Pichani ni Marehemu Major Generali Muhiddin Kimario, ni moja kati ya mawaziri wawili tu waliowahi kudumu katika nafasi zao za wizara ya mambo ya ndani kwa muda wa miaka mitano (5) katika Historia ya Tanzania.
Mwaka 1978 alitumwa kwenda mkoani Mwanza na Mwalimu Nyerere kwenda kuwaaga Wanajeshi waliokuwa wanakwenda kupigana Vita vya Kagera kumn'goa Idd Amin Dada, wakati akitoa Hotuba yake ndani ya Viwanja vya Nyamagana ghafla aliamua kujivua uwaziri na kuamua kwenda vitani "Mkuu wa Mkoa ninaomba ufikishe taarifa hii kwa mh Rais kwamba najivua Uwaziri na ninaamua kurudi jeshini kuungana na wenzangu leo kwenda kumshikisha Adabu Amin"
View attachment 1498576