Mfahamu Lean Feng Wang, mmiliki wa AI ya Deep Seek ambayo ni tishio kubwa kwa CHATGPT

Vijana UDSM wameshindwa hata ku renema deepsik na chatgpt wakaipa nickname yao? huu ubwege huu.. Africa yote tumeshindwa tunamwaza tu Kagame
Not that simple, even deepseek wametumia kiasi cha fedha kirefu kufikia hapo. Unadhan copy and past is that easy?
 
Tatizo ni kuwa DeepSeek siyo huru, ni politicised, ni utopolo mwingine.

Ukiuliza swali ambalo majibu yake siyo chanya kwa watawala, serikali ya China, unaambiwa hivi..
👇
I am sorry, I cannot answer that question. I am an AI assistant designed to provide helpful and harmless responses.
 
Tatizo ni kuwa DeepSeek siyo huru, ni politicised, ni utopolo mwingine.

Ukiuliza swali ambalo majibu yake siyo chanya kwa serikali ya China, unaambiwa hivi..
👇
Nyie hamjui kuzitumia hizi tools,sasa hizo politics zinakusaidia nini? Software Developers sasa hivi kazi walizokuwa wanazifanya mwaka,wana uwezo kufanya mwezi mmoja.Watu wa IT sasa hivi hawatumii nguvu kama zamani.

Sasa unauliza maswala ya kipolitics ya China yanakusaidia nini.Halafu hamna software ambayo haina backdoor, iwe Ulaya,US au China software zao zote zinabackdoor.
 
Deepseek imewavuruga US kwanza ni open source,pili imekuwa develop kwa kiasi kidogo 5.6 m USD ukilinganisha na za kwao,wawekezaji sasa hivi wanajiuliza je walipigwa? Halafu hata chips jamaa ametumia chips za kawaida ambazo sio powerful sana kama za AI nyingine ila performance yake ina karibia na za kwao.

Sasa hapo jiulize jamaa akifanikiwa kupata chips ambazo powerful na wawekezaji wakaweka mzigo wewe unazani hiyo DeepSeek itakiwaje miaka ya mbele.

Dunia ukiwa na watu,fedha,mfumo mzuri wa elimu na Research and Development centers kila kitu kinawezekana. Hata huko kwenye Quantum Computer Mchina hayupo nyuma. Ndio maana vikwazo vingi wanampiga still Mchina anasonga.

Hebu fuatilia hii documentary ya Bloomberg ya Hannah Fry
View: https://m.youtube.com/watch?v=1_gJp2uAjO0&pp=ygU0UXVhbnR1bSBjb21wdXRlcnMgZGV2ZWxvcG1lbnQgIGJsb29tYmVyZyBkb2N1bWVudGFyeQ%3D%3Dk 10 za mwisho atakuonesha hatua walizopiga China kwenye Quantum computers development.
 
Mkuu ni vitu gani vipya kabisa (original ideas) kutoka kwa Mchina?

Katika post yangu sijasema Deepseek haina ubora, nimesema Mchina hana ufunguo wa uvumbuzi...

Kuhusu suala la mtaji investors kudhani wamepigwa hilo ni jambo jingine... Ni masuala ya inputs, sasa sisi sote hatuko na team ya OpenAI, wao ndio wanajua...

Nikupe mfano hai, mkuu...

Inachukua muda kujua ikiwa hili tunda lililoko mtini, tuseme ni pera, inachukua muda kujua ni sumu au sio sumu, na ikishafahamika mtu atakayefuatia kutaka kula lile pera hatatumia gharama tena, sababu gharama zilishaingiwa mwanzoni.

Iphone imechukua miaka miwili watu wako lab wanafanya kuivent, leo inatangazwa-inazinduliwa, uliza ilichukua muda gani Android devices kupatikana sokoni, nafkri majibu utakuwa nayo mkuu...
 
Tatizo ni kuwa DeepSeek siyo huru, ni politicised, ni utopolo mwingine.

Ukiuliza swali ambalo majibu yake siyo chanya kwa serikali ya China, unaambiwa hivi..
👇
Kwani ni AI gani ipo huru ?
 
Kwani technology ya printing imeanzia wapi ?

Hiyo ni moja
 
Teknolojia sio lazima wewe ndio uwe mgunduzi wa kwanza ili iweze kuwa Bora! Hata inapokuwepo na wewe ukaiboresha na kupendwa ni mageuzi pia ya teknolojia!
 
Ma IT wetu wameitimu kuwa machawa wa kuprint chapa za ccm na picha za samia tu
 
Sawa hana ufumbuzi ila upande wa Innovation yupo vizuri na dunia unaweza ukagundua kitu ila kwenye innovation ukapigwa gap. Ndio maana vikwazo haviishi.
 
kuna kitu huelewi sio kwamba deep seek ina nguvu zaidi ya chatgpt, ni kwamba ilitumia gharama kidogo ila sio kwamba imeipita chatpt
 

Nilipoanza kusoma post yako nikadhani una point ila nimepuuzia wazo lako looote hapo mwisho ninukuu

"........,China ni ngumu kuwa kiongozi hata ikitokea akamzidi uchumi Marekani.........."

☝️☝️ kwenye masuala ya kiteknolojia usiwe unatumia neno NI NGUMU infact kwenye jambo lolote lile usije tumia kauli hiyo kabla haujajaribu kwa kila njia tena kwa kushirikisha vichwa tofauti tofauti kinyume na hapo hiyo inaonesha ufinyu wa ufikiriaji wako
 
Sawa hana ufumbuzi ila upande wa Innovation yupo vizuri na dunia unaweza ukagundua kitu ila kwenye innovation ukapigwa gap. Ndio maana vikwazo haviishi.
Sawa, tunaenda pamoja hapa kama umekubali hana uvumbuzi, mimi narudia sijasema kuwa deepseek haileti changamoto yoyote ile kwa Chatgpt, nachosema mimi ni kuwa ikiwa kila taifa litafuata njia ya China, bas sote tuko ndani ya cage kiakili!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…