sab
JF-Expert Member
- Jan 25, 2013
- 5,723
- 4,286
HahahahaSijui lini lakini mleta mada ndiyo kasema ni marehemu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
HahahahaSijui lini lakini mleta mada ndiyo kasema ni marehemu.
1984 mkuu, alikuwa ndiye Mkurugenzi wa CDA na walisimamishwa kazi kwa upotevu wa karibu 20$ mil kama sijakosea, kesi uso ilikuja kwisha kipindi cha mwinyi na wakatimuliwa , mijengo yake ipo pale Dom karibu na SIDO na ukumbi pale Makole karibu na CBE
alishafariki muda tuSijui lini lakini mleta mada ndiyo kasema ni marehemu.
Alizaliwa mwaka 1937 then akaasisi TANU hapo Moshi mwaka 1954,Kwa hiyo aliasisi Chama cha TANU akiwa na miaka 17,si kweli hio.View attachment 816435 Taarifa hii ina mushkeli kidogo, niliwahi kumuandika huko nyuma na hii ndiyo historia yake kwa ufupi!
1937 Alizaliwa, Moshi mjini.
1954 Muasisi wa TANU moshi Mjini
1957 Mwalimu Mkuu wa Kwanza wa Shule ya Mwenge (Moshi Mjini)
1962 TANU ilimchagua kwenda kusomea uongozi
1963 TANU ilimchagua ajiunge na Jeshi na kupelekwa Israel kusomea masuala ya kijeshi.
1964 Muasisi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
1964 Mzalendo wa kwanza kuwa mkuu wa kambi ya Calito (Lugalo)
1965 Muanzilishi wa kitengo cha intelejensia ndani ya jeshi
1966 Mkufunzi mkuu Kambi ya Kongwa kwa wapiganaji wa ukombozi wa Afrika kutoka nchi tofauti za kusini mwa afrika.
1967 Mkuu wa kambi ya Ukombozi wa Msumbiji Nachingwea (Farm 17)
o Muasisi wa vita vya ukombozi wa Msumbiji. Anaheshimika kama Shujaa katika nchi ya Msumbiji (barua kutoka Serikali ya Msumbiji iliyosomwa siku ya mazishi yake.
1970 Mkuu wa Kikosi Maalum (Ukombozi wa Afrika)
1972 Mshauri wa kivita OAU
1973 Mpelelezi Mkuu (Kamati ya OAU) wa mauaji ya Amilcar Cabralar mwana mapinduzi na mpigania uhuru wa Guinea Bissau na visiwa vya Cape Verde.
1973 Mkuu wa Kambi ya Kaboya (Kagera)
1975 Mbunge wa Moshi Mjini
Baada ya kumshinda Lucy Celina Lameck
1977 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
o Akajenga Uwanja wa kimataifa wa michezo wa CCM Kirumba kwa kuchangisha wananchi.
1978 Mkuu wa Kambi ya Nyuki (Zanzibar)
1979 Akimbizwa uwanja wa mapambano kuwa Mkuu wa Brigedi ya 205 (wakati wa Vita vya Kagera)
o Alimpokea Brigedia Lupogo, ndipo alipopata jina maarufu la Kamanda Mbogo.
1980 Apita ubunge bila kupingwa Moshi Mjini.
1981 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
1983 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
1985 Ashinda tena ubunge wa Moshi Mjini
1985 Waziri wa Mambo ya Ndani
o Aliyewatengenezea Waraka wa Utumishi (Scheme of Service) Jeshi la Polisi ambayo walikuwa hawana tangu kuanzishwa kwa jeshi na ndiyo inayotumika mpaka leo.
1985 Kamati ya Kumtoa Obote
1986 Kamati ya kumtoa Tito Okello na kumuweka Yoweri Museveni.
1990 Alishindwa ubunge wa Moshi mjini.
1991 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
1991 Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA)
1995 Alikatwa kabla ya kura za maoni kupitia CCM. Ripoti ilipelekwa kwenye Chama ikisema akija kugombania ubunge wa Moshi Mjini atapigwa mawe na kusababisha vurugu. Akatolewa kabla ya kura za maoni.
1996 Miezi michache baada ya kuingia madarakani Serikali ya awamu ya Tatu ilimfungulia kesi ya uhujumu uchumi kesi aliyoshinda mwaka 1998. Baada ya kushinda kesi alikataa kurudi CDA na ndiyo ukawa mwisho wa utumishi wake wa Umma.
2004 Alitunukiwa nishani ya utumishi bora na utiifu uliotukuka.
2014 Afariki dunia kwa ugonjwa wa saratani huko India.
Alizaliwa mwaka 1937 then akaasisi TANU hapo Moshi mwaka 1954,Kwa hiyo aliasisi Chama cha TANU akiwa na miaka 17,si kweli hio.
Muasisi wa TANU Moshi mjini alikuaga Ndugu Yussuf Ngozi.Labda utueleze kwa nini haliwezekani? Maana kwenye profile yako inaonekana unajua vitu vingi sana ndugu Mng'ato! Na labda utatusaidia katika historia uliyonayo ni wakina nani walikuwa vijana waasisi wa TANU mwaka 1954 pale Moshi, si unajua historia huchangiwa na watu tofauti!
Hili linawezekana mkuu kwa wakati ule na hata sasa.Hivi unajua kazi ya jeshi hata ukistaafu kuna wakati kama bado una nguvu unaweza kuitwa au ukajitolea kwenda kusaidia na ndio maana wastaafu wa jeshi wanaitwa Jeshi la akiba.Miaka ile achilia Muhidini Kimario yeye alikuwa ni askari kabisa kitaaluma lakini kuna wanafunzi waliosomea shule ya kijeshi ya Tabora boys wakati huo walikuwa tu uraiani wanafanya kazi za kiraia lakini wengine walijitolea na wengine walichukuliwa kwenda vitani.Wakati ule watu wenye nyadhifa kubwa kijeshi walikuwa na nyadhifa zingine kwenye chama na serikali lakini mtiti wa vita ulivoanza walitupa kalamu zao na kwenda kumtoa nduli aliyeingia nchini kwetu.Nyoka anapoingia nyumbani kwako kila mtu aliyeko ndani ya chumba anaacha kila anachokifanya hata kama anadeki au anafua anapambana na nyoka huyoMajor Gen. M Kimario alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani kati 1983-1989 kama sijakosea mwenye historia nzuri anaisaidie. Vita vya Kagera vilikwisha Mwaka 1979. Hii taarifa ina mapungufu makubwa sana na kama ni kweli alifanya jambo ambalo sio nidhamu ya kazi na jeshi , pia vita ni mpango mkakati uwezi kukurupuka na kujiendea tu unakwenda kukaa position gani katika ramati ya vita kuna mapungufu mengi sana kwa mtoaji taarifa
Huyu si ndiye aliifilisi CDA? Yeye na akina Feruzi na Aden Rage? Anaweza kasema ni mzarendo kwa kuipigania nchi yake, vipi kuliibia taifa kisa mjeda, haiingii akilini, hayupo kwenye kundi la mashujaa
Ila sio hio ya WasukumaNaithamini sana jwtz
Mimi namfahamu personally huyu mzee.Pascal Mayalla na Mohamed Said na wana history wengine njooni huku
View attachment 816435 Taarifa hii ina mushkeli kidogo, niliwahi kumuandika huko nyuma na hii ndiyo historia yake kwa ufupi!
1937 Alizaliwa, Moshi mjini.
1954 Muasisi wa TANU moshi Mjini
1957 Mwalimu Mkuu wa Kwanza wa Shule ya Mwenge (Moshi Mjini)
1962 TANU ilimchagua kwenda kusomea uongozi
1963 TANU ilimchagua ajiunge na Jeshi na kupelekwa Israel kusomea masuala ya kijeshi.
1964 Muasisi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
1964 Mzalendo wa kwanza kuwa mkuu wa kambi ya Calito (Lugalo)
1965 Muanzilishi wa kitengo cha intelejensia ndani ya jeshi
1966 Mkufunzi mkuu Kambi ya Kongwa kwa wapiganaji wa ukombozi wa Afrika kutoka nchi tofauti za kusini mwa afrika.
1967 Mkuu wa kambi ya Ukombozi wa Msumbiji Nachingwea (Farm 17)
o Muasisi wa vita vya ukombozi wa Msumbiji. Anaheshimika kama Shujaa katika nchi ya Msumbiji (barua kutoka Serikali ya Msumbiji iliyosomwa siku ya mazishi yake.
1970 Mkuu wa Kikosi Maalum (Ukombozi wa Afrika)
1972 Mshauri wa kivita OAU
1973 Mpelelezi Mkuu (Kamati ya OAU) wa mauaji ya Amilcar Cabralar mwana mapinduzi na mpigania uhuru wa Guinea Bissau na visiwa vya Cape Verde.
1973 Mkuu wa Kambi ya Kaboya (Kagera)
1975 Mbunge wa Moshi Mjini
Baada ya kumshinda Lucy Celina Lameck
1977 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
o Akajenga Uwanja wa kimataifa wa michezo wa CCM Kirumba kwa kuchangisha wananchi.
1978 Mkuu wa Kambi ya Nyuki (Zanzibar)
1979 Akimbizwa uwanja wa mapambano kuwa Mkuu wa Brigedi ya 205 (wakati wa Vita vya Kagera)
o Alimpokea Brigedia Lupogo, ndipo alipopata jina maarufu la Kamanda Mbogo.
1980 Apita ubunge bila kupingwa Moshi Mjini.
1981 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
1983 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
1985 Ashinda tena ubunge wa Moshi Mjini
1985 Waziri wa Mambo ya Ndani
o Aliyewatengenezea Waraka wa Utumishi (Scheme of Service) Jeshi la Polisi ambayo walikuwa hawana tangu kuanzishwa kwa jeshi na ndiyo inayotumika mpaka leo.
1985 Kamati ya Kumtoa Obote
1986 Kamati ya kumtoa Tito Okello na kumuweka Yoweri Museveni.
1990 Alishindwa ubunge wa Moshi mjini.
1991 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
1991 Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA)
1995 Alikatwa kabla ya kura za maoni kupitia CCM. Ripoti ilipelekwa kwenye Chama ikisema akija kugombania ubunge wa Moshi Mjini atapigwa mawe na kusababisha vurugu. Akatolewa kabla ya kura za maoni.
1996 Miezi michache baada ya kuingia madarakani Serikali ya awamu ya Tatu ilimfungulia kesi ya uhujumu uchumi kesi aliyoshinda mwaka 1998. Baada ya kushinda kesi alikataa kurudi CDA na ndiyo ukawa mwisho wa utumishi wake wa Umma.
2004 Alitunukiwa nishani ya utumishi bora na utiifu uliotukuka.
2014 Afariki dunia kwa ugonjwa wa saratani huko India.
Huo ndio uzalendo sio kama kina makonda et el hawana uzalendo kwakulifanya taifa lichafuke dhidi ya mataifa mengine badala ya kulifanya taifa ling`ae juu ya mataifa mengine.Marehemu Major Gen. Muhiddin Kimario, mmoja ya mawaziri wawili tu wa Mambo ya Ndani katika historia ya Tanzania kuwahi kudumu katika nafasi hiyo kwa zaidi ya miaka 5.
Alitumwa na Mwl Nyerere kuwaaga wanajeshi kwenda kumng'oa Nduli Idd Amin, akiwa anahutubia katika uwanja wa Nyamagana ghafla akajivua Uwaziri na yeye akaenda vitani.
" Mkuu wa mkoa naomba ufikishe taarifa hii kwa Mh Rais kwamba najivua Uwaziri na naamuwa kurudi Jeshini kuungana na wenzangu leo kwenda kumshikisha Adabu Amin"View attachment 812786
Shukran mkuundukulusudicho , MANCNOO ,
..unaweza kusoma taarifa za Maj.Gen.Muhidin Kimario ktk uzi huu.
..aliyeuanzisha ni moyafricatz. Anastahili pongezi.
Mwambie aache ungeseMarehemu Major Gen. Muhiddin Kimario, mmoja ya mawaziri wawili tu wa Mambo ya Ndani katika historia ya Tanzania kuwahi kudumu katika nafasi hiyo kwa zaidi ya miaka 5.