Mfahamu Mohamed Said: Maisha, Kazi na Historia yake

Mfahamu Mohamed Said: Maisha, Kazi na Historia yake

mwanahistoria alieandika mengi lakin hakuwah kumhoji Nyerere. anawahoji wale watakaompa majibu anayotaka. cjui alikuwa ana ballance vip stor zake.
🤔🤔🤔 Fikirishi
 
Ni mwandishi mzuri anajua historia ila ukizungumza nae kwa mawili matatu utagundua kuwa aidha anapindisha historia au anazo ajenda anataka kuzipenyeza
Hapa ngoja tumusubiri na yeye atutoe ualakini.
 
Dah.... Majibu yapo kwenye kitabu changu kinaitwa "Historia ya Baba, misimamo ya mtoto na bifu na Nyerere"....cha mwaka 1957......kanunue 🤣🤣🤣🤣🤭
Sawa mkuu ngoja tukitafute tukifanyie kazi.
 
Mtu anayemuita mwenzake mdini ni mdini wa kwanza….
Ukionesha kidole kimoja vinne vinakurudia mwenyewe
It takes a thief to catch one
Mohammed Said anaandika historia kwa mrengo wake na anavyofahamu
Kweli hapa umeeleweka kabisa
 
Historia yenyewe haijitoshelezi,, hujaandika kuhusu elimu yake wapi alisoma na hata kuajiriwa endapo kama aliajiliwa,, familia yake yani ana watoto au la,, alianza lini kujishugulisha na uandishi, kipi kilimsukuma mpaka kuwa muandishi,, kifupi hukumtendea haki kwenye hii historia yake japo kwa ufupi, sana sana nilichoona hapo umeelezea historia ya babu yake na hujasema huyo babu yake ni mzaa baba au mama!!
 
Historia yenyewe haijitoshelezi,, hujaandika kuhusu elimu yake wapi alisoma na hata kuajiriwa endapo kama aliajiliwa,, familia yake yani ana watoto au la,, alianza lini kujishugulisha na uandishi, kipi kilimsukuma mpaka kuwa muandishi,, kifupi hukumtendea haki kwenye hii historia yake japo kwa ufupi, sana sana nilichoona hapo umeelezea historia ya babu yake na hujasema huyo babu yake ni mzaa baba au mama!!
Asante kwa nyongeza ngoja nifanyie kazi nyogeza hiyo uliyo tolea ufafanuzi.
 
Mfahamu Mohamed Said mdau wa JF ambe ni JF expert Member tangu 2008

Mohamed Said Salum (alizaliwa tarehe 25 Februari, 1952, Gerezani, Dar es Salaam) ni mwandishi na mwanahistoria kutoka nchini Tanzania. Ametunga vitabu mbalimbali, lakini anafahamika zaidi kwa kitabu chake cha "Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes" kilichotolewa kwa lugha ya Kiingereza kwa mara ya kwanza 1998. Baadaye kikatafsiriwa kwa Kiswahili na kutolewa tena mnamo mwaka 2002.

Maisha na kazi
Sheikh Mohamed Said Abdallah alizaliwa mnamo tarehe 25 Februari katika mwaka wa 1952 huko Gerezani jijini Dar es Salaam - ambapo ndiko kulikokuwa na asili ya upinzani dhidi ya ukoloni wa Waingereza katika Tanganyika. Babu yake, Mzee Salum Abdallah Popo alikuwa muasisi wa harakati za vyama vya wafanyakazi na alikuwa mmoja kati ya watu wa awali kabisa kuanzisha upinzani na kuunga mkono hoja ya kupinga utawala wa kikoloni. Mwaka wa 1947, Mzee Popo aliongoza mgomo wa kwanza nchini Tanganyika katika majimbo ya kati nchi uliopangwa na wafanyakazi wa Tanganyika Railways. Tanganyika ilipopata uhuru wake mwaka 1961, Mzee Popo aliachana na mkono wa Nyerere kama jinsi wengi walivyofanya na alitiwa kizuizini na serikali kwa ajili ya msimamo wake wa kuwa vyama vya wafanyakazi sharti viwe huru. Akiwa mwenyekiti wa Tanganyika Railways African Union (TRAU) alipinga vyama vya wafanyakazi kuwekwa chini ya Tanganyika African National Union (TANU) chini ya Rais Julius Nyerere. Sheikh Mohamed Said ana shahada katika masuala ya Sayansi ya Siasa kutoka katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Vilevile ana Stashahada katika masuala ya Maritime Studies kutoka katika Chuo Kikuu cha Wales huko mjini [[Cardiff, Uingereza na nyingine ya BIMA kutoka katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha cha Dar es Salaam (IFM).

Utafiti juu ya historia ya uhuru wa Tangayika
Mohamed Said amefanya utafiti mwingi sana juu ya historia ya uhuru wa Tanganyika, historia ambayo kabla ya utafiti wake ilichukuliwa kama iliyohitimishwa na ameweza kufukua mambo muhimu ambayo yalifichwa katika historia iliyokuwa ikitambulikana rasmi. Alianza kufahamika zaidi katika miaka ya themanini kupitia makala zake za kusisimua zilizokuwa zinahangaisha fikra za wasomaji kwa kufichua yale yaliyofichwam zilizoelezea mchango muhimu wa Waislamu na Uislamu katika harakati za kupinga ukoloni katika Tanganyika na khiyana waliofanyiwa Waislamu na serikali zote mbili, yaani, kabla ya uhuru na baada ya uhuru - jambo ambalo kwa wakati ule lilikuwa mwiko kufanyiwa utafiti au kuandikwa. Makala hizo zilipata kuchapishwa katika magazeti na majarida maarufu barani Afrika na katika magazeti ndani na nje ya Tanzania. Baadhi tu ya makala zake za utafiti ni pamoja na "In Praise of Ancestors" (1988), "Africa Events (London), "Abdulwahid Sykes: Founder of a Political Movement" Africa Events - London (1988), "Islam and Politics in Tanzania" (1989), Al Haq Internation (Karachi), "The Plight of Tanzania Muslim" (1993) Change (Dar es Salaam) na "The Secular Unsecular State" (1995) Change (Dar es Salaam).

Huyo ndiye Mohamed Said na Kasomi
Asante sana kwa historia hii, ila ingenoga zaidi kama pia ungeeleza alisoma wapi primary na sekondari.
P
 
Back
Top Bottom