Achana na pembe ndogo maana huko utashindwa hoja asubuhi sana.Pia maandiko haya uliyoyanukuu nilikuwa namjibu huyo ndugu wala hayahusiani na kukujibu wewe hivyo achana nayo.....
Unataka tena kwenda kwenye vilima saba,hapa nimecheka sana.nimecheka kwasababu wewe unasema kitu tofauti kabisa na maandiko....
Maandiko yanasema vilima saba ni wafalme saba na wewe unasema ni vilima kama mlima Meru kwa kusema eti Vatican imezungukwa na vilima saba,unaandika mambo yaliyo kinyume kabisa na maandiko halafu unasema umethibitisha,umethibiotisha unayofundishwa kwenye dhehebu lako labda.....
Malizana na hoja ya mwanamke kwanza huku tutafika tu na hutaweza kujitetea popote....
Unaendelea tu kujichanganya kuwa mwanamke ni Kanisa mara Vatican wakati mwanamke kwenye huu unabii ana maana MOJA tu na ni MJI,hiyo ya kanisa haina back up yoyote ya unabii huu....
uwe unaweka MAANDIKO sio kuropoka tu,
Ngoja nikuoneshe mfano , hii ni INTRODUCTION
Ndio maana andiko linasema : "Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI".
UFUNUO 17 : 5
Unaona hapo juu kwenye fungu, yani jina BABELI NI LA SIRI, hii ikimaanisha, Babeli hii itafanya kazi kwa namna ya kujificha na kutotaka ijulikane kuwa ndio Babeli yenyewe.
HEBU TUISOME KWANZA KATIKA MAANDIKO TUONE BIBLIA INACHOTUAMBIA KUHUSU BABELI HUYO MKUU NA MAMA WA MAKAHABA.
"Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;
2 ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake.
3 Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.
4 Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.
5 Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.
6 Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu.
UFUNUO 17 : 1 - 6
Hapo tunaona Yesu akimfunulia mtumishi wake Yohana juu ya ujio mpya wa BABELI duniani. Haya matukio Yohana alifunuliwa kama matukio yaliyo mbele, yani yajayo baada ya siku zake. Yesu alifunua kuwa itaibuka tena BABELI lakini kwa sura tofauti kabisa na Babeli ile iliyozoeleka.
Kwa kutumia lugha ya mafumbo Yesu anamfunua BABELI huyo mkuu na MAMA WA MAKAHABA.
Sasa tunataka tumjue KAHABA HUYU MKUU NA AMBAYE NI MAMA WA MAKAHABA PIA, AITWAYE BABELI MKUU NI NANI?
Kwa kuwa haya ni mafumbo ya kimbingu, hatupaswi kujaribu kuyafumbua kibinadamu, tutaliacha Neno la Mungu litufunulie BABELI HUYU MKUU NA MAMA WA MAKAHABA ni nani?
BABELI MKUU MAMA WA MAKAHABA NI NANI AU NI NINI?
Biblia inamfunua..
1. Kwanza tunaona BABELI MKUU huyu ameonyeshwa kuwa ni mwanamke, maana anaitwa "mama" sote tunaelewa sifa ya mama ni ya jinsi ya kike.
Je, kwa mujibu wa Biblia mwanamke hutumika kuwakilisha nini anapotumika kama kielelezo?
- Katika Biblia "mwanamke" hutumika kuwakilisha "JAMII YA WATU WA MUNGU" ambao katika agano la kale watu hao walikuwa ni taifa la "ISRAELI"
Tunaona katika Hosea Mungu akiongea na watu wake kama aongeae na mwanamke
Nami nitakuposa uwe wangu kwa milele; naam, nitakuposa kwa haki, na kwa hukumu, na kwa ufadhili, na kwa rehema.
HOSEA 2 : 19
"Rudini, enyi watoto wenye kuasi, asema BWANA; maana mimi ni mume wenu; nami nitatwaa mtu mmoja wa mji mmoja, na wawili wa jamaa moja, nami nitawaleta hata Sayuni;
YEREMIA 3 : 14.
Katika zama za agani jipya, ambapo hakuna tofauti tena kati ya Myahudi na asiye Myahudi, mwanamke anawakilisha watu wa Mungu kwa maana ya "KANISA"
Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.
2 KORINTHO 11 : 2
Kwa sababu BABELI MKUU atatokea wakati wa Agano jipya, basi BABELI huyo ATAJITOJEZA KATIKA SURA YA KANISA!
Tumejua sasa KAHABA MKUU ni kanisa kumbe.
Tuendelee...,
KWA MAANA HIYO KUMBE, KATIKA KUMSEMA BABELI MKUU YESU ALIKUWA AKIFUNUA KUHUSU KUTOKEA KWA KANISA FULANI KATIKA SIKU ZA BAADAE TOKA KATIKA SIKU HIZO ZA YOHANA WA PATMO.
2. MWANAMKE HUYO BABELI MKUU ANAONEKANA ANA SIFA YA ZIADA MBALI YA UANAMKE WAKE, ANA SIFA YA "UKAHABA"
Hii maana yake ni nini?
Katika Maandiko, mahusiano baina ya Mungu na watu wake yamefananishwa na "MAHUSIANO YA NDOA"
rejea Yeremia 3 : 14, na 2 Wakorintho 11 : 2.
Yani kanisa ni mke wa Kristo, kwa maana hiyo UKAHABA NI TENDO LA KANISA KUTOKUWA NA UAMINIFU KWA KRISTO.
Hapo tunaona KANISA HILO (Babeli mkuu) litakuwa ni kanisa lisilo na uaminifu kwa KRISTO, yani litakuwa na mabwana wengine, na waume wengine tofauti na Kristo
Lakini pia katika Hosea 3 : 1 inaonyesha UKAHABA WA WATU WA MUNGU NI KUABUDU MIUNGU WENGINE, TOFAUTI NA MUNGU WAO.
Hivyo kanisa hilo litakuwa linachanganya ibada ya Mungu Muumbaji, na ibada za miungu wengine, HUO NDIO UKAHABA WA KANISA HILO.
BABELI MKUU ALIKUWA AMEKETI JUU YA MAJI MENGI.
Maji mengi ni nini?
"Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha".
UFUNUO 17 : 5
Hii inaonyesha kuwa kanisa hilo, litasambaa dunia nzima, kwenye kila makutano, kila kabila, kila lugha na kila jamaa litakuwepo.
Lakini pia, inaonyesha kanisa hili, litakuwa ni kanisa la WATU WENGI, litakuwa ni kanisa kubwa na lenye kila aina ya watu ndani yake, kwa idadi kubwa sana.
3. BABELI MKUU (kanisa) ALIKUWA AMEPANDA MNYAMA.
Mnyama anapotumika kama kielelezo huwakilisha "FALME au TAWALA.
Soma Daniel 7 : 17 na Daniel 7 : 23
"Wanyama hao wakubwa walio wanne ni wafalme wanne watakaotokea dunian".
DANIEL 7 : 17.
Kama ambavyo mtoto aliyebebwa anavyomtegemea aliyembeba, ndivyo kanisa hilo (BABELI MKUU). litakavyokuwa linategemezwa na serikali za kidunia. Nguvu zake, ustawi wake utatokana na kusaidiwa na mataifa au serikali za kidunia.
4. BABELI MKUU (kanisa) ATAZINI NA WAFALME.
Hii ina maana sawa na kubebwa juu ya mnyama, lakini imeongeza uzito wa kitendo chenyewe, neno KUZINI ina maana kanisa hilo litajitegemeza kwa wafalme wa dunia na kushikamana nao, kana kwamba wao ndio wenye kanisa. Nafasi ya Kristo itaondolewa na kama matokeo ya Kristo kwa kanisa hilo itatwaliwa na wafalme hao.
5. BABELI MKUU (kanisa) AMEWALEVYA WAKAAO JUU YA NCHI KWA MVINYO WA UASHERATI WAKE.
Kwanza kabisa tuliona UASHERATI WA KANISA HILO NI KUTANGA MBALI NA KRISTO, PIA KUABUDU VINGINE VISVYO MUNGU MUUMBAJI.
Sasa hapa twafunuliwa kuwa, KANISA HILO LITAWAAMBUKIZA WALIMWENGU UASHERATI WAKE, KWA NJIA YA MAFUNDISHO YA UONGO.
MAFUNDISHO YA UONGO ndio mvinyo wa uasherati wake. Watu wataabudishwa ibada zisizokubalika kimaandiko na kanisa hilo, watu watapiga magoti mbele ya miungu ya kigeni kwa maelekezo ya kanisa hilo.
Kulewa ni kuondolewa utambuzi, jambo ambalo ukiwa na akili timamu huwezi kukubali kulifanya, ukilewa unalifanya vzr tu.
Ndivyo itakavyokuwa kwa watu hao, kama wasingenyweshwa (wasingedanganywa) mvinyo (mafundisho ya uongo) wangetambua kuwa ibada hizo ni batili na hazikubaliki.
Lakini akili hiyo ya utamuzi imeondolewa na mvinyo huo wa uasherati wa kanisa hilo.
Na Biblia inathibitisha kuwa MAFUNDISHO YA UONGO YANALEVYA, Isaya 29 : 9, 10
6. ALIKUWA NA MAJINA YA MAKUFULU KATIKA KICHWA CHAKE.
Zingatia majina hayo hayakuwa mguuni, tumboni wala mgongoni, bali yalikuwa kichwani..,
Hii maana yake ni kuwa VIONGOZI WA KANISA HILO WATAJIPA MAJINA YANAYOMSTAHILI MUNGU.
7.BABELI MKUU ALIKUWA AMEVAA NGUO YA ZAMBARAU NA NYEKUNDU.
Hii nguo maana yake nini?
Tunaposoma maandiko, tunaona RANGI NYEKUNDU MAANA YAKE NI DHAMBI, Soma Isaya 1 : 18
"Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
ISAYA 1 : 18
Katika BIBLIA za lugha zingine mfano Biblia ya lugha ya kinyarwanda, imetaja kabisa na rangi ya zambarau pia katika fungu hilo la ISAYA.
Hivyo mavazi hayo yanaonyesha DHAMBI za kanisa. Litakuwa ni kanisa linalounga mkono dhambi, litakuwa ni kanisa ambalo lenyewe limeifanya dhambi kuwa ndio kanuni yake ya utendaji.
8. BABELI MKUU AMEPAMBWA KWA VITO, NA LULU
Hii inamaanisha nini?
Hizi, ni ishara za utajiri!
Kanisa hilo, litakuwa ni kanisa tajiri mno, lenye kuonekana wazi kwa utajiri wake, sawa na mapambo ya mwanamke yanavyoonekana wazi.
Litakuwa ni kanisa tajiri sana!
9.KIKOMBE CHA DHAHABU KILICHOJAA MACHUKIZO.
hii ina maanisha nini?
Dhahabu inaonyesha UPENDO., hili litakuwa ni kanisa ambalo litaonekana kuwa na matendo ya upendo.
Lakini kama ambavyo kikombe hicho cha dhahabu ndani kilivyokuwa na machukizo, kadhalika ndani ya hayo yatakayoonekana ni matendo ya Upendo kutakuwa na hila ya kuwaingiza watu katika kufanya MACHUKIZO dhidi ya Mungu.
10.AMELEWA KWA DAMU YA WATAKATIFU
Hii maana yake ni nini?
Kanisa hilo litawaua watu wa Mungu. Litamwaga damu ya watu ambao watakataa kushiriki uchafu wake.
11. Ana jina la siri "BABELI MKUU MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.
Hii inamaanisha nini?
Kwanza tunaona hilo ni jina la siri, jina ambalo hakutaka lifahamike. Ndio maana akaja kwa sura ya mwanamke, yani alitaka afahamike kama mwanamke, kumbe hasa si mwanamke bali ni BABELI MKUU!
umeelewa mchezo?
Tuonane katika sehemu inayofuata kwa ufafanuzi wa mbinu hiyo ya kuficha jina, kuna mambo ya muhimu na nyeti sana tupaswayo kuyafahamu
YHWH IS GOOD