Mfahamu kahaba mkuu wa Ufunuo 17

Mfahamu kahaba mkuu wa Ufunuo 17

NAMBA 666 AU 616 ILIYOANDIKWA KWENYE UFU 13:18 HAIMHUSU PAPA ISIPOKUWA ELLEN GOULD WHITE
Imbeni pamoja nami ALLELUYA! Kwa nini? Kwa sababu Mungu amenitendea makuu. Amenisaidia kukitegua kitendawili cha karibu karne mbili sasa, yaani kitendawili cha namba 666. Kwa muda mrefu tangu enzi za akina ELLEN GOULD WHITE, yaani miaka ile ya 1846, namba 666 ya katika Ufu 13:18 imekuwa ikielekezwa kwa majungu na matusi kwa Baba Mtakatifu. Ndugu zanguni, tulikuwa tunazugwa tu. Kumbe, siri ni kwamba ilikuwa inamwelekea mwenyewe aliyekuwa anaelekeza mashambulizi na matusi kwa Baba Mtakatifu, yaani ELLEN GOULD WHITE.
Nina furaha kubwa sana. Nawaalikeni mfurahi pamoja nami. Binafsi, nilikuwa napata taabu sana kujaribu kufumbua kitendawili hicho. Lakini, wakati huo huo, nilikuwa najiuliza kwa nini mashambulizi kwa Baba Mtakatifu ni makali hivyo? Kumbe, sasa tumefumbuliwa. Yote yalikuwa ni mbinu ya kutupoteza watu “maboya” tusijue kwamba namba inamwelekea mwenyewe anayetukana. Kumbe, ilikuwa ni mbinu ile ile ya mwizi kupiga kelele za “Mwizi, mwizi, mwizi huyo!” kusudi watu wamfukuze mtu mwingine na siyo yeye mwenyewe.
Acheni niwakumbusheni mambo. Nadhani nyote mna habari na mashtaka maarufu sana dhidi ya Wakatoliki kwamba namba 666 au 616 inamhusu kiongozi wetu mkuu yaani Papa au Baba Mtakatifu na kwamba namba hiyo imeandikwa kwenye mavazi yake na kofia yake. Zaidi ya hapo kuna madai kwamba namba hii ipo pia katika kompyuta na satelite. Leo nataka niwafunulieni mambo yalivyo.

Hii ni Mada ya Lugha na Hesabu Kidogo
Vijana wangu msishtuke na kuhangaika. Mada hii itahusisha herufi za Kiebrania na Kigiriki lakini zitakuwa chache tu nanyi mtaelewa yote nitakayoandika kwani ni masuala rahisi kuyafuatilia. (Kwa bahati mbaya herufi za Kigiriki zinakataa humu). Papo hapo, kutakuwa na hesabu. Hata hizo hazitawahangaisheni kwani ni hesabu za kujumlisha tu. Leo kumbukeni pia hesabu za Shule ya Msingi tulipokuwa tunatumia tarakimu za Kilatini, kwa mfano, I = 1, V = 5, X= 10, L = 50, C= 100, D = 500 na M = 1000.
Ili tuelewane, nitaanza na historia, kishapo nitakwenda nje ya Biblia ilikohamishiwa namba 666.

Mama ni Historia
Hebu nianze na jibu fupi linalolingana na historia. Wayahudi hujumlisha thamani ya kitarakimu majina ya watu na maneno mbalimbali na kuzaa namba mbalimbali. Kuhesabu kwa namna hii huitwa gematria nako kumetumika katika Ufu 13:18 na kuzaa namba 666 au katika nakala zingine za Biblia namba 616. Swali kubwa ni je, namba hiyo inamhusu nani? Ukweli ni kwamba namba 666 au 616 haimhusu Papa au Baba Mtakatifu hata kidogo. Tena haikuandikwa katika mavazi ya Papa na wala haimo katika kompyuta ama satelite.
Ukweli, kibiblia na kihistoria, ni kwamba namba hiyo ilimhusu na bado inamhusu kiongozi wa dola ya Kirumi zamani zile, yaani Kaisari Nero. Basi, namba 666 au 616 ndiyo hesabu ya jina la Nero aliyekuwa akiwadhulumu Wakristo katika karne ya kwanza ya Ukristo. Hesabu hiyo inapatikana kwa kukokotoa kigematria maneno NERON KAISAR (kwa Kiebrania - נרון קסר) au NERO KAISAR (kwa Kiebrania - נרו קסר) na KAISAR THEOS (kwa Kigiriki).

Jibu refu: Hakuna mahali po pote katika Biblia ambapo msomaji ameombwa kutumia akili isipokuwa hapa. Kwa kuwa ili kuipata hesabu hii kulihitaji kupiga hesabu, wasomaji wote wa kifungu kile walialikwa kupiga hesabu, gematria. Ndipo imeandikwa “Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili na aihesabu hesabu” (Ufu 13:18). Kumbe, kinyume na matumizi ya akili, hapa ndipo mahala wasomaji kadha wa kadha wasipotumia akili yoyote katika kusoma isipokuwa majungu na usingiziaji.
Ndugu yangu, wapo watu chungu nzima wanaoeneza tafsiri kwamba namba 666 au 616 inamhusu Baba Mtakatifu na imeandikwa kwenye mavazi yake kama nilivyosema hapo juu (rejea Ufu 13:18, 15:2). Je, mafundisho hayo yana ukweli? Najijibu mwenyewe: si ya kweli.
Tusisahau, kitabu cha Ufunuo wa Yohane kina mazingira yake ya kihistoria ambayo ni muhimu katika kuielewa sura ya 13. Mazingira hayo ni ya historia ya Dola ya Kirumi. Wakristo walipokuwa wakidhulumiwa na dola hiyo, mwandishi wa kitabu cha Ufunuo alichukua kalamu na kuandika ili kuwaliwaza ndugu zake aliokuwa akiteseka pamoja nao (rejea Ufu 1:9). Basi, katika kuandika akatumia lugha ya mafumbo ili watesi wasifahamu wanayosemwa. Ndicho kisa, basi, joka kuu lenye pembe na kadhalika linamaanisha Dola ya Kirumi. Mkubwa wa dola hiyo naye akapewa jina la kupanga au jina la kifumbo kwa mtindo wa kucheza na namba za jina lake (gematria).
Ukitaka kupata picha kidogo ya haya, chukulia mfano wa vitabu vya marehemu Shaban Robert. Yeye aliandika mashairi mengi ya kuwatia watu hamasa wapiganie uhuru. Katika mashairi hayo, wananchi anawaita, mathalani, siafu na wakoloni nyoka. Hao siafu wanakazana kumdhuru nyoka. Aidha, kitabu chake cha Kusadikika ni kitabu cha fumbo kinachofumbia hali ya mambo katika hewa ya kikoloni. Kwa hakika wakoloni hawakuambulia lolote katika mashairi na fasihi ya Shaban Robert. Kinyume chao, wananchi walielewa mada husika na “kuwaacha kwenye mataa” wakoloni. Ndivyo inavyotokea shuleni, mwalimu mbaya kupangwa jina ambalo mwenyewe halijui hata kama litatajwa mbele yake.
Upangaji wa jina la mtu kwa kutumia hesabu ya herufi za jina lake mwenyewe ulikuwa mtindo maarufu wa marabi na ulijulikana kama gematria. Ufu 13:18, si mahali pa kwanza kutumia gematria hata namba kumi na nne ya vizazi vilivyotajwa katika Mt 1:17 ni gematria ya jina Daudi (דוד) kwani d + w + d ni 6 + 4 + 6 = 14. Sasa ni nani katika karne ya kwanza aliyekuwa adui wa Wakristo na jina lake kigematria lilizaa namba 666 au 616? Hili ndilo swali la kuulizana. Alikuwa KAISARI NERO.
Tukitafsiri Biblia kwa usahihi huu, mtesi wa walengwa wa kitabu, aliyekuwa akifumbiwa katika 13:18 kwa kuhesabu jina lake kigematria, hawezi kuwa mtu wa karne ya tano au ya ishirini na moja. Walengwa walikuwa ni Wakristo wa karne ya kwanza na adui yao alikuwa akiishi nao kwa wakati huo huo. Basi, nani alikuwa mtesi maarufu katika mazingira ya karne ya kwanza? Wakati ule alikuwa Kaisari Nero ama Kaisari fulani aliyejidai kuwa Mungu na huyo ndiye kigematria jina lake linazaa namba 666 au 616.
Basi, gematria ikitumika kwa konsonanti za Kiebrania: נרון קסר - NERON KAISAR (yaani Kaisari Neron) au kwa maneno ya Kigiriki: KAISAR THEOS (yaani Kaisari Mungu) tunapata pasipo kuzunguka zunguka namba 666 au 616. Tazama hesabu zenyewe zinavyofanyika. (נרון קסר) r s q n w r n = 200 + 60 + 100 + 50 + 6 + 200 + 50 = 666.
k a i s a r th e o s = 20 + 1 + 10 + 200 + 1 + 100 + 9 + 5 + 70 + 200 = 616.
Angalia vyema. Hii tafsiri ya ‘KAISAR THEOS’ yaani ‘Mungu Kaisari’ ndiyo inayorejewa kwenye Biblia zenye kuandika jumla ya namba 616. Lakini vile vile 616 iliweza kupatikana kwa kuondoa “n” ya mwisho kwenye jina נרון (n w r n) katika Kiebrania. Kwa Wakristo, namba 666 ilipomtaja Neron ilisema pia kwamba ni MPINGA KRISTO kwani alikuwa kinyume cha utimilifu. Kinambari, utimilifu ni namba 777. Kumbe, yeye Kaisari Nero ni upungufu kwani hesabu yake ni 666 ambayo ni 777 kutoa 111.
Basi, kwa kuzingatia mazingira ya kitabu cha Ufunuo namba 666 au 616 haiwezi kusimama kwa ajili ya jina lingine kama Baba Mtakatifu, Mtume Mohamed au Mussolini. Haya ni baadhi ya majina wanayolazimisha watu yafanye hesabu ya 666. Na, kwa hakika, namba hiyo haimo katika mavazi wala kofia (mitra) ya Baba Mtakatifu. Hakuna mtu yeyote anayeweza kuonesha vazi hilo au kofia hiyo kwa ushahidi. Kwani ni vazi gani au kofia ipi? Basi, kama tunautafuta uzima wa milele, aheri tuache majungu na uongo kama huu. Kama ni maandishi, ni mitra yake tu yenye herufi mbili A na W yaani alpha na omega (rejea Ufu 1:8,17).
Acha tuendelee. Wanaombambikizia Baba Mtakatifu namba 666 hudai kuikokotoa nambari hiyo katika majina matatu tofauti: jina la Kilatini VICARIUS FILII DEI (Kaimu wa Mwana wa Mungu), jina la Kigiriki LATEINOS (Mlatini) na jina la Kiebrania ROMIITH (רמיית - Mrumi). Majina hayo huhesabiwa na wanaombambikizia Baba Mtakatifu namba hiyo kama ifuatavyo:
VICARIUS FILII DEI = 5 + 1 + 100 + 0 + 0 + 1 + 5 + 0 + 0 + 1 + 50 + 1 + 1 + 500 + 0 + 1 = 666.
LATEINOS = 30 + 1 + 300 +5 + 10 + 50 + 70 + 200 = 666.
ROMIITH yaani th y y m w r = 400 + 10 + 10 + 40 + 6 + 200 = 666.
Ndugu zangu, kwa misingi halali ya kusoma Biblia hatuwezi kuyapokea majina haya bila kuyafanyia tahakiki ya kihistoria. Bila kurefusha mjadala, majina haya hayajapata kutumiwa na Baba Mtakatifu yeyote, katika historia ya Kanisa sembuse wakati wa karne ya kwanza Baada ya Kristo wakati ambao hata upapa wenyewe ulikuwa haujakua. Mapapa wa karne zile hawakuwa hatari kwa mtu yeyote. Na watu wasio hatari watapewaje majina ya kupanga na ya siri? Wale wasomaji wa kitabu cha Ufunuo wangelielewaje aya ngumu inayotaja kitu kisichojulikana kwa jina hilo? Wangelifanyaje gematria kwa kutumia majina wasiyoyajua?
Aya 13:18 ilizungumzia jina ambalo wasomaji walikuwa wakilijua kama jina la adui yao aliyekuwa akiwadhulumu na si majina ya ndoto au majungu ya karne ya 20 na 21 B.K. Zaidi ya hayo majina mengine yamelazimishwa kihesabu ili jumla ya kiherufi iwe 666. Kwa ushuhuda tazama U ilivyolazimishwa imaanishe tarakimu 5. Katika Kilatini 5 ni V na wala siyo U. Zaidi ya hayo, jina “MLATINI” kama lingelitumika wakati huo, wasomaji wangelielewa kuwataja wakoloni au askari wa kirumi ambao walikuwa wakitawala ulimwengu wa wakati ule.
Hali kadhalika, kama jina “MRUMI” lingelitumika wakati huo, wasomaji wangelielewa kuwataja wakoloni au askari wa kirumi ambao walikuwa wakitawala ulimwengu wa wakati ule. Kwa hoja hizi, majina hayo ya majungu ni ya tangu karne ya 16, Kanisa Katoliki lilipoanza kupingwa kwa ari mpya na uongozi wake kukataliwa.
Nadhani hadi hapa kila mwenye kutaka kujua anajua kwamba majina waliyobuni Wasabato hayatumiwi na Baba Mtakatifu yeyote. Na zaidi ya hayo ni majina ambayo mwandishi wa kitabu cha Ufunuo hakuwa hata na habari nayo katika karne ile ya kwanza B.K. kwa vile alivyokiandika kitabu chake kwa Kigiriki na wala si kwa Kiebrania au Kilatini. Kumbe, kwa kufanya hivyo Wasabato huwa wanainyonga historia na kukizungumzia kitabu cha Ufunuo nje ya muktadha wake wa kihistoria. Hili ni kosa la kusiganisha nyakati za kikalenda (kwa Kiingereza “anachronism”).
Basi, kwa heshima ya Maandiko Matakatifu, tutafsiri namba 666 au 616 kwa gematria asilia na tukomee hapo hapo. Tusiihamishe namba hiyo na kuwapachika watu wasio na hatia. Kufanya hivyo ni kujitowelesha majungu na ni dhambi isiyo na maana yo yote. Lakini, basi namba 666 imetolewa nje ya mazingira ya Biblia na ndipo ilipowekwa sasa. Nami nimefika hapo hapo.

Namba 666 Imehamishiwa Nje ya Biblia
Ni kituko lakini ndivyo ilivyo. Watu wengine hudai kwamba namba hiyo imeandikwa shingoni kwenye nguo za Papa. Huo ndio uongo na usingiziaji usio na aibu kwa sababu nguo hizo hakuna anayeweza kutuonesha wenziwe. Siku moja niliwahi kuambiwa na wainjilisti wawili kwamba namba 666 ipo kwenye bidhaa za siku hizi, yaani kwenye kifungashio, pale inapochorwa mistari mingi mifupi na mirefu na kuandikwa namba kwa chini, na kwa namna hiyo ipo pia kwenye satelite. Siku hiyo niliwakamata kutokujua nilipowadai wanioneshe mfano. Basi, wakaleta baadhi ya bidhaa za kisasa, wakaniambia niangalie ile mistari iliyochorwa katika kifungashio cha kila bidhaa. Hapo walionesha pia mistari miwili miwili inayojitokeza zaidi kwa chini (jambo ambalo si kweli kwa kila bidhaa). Basi, hapo ndipo walipodai kuna namba 666.
Kumbe, huu ulikuwa ujinga wao mkubwa. Ndugu yangu, mistari hiyo, ndiyo bei ya bidhaa hasa kwa zile zinazouzwa „“supermarket. Katika nchi zilizoendelea watu hawaandiki bei shilingi fulani au fulani wakabandika kwenye bidhaa. Badala yake ndiyo hiyo mistari, kadiri ilivyochorwa ndivyo mashine ya kupigia hesabu inavyotambua na kutofautisha bei za bidhaa ambazo mnunuzi amezifikisha kwenye “kaunta” ya kulipia manunuzi. Na tena bei hizo hazikuingizwa katika satelite; zilivyo nyingi hazihusishwi na satelite yoyote.
Basi, niliwaonya wainjilisti wale wasiwadanganye watu kwa kutumia ujinga wao wakati wenyewe pia hawajui mambo ya kisasa. Hatimaye, niliwaambia, kwa uongo wa namna ile, wao si wainjilisti kwani Injili ni Habari Njema ya ukombozi wetu uliotufikia kwa kifo na ufufuko wa Yesu Kristo na wala siyo namba 666 inayodaiwa kuandikwa kwenye nguo za Papa na kuingizwa kwenye satelite kwa njia ya michoro ya bidhaa za kisasa. Kwa kweli niliwaambia kwa kueneza uongo na kuwatia watu hofu kwa kuwatinga, hawakuwa mbali sana na moto wa milele kwa vile wanamtumikia Shetani aliye baba wa uongo. Hapo nikapata mwanya wa kuwaalika watubu kwa haraka. Lakini, badala ya kupokea mafundisho yangu walisema sina Roho Mtakatifu na kuondoka. Waliondoka na hawakurudi tena kwangu. Kumbe, niliwafuma katika kutokujua kwao, yaani ujinga wao. Samahani kwa simulizi hili; majadiliano yetu yaliacha kuwa ya Kikristo.

Safari Ndefu ya Kutegua Kitendawili cha Kale
Kwa vile madai ya kwamba namba 666 inamhusu Baba Mtakatifu yametutoa sote kutoka kwenye Biblia na kutupa kazi ya kumtafuta nani mwingine anaweza kuwa anatajwa na namba hiyo, nilichukua kalamu na kuanza kuchunguza maneno ya wanaotukana kama hayahusiki vile vile. Utafutaji wangu ulizaa matunda mwaka ule ule 1998. Nikategua kitendawili kwa kugundua kwamba kauli za Wasabato wenyewe zilikuwa ndiyo namba 666.

Nilifanyaje? Nilichukua kauli tatu: PONYA SIKU MUHIMU YA SABA (kwa Kiingereza CURE VITAL SEVENTH DAY, kwa Kilatini CURATUS VITALE SABBATA DIES) na WOKOVU, PONYA SIKU YA SABA (kwa Kiingereza SALVATION, CURE SEVENTH DAY, kwa Kilatini SALVUS, CURARE SABBATA DIES) na VUNJA, CHUKIA UPAPA (kwa Kiingereza DEAL AXE, VIE PAPACY). Nilistaajabu sana kuona ndiyo inakuja 666 ndipo mara moja nikaingiza ugunduzi wangu katika kitabu changu KISA CHA IMANI namba 1.

Ni kweli. Kauli mbiu za Wasabato ni namba hiyo hiyo 666. Angalia gematria inavyokwenda:
CURE VITAL SEVENTH DAY = 100 + 5 + 0 + 0 + 5 + 1+ 0 + 0 + 50 + 0 + 0 + 5 + 0 + 0 + 0 + 0 + 500 + 0 + 0 = 666
CURATUS VITALE SABBATA DIES = 100 + 5 + 0 + 0 + 0 + 5 + 0 + 5 + 1 + 0 + 0 + 50 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 500 + 1 + 0 + 0 = 666
SALVATION, CURE SEVENTH DAY = 0 + 0 + 50 + 5 + 0 + 0 + 1 + 0 + 0 + 100 + 5 + 0 + 0 + 0 + 0 + 5 + 0 + 0 + 0 + 0 + 500 + 0 + 0 = 666
SALVUS, CURARE SABBATA DIES = 0 + 0 + 50 + 5 + 5 + 0 + 100 + 5 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 500 + 1 + 0 + 0 = 666
DEAL AXE VIE PAPACY = 500 + 0 + 0 + 50 + 0 + 1 0 + 0 + 5 + 1 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 100 + 0 = 666

Kuendelea Kutafuta
Basi, kwa kuwa nilikuwa namtafuta nani mwingine anayesemwa na namba 666 au 616, nikagundua kumbe ni hao hao wanaotukana. Lakini, sikukomea hapo mwaka huu 2017 macho yangu yakasaidiwa kuona zaidi. Nilichukua jina la mwasisi wa matusi mwenyewe ELLEN GOULD WHITE ndipo nikashtuka kabisa kumbe ni namba 666. Kwa kisa hiki, leo nawaomba tuimbe alleluya pamoja.

ALLELUYA! KUMBE NAMBA 666 NI ELLEN GOULD WHITE MWENYEWE
Sasa nawapeni habari njema kabisa. Tusi la namba 666 limefumbua macho yangu kwa namna ya ajabu na sasa nawatangazia wote nilichokigundua ili kiwafumbue macho ninyi pia. Kifupi, nimefikishwa kwenye ugunduzi huo kwa kupitia tahadhari ya wahenga. Wao walisema, “Unapokula na kipofu, usimguse kipofu mkono!” Msidanganyike tena, namba 666 ni ELLEN GOULD WHITE mwenyewe.

Nawasimulieni. Kwa kuzidi kutukana, niliwatazama watukanaji nione kama matusi hayawahusu wenyewe. Nikagundua kumbe ndiyo hivyo hivyo. Kumbe, wakati mwingine heri utukanwe maana waweza kufunguliwa mlango kwa jambo jema fulani. Basi, natangaza kadamnasi kwamba tusi la namba 666 limekuwa tusi la neema na heri sana kwetu Wakatoliki, tulionyanyasika kwalo kwa muda mrefu. Linawahusu wanaotutukana hao hao. Kumbe, walikuwa wanapiga kelele za “Mwizi, mwizi!“ ili kutupoteza maboya tu. Wezi ni wenyewe.

Tuamke. Jamani, Bi Ellen Gould White alikuwa anapiga kelele na kutukana kusudi tusishughulike na jina lake. Wafuasi wake wakadakia mbinu hiyo hiyo. Kumbe, Wasabato hukazania namba 666 imwelekee Baba Mtakatifu kwa sababu walitaka tusijue kwamba namba 666 inamwelekea “nabii” wao ELLEN GOULD WHITE! Walitaka tukamsake sungura katika kichaka kingine. Kumbe, Ufu 13:18 inamtaja Bi Ellen White moja kwa moja kama mnyama ambaye jina lake ukilikokotoa linakuja moja kwa moja kwenye namba 666. Yaani linakuja 666 taslimu!
Je, unaniuliza kwa vipi? Ni hivi ifuatavyo. Ukiliandika jina la Bi ELLEN WHITE pamoja na jina la asili yake GOULD unakuja kwenye namba 666 juu ya alama. Nifuatilie vyema hapa kusudi tukokotoe tarakimu pamoja. Lakini, angalia vyema, jambo lile la kuhitajika hekima, linahusisha pia kuirudisha “W” ya WHITE kwenye uasilia wake yaani V maradufu (kwa Kiingereza “double v”). Kwa taarifa yako, tangu kale “W” ni “V” mbili na ni kwa sababu ya asili hiyo Wajerumani huitamka “W” kama “V”. Umeshanielewa uzuri? Kama umeshanielewa, sasa tazama “gematria“ inavyokubali:
E L L E N G O U L D W H I T E
0+ 50 + 50 + 0 + 0 + 0 + 0 + 5 + 50 + 500+ 10+0+1+0+0 = 666

Je, unaona jinsi jina la Bi Ellen White linavyokubali kama jina la mnyama yule? Yaani sawa sawa pasipo kuacha mashaka yoyote. Kinyume chake, jiulize ni Baba Mtakatifu gani mwenye jina kama hilo? Maskini, Wasabato walisahau jambo hili la kimahesabu! Lakini nadhani wanalifahamu na ndiyo maana hufanya juhudi kubwa kulikoneshea tusi la namba 666 kwa Baba Mtakatifu. Ni janja yao lakini sasa ipo hadharani.
Narudia. Wanachofanya Wasabato ni mbinu ya kawaida tu, yaani kwamba ukitaka watu wasikuangalie wewe elekeza umakini wao kwa mtu mwingine au kitu tofauti. Ndipo, badala ya watu kuelekeza umakini kwenye jina “ELLEN GOULD WHITE” huzugwa waelekeze kwenye majina ya kubuni ya “VICARIUS FILII DEI”, “LATEINOS” na “ROMIITH”, majina yasiyo na maana yoyote kihistoria na muktadha wa kitabu cha Ufunuo.
Je, umeona eh! Kumbe, mambo yako kwenye majina “ELLEN GOULD WHITE”. Namba 666 inakubali taslimu kabisa. Chukua hii!

Hatima
Naona imetosha, nanyi, bila shaka, mnaniambia kwa Kiingereza “Stop, it is enough and clear!” kwa maana ya “Acha inatosha na imeeleweka!” Alamsiki!

Pd Titus Amigu
Endeleeni kujifariji. Shetani kamwe hawezi kupindisha ukweli wa Biblia.
1. Alama ya Mnyama ni ibada ya jumapili
2. 666 ni alama ya mpinga kristo ambaye ni papa
3. kahaba mkuu wa Ufunuo 17:5 ni Roman Catholic

Hata mjikatekate kama manbii wa baali ukweli unabaki palepale.
 
1. Unaweza kuonyesha katika biblia kua alama ya mnyama ni ibada ya jumapili
2. Nakubaliana na ww 666 ni alama ya mpinga kristu,hbu iunganishe na papa kwa kutumia biblia yako!
Mbna hujibu hoja unaruka ruka tu
 
Unasema kahaba wa ufunuo n RC...unaambiwa ktk hyo ufunuo 17:10&11 anaelezea wafalme saba waliomtawala huyo mwanamke na vichwa kumi vitakavyokua na shaur moja ktk mstari wa 13 ili kufanya vita na huyo mwanamke...hebu weka upapa hapo ss uoneshe hao wafalme saba na hayo mataifa kumi ya kufanya shaur juu ya mwanamke kahaba ambaye ww wamterm Rc
Note: soma ezekieli 16 uone Mungu anavolaani israeli na kuiita kahaba kwa kuwafanyia yte na bado wakaenda kufanya uasherati(kuchukuana na miungu) ya nchi jirani ya alipowapa
 
Endeleeni kujifariji. Shetani kamwe hawezi kupindisha ukweli wa Biblia.
1. Alama ya Mnyama ni ibada ya jumapili
2. 666 ni alama ya mpinga kristo ambaye ni papa
3. kahaba mkuu wa Ufunuo 17:5 ni Roman Catholic

Hata mjikatekate kama manbii wa baali ukweli unabaki palepale.
umeelewa alichoandika zuzu wewe....

ulikuwa hujui practicall Nabii Mke Ellen g White alikuwa Kahaba...?
 
Hakuna sehemu kwenye bibilia inayosema sabato ni dini au dhehebu.Sabato ni siku ya kumtukuza mungu na wala sio Dini au dhehebu.Bibilia inazungumzia zaidi Kufuata mafundisho ya mungu.Hakuna sehemu kwenye bibilia mungu amesema lipi ni dhehebu lake.Tuache kupotosha hapa.
 
Mimi nikienda kanisani nikiona mchungaji anaongea sana habari za utajiri na kukuingiza kingi ujione na wewe ni tajiri wa roho wakati maisha yako hayapo hivyo huku akisisitiza maswala ya kutoa sadaka sana, hua natoka kati kati ya ibada na sirudi tena.

Mara ya mwisho ilikua kanisa la Kinondoni maarufu kwa Mchungaji Swai, yule bwana alivyosema sadaka haiwezi kua 500 pale pale nikaondoka.
Imani yako itakuokoa,Mungu ni mwenye wivu,we unaenda kwa mganga unatoa more than 50K,afu kwa mchungaji unampa jero ...hahaha my friend ur not serious, kama ana hubiri injili,lazima ale madhabauni ndugu
 
Sijawahi kwenda kwa mganga na sitarajii.
 
Hiyo tafsiri unaipata kwa uongoz wa roho mtakatifu

Kitabu cha ufunuo kimeandikwa kwa kificho
Dont be stingy !fichua sasa! Imeandikwa kwa kificho afichwe nani? Tafadhali kwa hisani yako wewe mwenye roho mtakatifu fichua !
 
Tunaomba aliye na hiyo ufunuo 17, aiweke hapa
Revelation 17:1-8,10-18
[1]And there came one of the seven angels which had the seven vials, and talked with me, saying unto me, Come hither; I will shew unto thee the judgment of the great whore that sitteth upon many waters:
Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;
[2]With whom the kings of the earth have committed fornication, and the inhabitants of the earth have been made drunk with the wine of her fornication.
ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake.
[3]So he carried me away in the spirit into the wilderness: and I saw a woman sit upon a scarlet coloured beast, full of names of blasphemy, having seven heads and ten horns.
Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.
[4]And the woman was arrayed in purple and scarlet colour, and decked with gold and precious stones and pearls, having a golden cup in her hand full of abominations and filthiness of her fornication:
Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.
[5]And upon her forehead was a name written, MYSTERY, BABYLON THE GREAT, THE MOTHER OF HARLOTS AND ABOMINATIONS OF THE EARTH.
Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.
[6]And I saw the woman drunken with the blood of the saints, and with the blood of the martyrs of Jesus: and when I saw her, I wondered with great admiration.
Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu.
[7]And the angel said unto me, Wherefore didst thou marvel? I will tell thee the mystery of the woman, and of the beast that carrieth her, which hath the seven heads and ten horns.
Na yule malaika akaniambia, Kwani kustaajabu? Nitakuambia siri ya mwanamke huyu, na ya mnyama huyu amchukuaye, mwenye vile vichwa saba na zile pembe kumi.
[8]The beast that thou sawest was, and is not; and shall ascend out of the bottomless pit, and go into perdition: and they that dwell on the earth shall wonder, whose names were not written in the book of life from the foundation of the world, when they behold the beast that was, and is not, and yet is.
Yule mnyama uliyemwona alikuwako, naye hayuko, naye yu tayari kupanda kutoka kuzimu na kwenda kwenye uharibifu. Na hao wakaao juu ya nchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watastaajabu wamwonapo yule mnyama, ya kwamba alikuwako, naye hayuko, naye atakuwako.
[10]And there are seven kings: five are fallen, and one is, and the other is not yet come; and when he cometh, he must continue a short space.
Navyo ni wafalme saba. Watano wamekwisha kuanguka, na mmoja yupo, na mwingine hajaja bado. Naye atakapokuja imempasa kukaa muda mchache.
[11]And the beast that was, and is not, even he is the eighth, and is of the seven, and goeth into perdition.
Na yule mnyama aliyekuwako naye hayuko, yeye ndiye wa nane, naye ni mmoja wa wale saba, naye aenenda kwenye uharibifu.
[12]And the ten horns which thou sawest are ten kings, which have received no kingdom as yet; but receive power as kings one hour with the beast.
Na zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi, ambao hawajapokea ufalme bado, lakini wapokea mamlaka kama wafalme muda wa saa moja pamoja na yule mnyama.
[13]These have one mind, and shall give their power and strength unto the beast.
Hawa wana shauri moja, nao wampa yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao.
[14]These shall make war with the Lamb, and the Lamb shall overcome them: for he is Lord of lords, and King of kings: and they that are with him are called, and chosen, and faithful.
Hawa watafanya vita na Mwana-Kondoo, na Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu.
[15]And he saith unto me, The waters which thou sawest, where the whore sitteth, are peoples, and multitudes, and nations, and tongues.
Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha.
[16]And the ten horns which thou sawest upon the beast, these shall hate the whore, and shall make her desolate and naked, and shall eat her flesh, and burn her with fire.
Na zile pembe kumi ulizoziona, na huyo mnyama, hao watamchukia yule kahaba, nao watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kabisa kwa moto.
[17]For God hath put in their hearts to fulfil his will, and to agree, and give their kingdom unto the beast, until the words of God shall be fulfilled.
Maana Mungu ametia mioyoni mwao kufanya shauri lake, na kufanya shauri moja, na kumpa yule mnyama ufalme wao hata maneno ya Mungu yatimizwe.
[18]And the woman which thou sawest is that great city, which reigneth over the kings of the earth.
Na yule mwanamke uliyemwona, ni mji ule mkubwa, wenye ufalme juu ya wafalme wa nchi.
 
Nakuletea na ezekiel 16 ili ulinganishe kahaba ni nani
Ezekiel 16:1-30,34-37,39
[1]Again the word of the LORD came unto me, saying,
Neno la BWANA likanijia tena, kusema,
[2]Son of man, cause Jerusalem to know her abominations,
Mwanadamu, uujulishe Yerusalemu machukizo yake,
[3]And say, Thus saith the Lord GOD unto Jerusalem; Thy birth and thy nativity is of the land of Canaan; thy father was an Amorite, and thy mother an Hittite.
useme, Bwana MUNGU auambia Yerusalemu hivi; Asili yako na kuzaliwa kwako kwatoka katika nchi ya Mkanaani; Mwamori alikuwa baba yako, na mama yako alikuwa Mhiti.
[4]And as for thy nativity, in the day thou wast born thy navel was not cut, neither wast thou washed in water to supple thee; thou wast not salted at all, nor swaddled at all.
Na katika habari za kuzaliwa kwako, siku ile uliyozaliwa, kitovu chako hakikukatwa, wala hukuoshwa kwa maji usafishwe; hukutiwa chumvi hata kidogo, wala hukutiwa katika nguo kabisa.
[5]None eye pitied thee, to do any of these unto thee, to have compassion upon thee; but thou wast cast out in the open field, to the lothing of thy person, in the day that thou wast born.
Hapana jicho lililokuhurumia, ili kukutendea lo lote la mambo hayo kwa kukuhurumia; lakini ulitupwa nje uwandani, kwa kuwa nafsi yako ilichukiwa, katika siku ile uliyozaliwa.
[6]And when I passed by thee, and saw thee polluted in thine own blood, I said unto thee when thou wast in thy blood, Live; yea, I said unto thee when thou wast in thy blood, Live.
Nami nilipopita karibu nawe, nikakuona ukigaagaa katika damu yako, nalikuambia, Ujapokuwa katika damu yako, uwe hai; naam, nalikuambia, Ujapokuwa katika damu yako, uwe hai.
[7]I have caused thee to multiply as the bud of the field, and thou hast increased and waxen great, and thou art come to excellent ornaments: thy breasts are fashioned, and thine hair is grown, whereas thou wast naked and bare.
Nalikufanya kuwa maelfu-elfu, kama mimea ya mashamba, ukaongezeka, na kuzidi kuwa mkubwa, ukapata kuwa na uzuri mno; matiti yako yakaumbwa, nywele zako zikawa zimeota; lakini ulikuwa uchi, huna nguo.
[8]Now when I passed by thee, and looked upon thee, behold, thy time was the time of love; and I spread my skirt over thee, and covered thy nakedness: yea, I sware unto thee, and entered into a covenant with thee, saith the Lord GOD, and thou becamest mine.
Basi, nilipopita karibu nawe, nikakutazama; tazama, wakati wako ulikuwa wakati wa upendo; nikatandika upindo wa vazi langu juu yako, nikakufunika uchi wako; naam, nalikuapia, nikafanya agano nawe, asema Bwana MUNGU, ukawa wangu.
[9]Then washed I thee with water; yea, I throughly washed away thy blood from thee, and I anointed thee with oil.
Kisha nikakuosha kwa maji; naam, nalikuosha kabisa damu yako, nikakupaka mafuta;
[10]I clothed thee also with broidered work, and shod thee with badgers' skin, and I girded thee about with fine linen, and I covered thee with silk.
nikakuvika nguo ya taraza, nikakupa viatu vya ngozi ya pomboo, nikakufunga nguo ya kitani safi kiunoni mwako, nikakufunika kwa hariri.
[11]I decked thee also with ornaments, and I put bracelets upon thy hands, and a chain on thy neck.
Nikakupamba kwa mapambo pia, nikatia vikuku mikononi mwako, na mkufu shingoni mwako.
[12]And I put a jewel on thy forehead, and earrings in thine ears, and a beautiful crown upon thine head.
Nikatia hazama puani mwako, na pete masikioni mwako, na taji nzuri juu ya kichwa chako.
[13]Thus wast thou decked with gold and silver; and thy raiment was of fine linen, and silk, and broidered work; thou didst eat fine flour, and honey, and oil: and thou wast exceeding beautiful, and thou didst prosper into a kingdom.
Hivyo ulipambwa kwa dhahabu na fedha; na mavazi yako yalikuwa ya kitani safi, na hariri, na kazi ya taraza; ulikula unga mzuri, na asali, na mafuta; nawe ulikuwa mzuri mno, ukafanikiwa hata kufikilia hali ya kifalme.
[14]And thy renown went forth among the heathen for thy beauty: for it was perfect through my comeliness, which I had put upon thee, saith the Lord GOD.
Sifa zako zikaenea kati ya mataifa kwa sababu ya uzuri wako; kwa maana ulikuwa mkamilifu, kwa sababu ya utukufu wangu niliokutia, asema Bwana MUNGU.
[15]But thou didst trust in thine own beauty, and playedst the harlot because of thy renown, and pouredst out thy fornications on every one that passed by; his it was.
Lakini uliutumainia uzuri wako, ukafanya mambo ya kikahaba kwa sababu ya sifa zako, ukamwaga mambo yako ya kikahaba juu ya kila mtu aliyepita; ulikuwa wake.
[16]And of thy garments thou didst take, and deckedst thy high places with divers colours, and playedst the harlot thereupon: the like things shall not come, neither shall it be so.
Ukatwaa baadhi ya mavazi yako, ukajifanyia mahali palipoinuka, palipopambwa kwa rangi mbalimbali, ukafanya mambo ya kikahaba juu yake; mambo kama hayo hayatakuja wala hayatakuwako.
[17]Thou hast also taken thy fair jewels of my gold and of my silver, which I had given thee, and madest to thyself images of men, and didst commit whoredom with them,
Pia ulivitwaa vyombo vyako vya uzuri, vya dhahabu yangu na vya fedha yangu, nilivyokupa, ukajifanyia sanamu za wanaume, ukafanya mambo ya kikahaba pamoja nazo;
[18]And tookest thy broidered garments, and coveredst them: and thou hast set mine oil and mine incense before them.
ukatwaa nguo zako za kazi ya taraza, ukawafunika, ukaweka mafuta yangu na uvumba wangu mbele yao.
[19]My meat also which I gave thee, fine flour, and oil, and honey, wherewith I fed thee, thou hast even set it before them for a sweet savour: and thus it was, saith the Lord GOD.
Mkate wangu niliokupa, unga mzuri, na mafuta, na asali, nilivyokulisha, ukaviweka mbele yao viwe harufu ya kupendeza; na ndivyo vilivyokuwa; asema Bwana MUNGU.
[20]Moreover thou hast taken thy sons and thy daughters, whom thou hast borne unto me, and these hast thou sacrificed unto them to be devoured. Is this of thy whoredoms a small matter,
Pamoja na hayo uliwatwaa wana wako na binti zako, ulionizalia, ukawatoa sadaka kwao ili waliwe. Je! Mambo yako ya kikahaba ni kitu kidogo tu,
[21]That thou hast slain my children, and delivered them to cause them to pass through the fire for them?
hata ukawaua watoto wangu, na kuwatoa kwa kuwapitisha motoni kwa hao?
[22]And in all thine abominations and thy whoredoms thou hast not remembered the days of thy youth, when thou wast naked and bare, and wast polluted in thy blood.
Na katika machukizo yako yote, na mambo yako ya kikahaba, hukuzikumbuka siku za ujana wako, ulipokuwa uchi, huna nguo, ukawa ukigaagaa katika damu yako.
[23]And it came to pass after all thy wickedness, (woe, woe unto thee! saith the Lord GOD😉
Tena, imekuwa baada ya uovu wako wote, (ole wako! ole wako! Asema Bwana MUNGU,)
[24]That thou hast also built unto thee an eminent place, and hast made thee an high place in every street.
ulijijengea mahali palipoinuka, ukajifanyia mahali palipoinuka katika kila njia kuu.
[25]Thou hast built thy high place at every head of the way, and hast made thy beauty to be abhorred, and hast opened thy feet to every one that passed by, and multiplied thy whoredoms.
Umejenga mahali pako palipoinuka penye kichwa cha kila njia, ukaufanya uzuri wako kuwa chukizo, ukatanua miguu yako kwa kila mtu aliyepita karibu, ukaongeza mambo yako ya kikahaba.
[26]Thou hast also committed fornication with the Egyptians thy neighbours, great of flesh; and hast increased thy whoredoms, to provoke me to anger.
Tena umezini na Wamisri, jirani zako, wakuu wa mwili; ukaongeza mambo yako ya kikahaba, ili kunikasirisha.
[27]Behold, therefore I have stretched out my hand over thee, and have diminished thine ordinary food, and delivered thee unto the will of them that hate thee, the daughters of the Philistines, which are ashamed of thy lewd way.
Basi, tazama, kwa ajili ya hayo nimenyosha mkono wangu juu yako, nami nimelipunguza posho lako, na kukutoa kwa mapenzi yao wanaokuchukia, binti za Wafilisti, walioyaonea haya mambo yako ya uasherati.
[28]Thou hast played the whore also with the Assyrians, because thou wast unsatiable; yea, thou hast played the harlot with them, and yet couldest not be satisfied.
Pia umefanya mambo ya kikahaba pamoja na Waashuri, kwa sababu ulikuwa huwezi kushibishwa; naam, umefanya mambo ya kikahaba pamoja nao, wala hujashiba bado.
[29]Thou hast moreover multiplied thy fornication in the land of Canaan unto Chaldea; and yet thou wast not satisfied herewith.
Pamoja na hayo umeongeza mambo yako ya kikahaba katika nchi ya Kanaani, mpaka Ukaldayo, wala hujashibishwa kwa hayo.
[30]How weak is thine heart, saith the Lord GOD, seeing thou doest all these things, the work of an imperious whorish woman;
Jinsi moyo wako ulivyokuwa dhaifu, asema Bwana MUNGU, ikiwa unafanya mambo hayo yote, kazi ya mwanamke mzinzi,
[34]And the contrary is in thee from other women in thy whoredoms, whereas none followeth thee to commit whoredoms: and in that thou givest a reward, and no reward is given unto thee, therefore thou art contrary.
Tena, katika mambo yako ya kikahaba, wewe na wanawake wengine ni mbalimbali, kwa kuwa hapana akufuataye katika mambo yako ya kikahaba; tena kwa kuwa unatoa ujira, wala hupewi ujira; basi, njia yako na njia yao ni mbalimbali.
[35]Wherefore, O harlot, hear the word of the LORD:
Kwa sababu hiyo, Ewe kahaba, lisikie neno la BWANA;
[36]Thus saith the Lord GOD; Because thy filthiness was poured out, and thy nakedness discovered through thy whoredoms with thy lovers, and with all the idols of thy abominations, and by the blood of thy children, which thou didst give unto them;
Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu uchafu wako umemwagwa, na uchi wako umefunuliwa, kwa njia ya uzinzi wako pamoja na wapenzi wako; na kwa sababu ya vinyago vyote vya machukizo yako; na kwa sababu ya damu ya watoto wako, uliyowapa;
[37]Behold, therefore I will gather all thy lovers, with whom thou hast taken pleasure, and all them that thou hast loved, with all them that thou hast hated; I will even gather them round about against thee, and will discover thy nakedness unto them, that they may see all thy nakedness.
basi, tazama, nitawakusanya wapenzi wako wote ambao umejifurahisha pamoja nao, nao wote uliowapenda, pamoja na watu wote uliowachukia; naam, nitawakusanya juu yako pande zote, na kuwafunulia uchi wako, wapate kuuona uchi wako wote.
[39]And I will also give thee into their hand, and they shall throw down thine eminent place, and shall break down thy high places: they shall strip thee also of thy clothes, and shall take thy fair jewels, and leave thee naked and bare.
Tena nitakutia katika mikono yao, nao watapaangusha mahali pako pakuu, na kupabomoa mahali pako palipoinuka, nao watakuvua nguo zako, na kutwaa vyombo vyako vya uzuri, nao watakuacha uchi, huna nguo.
 
Mungu hakuwahi kuteua kanisa fulani kuwa alama yake, ila kanisa lake ni wale ambao huzishika amri zake na kuzifuata, acha kupotosha watu na kujipotosha kuhusu SDA na upendeleo wa Mungu kwao
Daah asee!!...umenena vema mkuu,mtu akisoma hii point yako sidhan hata kama ataendelea kubishana.
 
Yesu mwenyewe alipingana na wayahudi khs sabato nashangaa leo watu wanatoka mapovu kuhusu sabato ambayo yesu mwenyewe aliiponda. Kujua maandiko saana si kuuona ufalme wa mungu. Matendo mema ndipo ufunguo wa kwenda kwa mungu. Dini nzuri ni ile inayomlea binadamu kiroho na kimwili. Hayo majisifu mengine ni ushetani tu. Maana hata yesu alipojaribiwa na shetani alijisifu Sana mbele Ya yesu lkn kwakua yesu alikua na hekima za kimungu alimwambia shetani ondoka kwangu haraka. Hivyo hata sisi wakatoliki tunasema ondoka kwangu haraka enyi wapotoshaji watu mnaodhani ili muwapate watu kwenye dhehebu lenu lzm muwatukane wakatoliki Poleni sana sisi tunasonga mbele mana unajua nyinyi ni yule shetani aliemjaribu yesu.. Majisifu yenu nikama mafarisayo tu. Mmejaza maandiko vichwani lkn matendo yenu ni tatizo.
 
Je unajua roman empire ilgawanyika mara mbili na kua eastern(byzantine) na western?unajua western ilyokua na makao makuu roma ilkufa mwaka 476AD na hii eastern iliyokua na makao makuu constaninople mji aliokua akikaa mfalme costantine ulkufa mwaka 1436AD na Kuwa chini ya Ottoman empire au hujui kisa cha constantinople kuitwa instambul ss?
Nikupe tu kdgo,unabii wa danieli wahusu nyakati za mwisho na yatakayoipata Yerusalem mji wa bwana(tizama danieli 9) anaambiwa kuna majuma 62 na juma la 70(miaka saba ya mwsho itagawanyika mara mbili ambapo mitatu ya mwsho itakua hyo ya mpinga kristo(miez 42)) hebu hata soma mathayo 24:15 wanafunz wanapomuulza siku za mwsho znakuaje na anaeleza ni mpaka hapo hlo chukizo la uharibifu(mpinga kristo) litakaposimama patakatfu yan hekaluni
Siendelei nione mana umeleta stori hujaleta raman na hta hlo jeraha unalosema lililoandikwa ktk ufunuo 13 hbu bas onesha huo upapa wa 1920 ulivotawala dunia mna haukuvuka mipaka yake nliyosema hapo juu...rud soma stori vzr ya wanyama
Kabla ya huo mwaka 476AD tayari utawala wa kirumi ulikuwa umegawanyika sehemu kumi (pembe kumi zinazotajwa katika ufunuo na daniel 7). Hayo ndiyo mataifa ya ulaya sasa, yote ilikuwa dola ya rumi. Baadae, ndipo papa alipoamua kuyafutilia mbali mataifa matatu yaliyokataa kumtii ambayo ni heruli, vandals na ostrogoths. Hapo ndipo unabii wa Daniel 7 ulitimia hapo aliposema na tazama pembe ndogo iliziangusha pembe tatu. Hii pembe ndogo inayozuka kati ya pembe kumi katika Daniel sura ya saba, ndio upapa ulioibuka katikati ya rumi iliyogawanyika katika falme kumi za ulaya ya sasa.

Kwa hoja hizi papa ndiye mpinga Kristo jiepusheni naye.
 
Yesu mwenyewe alipingana na wayahudi khs sabato nashangaa leo watu wanatoka mapovu kuhusu sabato ambayo yesu mwenyewe aliiponda. Kujua maandiko saana si kuuona ufalme wa mungu. Matendo mema ndipo ufunguo wa kwenda kwa mungu. Dini nzuri ni ile inayomlea binadamu kiroho na kimwili. Hayo majisifu mengine ni ushetani tu. Maana hata yesu alipojaribiwa na shetani alijisifu Sana mbele Ya yesu lkn kwakua yesu alikua na hekima za kimungu alimwambia shetani ondoka kwangu haraka. Hivyo hata sisi wakatoliki tunasema ondoka kwangu haraka enyi wapotoshaji watu mnaodhani ili muwapate watu kwenye dhehebu lenu lzm muwatukane wakatoliki Poleni sana sisi tunasonga mbele mana unajua nyinyi ni yule shetani aliemjaribu yesu.. Majisifu yenu nikama mafarisayo tu. Mmejaza maandiko vichwani lkn matendo yenu ni tatizo.

Mathayo 5:17." Msidhani nalikuja kuitangua torati wala manabii. La hasha bali kutimiliza."

Soma Biblia upate maarifa. Acha kufuata simulizi za mapadri
 
umeelewa alichoandika zuzu wewe....

ulikuwa hujui practicall Nabii Mke Ellen g White alikuwa Kahaba...?
Wewe muabudu sanamu nikishakuambia siku nyingi. Hadi uachane na sanamu ndipo akili yako itakuwa sawa.
 
NAMBA 666 AU 616 ILIYOANDIKWA KWENYE UFU 13:18 HAIMHUSU PAPA ISIPOKUWA ELLEN GOULD WHITE
Imbeni pamoja nami ALLELUYA! Kwa nini? Kwa sababu Mungu amenitendea makuu. Amenisaidia kukitegua kitendawili cha karibu karne mbili sasa, yaani kitendawili cha namba 666. Kwa muda mrefu tangu enzi za akina ELLEN GOULD WHITE, yaani miaka ile ya 1846, namba 666 ya katika Ufu 13:18 imekuwa ikielekezwa kwa majungu na matusi kwa Baba Mtakatifu. Ndugu zanguni, tulikuwa tunazugwa tu. Kumbe, siri ni kwamba ilikuwa inamwelekea mwenyewe aliyekuwa anaelekeza mashambulizi na matusi kwa Baba Mtakatifu, yaani ELLEN GOULD WHITE.
Nina furaha kubwa sana. Nawaalikeni mfurahi pamoja nami. Binafsi, nilikuwa napata taabu sana kujaribu kufumbua kitendawili hicho. Lakini, wakati huo huo, nilikuwa najiuliza kwa nini mashambulizi kwa Baba Mtakatifu ni makali hivyo? Kumbe, sasa tumefumbuliwa. Yote yalikuwa ni mbinu ya kutupoteza watu “maboya” tusijue kwamba namba inamwelekea mwenyewe anayetukana. Kumbe, ilikuwa ni mbinu ile ile ya mwizi kupiga kelele za “Mwizi, mwizi, mwizi huyo!” kusudi watu wamfukuze mtu mwingine na siyo yeye mwenyewe.
Acheni niwakumbusheni mambo. Nadhani nyote mna habari na mashtaka maarufu sana dhidi ya Wakatoliki kwamba namba 666 au 616 inamhusu kiongozi wetu mkuu yaani Papa au Baba Mtakatifu na kwamba namba hiyo imeandikwa kwenye mavazi yake na kofia yake. Zaidi ya hapo kuna madai kwamba namba hii ipo pia katika kompyuta na satelite. Leo nataka niwafunulieni mambo yalivyo.

Hii ni Mada ya Lugha na Hesabu Kidogo
Vijana wangu msishtuke na kuhangaika. Mada hii itahusisha herufi za Kiebrania na Kigiriki lakini zitakuwa chache tu nanyi mtaelewa yote nitakayoandika kwani ni masuala rahisi kuyafuatilia. (Kwa bahati mbaya herufi za Kigiriki zinakataa humu). Papo hapo, kutakuwa na hesabu. Hata hizo hazitawahangaisheni kwani ni hesabu za kujumlisha tu. Leo kumbukeni pia hesabu za Shule ya Msingi tulipokuwa tunatumia tarakimu za Kilatini, kwa mfano, I = 1, V = 5, X= 10, L = 50, C= 100, D = 500 na M = 1000.
Ili tuelewane, nitaanza na historia, kishapo nitakwenda nje ya Biblia ilikohamishiwa namba 666.

Mama ni Historia
Hebu nianze na jibu fupi linalolingana na historia. Wayahudi hujumlisha thamani ya kitarakimu majina ya watu na maneno mbalimbali na kuzaa namba mbalimbali. Kuhesabu kwa namna hii huitwa gematria nako kumetumika katika Ufu 13:18 na kuzaa namba 666 au katika nakala zingine za Biblia namba 616. Swali kubwa ni je, namba hiyo inamhusu nani? Ukweli ni kwamba namba 666 au 616 haimhusu Papa au Baba Mtakatifu hata kidogo. Tena haikuandikwa katika mavazi ya Papa na wala haimo katika kompyuta ama satelite.
Ukweli, kibiblia na kihistoria, ni kwamba namba hiyo ilimhusu na bado inamhusu kiongozi wa dola ya Kirumi zamani zile, yaani Kaisari Nero. Basi, namba 666 au 616 ndiyo hesabu ya jina la Nero aliyekuwa akiwadhulumu Wakristo katika karne ya kwanza ya Ukristo. Hesabu hiyo inapatikana kwa kukokotoa kigematria maneno NERON KAISAR (kwa Kiebrania - נרון קסר) au NERO KAISAR (kwa Kiebrania - נרו קסר) na KAISAR THEOS (kwa Kigiriki).

Jibu refu: Hakuna mahali po pote katika Biblia ambapo msomaji ameombwa kutumia akili isipokuwa hapa. Kwa kuwa ili kuipata hesabu hii kulihitaji kupiga hesabu, wasomaji wote wa kifungu kile walialikwa kupiga hesabu, gematria. Ndipo imeandikwa “Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili na aihesabu hesabu” (Ufu 13:18). Kumbe, kinyume na matumizi ya akili, hapa ndipo mahala wasomaji kadha wa kadha wasipotumia akili yoyote katika kusoma isipokuwa majungu na usingiziaji.
Ndugu yangu, wapo watu chungu nzima wanaoeneza tafsiri kwamba namba 666 au 616 inamhusu Baba Mtakatifu na imeandikwa kwenye mavazi yake kama nilivyosema hapo juu (rejea Ufu 13:18, 15:2). Je, mafundisho hayo yana ukweli? Najijibu mwenyewe: si ya kweli.
Tusisahau, kitabu cha Ufunuo wa Yohane kina mazingira yake ya kihistoria ambayo ni muhimu katika kuielewa sura ya 13. Mazingira hayo ni ya historia ya Dola ya Kirumi. Wakristo walipokuwa wakidhulumiwa na dola hiyo, mwandishi wa kitabu cha Ufunuo alichukua kalamu na kuandika ili kuwaliwaza ndugu zake aliokuwa akiteseka pamoja nao (rejea Ufu 1:9). Basi, katika kuandika akatumia lugha ya mafumbo ili watesi wasifahamu wanayosemwa. Ndicho kisa, basi, joka kuu lenye pembe na kadhalika linamaanisha Dola ya Kirumi. Mkubwa wa dola hiyo naye akapewa jina la kupanga au jina la kifumbo kwa mtindo wa kucheza na namba za jina lake (gematria).
Ukitaka kupata picha kidogo ya haya, chukulia mfano wa vitabu vya marehemu Shaban Robert. Yeye aliandika mashairi mengi ya kuwatia watu hamasa wapiganie uhuru. Katika mashairi hayo, wananchi anawaita, mathalani, siafu na wakoloni nyoka. Hao siafu wanakazana kumdhuru nyoka. Aidha, kitabu chake cha Kusadikika ni kitabu cha fumbo kinachofumbia hali ya mambo katika hewa ya kikoloni. Kwa hakika wakoloni hawakuambulia lolote katika mashairi na fasihi ya Shaban Robert. Kinyume chao, wananchi walielewa mada husika na “kuwaacha kwenye mataa” wakoloni. Ndivyo inavyotokea shuleni, mwalimu mbaya kupangwa jina ambalo mwenyewe halijui hata kama litatajwa mbele yake.
Upangaji wa jina la mtu kwa kutumia hesabu ya herufi za jina lake mwenyewe ulikuwa mtindo maarufu wa marabi na ulijulikana kama gematria. Ufu 13:18, si mahali pa kwanza kutumia gematria hata namba kumi na nne ya vizazi vilivyotajwa katika Mt 1:17 ni gematria ya jina Daudi (דוד) kwani d + w + d ni 6 + 4 + 6 = 14. Sasa ni nani katika karne ya kwanza aliyekuwa adui wa Wakristo na jina lake kigematria lilizaa namba 666 au 616? Hili ndilo swali la kuulizana. Alikuwa KAISARI NERO.
Tukitafsiri Biblia kwa usahihi huu, mtesi wa walengwa wa kitabu, aliyekuwa akifumbiwa katika 13:18 kwa kuhesabu jina lake kigematria, hawezi kuwa mtu wa karne ya tano au ya ishirini na moja. Walengwa walikuwa ni Wakristo wa karne ya kwanza na adui yao alikuwa akiishi nao kwa wakati huo huo. Basi, nani alikuwa mtesi maarufu katika mazingira ya karne ya kwanza? Wakati ule alikuwa Kaisari Nero ama Kaisari fulani aliyejidai kuwa Mungu na huyo ndiye kigematria jina lake linazaa namba 666 au 616.
Basi, gematria ikitumika kwa konsonanti za Kiebrania: נרון קסר - NERON KAISAR (yaani Kaisari Neron) au kwa maneno ya Kigiriki: KAISAR THEOS (yaani Kaisari Mungu) tunapata pasipo kuzunguka zunguka namba 666 au 616. Tazama hesabu zenyewe zinavyofanyika. (נרון קסר) r s q n w r n = 200 + 60 + 100 + 50 + 6 + 200 + 50 = 666.
k a i s a r th e o s = 20 + 1 + 10 + 200 + 1 + 100 + 9 + 5 + 70 + 200 = 616.
Angalia vyema. Hii tafsiri ya ‘KAISAR THEOS’ yaani ‘Mungu Kaisari’ ndiyo inayorejewa kwenye Biblia zenye kuandika jumla ya namba 616. Lakini vile vile 616 iliweza kupatikana kwa kuondoa “n” ya mwisho kwenye jina נרון (n w r n) katika Kiebrania. Kwa Wakristo, namba 666 ilipomtaja Neron ilisema pia kwamba ni MPINGA KRISTO kwani alikuwa kinyume cha utimilifu. Kinambari, utimilifu ni namba 777. Kumbe, yeye Kaisari Nero ni upungufu kwani hesabu yake ni 666 ambayo ni 777 kutoa 111.
Basi, kwa kuzingatia mazingira ya kitabu cha Ufunuo namba 666 au 616 haiwezi kusimama kwa ajili ya jina lingine kama Baba Mtakatifu, Mtume Mohamed au Mussolini. Haya ni baadhi ya majina wanayolazimisha watu yafanye hesabu ya 666. Na, kwa hakika, namba hiyo haimo katika mavazi wala kofia (mitra) ya Baba Mtakatifu. Hakuna mtu yeyote anayeweza kuonesha vazi hilo au kofia hiyo kwa ushahidi. Kwani ni vazi gani au kofia ipi? Basi, kama tunautafuta uzima wa milele, aheri tuache majungu na uongo kama huu. Kama ni maandishi, ni mitra yake tu yenye herufi mbili A na W yaani alpha na omega (rejea Ufu 1:8,17).
Acha tuendelee. Wanaombambikizia Baba Mtakatifu namba 666 hudai kuikokotoa nambari hiyo katika majina matatu tofauti: jina la Kilatini VICARIUS FILII DEI (Kaimu wa Mwana wa Mungu), jina la Kigiriki LATEINOS (Mlatini) na jina la Kiebrania ROMIITH (רמיית - Mrumi). Majina hayo huhesabiwa na wanaombambikizia Baba Mtakatifu namba hiyo kama ifuatavyo:
VICARIUS FILII DEI = 5 + 1 + 100 + 0 + 0 + 1 + 5 + 0 + 0 + 1 + 50 + 1 + 1 + 500 + 0 + 1 = 666.
LATEINOS = 30 + 1 + 300 +5 + 10 + 50 + 70 + 200 = 666.
ROMIITH yaani th y y m w r = 400 + 10 + 10 + 40 + 6 + 200 = 666.
Ndugu zangu, kwa misingi halali ya kusoma Biblia hatuwezi kuyapokea majina haya bila kuyafanyia tahakiki ya kihistoria. Bila kurefusha mjadala, majina haya hayajapata kutumiwa na Baba Mtakatifu yeyote, katika historia ya Kanisa sembuse wakati wa karne ya kwanza Baada ya Kristo wakati ambao hata upapa wenyewe ulikuwa haujakua. Mapapa wa karne zile hawakuwa hatari kwa mtu yeyote. Na watu wasio hatari watapewaje majina ya kupanga na ya siri? Wale wasomaji wa kitabu cha Ufunuo wangelielewaje aya ngumu inayotaja kitu kisichojulikana kwa jina hilo? Wangelifanyaje gematria kwa kutumia majina wasiyoyajua?
Aya 13:18 ilizungumzia jina ambalo wasomaji walikuwa wakilijua kama jina la adui yao aliyekuwa akiwadhulumu na si majina ya ndoto au majungu ya karne ya 20 na 21 B.K. Zaidi ya hayo majina mengine yamelazimishwa kihesabu ili jumla ya kiherufi iwe 666. Kwa ushuhuda tazama U ilivyolazimishwa imaanishe tarakimu 5. Katika Kilatini 5 ni V na wala siyo U. Zaidi ya hayo, jina “MLATINI” kama lingelitumika wakati huo, wasomaji wangelielewa kuwataja wakoloni au askari wa kirumi ambao walikuwa wakitawala ulimwengu wa wakati ule.
Hali kadhalika, kama jina “MRUMI” lingelitumika wakati huo, wasomaji wangelielewa kuwataja wakoloni au askari wa kirumi ambao walikuwa wakitawala ulimwengu wa wakati ule. Kwa hoja hizi, majina hayo ya majungu ni ya tangu karne ya 16, Kanisa Katoliki lilipoanza kupingwa kwa ari mpya na uongozi wake kukataliwa.
Nadhani hadi hapa kila mwenye kutaka kujua anajua kwamba majina waliyobuni Wasabato hayatumiwi na Baba Mtakatifu yeyote. Na zaidi ya hayo ni majina ambayo mwandishi wa kitabu cha Ufunuo hakuwa hata na habari nayo katika karne ile ya kwanza B.K. kwa vile alivyokiandika kitabu chake kwa Kigiriki na wala si kwa Kiebrania au Kilatini. Kumbe, kwa kufanya hivyo Wasabato huwa wanainyonga historia na kukizungumzia kitabu cha Ufunuo nje ya muktadha wake wa kihistoria. Hili ni kosa la kusiganisha nyakati za kikalenda (kwa Kiingereza “anachronism”).
Basi, kwa heshima ya Maandiko Matakatifu, tutafsiri namba 666 au 616 kwa gematria asilia na tukomee hapo hapo. Tusiihamishe namba hiyo na kuwapachika watu wasio na hatia. Kufanya hivyo ni kujitowelesha majungu na ni dhambi isiyo na maana yo yote. Lakini, basi namba 666 imetolewa nje ya mazingira ya Biblia na ndipo ilipowekwa sasa. Nami nimefika hapo hapo.

Namba 666 Imehamishiwa Nje ya Biblia
Ni kituko lakini ndivyo ilivyo. Watu wengine hudai kwamba namba hiyo imeandikwa shingoni kwenye nguo za Papa. Huo ndio uongo na usingiziaji usio na aibu kwa sababu nguo hizo hakuna anayeweza kutuonesha wenziwe. Siku moja niliwahi kuambiwa na wainjilisti wawili kwamba namba 666 ipo kwenye bidhaa za siku hizi, yaani kwenye kifungashio, pale inapochorwa mistari mingi mifupi na mirefu na kuandikwa namba kwa chini, na kwa namna hiyo ipo pia kwenye satelite. Siku hiyo niliwakamata kutokujua nilipowadai wanioneshe mfano. Basi, wakaleta baadhi ya bidhaa za kisasa, wakaniambia niangalie ile mistari iliyochorwa katika kifungashio cha kila bidhaa. Hapo walionesha pia mistari miwili miwili inayojitokeza zaidi kwa chini (jambo ambalo si kweli kwa kila bidhaa). Basi, hapo ndipo walipodai kuna namba 666.
Kumbe, huu ulikuwa ujinga wao mkubwa. Ndugu yangu, mistari hiyo, ndiyo bei ya bidhaa hasa kwa zile zinazouzwa „“supermarket. Katika nchi zilizoendelea watu hawaandiki bei shilingi fulani au fulani wakabandika kwenye bidhaa. Badala yake ndiyo hiyo mistari, kadiri ilivyochorwa ndivyo mashine ya kupigia hesabu inavyotambua na kutofautisha bei za bidhaa ambazo mnunuzi amezifikisha kwenye “kaunta” ya kulipia manunuzi. Na tena bei hizo hazikuingizwa katika satelite; zilivyo nyingi hazihusishwi na satelite yoyote.
Basi, niliwaonya wainjilisti wale wasiwadanganye watu kwa kutumia ujinga wao wakati wenyewe pia hawajui mambo ya kisasa. Hatimaye, niliwaambia, kwa uongo wa namna ile, wao si wainjilisti kwani Injili ni Habari Njema ya ukombozi wetu uliotufikia kwa kifo na ufufuko wa Yesu Kristo na wala siyo namba 666 inayodaiwa kuandikwa kwenye nguo za Papa na kuingizwa kwenye satelite kwa njia ya michoro ya bidhaa za kisasa. Kwa kweli niliwaambia kwa kueneza uongo na kuwatia watu hofu kwa kuwatinga, hawakuwa mbali sana na moto wa milele kwa vile wanamtumikia Shetani aliye baba wa uongo. Hapo nikapata mwanya wa kuwaalika watubu kwa haraka. Lakini, badala ya kupokea mafundisho yangu walisema sina Roho Mtakatifu na kuondoka. Waliondoka na hawakurudi tena kwangu. Kumbe, niliwafuma katika kutokujua kwao, yaani ujinga wao. Samahani kwa simulizi hili; majadiliano yetu yaliacha kuwa ya Kikristo.

Safari Ndefu ya Kutegua Kitendawili cha Kale
Kwa vile madai ya kwamba namba 666 inamhusu Baba Mtakatifu yametutoa sote kutoka kwenye Biblia na kutupa kazi ya kumtafuta nani mwingine anaweza kuwa anatajwa na namba hiyo, nilichukua kalamu na kuanza kuchunguza maneno ya wanaotukana kama hayahusiki vile vile. Utafutaji wangu ulizaa matunda mwaka ule ule 1998. Nikategua kitendawili kwa kugundua kwamba kauli za Wasabato wenyewe zilikuwa ndiyo namba 666.

Nilifanyaje? Nilichukua kauli tatu: PONYA SIKU MUHIMU YA SABA (kwa Kiingereza CURE VITAL SEVENTH DAY, kwa Kilatini CURATUS VITALE SABBATA DIES) na WOKOVU, PONYA SIKU YA SABA (kwa Kiingereza SALVATION, CURE SEVENTH DAY, kwa Kilatini SALVUS, CURARE SABBATA DIES) na VUNJA, CHUKIA UPAPA (kwa Kiingereza DEAL AXE, VIE PAPACY). Nilistaajabu sana kuona ndiyo inakuja 666 ndipo mara moja nikaingiza ugunduzi wangu katika kitabu changu KISA CHA IMANI namba 1.

Ni kweli. Kauli mbiu za Wasabato ni namba hiyo hiyo 666. Angalia gematria inavyokwenda:
CURE VITAL SEVENTH DAY = 100 + 5 + 0 + 0 + 5 + 1+ 0 + 0 + 50 + 0 + 0 + 5 + 0 + 0 + 0 + 0 + 500 + 0 + 0 = 666
CURATUS VITALE SABBATA DIES = 100 + 5 + 0 + 0 + 0 + 5 + 0 + 5 + 1 + 0 + 0 + 50 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 500 + 1 + 0 + 0 = 666
SALVATION, CURE SEVENTH DAY = 0 + 0 + 50 + 5 + 0 + 0 + 1 + 0 + 0 + 100 + 5 + 0 + 0 + 0 + 0 + 5 + 0 + 0 + 0 + 0 + 500 + 0 + 0 = 666
SALVUS, CURARE SABBATA DIES = 0 + 0 + 50 + 5 + 5 + 0 + 100 + 5 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 500 + 1 + 0 + 0 = 666
DEAL AXE VIE PAPACY = 500 + 0 + 0 + 50 + 0 + 1 0 + 0 + 5 + 1 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 100 + 0 = 666

Kuendelea Kutafuta
Basi, kwa kuwa nilikuwa namtafuta nani mwingine anayesemwa na namba 666 au 616, nikagundua kumbe ni hao hao wanaotukana. Lakini, sikukomea hapo mwaka huu 2017 macho yangu yakasaidiwa kuona zaidi. Nilichukua jina la mwasisi wa matusi mwenyewe ELLEN GOULD WHITE ndipo nikashtuka kabisa kumbe ni namba 666. Kwa kisa hiki, leo nawaomba tuimbe alleluya pamoja.

ALLELUYA! KUMBE NAMBA 666 NI ELLEN GOULD WHITE MWENYEWE
Sasa nawapeni habari njema kabisa. Tusi la namba 666 limefumbua macho yangu kwa namna ya ajabu na sasa nawatangazia wote nilichokigundua ili kiwafumbue macho ninyi pia. Kifupi, nimefikishwa kwenye ugunduzi huo kwa kupitia tahadhari ya wahenga. Wao walisema, “Unapokula na kipofu, usimguse kipofu mkono!” Msidanganyike tena, namba 666 ni ELLEN GOULD WHITE mwenyewe.

Nawasimulieni. Kwa kuzidi kutukana, niliwatazama watukanaji nione kama matusi hayawahusu wenyewe. Nikagundua kumbe ndiyo hivyo hivyo. Kumbe, wakati mwingine heri utukanwe maana waweza kufunguliwa mlango kwa jambo jema fulani. Basi, natangaza kadamnasi kwamba tusi la namba 666 limekuwa tusi la neema na heri sana kwetu Wakatoliki, tulionyanyasika kwalo kwa muda mrefu. Linawahusu wanaotutukana hao hao. Kumbe, walikuwa wanapiga kelele za “Mwizi, mwizi!“ ili kutupoteza maboya tu. Wezi ni wenyewe.

Tuamke. Jamani, Bi Ellen Gould White alikuwa anapiga kelele na kutukana kusudi tusishughulike na jina lake. Wafuasi wake wakadakia mbinu hiyo hiyo. Kumbe, Wasabato hukazania namba 666 imwelekee Baba Mtakatifu kwa sababu walitaka tusijue kwamba namba 666 inamwelekea “nabii” wao ELLEN GOULD WHITE! Walitaka tukamsake sungura katika kichaka kingine. Kumbe, Ufu 13:18 inamtaja Bi Ellen White moja kwa moja kama mnyama ambaye jina lake ukilikokotoa linakuja moja kwa moja kwenye namba 666. Yaani linakuja 666 taslimu!
Je, unaniuliza kwa vipi? Ni hivi ifuatavyo. Ukiliandika jina la Bi ELLEN WHITE pamoja na jina la asili yake GOULD unakuja kwenye namba 666 juu ya alama. Nifuatilie vyema hapa kusudi tukokotoe tarakimu pamoja. Lakini, angalia vyema, jambo lile la kuhitajika hekima, linahusisha pia kuirudisha “W” ya WHITE kwenye uasilia wake yaani V maradufu (kwa Kiingereza “double v”). Kwa taarifa yako, tangu kale “W” ni “V” mbili na ni kwa sababu ya asili hiyo Wajerumani huitamka “W” kama “V”. Umeshanielewa uzuri? Kama umeshanielewa, sasa tazama “gematria“ inavyokubali:
E L L E N G O U L D W H I T E
0+ 50 + 50 + 0 + 0 + 0 + 0 + 5 + 50 + 500+ 10+0+1+0+0 = 666

Je, unaona jinsi jina la Bi Ellen White linavyokubali kama jina la mnyama yule? Yaani sawa sawa pasipo kuacha mashaka yoyote. Kinyume chake, jiulize ni Baba Mtakatifu gani mwenye jina kama hilo? Maskini, Wasabato walisahau jambo hili la kimahesabu! Lakini nadhani wanalifahamu na ndiyo maana hufanya juhudi kubwa kulikoneshea tusi la namba 666 kwa Baba Mtakatifu. Ni janja yao lakini sasa ipo hadharani.
Narudia. Wanachofanya Wasabato ni mbinu ya kawaida tu, yaani kwamba ukitaka watu wasikuangalie wewe elekeza umakini wao kwa mtu mwingine au kitu tofauti. Ndipo, badala ya watu kuelekeza umakini kwenye jina “ELLEN GOULD WHITE” huzugwa waelekeze kwenye majina ya kubuni ya “VICARIUS FILII DEI”, “LATEINOS” na “ROMIITH”, majina yasiyo na maana yoyote kihistoria na muktadha wa kitabu cha Ufunuo.
Je, umeona eh! Kumbe, mambo yako kwenye majina “ELLEN GOULD WHITE”. Namba 666 inakubali taslimu kabisa. Chukua hii!

Hatima
Naona imetosha, nanyi, bila shaka, mnaniambia kwa Kiingereza “Stop, it is enough and clear!” kwa maana ya “Acha inatosha na imeeleweka!” Alamsiki!

Pd Titus Amigu
AHSANTE KAKA
TUNASHUKURU SANA
ILA USHAURI WANGU,
NAKUOMBA HIYO POST YAKO, IWEKE KAMA MADA (UZI)
NA ATAKAYEULIZA MASWALI TUTAKUSAIDIA KUMPA MAJIBU, USIGOPE

mimi nilijaribu kuelezea vyema hapa ndani kuhusu 666, lakini nimeona yangu ilikuwa ni fupi sana, ila hayo maelezo ulioleta ni kiboko nimeyependa na naona yamejitosheleza na yanakata kiu ya maswali kabisa

MUNGU AKUBARIKI
 
Kipofu akimwongoza kipofu mwenzie wote hutumbukia shimoni
 
Kabla ya huo mwaka 476AD tayari utawala wa kirumi ulikuwa umegawanyika sehemu kumi (pembe kumi zinazotajwa katika ufunuo na daniel 7). Hayo ndiyo mataifa ya ulaya sasa, yote ilikuwa dola ya rumi. Baadae, ndipo papa alipoamua kuyafutilia mbali mataifa matatu yaliyokataa kumtii ambayo ni heruli, vandals na ostrogoths. Hapo ndipo unabii wa Daniel 7 ulitimia hapo aliposema na tazama pembe ndogo iliziangusha pembe tatu. Hii pembe ndogo inayozuka kati ya pembe kumi katika Daniel sura ya saba, ndio upapa ulioibuka katikati ya rumi iliyogawanyika katika falme kumi za ulaya ya sasa.

Kwa hoja hizi papa ndiye mpinga Kristo jiepusheni naye.
Umekuja na majibu rahisi kwa hoja nyepesi!
Ngoja nikujibu hivi ifuatavyo:
1) utawala wa rumi
Utawala wa rumi mpka unaanguka mwaka 476AD kwa (western empire) na mwaka 1400AD kwa Eastern empire haukuwahi na kuwa na papa kama kiongozi wa kidini na kiserikali(kama unabisha leta facts). Iko hivi wakati mfalme Costantine anaruhusu ukristu kuwa dini ya serikali ya rumi mwaka wa 303BK hakukuwa na upapa wala ukristu hapo kwanza!aliporuhusu ndipo akatangaza na jumapili kama siku ya mapumzko sababu kanisa au wakristo walikua wakisali siku hyo(kama wabisha leta facts). Baada ya kufa kwake serikali ya rumi iliendelea kuzorota kufuatia civil wars na uroho wa madaraka mpaka kupelekea kugawanyika kwa west na east. Western empire ikawa na italia,hispania na part za ufaransa wakati eastern ikawa na nchi za ugiriki,uturuki na nyngne za mashariki ya kati hadi Yerusalem,kumbuka pia katika kipind chote kulkua na emperor(kiongozi wa serikali) pamoja na askofu aliyekua akichaguliwa na huyo emperor au mfalme ndan ya eneo lake.katika upande wa dini,western wakawa na papa ambaye ni mkuu wa maaskofu na pia akiwa askofu wa roma wakati eastern wakawa na patriarch kma kiongozi wa maaskofu mahalia. Upapa ulikua na kuanzia mwaka wa 500-1303 papa alikua na mamlaka ya kiserikali na kidini akiongoza na kuchagua wafalme kwa ufaransa,spain na roma!mwaka 1303 mfalme wa ufaransa alikataa kutii mamlaka ya papa na kuangusha upapa,kwahyo tokea hapo mfalme wa roma akabaki mtawala na papa akabaki kidini tu mpaka alipoingia makubaliano na serikali ya itali kuhama na kuwa mtawala wa vatican(kama wapinga njoo na facts) mwaka 1929. Hakuna kipindi sasa papa alitawala dunia mana hata kwa western tu hakufika alipokuepo patriach. Kwa kukupa tu maarifa atizame papal state. Sijui hzo falme tatu alizofuta umetoa wap.
Tuje katika hoja ya papa kuwa mpinga kristu...labda nikupe sifa za mpinga kristu toka katika biblia afu utapata jibu mwenyewe.
Biblia inasema mpinga kristu ni nan?
1Yohana2:22-1 John 2:22
Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye mpinga Kristo, yeye amkanaye Baba na Mwana.
Sasa labda unaweza ukataja ni papa yupi mwongo na ambaye ameleta mafundsho ya kumkataa baba na mwana kama mstari usemavyo hapo juu?waweza kumtaja?
Tuangalie pia 1yohana4:2-3
1 John 4:2-3
[2]Hereby know ye the Spirit of God: Every spirit that confesseth that Jesus Christ is come in the flesh is of God:
Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu.
[3]And every spirit that confesseth not that Jesus Christ is come in the flesh is not of God: and this is that spirit of antichrist, whereof ye have heard that it should come; and even now already is it in the world.
Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.
Je kuna papa au kanisa katoliki ambalo halimkiri Kristo mana maandiko juu hapo yasema hiyo ndio roho ya mpinga kristo na imeshakua tyr duniani(ni roho lakini yeye bado hajaja) kma ni roho basi hatuwez sema ni papa au ni RC mana hawa wamkiri Kristu.
Tizama pia hapa 2wathesalonike 2:1-4,7-10
2 Thessalonians 2:3-4,7-10
[3]Let no man deceive you by any means: for that day shall not come, except there come a falling away first, and that man of sin be revealed, the son of perdition;
Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu;
[4]Who opposeth and exalteth himself above all that is called God, or that is worshipped; so that he as God sitteth in the temple of God, shewing himself that he is God.
yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.
[7]For the mystery of iniquity doth already work: only he who now letteth will let, until he be taken out of the way.
Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.
[8]And then shall that Wicked be revealed, whom the Lord shall consume with the spirit of his mouth, and shall destroy with the brightness of his coming:
Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake;
[9]Even him, whose coming is after the working of Satan with all power and signs and lying wonders,
yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo;
[10]And with all deceivableness of unrighteousness in them that perish; because they received not the love of the truth, that they might be saved.
na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.
Haya kutokana na mistari hapo juu bado tu uko na papa?(labda kma una kingine)
Mathayo 24 inaelezea mwshocwa dunia ambapo huyo mpinga kristu atakuja kusimama ndan ya hekaru la tatu na kunena makufuru akiwadanganya watu kua ndiye masihi(chukizo la uharibifu). Hili hekaru la tatu halijajengwa(limetabiriwa katika ezekieli 42&43).
Niishie hapa na kuhifadhi mengine ili utakapojileta nkufunze zaid
 
Back
Top Bottom