Mfahamu kahaba mkuu wa Ufunuo 17

Mfahamu kahaba mkuu wa Ufunuo 17

Kwanini usipinge hoja au hii mada kwa kukanusha na ukaeleza mstari kwa mstari kahaba mkuu ni nani?? Kuliko kubwabwaja tu
Hii fasiri yenu ya huu unabii ina matatizo mengi sana....

Kahaba wa ufunuo 17 siyo kanisa maana malaika alishamueleza Yohana mwanamke huyo ni nani na sijui ni kwanini huwa mnang'ang'ania ni kanisa....

Soma Ufunuo 17:18 utaona huyo kahaba ametajwa kuwa ni nani....

Kama hapa tu ambako ni msingi wa unabii wako ni makosa unabii mzima na mengine yote uliyoandika hapa yanakosa maana....

Sent from my TECNO P5 using JamiiForums mobile app
 
Aroon acha kupotosha, kila mtu ana sababu za kuabudu anapoabudu, wote twamuabudu Mungu. Na ikumbukwe sio dini itakayompeleka mtu mbinguni, matendo,...ndo jambo LA msingi zaid.

Sent from my TECNO-N8 using JamiiForums mobile app
Leta sapoti ya maneno yako kwa biblia
 
Hii fasiri yenu ya huu unabii ina matatizo mengi sana....

Kahaba wa ufunuo 17 siyo kanisa maana malaika alishamueleza Yohana mwanamke huyo ni nani na sijui ni kwanini huwa mnang'ang'ania ni kanisa....

Soma Ufunuo 17:18 utaona huyo kahaba ametajwa kuwa ni nani....

Kama hapa tu ambako ni msingi wa unabii wako ni makosa unabii mzima na mengine yote uliyoandika hapa yanakosa maana....

Sent from my TECNO P5 using JamiiForums mobile app
Acha kudanganya , kama sio kanisa maana mm nimefafanua. Sasa sema ni nani huyo kahaba mkuu

Na uanze kuonyesha aya kwa aya kuhusu huyo kahaba ktk ufunuo 17 ilivyotimia

Kama sijakushika uongo

Ndio maana unaishia juu juu tu
 
Wewe ni wa ajabu kweli kweli..

Hoja yako unaijenga kwenye msingi wenye makosa sana.Ninasema hivyo kwasababu unapomuuliza mtu "onesha namna huo unabii ulivyotimia" unakuwa unadhani kila mtu anafikiria kama wewe kuwa unabii umetimia wakati kuna watu wengi tu wanaamini huo unabii haujatimia lakini tayari maandiko yameshatoa fasiri ya mwanamke kwenye huo unabii ni nani....

Nimekuwekea hapo mstari wa kwenye biblia bado unajidai hujauona,ngoja sasa nikuwekee na maandishi kabisa....

Ufunuo 17:18
18 Na yule mwanamke uliyemwona, ni mji ule mkubwa, wenye ufalme juu ya wafalme wa nchi.

Hapo kwenye bold na nyekundi ni jibu la swali lako,sasa hangaika na maadniko uyabishie maana yameshaweka wazi kabisa....

Maandiko yanasema mwanamke ni MJI wewe unasema ni kanisa,sijui ni kwanini huwa mnaparuka hapo....
 
Povu

Lazima dawa iwaingie enyi waabudu sanamu
Sasa ndugu jione hata aibu...uzi ni wako ila umekosa support ya Wasabato wenzako...kifupi uzi ni wakwetu sisi....yani sindano umeileta ila tumekuchoma sisi....na tutaendelea kukuchoma...
 
Kaka mkuu ndio maana nilikuuliza sababu hizi tafsiri za 'mnyama' naona ni nyingi sana
Halafu tatizo ni pale Bible inaposema kuwa ni MJI na baadhi yetu tunasema ni Kanisa[emoji23][emoji23] sababu ndivyo Watu walivyofundishwa na hawataki kujiongeza
Sasa mtu/watu kama hao itakuchukulia muda wako mwingi kumuelewesha sababu huyu amefundishwa tangu utotoni mpaka kakua anajua lile kanisa ndio MJI sasa kumtoa katika hicho alichofundishwa to tje truth side is not gonna be a ONE DAY JOB sababu huyu mtu amejifunza kwa miaka mingi

Sent from my HUAWEI SCL-L01 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu

Unajua kuna wakati huwa ninashangaa sana tena sana haya masuala namna watu wanavyoyachukulia maana wanayachukulia kwa namna ya kustaajabisha sana....

Huu unabii kwa mfano ni unabii ambao unaonekana kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele unazidi kuwatoa watu kamasi na mojawapo wa watu ni hawa wanaouhusisha unabii huu na kanisa Katoliki....

Ukiangalia kuanzia Danieli na vitabu vyote vya unabii hadi kuja kwa Ufunuo ushahidi unaonesha kabisa kuwa kinachosemwa hapo siyo kanisa wa na kundi lolote la kiimani bali ni kitu kingine kabisa....

Hawa wanaosema ni kanisa wamekuwa waking'ang'ania kwamba tafsiri ya mwanamke kiunabii ni mwanamke,wanaweza kuwa sahihi lakini siyo kwenye kila unabii maana Mungu anaweza akatumia mwanamke kwenye nabii tofauti tofauti na asimaanishe kitu kile kile na mfano hai ni huu unabii wa Ufunuo.....

Hapa amemtaja mwanamke lakini hapa hajamaanisha kanisa na amesema anamaanisha nini.Ukiusoma huu unabii utaona kabisa kuwa unalenga mamlaka ya kisiasa kwa asilimia 100 na siyo mchanganyiko wa siasa na dini au dini kama hawa ndugu wanavyodai....

Maandiko yako wazi kabisa na yamesema mnyama ni nani,vichwa ni nani,pembe ni nani na pia mwanamke ni nani,kwanini tuache kile ambacho maandiko yanasema halafu tufuate mtu anavyosema?

Moja ya maajabu ni hili la watu kulazimisha mawazo yao huku wakiyaacha maandiko....

Mkuu,wengi hawajui ni kwanini Mungu ameuita mji huo Babeli,hawajui Babeli ilikuwaje hadi Mungu akauita mji huo Babeli.Babeli ulikuwa ni mji kama ambavyo future Babeli itakavyokuwa na kuna sababu za msingi kabisa ambazo zilimfanya Mungu akauita mji huo kwa jina hilo lakini watu hawaelewi kabisa jambo hili....

Nisiandike mengi sana lakini haya mambo wengi wanayakurupukia na matokeo yake ni haya.Huwa nikisoma naishia kusikitika tu mkuu.....
 
Wewe ni wa ajabu kweli kweli..

Hoja yako unaijenga kwenye msingi wenye makosa sana.Ninasema hivyo kwasababu unapomuuliza mtu "onesha namna huo unabii ulivyotimia" unakuwa unadhani kila mtu anafikiria kama wewe kuwa unabii umetimia wakati kuna watu wengi tu wanaamini huo unabii haujatimia lakini tayari maandiko yameshatoa fasiri ya mwanamke kwenye huo unabii ni nani....

Nimekuwekea hapo mstari wa kwenye biblia bado unajidai hujauona,ngoja sasa nikuwekee na maandishi kabisa....

Ufunuo 17:18
18 Na yule mwanamke uliyemwona, ni mji ule mkubwa, wenye ufalme juu ya wafalme wa nchi.

Hapo kwenye bold na nyekundi ni jibu la swali lako,sasa hangaika na maadniko uyabishie maana yameshaweka wazi kabisa....

Maandiko yanasema mwanamke ni MJI wewe unasema ni kanisa,sijui ni kwanini huwa mnaparuka hapo....
Huwezi kukomaa na kamstari kamoja tu

Huo mji mkubwa ni Vatican

Na hiyo mistari ya ufunuo 17:1-17

Inamuelezea huyo mwanamke ambaye biblia inamtafsir ni kanisa

Sasa jiulize

Hapo vatican kuna kanisa gani

NA NDIO MAANA NIMEKUOMBA UJENGE HOJA AYA KWA AYA

Sasa unakimbilia aya moja ,unaacha aya 16

Upo seriously kweli wewe!

YHWH IS GOOD
 
Mkuu

Unajua kuna wakati huwa ninashangaa sana tena sana haya masuala namna watu wanavyoyachukulia maana wanayachukulia kwa namna ya kustaajabisha sana....

Huu unabii kwa mfano ni unabii ambao unaonekana kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele unazidi kuwatoa watu kamasi na mojawapo wa watu ni hawa wanaouhusisha unabii huu na kanisa Katoliki....

Ukiangalia kuanzia Danieli na vitabu vyote vya unabii hadi kuja kwa Ufunuo ushahidi unaonesha kabisa kuwa kinachosemwa hapo siyo kanisa wa na kundi lolote la kiimani bali ni kitu kingine kabisa....

Hawa wanaosema ni kanisa wamekuwa waking'ang'ania kwamba tafsiri ya mwanamke kiunabii ni mwanamke,wanaweza kuwa sahihi lakini siyo kwenye kila unabii maana Mungu anaweza akatumia mwanamke kwenye nabii tofauti tofauti na asimaanishe kitu kile kile na mfano hai ni huu unabii wa Ufunuo.....

Hapa amemtaja mwanamke lakini hapa hajamaanisha kanisa na amesema anamaanisha nini.Ukiusoma huu unabii utaona kabisa kuwa unalenga mamlaka ya kisiasa kwa asilimia 100 na siyo mchanganyiko wa siasa na dini au dini kama hawa ndugu wanavyodai....

Maandiko yako wazi kabisa na yamesema mnyama ni nani,vichwa ni nani,pembe ni nani na pia mwanamke ni nani,kwanini tuache kile ambacho maandiko yanasema halafu tufuate mtu anavyosema?

Moja ya maajabu ni hili la watu kulazimisha mawazo yao huku wakiyaacha maandiko....

Mkuu,wengi hawajui ni kwanini Mungu ameuita mji huo Babeli,hawajui Babeli ilikuwaje hadi Mungu akauita mji huo Babeli.Babeli ulikuwa ni mji kama ambavyo future Babeli itakavyokuwa na kuna sababu za msingi kabisa ambazo zilimfanya Mungu akauita mji huo kwa jina hilo lakini watu hawaelewi kabisa jambo hili....

Nisiandike mengi sana lakini haya mambo wengi wanayakurupukia na matokeo yake ni haya.Huwa nikisoma naishia kusikitika tu mkuu.....
Mbona unajitia mjuaji

Kwanini usipinge hoja zangu kwa maandiko

Toka karne ya 15 kina john huss

Martin luther, knox, sir isack newton walisema wazi wazi UFUNUO 13,. 17 , PEMBE NDOGO INALIHUSU KANISA KATOLIKI DHAHIRI

SASA WEW UNAPINGA BILA ANY EVIDENCE

HUSEMI HIYO PEMBE NDOGO AU HUYO KAHABA MKUU NI NANI

umebaki kulalamika tu

Sema ni nani, nianze aya moja moja unithibitishie inahusika vipi

MBONA MIMI NIMEKUONESHA KAHABA MKUU WA UF 17 NI KANISA KATOLIKI

TENA NIMETHIBITISHA AYA KWA AYA

unakimbilia aya ya 18

Huo mji ni VATICAN tena biblia inasema katika hiyo sura HUO MJI UPO KTK VILIMA 7 na ndio anakalia huyo mwanamke

Bado tu hufunguki?

Hujui ROMA VATICAN IMEZUNGUKWA NA VILIMA 7 ?

Au nikutajie kwa majina?

haya NJOO NA POROJO ZAKO

YHWH IS GOOD
 
Huwezi kukomaa na kamstari kamoja tu

Huo mji mkubwa ni Vatican

Na hiyo mistari ya ufunuo 17:1-17

Inamuelezea huyo mwanamke ambaye biblia inamtafsir ni kanisa

Sasa jiulize

Hapo vatican kuna kanisa gani

NA NDIO MAANA NIMEKUOMBA UJENGE HOJA AYA KWA AYA

Sasa unakimbilia aya moja ,unaacha aya 16

Upo seriously kweli wewe!

YHWH IS GOOD
Umeanza kwa kusema kuwa huo mji ni Vatican lakini baadaye unasema yule mwanamke ni kanisa,hili ni kosa la kwanza,ni kwanini nasema ni kosa?

Ni kwasababu kwenye unabii huu mwanamke hana fasiri mbili,anayo moja tu ambayo maandiko yamesema ni MJI na wala siyo kanisa.Kwa maana hii either useme ni kanisa au useme ni Mji maana haiwezekani iwe vyote viwili.Kwa lugha nyingine tunasema umejichanganya tena vibaya sana.....

Umejichanganya kwasababu unatamani ukubaliane na maandiko lakini hapo hapo unatamani ukubaliane na maelekezo ya dhehebu lako.Huwezi kupanda farasi wawili,ni lazima utaanguka tu.....

Hoja yako ya pili umesema nasimamia mstari mmoja halafu naacha mistari mingine 16.Hoja hii haina mashiko na nitakueleza ni kwanini....

1;Mistari mingine 16 inaelezea mwanamke ni nani na alifanya na anendelea kufanya nini pamoja na mnyama huyo na mistari hiyo haielezei maana ya mwanamke hivyo haina msaada kwenye hiki tunachokijadili hapa......

2;Hoja kubwa ambayo mimi na wewe tunaijadili hapa ni maana ya mwanamke kwenye unabii huu,mstari wa 18 kwenye hiyo Ufunuo 17 ndiyo inatupa jibu la mwanamke ni nani ni kwanini tuhangaike na mistari mingine ambayo kimsingi haina jibu?

Binafsi ungesema hata tusome Ufunuo 18 ningeweza kukuelewa maana kule kunaelezwa atakachofanywa mwanamke huyu na kinasimuliwa kwa matukio ambayo moja kwa moja yanaweza kukuonesha ni nani....

Ufunuo 18 ndiyo inamaliza kabisa ubishi maana inaelezea namna MJI huo utakavyoangamizwa na hiyo inaonekana wazi kabisa,suala la mwanamke kuwa ni kanisa halina mashiko hata kidogo maana halina back up ya maandiko popote....

Kwa maana hii mwanamke ni mji wala siyo kanisa.....
 
Sasa ndugu jione hata aibu...uzi ni wako ila umekosa support ya Wasabato wenzako...kifupi uzi ni wakwetu sisi....yani sindano umeileta ila tumekuchoma sisi....na tutaendelea kukuchoma...
Kwan huu uz nimeanzisha ili nisaidiwe ?

Kweli her kuabudu mmakonde kuliko kuabudu kinyago akichongacho

Naona bado kidogo utafunga ndoa ,

Kanisa katoliki nchini Malta labariki Ushoga

YHWH IS GOOD
 
Mbona unajitia mjuaji

Kwanini usipinge hoja zangu kwa maandiko

Toka karne ya 15 kina john huss

Martin luther, knox, sir isack newton walisema wazi wazi UFUNUO 13,. 17 , PEMBE NDOGO INALIHUSU KANISA KATOLIKI DHAHIRI

SASA WEW UNAPINGA BILA ANY EVIDENCE

HUSEMI HIYO PEMBE NDOGO AU HUYO KAHABA MKUU NI NANI

umebaki kulalamika tu

Sema ni nani, nianze aya moja moja unithibitishie inahusika vipi

MBONA MIMI NIMEKUONESHA KAHABA MKUU WA UF 17 NI KANISA KATOLIKI

TENA NIMETHIBITISHA AYA KWA AYA

unakimbilia aya ya 18

Huo mji ni VATICAN tena biblia inasema katika hiyo sura HUO MJI UPO KTK VILIMA 7 na ndio anakalia huyo mwanamke

Bado tu hufunguki?

Hujui ROMA VATICAN IMEZUNGUKWA NA VILIMA 7 ?

Au nikutajie kwa majina?

haya NJOO NA POROJO ZAKO

YHWH IS GOOD
Achana na pembe ndogo maana huko utashindwa hoja asubuhi sana.Pia maandiko haya uliyoyanukuu nilikuwa namjibu huyo ndugu wala hayahusiani na kukujibu wewe hivyo achana nayo.....

Unataka tena kwenda kwenye vilima saba,hapa nimecheka sana.nimecheka kwasababu wewe unasema kitu tofauti kabisa na maandiko....

Maandiko yanasema vilima saba ni wafalme saba na wewe unasema ni vilima kama mlima Meru kwa kusema eti Vatican imezungukwa na vilima saba,unaandika mambo yaliyo kinyume kabisa na maandiko halafu unasema umethibitisha,umethibiotisha unayofundishwa kwenye dhehebu lako labda.....

Malizana na hoja ya mwanamke kwanza huku tutafika tu na hutaweza kujitetea popote....

Unaendelea tu kujichanganya kuwa mwanamke ni Kanisa mara Vatican wakati mwanamke kwenye huu unabii ana maana MOJA tu na ni MJI,hiyo ya kanisa haina back up yoyote ya unabii huu....
 
Mkuu acha ujuaji

Wewe njoo kuhusu hiyo pembe ndogo , maana mm nishaeleza,

Wewe si uje tuone nani atashindwa asubuhi kuliko kulalama tu, haitakusaidia kitu

uwe unaweka MAANDIKO sio kuropoka tu,

Ngoja nikuoneshe mfano , hii ni INTRODUCTION

Ndio maana andiko linasema : "Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI".
UFUNUO 17 : 5
Unaona hapo juu kwenye fungu, yani jina BABELI NI LA SIRI, hii ikimaanisha, Babeli hii itafanya kazi kwa namna ya kujificha na kutotaka ijulikane kuwa ndio Babeli yenyewe.
HEBU TUISOME KWANZA KATIKA MAANDIKO TUONE BIBLIA INACHOTUAMBIA KUHUSU BABELI HUYO MKUU NA MAMA WA MAKAHABA.
"Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;
2 ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake.
3 Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.
4 Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.
5 Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.
6 Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu.
UFUNUO 17 : 1 - 6
Hapo tunaona Yesu akimfunulia mtumishi wake Yohana juu ya ujio mpya wa BABELI duniani. Haya matukio Yohana alifunuliwa kama matukio yaliyo mbele, yani yajayo baada ya siku zake. Yesu alifunua kuwa itaibuka tena BABELI lakini kwa sura tofauti kabisa na Babeli ile iliyozoeleka.
Kwa kutumia lugha ya mafumbo Yesu anamfunua BABELI huyo mkuu na MAMA WA MAKAHABA.
Sasa tunataka tumjue KAHABA HUYU MKUU NA AMBAYE NI MAMA WA MAKAHABA PIA, AITWAYE BABELI MKUU NI NANI?
Kwa kuwa haya ni mafumbo ya kimbingu, hatupaswi kujaribu kuyafumbua kibinadamu, tutaliacha Neno la Mungu litufunulie BABELI HUYU MKUU NA MAMA WA MAKAHABA ni nani?
BABELI MKUU MAMA WA MAKAHABA NI NANI AU NI NINI?
Biblia inamfunua..
1. Kwanza tunaona BABELI MKUU huyu ameonyeshwa kuwa ni mwanamke, maana anaitwa "mama" sote tunaelewa sifa ya mama ni ya jinsi ya kike.
Je, kwa mujibu wa Biblia mwanamke hutumika kuwakilisha nini anapotumika kama kielelezo?
- Katika Biblia "mwanamke" hutumika kuwakilisha "JAMII YA WATU WA MUNGU" ambao katika agano la kale watu hao walikuwa ni taifa la "ISRAELI"
Tunaona katika Hosea Mungu akiongea na watu wake kama aongeae na mwanamke
Nami nitakuposa uwe wangu kwa milele; naam, nitakuposa kwa haki, na kwa hukumu, na kwa ufadhili, na kwa rehema.
HOSEA 2 : 19
"Rudini, enyi watoto wenye kuasi, asema BWANA; maana mimi ni mume wenu; nami nitatwaa mtu mmoja wa mji mmoja, na wawili wa jamaa moja, nami nitawaleta hata Sayuni;
YEREMIA 3 : 14.
Katika zama za agani jipya, ambapo hakuna tofauti tena kati ya Myahudi na asiye Myahudi, mwanamke anawakilisha watu wa Mungu kwa maana ya "KANISA"
Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.
2 KORINTHO 11 : 2
Kwa sababu BABELI MKUU atatokea wakati wa Agano jipya, basi BABELI huyo ATAJITOJEZA KATIKA SURA YA KANISA!
Tumejua sasa KAHABA MKUU ni kanisa kumbe.
Tuendelee...,
KWA MAANA HIYO KUMBE, KATIKA KUMSEMA BABELI MKUU YESU ALIKUWA AKIFUNUA KUHUSU KUTOKEA KWA KANISA FULANI KATIKA SIKU ZA BAADAE TOKA KATIKA SIKU HIZO ZA YOHANA WA PATMO.
2. MWANAMKE HUYO BABELI MKUU ANAONEKANA ANA SIFA YA ZIADA MBALI YA UANAMKE WAKE, ANA SIFA YA "UKAHABA"
Hii maana yake ni nini?
Katika Maandiko, mahusiano baina ya Mungu na watu wake yamefananishwa na "MAHUSIANO YA NDOA"
rejea Yeremia 3 : 14, na 2 Wakorintho 11 : 2.
Yani kanisa ni mke wa Kristo, kwa maana hiyo UKAHABA NI TENDO LA KANISA KUTOKUWA NA UAMINIFU KWA KRISTO.
Hapo tunaona KANISA HILO (Babeli mkuu) litakuwa ni kanisa lisilo na uaminifu kwa KRISTO, yani litakuwa na mabwana wengine, na waume wengine tofauti na Kristo
Lakini pia katika Hosea 3 : 1 inaonyesha UKAHABA WA WATU WA MUNGU NI KUABUDU MIUNGU WENGINE, TOFAUTI NA MUNGU WAO.
Hivyo kanisa hilo litakuwa linachanganya ibada ya Mungu Muumbaji, na ibada za miungu wengine, HUO NDIO UKAHABA WA KANISA HILO.
BABELI MKUU ALIKUWA AMEKETI JUU YA MAJI MENGI.
Maji mengi ni nini?
"Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha".
UFUNUO 17 : 5
Hii inaonyesha kuwa kanisa hilo, litasambaa dunia nzima, kwenye kila makutano, kila kabila, kila lugha na kila jamaa litakuwepo.
Lakini pia, inaonyesha kanisa hili, litakuwa ni kanisa la WATU WENGI, litakuwa ni kanisa kubwa na lenye kila aina ya watu ndani yake, kwa idadi kubwa sana.
3. BABELI MKUU (kanisa) ALIKUWA AMEPANDA MNYAMA.
Mnyama anapotumika kama kielelezo huwakilisha "FALME au TAWALA.
Soma Daniel 7 : 17 na Daniel 7 : 23
"Wanyama hao wakubwa walio wanne ni wafalme wanne watakaotokea dunian".
DANIEL 7 : 17.
Kama ambavyo mtoto aliyebebwa anavyomtegemea aliyembeba, ndivyo kanisa hilo (BABELI MKUU). litakavyokuwa linategemezwa na serikali za kidunia. Nguvu zake, ustawi wake utatokana na kusaidiwa na mataifa au serikali za kidunia.
4. BABELI MKUU (kanisa) ATAZINI NA WAFALME.
Hii ina maana sawa na kubebwa juu ya mnyama, lakini imeongeza uzito wa kitendo chenyewe, neno KUZINI ina maana kanisa hilo litajitegemeza kwa wafalme wa dunia na kushikamana nao, kana kwamba wao ndio wenye kanisa. Nafasi ya Kristo itaondolewa na kama matokeo ya Kristo kwa kanisa hilo itatwaliwa na wafalme hao.
5. BABELI MKUU (kanisa) AMEWALEVYA WAKAAO JUU YA NCHI KWA MVINYO WA UASHERATI WAKE.
Kwanza kabisa tuliona UASHERATI WA KANISA HILO NI KUTANGA MBALI NA KRISTO, PIA KUABUDU VINGINE VISVYO MUNGU MUUMBAJI.
Sasa hapa twafunuliwa kuwa, KANISA HILO LITAWAAMBUKIZA WALIMWENGU UASHERATI WAKE, KWA NJIA YA MAFUNDISHO YA UONGO.
MAFUNDISHO YA UONGO ndio mvinyo wa uasherati wake. Watu wataabudishwa ibada zisizokubalika kimaandiko na kanisa hilo, watu watapiga magoti mbele ya miungu ya kigeni kwa maelekezo ya kanisa hilo.
Kulewa ni kuondolewa utambuzi, jambo ambalo ukiwa na akili timamu huwezi kukubali kulifanya, ukilewa unalifanya vzr tu.
Ndivyo itakavyokuwa kwa watu hao, kama wasingenyweshwa (wasingedanganywa) mvinyo (mafundisho ya uongo) wangetambua kuwa ibada hizo ni batili na hazikubaliki.
Lakini akili hiyo ya utamuzi imeondolewa na mvinyo huo wa uasherati wa kanisa hilo.
Na Biblia inathibitisha kuwa MAFUNDISHO YA UONGO YANALEVYA, Isaya 29 : 9, 10
6. ALIKUWA NA MAJINA YA MAKUFULU KATIKA KICHWA CHAKE.
Zingatia majina hayo hayakuwa mguuni, tumboni wala mgongoni, bali yalikuwa kichwani..,
Hii maana yake ni kuwa VIONGOZI WA KANISA HILO WATAJIPA MAJINA YANAYOMSTAHILI MUNGU.
7.BABELI MKUU ALIKUWA AMEVAA NGUO YA ZAMBARAU NA NYEKUNDU.
Hii nguo maana yake nini?
Tunaposoma maandiko, tunaona RANGI NYEKUNDU MAANA YAKE NI DHAMBI, Soma Isaya 1 : 18
"Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
ISAYA 1 : 18
Katika BIBLIA za lugha zingine mfano Biblia ya lugha ya kinyarwanda, imetaja kabisa na rangi ya zambarau pia katika fungu hilo la ISAYA.
Hivyo mavazi hayo yanaonyesha DHAMBI za kanisa. Litakuwa ni kanisa linalounga mkono dhambi, litakuwa ni kanisa ambalo lenyewe limeifanya dhambi kuwa ndio kanuni yake ya utendaji.
8. BABELI MKUU AMEPAMBWA KWA VITO, NA LULU
Hii inamaanisha nini?
Hizi, ni ishara za utajiri!
Kanisa hilo, litakuwa ni kanisa tajiri mno, lenye kuonekana wazi kwa utajiri wake, sawa na mapambo ya mwanamke yanavyoonekana wazi.
Litakuwa ni kanisa tajiri sana!
9.KIKOMBE CHA DHAHABU KILICHOJAA MACHUKIZO.
hii ina maanisha nini?
Dhahabu inaonyesha UPENDO., hili litakuwa ni kanisa ambalo litaonekana kuwa na matendo ya upendo.
Lakini kama ambavyo kikombe hicho cha dhahabu ndani kilivyokuwa na machukizo, kadhalika ndani ya hayo yatakayoonekana ni matendo ya Upendo kutakuwa na hila ya kuwaingiza watu katika kufanya MACHUKIZO dhidi ya Mungu.
10.AMELEWA KWA DAMU YA WATAKATIFU
Hii maana yake ni nini?
Kanisa hilo litawaua watu wa Mungu. Litamwaga damu ya watu ambao watakataa kushiriki uchafu wake.
11. Ana jina la siri "BABELI MKUU MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.
Hii inamaanisha nini?
Kwanza tunaona hilo ni jina la siri, jina ambalo hakutaka lifahamike. Ndio maana akaja kwa sura ya mwanamke, yani alitaka afahamike kama mwanamke, kumbe hasa si mwanamke bali ni BABELI MKUU!
umeelewa mchezo?
Tuonane katika sehemu inayofuata kwa ufafanuzi wa mbinu hiyo ya kuficha jina, kuna mambo ya muhimu na nyeti sana tupaswayo kuyafahamu

YHWH IS GOOD
 
Mkuu acha ujuaji

Wewe njoo kuhusu hiyo pembe ndogo , maana mm nishaeleza,

Wewe si uje tuone nani atashindwa asubuhi kuliko kulalama tu, haitakusaidia kitu

YHWH IS GOOD
mimi ni ROMAN CATHOLIC na sitoacha kwenda kanisani sababu ya nyie manabii watu kwa sababu namuomba Mungu huko huko RC na nnabarikiwa sababu hiyo....so bro endelea kutafuta wakukuletea sadaka mi umenikosaa[emoji2][emoji2]

Sent from my SM-J200H using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom