View attachment 816435 Taarifa hii ina mushkeli kidogo, niliwahi kumuandika huko nyuma na hii ndiyo historia yake kwa ufupi!
1937 Alizaliwa, Moshi mjini.
1954 Muasisi wa TANU moshi Mjini
1957 Mwalimu Mkuu wa Kwanza wa Shule ya Mwenge (Moshi Mjini)
1962 TANU ilimchagua kwenda kusomea uongozi
1963 TANU ilimchagua ajiunge na Jeshi na kupelekwa Israel kusomea masuala ya kijeshi.
1964 Muasisi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
1964 Mzalendo wa kwanza kuwa mkuu wa kambi ya Calito (Lugalo)
1965 Muanzilishi wa kitengo cha intelejensia ndani ya jeshi
1966 Mkufunzi mkuu Kambi ya Kongwa kwa wapiganaji wa ukombozi wa Afrika kutoka nchi tofauti za kusini mwa afrika.
1967 Mkuu wa kambi ya Ukombozi wa Msumbiji Nachingwea (Farm 17)
o Muasisi wa vita vya ukombozi wa Msumbiji. Anaheshimika kama Shujaa katika nchi ya Msumbiji (barua kutoka Serikali ya Msumbiji iliyosomwa siku ya mazishi yake.
1970 Mkuu wa Kikosi Maalum (Ukombozi wa Afrika)
1972 Mshauri wa kivita OAU
1973 Mpelelezi Mkuu (Kamati ya OAU) wa mauaji ya Amilcar Cabralar mwana mapinduzi na mpigania uhuru wa Guinea Bissau na visiwa vya Cape Verde.
1973 Mkuu wa Kambi ya Kaboya (Kagera)
1975 Mbunge wa Moshi Mjini
Baada ya kumshinda Lucy Celina Lameck
1977 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
o Akajenga Uwanja wa kimataifa wa michezo wa CCM Kirumba kwa kuchangisha wananchi.
1978 Mkuu wa Kambi ya Nyuki (Zanzibar)
1979 Akimbizwa uwanja wa mapambano kuwa Mkuu wa Brigedi ya 205 (wakati wa Vita vya Kagera)
o Alimpokea Brigedia Lupogo, ndipo alipopata jina maarufu la Kamanda Mbogo.
1980 Apita ubunge bila kupingwa Moshi Mjini.
1981 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
1983 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
1985 Ashinda tena ubunge wa Moshi Mjini
1985 Waziri wa Mambo ya Ndani
o Aliyewatengenezea Waraka wa Utumishi (Scheme of Service) Jeshi la Polisi ambayo walikuwa hawana tangu kuanzishwa kwa jeshi na ndiyo inayotumika mpaka leo.
1985 Kamati ya Kumtoa Obote
1986 Kamati ya kumtoa Tito Okello na kumuweka Yoweri Museveni.
1990 Alishindwa ubunge wa Moshi mjini.
1991 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
1991 Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA)
1995 Alikatwa kabla ya kura za maoni kupitia CCM. Ripoti ilipelekwa kwenye Chama ikisema akija kugombania ubunge wa Moshi Mjini atapigwa mawe na kusababisha vurugu. Akatolewa kabla ya kura za maoni.
1996 Miezi michache baada ya kuingia madarakani Serikali ya awamu ya Tatu ilimfungulia kesi ya uhujumu uchumi kesi aliyoshinda mwaka 1998. Baada ya kushinda kesi alikataa kurudi CDA na ndiyo ukawa mwisho wa utumishi wake wa Umma.
2004 Alitunukiwa nishani ya utumishi bora na utiifu uliotukuka.
2014 Afariki dunia kwa ugonjwa wa saratani huko India.