Mfahamu Mchungaji kutoka Afrika aliyealikwa kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais Trump

Mfahamu Mchungaji kutoka Afrika aliyealikwa kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais Trump

Trump yeye ni muumini wa dhehebu gani huko Marekani? Au ni Mfuasi wa kanisa gani? Na je anaenda kanisani na kama ni ndiyo anaenda kanisa gani? Au naye anaenda kwenye kanisa linaloongozwa na huyo Mchungaji?

Unaweza kujibu kuhusu "Trump Bible"? Imesheheni nini humo ndani na anaiuza bei ghali kwa nini?

Siku ya Kuapa kwake Hakuweka mkono wake kwenye biblia kama wafanyavyo wengine waliopita, alikuwa anaiogopa au alikataa makusudi, na je hili alimuondolei uaminifu wake kwa makanisa?
  • Donald Trump anahusishwa zaidi na kanisa la Presbyterian, ingawa hajawa mshirika wa karibu wa dhehebu hilo. Mara nyingi amekuwa na uhusiano mkubwa na makanisa ya kiinjili (Evangelicals), labda ndio sababu alimualika Mchg. Kumuyi.
  • Trump ameonekana mara chache akihudhuria ibada kanisani. Alipokuwa rais, awamu ile ya kwanza, alitembelea makanisa kadhaa ya kiinjili na mara nyingine alionekana katika ibada maalum za maombi.
  • Trump Bible, inajulikana pia kama "The God Bless the U.S.A. Bible," hiyo ni Biblia ya toleo la King James Version, ila ina mambo mengine ya ziada yanayohusiana na Taifa la Marekani. Suala la kwanini anaiuza ghali mimi sijui. Labda kwa sababu ya hiyo "additional content."
  • Ni kweli Trump wakati wa kuapishwa kwake, hakuweka mkono wake kwenye Biblia kama ilivyo ada; lakini Katiba ya nchi hiyo haimlazimishi Rais kuweka mkono kwenye Biblia anapoapishwa. Kilichofanyika ni kwamba mke wake alishikilia Biblia mbili wakati Trump akiapishwa
  • Maswali yako, hata hivyo, yako nje kidogo ya uzi huu. Niulize zaidi kuhusu Mchg. Kumuyi. Asante
 
Toilet paper zikiingia katika shimo la choo huwa zinatoka tena na kutumika? Mbona unajichanganya ndugu? Halafu wewe uzuie ulimi wako usinene matusi yasije yakakupata yaliyowapata kina Miriam na Haruni kwa kumnenea mabaya Mtumishi wa Mungu, Musa.
Mtu hawezi kulialika mavi, maana kinachotoka shimo la choo ni mavi, sasa iweje atuite shimo la choo halafu amualike mmoja wa watokao ndani ya shimo la mavi?
 
Mtu hawezi kulialika mavi, maana kinachotoka shimo la choo ni mavi, sasa iweje atuite shimo la choo halafu amualike mmoja wa watokao ndani ya shimo la mavi?
Hilo swali muulize yeye kwenye ukurasa wake wa X
 
Siwezi kumuuliza, maana sababu naijua, huyo ameenda kutumia kama acceptance card kwa waAfrika, kaenda kutumika tu kama toilet paper..
Mchungaji Kumuyi ameisharudi Nigeria na hayo unayosema hayakufanyika. Hiyo chuki yako kwa Trump haitakusaidia.
 
Unaota ndoto? Ndoto huwa zina michanganyiko mingi
Huyajui haya mambo. Tulia! Laiti ungeujua undani wa Kila mtu mashuhuri hapa nchini au duniani hapa ungebaki mdomo wazi.

Kusoma na kujifunza mambo hamtaki mnakalia ujinga ujinga tu na umbea
 
Trump ameonekana mara chache akihudhuria ibada kanisani. Alipokuwa rais, awamu ile ya kwanza, alitembelea makanisa kadhaa ya kiinjili na mara nyingine alionekana katika ibada maalum za maombi
Trump ni mlokole kipindi chake cha kwanxa alikuwa na mchungaji wake Ikulu wa kumsalisha ibada zake ikulu huyo mchungaji ni mwanamama Mchungaji Paula white
 
Huyajui haya mambo. Tulia! Laiti ungeujua undani wa Kila mtu mashuhuri hapa nchini au duniani hapa ungebaki mdomo wazi.

Kusoma na kujifunza mambo hamtaki mnakalia ujinga ujinga tu na umbea
Kwa mawazo yako wewe unafikiri duniani hakuna watakatifu. Pole sana.

Umbeya wanaufanya wasiomjua Mungu. Mimi simo katika kundi hilo.

Mchungaji anayeishi maisha ya dhambi utamjua tu kwa kusema kwake na kwa kutenda kwake. Chunguza maisha ya Mchungaji Kumuyi halafu uniambie dhambi yake ni nini
 
Gwajima mbona hakualikwa
Mswiga mbona hakualikwa
aaaa shapata jibu.Wanachanganya dini na siasa shauri ya matumbo yao
Wangemuiga Kakobe
Kakobe kweli hakualikwa lakini ni bahati mbaya tu Trump hawezi wakumbuka wote ila alistahili
 
Gwajima mbona hakualikwa
Mswiga mbona hakualikwa
aaaa shapata jibu.Wanachanganya dini na siasa shauri ya matumbo yao
Wangemuiga Kakobe
Kakobe kweli hakualikwa lakini ni bahati mbaya tu Trump hawezi wakumbuka wote ila alistahili
Duh, unauliza swali na kujijibu
 
Mwamposa ni nani? Labda bado hajafahamika kimataifa. Rais Trump mpaka akupe mwaliko anakuwa amechunguza vitu vingi sana.
Huyo ataalikwa Dodoma inatosha sana Ualikwe DC uanze habari za kutapika mijusi mara chura mtu anatoa ushuhuda eti niikunya paka si upuuzi huo?
 
Back
Top Bottom