatia utoko. Mtahenya na kanisa katoliki. Tena kwenye mitandao ndo mtapumulia masikio!
 
Asante sana mkuu. Kwa Wasabato hata nyie Walutheran ni wafuasi wa ajenti wa Shetani tu (Papa). Mkitaka kuwa watakatifu badilisheni siku ya kusali na anzeni kusali Jumamosi. Vinginevyo, kulingana na Wasabato, mbingu mtaishia kuisikia tu. Wao peke yao ndo watakwenda mbinguni!
dc36edaf8164b3fa939187123437874f.jpg
Yaan hawa jamaa Wasabato huwa sitaki hata kuwasikiliza, nulishawapuuza kabsa
 
i think dini zote hakuna cha usabato wala ukatoliki zimeletwa kwa madhumuni maalumu hasa huku kwetu Africa kutunonya na kuiba maliasili zetu bila hivo hizi dini tusingezijua , Itakuwa ni uwenda wazimu kujiita msabato au mkatoliki au mluteri kama huna upendo,mwizi mzinzi mchonganishi, majivuno n.k, Na pia tufikie hatua tuheshimu imani za watu wengine.Wote hatuwezi kuabudu sawa kama ambavyo hatuishi sawa kila mtu na style yake ya maisha, Watu waliostaarabika wanadiscuss issues but inaonekana sisi tunadiscuss events ,historia sijui ukatoliki uliua sijui uchoma vitabu for what? je kama ulifanya hivo kwa sasa unafanya tena? je ukatoliki unakuzuia kuabudu kwa jinsi unavyotaka? Dini zikitumika vizuri ni chanzo cha maendeleo zikitumika vibaya ni chanzo cha umaskini na migogoro
 
Hizi tofauti za madhehebu zinachanganya kiasi cha kushindwa kujua ni zipi sifa za mkristo. Kwa ukubwa wa tofauti ya haya madhehebu haiwezekani wote wakawa ni wakristo.

Ni yapi ya kumfanya mtu awe mkristo?
Soma biblia Hamn kanisa mle chagua njia y'a kweli
 
Naomba nkujibu aaron uliyeandika post hii!
Nianze na hilo neno kahaba:kahaba kama ilivotumika katika biblia inaamanisha taifa la israel baada ya kuasi kwa Mungu,tizama kitabu cha Ezekieli 16,israeli anafamanishwa na kahaba na Mungu anaongelea vyte alivofanya kwake na namna alivojichanganya yy(kahaba)na miungu mingine(wanaume) wengine alipowekwa katila nchi ya ahadi.waume ndo hao waliomzunguka na sura hiyo inaelezea kwa uzuri zaid kuasi mpka adhabu ya kupelekwa uhamishoni..ushahidi mwingine wa huyo kahaba tizama katika ufunuo 17:18 inasema "na huyo mwanamke uliyemwona ni mji ule mkubwa wenye ufalme juu ya wafalme wa nchi"
Pia ukirudi ufunuo hyohyo 17:1 inasema "njoo nikuoneshe hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi ambaye wafalme wa nchi wamezini naye(wamemtoa kwny kumuambudu na kumtegemea Mungu pekee mpka kumchafua na kuabudu miungu yao)" .mstari wa 7 inasema "nitakuambia siri ya mwanamke huyu na mnyama huyu amchukuaye mwenye vile vichwa saba na zile pembe kumi"
Mnyama anaongelewa katika danieli kwa sehemu tatu tofauti;
Sehemu ya kwanza n danieli 2,sehemu ya pili ni danieli 7 na ufafanuzi wa yote ni danieli 9
Ss kama umesoma vzr huu ulkuani utabiri wa siku za mwsho ambapo una majuma 70 mpka kurud tena kwa masihi(Yesu Kristo) na danieli hyo sura ya tisa anaambiwa juma la 62 litakamilika masihi atakapouliwa(danieli 9:24).ss hyo hesabu yako ya 42 umepotosha pia nakushaur urud pia kusoma ufunuo 13:1-3 ilinganishe na ufunuo 17:9 na mstari wa 10 anakuambia hivyo vichwa saba ni wafalme saba na ufunuo 17:11 inasema huyu wa saba mwny jeraha alikuepo nae hayupo na ndiye wa nane. Mstari wa 13 unasema hawa wte wafalme wana shauri moja(labda nkudokeze tu wte shaur lao ni kuitawala israel au kuifuta kabsa katika uso wa dunia na hii ipo ufunuo17:15-18)
Hzo miezi 42 ni miaka mitatu na nusu ambapo katika daniel tisa unaambiwa juma la mwsho(miaka saba ya mwsho) ndicho kiama na miaka mitatu ya kwanza atatawala mnyama huyo(42) ya kwanza(ufunuo 13:5)
Niishie hapa kama bado huelewi na una hoja ilete nitakufafanulia zaid na hata habari za hao wafalme
 
Rudi haraka kwa aliyekutuma mwambie amekuingiza chaka. Daniel 2, 7 na kitabu cha ufunuo 13, 14 , 17 vyote huzungumzia utawala mmoja nao ni upapa. Mwanamke kiinabii ni kanisa. Kwa muktadha wa ufunuo 12 na ufunuo 17. Haya ni makanisa mawili tofauti. Moja ni kanisa la Mungu na linatii maagizo yake hufananishwa na bikra. Mwanamke wa ufunuo 17:5 ni kahaba kwa kuwa ameasi maagizo ya Mungu. Kwa muujibu wa mifano iliyopo, kanisa katoliki ndilo mwasisi wa kuasi amri za Mungu kwa kubadili sabato toka jumamosi na kuifanya jumapili ndio siku ya ibada, ubatizo wa kunyunyizia, ibada ya sanamu na umizimu yaani kuwaomba wafu. Kahaba wa ufunuo 17:5 ni Roman Catholic.ushahidi wa hili ni mwingi sana tuliishauweka humu.
 
Mbona mnaangaika huku mkijitutumua kwa majigambo na majivuno? Ingawa inawezekana wote hamujui zaidi au mnajua lakini mkionekana hamjui. Kwani ili ufike mbinguni unapaswa ushike bakora au panga na kuanza kumlazimisha mtu mwingine afuate njia ya mbinguni. Ukiona unatumia nguvu nyingi basi ujue haupo na roho msafi una kiburi na majivuno. Toa unachoelewa na wala usimwambie mwingine hajui maana hakuna anaejua zaidi wote ni vipofu wa kuongozwa na wanaojua kesho, uvumilivu, hekima na busara ni heri na bora zaidi kuliko mimi kung'ang'ania kutaka kumjua kahaba huku sijasafisha moyo wangu na mwili wangu itakua hopeless kabisa. Nyie acheni hizo habari kwa sababu je mnaamini kuwa baba zenu wa kiroho wanayajua mengi kuliko nyie? Kama mnaamini hayo je wao pekee ndio wataiona pepo kwa kuwa wanajua mengi kuliko nyie? Ni bora zaidi nikauliza nifanye nini ili kuuona ufalme wa mbigu kuliko kuuliza kahaba ni nani?
 
Mimi ni roman catholic
kwa mroma mwenzangu
atakayeweza kunielewesha, kiunagaubaga zile sanamu kanisani ni za nini? Kwanini maandiko yamepinga na still bado zipo? vp kwenye salama Maria kuna sehemu tunatamka mama wa Mungu je ni halali?. Ntaendelea kuuliza zaidi
Nb hayo maswali hasa la sanamu limenifanya niwe mgumu wa kwenda kanisani kabisa.
Kama umeshindwa si uungane na huyo mpendwa mleta mada mjukuu wa damu, wa bibi G.nyeupe.
 
Mbona mnaangaika huku mkijitutumua kwa majigambo na majivuno? Ingawa inawezekana wote hamujui zaidi au mnajua lakini mkionekana hamjui. Kwani ili ufike mbinguni unapaswa ushike bakora au panga na kuanza kumlazimisha mtu mwingine afuate njia ya mbinguni. Ukiona unatumia nguvu nyingi basi ujue haupo na roho msafi una kiburi na majivuno. Toa unachoelewa na wala usimwambie mwingine hajui maana hakuna anaejua zaidi wote ni vipofu wa kuongozwa na wanaojua kesho, uvumilivu, hekima na busara ni heri na bora zaidi kuliko mimi kung'ang'ania kutaka kumjua kahaba huku sijasafisha moyo wangu na mwili wangu itakua hopeless kabisa. Nyie acheni hizo habari kwa sababu je mnaamini kuwa baba zenu wa kiroho wanayajua mengi kuliko nyie? Kama mnaamini hayo je wao pekee ndio wataiona pepo kwa kuwa wanajua mengi kuliko nyie? Ni bora zaidi nikauliza nifanye nini ili kuuona ufalme wa mbigu kuliko kuuliza kahaba ni nani?
Ndugu mpendwa, ibada ya kweli kwa Mungu wa Mbinguni ndio itatupeleka mbinguni. Mtu awaye yote asikudanganye kuwa njia yeyote utakayoichagua itakufikisha mbuinguni. kahaba anayesemwa hapa ndiyo ibada ya uongo ambayo mwisho wake ni katika ziwa la moto. lazima tupaaze sauti kuwaonya watu. Isaya 58:1 "Piga kele usiache, paaza sauti yako kama tarumbeta, uwaonye watu makosa yao."
 
Rudi haraka kwa aliyekutuma mwambie amekuingiza chaka. Daniel 2, 7 na kitabu cha ufunuo 13, 14 , 17 vyote huzungumzia utawala mmoja nao ni upapa. Mwanamke kiinabii ni kanisa. Kwa muktadha wa ufunuo 12 na ufunuo 17. Haya ni makanisa mawili tofauti. Moja ni kanisa la Mungu na linatii maagizo yake hufananishwa na bikra. Mwanamke wa ufunuo 17:5 ni kahaba kwa kuwa ameasi maagizo ya Mungu. Kwa muujibu wa mifano iliyopo, kanisa katoliki ndilo mwasisi wa kuasi amri za Mungu kwa kubadili sabato toka jumamosi na kuifanya jumapili ndio siku ya ibada, ubatizo wa kunyunyizia, ibada ya sanamu na umizimu yaani kuwaomba wafu. Kahaba wa ufunuo 17:5 ni Roman Catholic.ushahidi wa hili ni mwingi sana tuliishauweka humu.
Unaweza kuonyesha ni lini upapa ulitawala dunia...upapa zaid ya kua wa eneo lile lile haujawah kutawala dunia au hata kuleta ramani ya empire ya papa? Labda nkupe tu kua upapa hautoki zaid ya nchi ya vatican na waumin wa katoliki tena wa Roma mana wale byzantine catholics wana mfumo wao?ufunuo 2,7,13 hazizungumzii tu utawala wa rumi ambao ww wauita wa papa unazungumzia tawala nyingine tatu pia.
 
Chimbuko la upapa ni utawala wa rumi ya kipagani. Baada ya kuona warumi wanaua wakristo lakini hawafanikiwi, ndiyo maana Constantino, mfalme wa kipagani wa kirumi pamoja na mama yake kwa hila wakajifanya wameongoka na kuukubali ukristo. Lakini alichokifanya ni kuleta ibada za kipagani kanisani pamoja na siku ya jua yaani "Sunday". Wakati huo mamlaka ya ya kidunia ilikuwa bado chini ya rumi. Ili kuongeza mvuto, warumi wa kiapagani wakaamua kumpa askofu mkuu wa kanisa la roma mamlaka ya kidini na kiserikali pia. hii ilitokea kwa mfame Justinian Mwaka 476 AD. Kwa hiyo kipindi hicho kanisa na dini vikaungana na kuwa chini ya Papa. Mwaka 538AD papa kwa kutumia kofia yake ya kidini na kiserikali alianzisha mateso na mauaji kwa wote walikataa kutii mafundisho yake ya uongo. hayo yaliendelea hadi mwaka 1798 ( miaka 1260 kamili iliyotajwa kwenye Daniel na Ufunuo) kipindi ambacho papa aliuawawa na mfame wa ufaransa Napoleon kwa kumtumia kamada wake berthia. Kwa hiyo Roma imekoma kutawala dunia mwaka huo 1798. Japo upapa ulikuja kuibuka tena mwaka 1920, kupitia Vatican ( jeraha la mauti lilipona kama Biblia ilivyosema) lakini hauna nguvu kama ile ya awali. New World Order inajaribu kurejesha nguvu ya upapa lakini hawatafanikiwa kwani huo ndio utakuwa mwisho. Soma Biblia upate maarifa.
 
Je unajua roman empire ilgawanyika mara mbili na kua eastern(byzantine) na western?unajua western ilyokua na makao makuu roma ilkufa mwaka 476AD na hii eastern iliyokua na makao makuu constaninople mji aliokua akikaa mfalme costantine ulkufa mwaka 1436AD na Kuwa chini ya Ottoman empire au hujui kisa cha constantinople kuitwa instambul ss?
Nikupe tu kdgo,unabii wa danieli wahusu nyakati za mwisho na yatakayoipata Yerusalem mji wa bwana(tizama danieli 9) anaambiwa kuna majuma 62 na juma la 70(miaka saba ya mwsho itagawanyika mara mbili ambapo mitatu ya mwsho itakua hyo ya mpinga kristo(miez 42)) hebu hata soma mathayo 24:15 wanafunz wanapomuulza siku za mwsho znakuaje na anaeleza ni mpaka hapo hlo chukizo la uharibifu(mpinga kristo) litakaposimama patakatfu yan hekaluni
Siendelei nione mana umeleta stori hujaleta raman na hta hlo jeraha unalosema lililoandikwa ktk ufunuo 13 hbu bas onesha huo upapa wa 1920 ulivotawala dunia mna haukuvuka mipaka yake nliyosema hapo juu...rud soma stori vzr ya wanyama
 
Hata chimbuko la upapa hulijui jaribu hata kugoogle bac ndugu hawakuleta ukristu kisa hawafanikiwi...mana back walkua na civil war wao kwa wao ndan
 
NAMBA 666 AU 616 ILIYOANDIKWA KWENYE UFU 13:18 HAIMHUSU PAPA ISIPOKUWA ELLEN GOULD WHITE
Imbeni pamoja nami ALLELUYA! Kwa nini? Kwa sababu Mungu amenitendea makuu. Amenisaidia kukitegua kitendawili cha karibu karne mbili sasa, yaani kitendawili cha namba 666. Kwa muda mrefu tangu enzi za akina ELLEN GOULD WHITE, yaani miaka ile ya 1846, namba 666 ya katika Ufu 13:18 imekuwa ikielekezwa kwa majungu na matusi kwa Baba Mtakatifu. Ndugu zanguni, tulikuwa tunazugwa tu. Kumbe, siri ni kwamba ilikuwa inamwelekea mwenyewe aliyekuwa anaelekeza mashambulizi na matusi kwa Baba Mtakatifu, yaani ELLEN GOULD WHITE.
Nina furaha kubwa sana. Nawaalikeni mfurahi pamoja nami. Binafsi, nilikuwa napata taabu sana kujaribu kufumbua kitendawili hicho. Lakini, wakati huo huo, nilikuwa najiuliza kwa nini mashambulizi kwa Baba Mtakatifu ni makali hivyo? Kumbe, sasa tumefumbuliwa. Yote yalikuwa ni mbinu ya kutupoteza watu “maboya” tusijue kwamba namba inamwelekea mwenyewe anayetukana. Kumbe, ilikuwa ni mbinu ile ile ya mwizi kupiga kelele za “Mwizi, mwizi, mwizi huyo!” kusudi watu wamfukuze mtu mwingine na siyo yeye mwenyewe.
Acheni niwakumbusheni mambo. Nadhani nyote mna habari na mashtaka maarufu sana dhidi ya Wakatoliki kwamba namba 666 au 616 inamhusu kiongozi wetu mkuu yaani Papa au Baba Mtakatifu na kwamba namba hiyo imeandikwa kwenye mavazi yake na kofia yake. Zaidi ya hapo kuna madai kwamba namba hii ipo pia katika kompyuta na satelite. Leo nataka niwafunulieni mambo yalivyo.

Hii ni Mada ya Lugha na Hesabu Kidogo
Vijana wangu msishtuke na kuhangaika. Mada hii itahusisha herufi za Kiebrania na Kigiriki lakini zitakuwa chache tu nanyi mtaelewa yote nitakayoandika kwani ni masuala rahisi kuyafuatilia. (Kwa bahati mbaya herufi za Kigiriki zinakataa humu). Papo hapo, kutakuwa na hesabu. Hata hizo hazitawahangaisheni kwani ni hesabu za kujumlisha tu. Leo kumbukeni pia hesabu za Shule ya Msingi tulipokuwa tunatumia tarakimu za Kilatini, kwa mfano, I = 1, V = 5, X= 10, L = 50, C= 100, D = 500 na M = 1000.
Ili tuelewane, nitaanza na historia, kishapo nitakwenda nje ya Biblia ilikohamishiwa namba 666.

Mama ni Historia
Hebu nianze na jibu fupi linalolingana na historia. Wayahudi hujumlisha thamani ya kitarakimu majina ya watu na maneno mbalimbali na kuzaa namba mbalimbali. Kuhesabu kwa namna hii huitwa gematria nako kumetumika katika Ufu 13:18 na kuzaa namba 666 au katika nakala zingine za Biblia namba 616. Swali kubwa ni je, namba hiyo inamhusu nani? Ukweli ni kwamba namba 666 au 616 haimhusu Papa au Baba Mtakatifu hata kidogo. Tena haikuandikwa katika mavazi ya Papa na wala haimo katika kompyuta ama satelite.
Ukweli, kibiblia na kihistoria, ni kwamba namba hiyo ilimhusu na bado inamhusu kiongozi wa dola ya Kirumi zamani zile, yaani Kaisari Nero. Basi, namba 666 au 616 ndiyo hesabu ya jina la Nero aliyekuwa akiwadhulumu Wakristo katika karne ya kwanza ya Ukristo. Hesabu hiyo inapatikana kwa kukokotoa kigematria maneno NERON KAISAR (kwa Kiebrania - נרון קסר) au NERO KAISAR (kwa Kiebrania - נרו קסר) na KAISAR THEOS (kwa Kigiriki).

Jibu refu: Hakuna mahali po pote katika Biblia ambapo msomaji ameombwa kutumia akili isipokuwa hapa. Kwa kuwa ili kuipata hesabu hii kulihitaji kupiga hesabu, wasomaji wote wa kifungu kile walialikwa kupiga hesabu, gematria. Ndipo imeandikwa “Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili na aihesabu hesabu” (Ufu 13:18). Kumbe, kinyume na matumizi ya akili, hapa ndipo mahala wasomaji kadha wa kadha wasipotumia akili yoyote katika kusoma isipokuwa majungu na usingiziaji.
Ndugu yangu, wapo watu chungu nzima wanaoeneza tafsiri kwamba namba 666 au 616 inamhusu Baba Mtakatifu na imeandikwa kwenye mavazi yake kama nilivyosema hapo juu (rejea Ufu 13:18, 15:2). Je, mafundisho hayo yana ukweli? Najijibu mwenyewe: si ya kweli.
Tusisahau, kitabu cha Ufunuo wa Yohane kina mazingira yake ya kihistoria ambayo ni muhimu katika kuielewa sura ya 13. Mazingira hayo ni ya historia ya Dola ya Kirumi. Wakristo walipokuwa wakidhulumiwa na dola hiyo, mwandishi wa kitabu cha Ufunuo alichukua kalamu na kuandika ili kuwaliwaza ndugu zake aliokuwa akiteseka pamoja nao (rejea Ufu 1:9). Basi, katika kuandika akatumia lugha ya mafumbo ili watesi wasifahamu wanayosemwa. Ndicho kisa, basi, joka kuu lenye pembe na kadhalika linamaanisha Dola ya Kirumi. Mkubwa wa dola hiyo naye akapewa jina la kupanga au jina la kifumbo kwa mtindo wa kucheza na namba za jina lake (gematria).
Ukitaka kupata picha kidogo ya haya, chukulia mfano wa vitabu vya marehemu Shaban Robert. Yeye aliandika mashairi mengi ya kuwatia watu hamasa wapiganie uhuru. Katika mashairi hayo, wananchi anawaita, mathalani, siafu na wakoloni nyoka. Hao siafu wanakazana kumdhuru nyoka. Aidha, kitabu chake cha Kusadikika ni kitabu cha fumbo kinachofumbia hali ya mambo katika hewa ya kikoloni. Kwa hakika wakoloni hawakuambulia lolote katika mashairi na fasihi ya Shaban Robert. Kinyume chao, wananchi walielewa mada husika na “kuwaacha kwenye mataa” wakoloni. Ndivyo inavyotokea shuleni, mwalimu mbaya kupangwa jina ambalo mwenyewe halijui hata kama litatajwa mbele yake.
Upangaji wa jina la mtu kwa kutumia hesabu ya herufi za jina lake mwenyewe ulikuwa mtindo maarufu wa marabi na ulijulikana kama gematria. Ufu 13:18, si mahali pa kwanza kutumia gematria hata namba kumi na nne ya vizazi vilivyotajwa katika Mt 1:17 ni gematria ya jina Daudi (דוד) kwani d + w + d ni 6 + 4 + 6 = 14. Sasa ni nani katika karne ya kwanza aliyekuwa adui wa Wakristo na jina lake kigematria lilizaa namba 666 au 616? Hili ndilo swali la kuulizana. Alikuwa KAISARI NERO.
Tukitafsiri Biblia kwa usahihi huu, mtesi wa walengwa wa kitabu, aliyekuwa akifumbiwa katika 13:18 kwa kuhesabu jina lake kigematria, hawezi kuwa mtu wa karne ya tano au ya ishirini na moja. Walengwa walikuwa ni Wakristo wa karne ya kwanza na adui yao alikuwa akiishi nao kwa wakati huo huo. Basi, nani alikuwa mtesi maarufu katika mazingira ya karne ya kwanza? Wakati ule alikuwa Kaisari Nero ama Kaisari fulani aliyejidai kuwa Mungu na huyo ndiye kigematria jina lake linazaa namba 666 au 616.
Basi, gematria ikitumika kwa konsonanti za Kiebrania: נרון קסר - NERON KAISAR (yaani Kaisari Neron) au kwa maneno ya Kigiriki: KAISAR THEOS (yaani Kaisari Mungu) tunapata pasipo kuzunguka zunguka namba 666 au 616. Tazama hesabu zenyewe zinavyofanyika. (נרון קסר) r s q n w r n = 200 + 60 + 100 + 50 + 6 + 200 + 50 = 666.
k a i s a r th e o s = 20 + 1 + 10 + 200 + 1 + 100 + 9 + 5 + 70 + 200 = 616.
Angalia vyema. Hii tafsiri ya ‘KAISAR THEOS’ yaani ‘Mungu Kaisari’ ndiyo inayorejewa kwenye Biblia zenye kuandika jumla ya namba 616. Lakini vile vile 616 iliweza kupatikana kwa kuondoa “n” ya mwisho kwenye jina נרון (n w r n) katika Kiebrania. Kwa Wakristo, namba 666 ilipomtaja Neron ilisema pia kwamba ni MPINGA KRISTO kwani alikuwa kinyume cha utimilifu. Kinambari, utimilifu ni namba 777. Kumbe, yeye Kaisari Nero ni upungufu kwani hesabu yake ni 666 ambayo ni 777 kutoa 111.
Basi, kwa kuzingatia mazingira ya kitabu cha Ufunuo namba 666 au 616 haiwezi kusimama kwa ajili ya jina lingine kama Baba Mtakatifu, Mtume Mohamed au Mussolini. Haya ni baadhi ya majina wanayolazimisha watu yafanye hesabu ya 666. Na, kwa hakika, namba hiyo haimo katika mavazi wala kofia (mitra) ya Baba Mtakatifu. Hakuna mtu yeyote anayeweza kuonesha vazi hilo au kofia hiyo kwa ushahidi. Kwani ni vazi gani au kofia ipi? Basi, kama tunautafuta uzima wa milele, aheri tuache majungu na uongo kama huu. Kama ni maandishi, ni mitra yake tu yenye herufi mbili A na W yaani alpha na omega (rejea Ufu 1:8,17).
Acha tuendelee. Wanaombambikizia Baba Mtakatifu namba 666 hudai kuikokotoa nambari hiyo katika majina matatu tofauti: jina la Kilatini VICARIUS FILII DEI (Kaimu wa Mwana wa Mungu), jina la Kigiriki LATEINOS (Mlatini) na jina la Kiebrania ROMIITH (רמיית - Mrumi). Majina hayo huhesabiwa na wanaombambikizia Baba Mtakatifu namba hiyo kama ifuatavyo:
VICARIUS FILII DEI = 5 + 1 + 100 + 0 + 0 + 1 + 5 + 0 + 0 + 1 + 50 + 1 + 1 + 500 + 0 + 1 = 666.
LATEINOS = 30 + 1 + 300 +5 + 10 + 50 + 70 + 200 = 666.
ROMIITH yaani th y y m w r = 400 + 10 + 10 + 40 + 6 + 200 = 666.
Ndugu zangu, kwa misingi halali ya kusoma Biblia hatuwezi kuyapokea majina haya bila kuyafanyia tahakiki ya kihistoria. Bila kurefusha mjadala, majina haya hayajapata kutumiwa na Baba Mtakatifu yeyote, katika historia ya Kanisa sembuse wakati wa karne ya kwanza Baada ya Kristo wakati ambao hata upapa wenyewe ulikuwa haujakua. Mapapa wa karne zile hawakuwa hatari kwa mtu yeyote. Na watu wasio hatari watapewaje majina ya kupanga na ya siri? Wale wasomaji wa kitabu cha Ufunuo wangelielewaje aya ngumu inayotaja kitu kisichojulikana kwa jina hilo? Wangelifanyaje gematria kwa kutumia majina wasiyoyajua?
Aya 13:18 ilizungumzia jina ambalo wasomaji walikuwa wakilijua kama jina la adui yao aliyekuwa akiwadhulumu na si majina ya ndoto au majungu ya karne ya 20 na 21 B.K. Zaidi ya hayo majina mengine yamelazimishwa kihesabu ili jumla ya kiherufi iwe 666. Kwa ushuhuda tazama U ilivyolazimishwa imaanishe tarakimu 5. Katika Kilatini 5 ni V na wala siyo U. Zaidi ya hayo, jina “MLATINI” kama lingelitumika wakati huo, wasomaji wangelielewa kuwataja wakoloni au askari wa kirumi ambao walikuwa wakitawala ulimwengu wa wakati ule.
Hali kadhalika, kama jina “MRUMI” lingelitumika wakati huo, wasomaji wangelielewa kuwataja wakoloni au askari wa kirumi ambao walikuwa wakitawala ulimwengu wa wakati ule. Kwa hoja hizi, majina hayo ya majungu ni ya tangu karne ya 16, Kanisa Katoliki lilipoanza kupingwa kwa ari mpya na uongozi wake kukataliwa.
Nadhani hadi hapa kila mwenye kutaka kujua anajua kwamba majina waliyobuni Wasabato hayatumiwi na Baba Mtakatifu yeyote. Na zaidi ya hayo ni majina ambayo mwandishi wa kitabu cha Ufunuo hakuwa hata na habari nayo katika karne ile ya kwanza B.K. kwa vile alivyokiandika kitabu chake kwa Kigiriki na wala si kwa Kiebrania au Kilatini. Kumbe, kwa kufanya hivyo Wasabato huwa wanainyonga historia na kukizungumzia kitabu cha Ufunuo nje ya muktadha wake wa kihistoria. Hili ni kosa la kusiganisha nyakati za kikalenda (kwa Kiingereza “anachronism”).
Basi, kwa heshima ya Maandiko Matakatifu, tutafsiri namba 666 au 616 kwa gematria asilia na tukomee hapo hapo. Tusiihamishe namba hiyo na kuwapachika watu wasio na hatia. Kufanya hivyo ni kujitowelesha majungu na ni dhambi isiyo na maana yo yote. Lakini, basi namba 666 imetolewa nje ya mazingira ya Biblia na ndipo ilipowekwa sasa. Nami nimefika hapo hapo.

Namba 666 Imehamishiwa Nje ya Biblia
Ni kituko lakini ndivyo ilivyo. Watu wengine hudai kwamba namba hiyo imeandikwa shingoni kwenye nguo za Papa. Huo ndio uongo na usingiziaji usio na aibu kwa sababu nguo hizo hakuna anayeweza kutuonesha wenziwe. Siku moja niliwahi kuambiwa na wainjilisti wawili kwamba namba 666 ipo kwenye bidhaa za siku hizi, yaani kwenye kifungashio, pale inapochorwa mistari mingi mifupi na mirefu na kuandikwa namba kwa chini, na kwa namna hiyo ipo pia kwenye satelite. Siku hiyo niliwakamata kutokujua nilipowadai wanioneshe mfano. Basi, wakaleta baadhi ya bidhaa za kisasa, wakaniambia niangalie ile mistari iliyochorwa katika kifungashio cha kila bidhaa. Hapo walionesha pia mistari miwili miwili inayojitokeza zaidi kwa chini (jambo ambalo si kweli kwa kila bidhaa). Basi, hapo ndipo walipodai kuna namba 666.
Kumbe, huu ulikuwa ujinga wao mkubwa. Ndugu yangu, mistari hiyo, ndiyo bei ya bidhaa hasa kwa zile zinazouzwa „“supermarket. Katika nchi zilizoendelea watu hawaandiki bei shilingi fulani au fulani wakabandika kwenye bidhaa. Badala yake ndiyo hiyo mistari, kadiri ilivyochorwa ndivyo mashine ya kupigia hesabu inavyotambua na kutofautisha bei za bidhaa ambazo mnunuzi amezifikisha kwenye “kaunta” ya kulipia manunuzi. Na tena bei hizo hazikuingizwa katika satelite; zilivyo nyingi hazihusishwi na satelite yoyote.
Basi, niliwaonya wainjilisti wale wasiwadanganye watu kwa kutumia ujinga wao wakati wenyewe pia hawajui mambo ya kisasa. Hatimaye, niliwaambia, kwa uongo wa namna ile, wao si wainjilisti kwani Injili ni Habari Njema ya ukombozi wetu uliotufikia kwa kifo na ufufuko wa Yesu Kristo na wala siyo namba 666 inayodaiwa kuandikwa kwenye nguo za Papa na kuingizwa kwenye satelite kwa njia ya michoro ya bidhaa za kisasa. Kwa kweli niliwaambia kwa kueneza uongo na kuwatia watu hofu kwa kuwatinga, hawakuwa mbali sana na moto wa milele kwa vile wanamtumikia Shetani aliye baba wa uongo. Hapo nikapata mwanya wa kuwaalika watubu kwa haraka. Lakini, badala ya kupokea mafundisho yangu walisema sina Roho Mtakatifu na kuondoka. Waliondoka na hawakurudi tena kwangu. Kumbe, niliwafuma katika kutokujua kwao, yaani ujinga wao. Samahani kwa simulizi hili; majadiliano yetu yaliacha kuwa ya Kikristo.

Safari Ndefu ya Kutegua Kitendawili cha Kale
Kwa vile madai ya kwamba namba 666 inamhusu Baba Mtakatifu yametutoa sote kutoka kwenye Biblia na kutupa kazi ya kumtafuta nani mwingine anaweza kuwa anatajwa na namba hiyo, nilichukua kalamu na kuanza kuchunguza maneno ya wanaotukana kama hayahusiki vile vile. Utafutaji wangu ulizaa matunda mwaka ule ule 1998. Nikategua kitendawili kwa kugundua kwamba kauli za Wasabato wenyewe zilikuwa ndiyo namba 666.

Nilifanyaje? Nilichukua kauli tatu: PONYA SIKU MUHIMU YA SABA (kwa Kiingereza CURE VITAL SEVENTH DAY, kwa Kilatini CURATUS VITALE SABBATA DIES) na WOKOVU, PONYA SIKU YA SABA (kwa Kiingereza SALVATION, CURE SEVENTH DAY, kwa Kilatini SALVUS, CURARE SABBATA DIES) na VUNJA, CHUKIA UPAPA (kwa Kiingereza DEAL AXE, VIE PAPACY). Nilistaajabu sana kuona ndiyo inakuja 666 ndipo mara moja nikaingiza ugunduzi wangu katika kitabu changu KISA CHA IMANI namba 1.

Ni kweli. Kauli mbiu za Wasabato ni namba hiyo hiyo 666. Angalia gematria inavyokwenda:
CURE VITAL SEVENTH DAY = 100 + 5 + 0 + 0 + 5 + 1+ 0 + 0 + 50 + 0 + 0 + 5 + 0 + 0 + 0 + 0 + 500 + 0 + 0 = 666
CURATUS VITALE SABBATA DIES = 100 + 5 + 0 + 0 + 0 + 5 + 0 + 5 + 1 + 0 + 0 + 50 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 500 + 1 + 0 + 0 = 666
SALVATION, CURE SEVENTH DAY = 0 + 0 + 50 + 5 + 0 + 0 + 1 + 0 + 0 + 100 + 5 + 0 + 0 + 0 + 0 + 5 + 0 + 0 + 0 + 0 + 500 + 0 + 0 = 666
SALVUS, CURARE SABBATA DIES = 0 + 0 + 50 + 5 + 5 + 0 + 100 + 5 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 500 + 1 + 0 + 0 = 666
DEAL AXE VIE PAPACY = 500 + 0 + 0 + 50 + 0 + 1 0 + 0 + 5 + 1 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 100 + 0 = 666

Kuendelea Kutafuta
Basi, kwa kuwa nilikuwa namtafuta nani mwingine anayesemwa na namba 666 au 616, nikagundua kumbe ni hao hao wanaotukana. Lakini, sikukomea hapo mwaka huu 2017 macho yangu yakasaidiwa kuona zaidi. Nilichukua jina la mwasisi wa matusi mwenyewe ELLEN GOULD WHITE ndipo nikashtuka kabisa kumbe ni namba 666. Kwa kisa hiki, leo nawaomba tuimbe alleluya pamoja.

ALLELUYA! KUMBE NAMBA 666 NI ELLEN GOULD WHITE MWENYEWE
Sasa nawapeni habari njema kabisa. Tusi la namba 666 limefumbua macho yangu kwa namna ya ajabu na sasa nawatangazia wote nilichokigundua ili kiwafumbue macho ninyi pia. Kifupi, nimefikishwa kwenye ugunduzi huo kwa kupitia tahadhari ya wahenga. Wao walisema, “Unapokula na kipofu, usimguse kipofu mkono!” Msidanganyike tena, namba 666 ni ELLEN GOULD WHITE mwenyewe.

Nawasimulieni. Kwa kuzidi kutukana, niliwatazama watukanaji nione kama matusi hayawahusu wenyewe. Nikagundua kumbe ndiyo hivyo hivyo. Kumbe, wakati mwingine heri utukanwe maana waweza kufunguliwa mlango kwa jambo jema fulani. Basi, natangaza kadamnasi kwamba tusi la namba 666 limekuwa tusi la neema na heri sana kwetu Wakatoliki, tulionyanyasika kwalo kwa muda mrefu. Linawahusu wanaotutukana hao hao. Kumbe, walikuwa wanapiga kelele za “Mwizi, mwizi!“ ili kutupoteza maboya tu. Wezi ni wenyewe.

Tuamke. Jamani, Bi Ellen Gould White alikuwa anapiga kelele na kutukana kusudi tusishughulike na jina lake. Wafuasi wake wakadakia mbinu hiyo hiyo. Kumbe, Wasabato hukazania namba 666 imwelekee Baba Mtakatifu kwa sababu walitaka tusijue kwamba namba 666 inamwelekea “nabii” wao ELLEN GOULD WHITE! Walitaka tukamsake sungura katika kichaka kingine. Kumbe, Ufu 13:18 inamtaja Bi Ellen White moja kwa moja kama mnyama ambaye jina lake ukilikokotoa linakuja moja kwa moja kwenye namba 666. Yaani linakuja 666 taslimu!
Je, unaniuliza kwa vipi? Ni hivi ifuatavyo. Ukiliandika jina la Bi ELLEN WHITE pamoja na jina la asili yake GOULD unakuja kwenye namba 666 juu ya alama. Nifuatilie vyema hapa kusudi tukokotoe tarakimu pamoja. Lakini, angalia vyema, jambo lile la kuhitajika hekima, linahusisha pia kuirudisha “W” ya WHITE kwenye uasilia wake yaani V maradufu (kwa Kiingereza “double v”). Kwa taarifa yako, tangu kale “W” ni “V” mbili na ni kwa sababu ya asili hiyo Wajerumani huitamka “W” kama “V”. Umeshanielewa uzuri? Kama umeshanielewa, sasa tazama “gematria“ inavyokubali:
E L L E N G O U L D W H I T E
0+ 50 + 50 + 0 + 0 + 0 + 0 + 5 + 50 + 500+ 10+0+1+0+0 = 666

Je, unaona jinsi jina la Bi Ellen White linavyokubali kama jina la mnyama yule? Yaani sawa sawa pasipo kuacha mashaka yoyote. Kinyume chake, jiulize ni Baba Mtakatifu gani mwenye jina kama hilo? Maskini, Wasabato walisahau jambo hili la kimahesabu! Lakini nadhani wanalifahamu na ndiyo maana hufanya juhudi kubwa kulikoneshea tusi la namba 666 kwa Baba Mtakatifu. Ni janja yao lakini sasa ipo hadharani.
Narudia. Wanachofanya Wasabato ni mbinu ya kawaida tu, yaani kwamba ukitaka watu wasikuangalie wewe elekeza umakini wao kwa mtu mwingine au kitu tofauti. Ndipo, badala ya watu kuelekeza umakini kwenye jina “ELLEN GOULD WHITE” huzugwa waelekeze kwenye majina ya kubuni ya “VICARIUS FILII DEI”, “LATEINOS” na “ROMIITH”, majina yasiyo na maana yoyote kihistoria na muktadha wa kitabu cha Ufunuo.
Je, umeona eh! Kumbe, mambo yako kwenye majina “ELLEN GOULD WHITE”. Namba 666 inakubali taslimu kabisa. Chukua hii!

Hatima
Naona imetosha, nanyi, bila shaka, mnaniambia kwa Kiingereza “Stop, it is enough and clear!” kwa maana ya “Acha inatosha na imeeleweka!” Alamsiki!

Pd Titus Amigu
 
Back
Top Bottom