Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Hii nayo ni uwongo mtupu; Muhidini Kimario baada ya vita alikuwa waziri wa mambo ya ndani kuanzia mwaka 1983. Hata ukienda tovuti ya Wizara hiyo utakuta kuwa yeye aliendelea kuongoza wizara hiyo hadi 1988, yaani miaka kumi baada ya vita. Kabla ya Vita alikuwa Mkuu wa Mkoa wa MwanzaAmefariki 2005, ila Kisa chake cha kusikitisha ndio hiki
Kuna askari wengi waliokuwa mstari wa mbele wanasema Lupogo alishindwa KABISA kuendesha vita na kurudishwa makao makuu. Kikosi chake cha 205 kuchukuliwa na Kimario. Kimario aliendesha mapigano makali na kikosi chake cha 205 kiliweza kukata katikati ya Uganda mpaka Nimule kwenye mpaka wa Uganda na Sudan. 205 ndiyo kikosi kilichopoteza kifaru kimoja baada ya mapigano makali ya masaa 8 ili kuteka daraja muhimu la Maporomoko ya Karuma Kwa maajabu,Mwl Nyerere alimpandisha cheo Lupogo kuwa Meja Jenerali na kumuacha yule aliyepiganisha vita na kushinda Kimario. Wewe jiulize inakuaje aliyeshindwa vita kupandishwa cheo na yule liyeshinda kuachwa mpaka alipopandishwa cheo na Rais A.H Mwinyi.Hizo ndizo changamoto za Mstari wa mbele walizokuwa wanazipata wapiganishaji wetu
Hizi conspiracy theories mnazitoa wapi?