Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 1,679
- 2,123
Mchungaji William Folorunsho Kumuyi ni Mchungaji Mwafrika, aliyepata heshima ya kualikwa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Marekani, Donald Trump, tarehe 20/1/2025. Mchungaji huyo alipata nafasi ya kushiriki ibada rasmi ya kumuombea Rais Trump. Mchungaji huyo ni nani hasa na kwanini alialikwa? Mchungaji Kumuyi ni Askofu Mkuu, au kama anavyojulikana zaidi “Mwangalizi Mkuu” na Mwanzilishi wa Kanisa la “Deeper Life Bible Church” lenye makao yake makuu Gbagada, Lagos, Nigeria. Alizaliwa tarehe 6 Juni 1941. Kabla hajapata wito wa kuwa Mchungaji , alikuwa Profesa wa Hesabu katika Chuo Kikuu cha Lagos, Nigeria.
Kanisa la Deeper Life alilianzisha mwaka 1973 likiwa na watu wachache lakini sasa lina mamilioni ya waumini katika nchi mbalimbali duniani. Mchungaji Kumuyi anaheshimiwa sana kwa jinsi asivyopenda makuu na pia kwa jinsi alivyo mnyenyekevu. Mchungaji Kumuyi amejitoa kufundisha Neno la Mungu huku akiweka msisitizo kuhusu utakatifu na haki. Chini ya uongozi wake, jengo la Kanisa hilo lina uwezo wa kuketisha watu 30,000 kwa wakati mmoja. Kanisa hilo kila Jumapili linakuwa na ibada tano zinazohudhuriwa na washirika wapatao 150,000. Kanisa hilo lina matawi Marekani, Uingereza, Ujerumani, Canada, India, Dubai na nchi kadhaa za Afrika. Mchungaji Kumuyi, katika mafundisho yake, anaeleza kwamba wokovu unapatikana kwa imani katika Yesu Kristo, na kwamba ni muhimu mtu apate utakaso na kuishi maisha matakatifu ili aweze kumuona Mungu(Ebr 12:14).
Yamkini hizo ndizo sababu zilizomfanya Mchungaji Kumuyi apate heshima ya kupata mwaliko huo wa kipekee. Kitendo cha kualikwa kwa Mchungaji Kumuyi katika sherehe ya uapisho wa Rais Trump, kinaonyesha wazi dhamira aliyo nayo Rais Trump ya kulinda na kukuza uhuru wa kuabudu nchini Marekani na kimataifa.
Mchungaji William Kumuyi