Mfahamu mzee mwenye nyaraka za ardhi ya Palestina ambayo Waisraeli wamevamia


Ibrahim ni mkaldayo wa Iraq,mji ulio 300km kusini mwa Baghdad q,ambako huko kusini ndipo Iraq inakopakana na Saudi Arabia
 
PART 1

Yesu aliwachana waziwazi Wayahudi (Waisraeli) kwa kuwa waliwakataa na hata kuwaua manabii wa Mungu adhabu yao wangetawanywa kutoka kwenye ardhi yao

Na kweli wakati wa utawala wa Roma wakawa watumwa wa Roma na wakatawanyika kutoka kwenye ardhi yao wakaanza kutangatanga

Wengine walikimbilia Ulaya, Marekani na nchi nyingine duniani (Huwa nashangaa wanaosema Israeli taifa teule la Mungu hawa jamaa walilaaniwa na hii ilikuwa adhabu yao)

Turudi kwenye historia;

Walipoanza kutanga tanga ardhi yao ikamilikiwa na Wapalestina

Baada ya Wayahudi zaidi ya milioni 6 kuuawa na Hitler na kutokea kwa vuguvugu la Wayahudi kubaguliwa kwenye baadhi ya mataifa waliyokimbilia, mwaka 1948 Wayahudi wakaanzisha movement iliyoitwa Zionism

Lengo la movement lilikuwa kuitwaa ardhi ambayo kihistoria wanadai ilikuwa yao ila wakati huo ilikuwa inamilikiwa na Wapelestina

Sasa wangeingiaje kuitwaa hiyo ardhi? Inaendelea PART 2
 
Huyu mzee ni kama wale wanasiasa wa bongo ambao walisajiri vyama vya siasa wakaishia kutembea na vyama hivyo kwenye briefcases zao, wakizunguko vijiwe vya kahawa wakianzisha ubishi utakaopelekea kufungua briefcase kuonyesha hati za vyama.
Siku walipopigwa mitama na kuporwa briefcase na vyama navyo vikapotelea hapohapo
 
PART 2
Sasa wangeingiaje kuitwaa hiyo ardhi?

Israel wakapata support ya Marekani, Uingereza na Umoja wa Mataifa

Kilichofanyika Wayahudi walipojiorganise wakawapa mitaji Wayahudi wenzao waende kwenye ardhi ya Palestina ambayo kihistoria wanadai yao

Wayahudi hao walienda kama wakulima wakubwa kuwekeza (settlers) na walihodhi maeneo makubwa sana

Na mbinu hii Wapalestina hawakuigundua na kama wangeigundua wasingekubali si tu kuwapa ardhi ya kilimo bali hata wasingewakaribisha

Basi wakulima hao feki Wakiyahudi wakaanza kuchukua ardhi kubwa wakaanza na kuwaleta wenzao kutoka Ulaya, Marekani na pande zote za dunia

Mdogomdogo kizazi cha Wayahudi kikaanza kuongezeka

Kwa msaada wa Marekani, Ungereza na Umoja wa Mataifa wakaanza kuipora ardhi ya Wapestina mpaka leo tunavyoona

NB: Kabla ya 1948 hakukuwa na nchi ya Israel kwenye ramani ya dunia. Na ndio nchi pekee mipaka yake inaongezeka kwenye ramani ya dunia kadiri wanavyoipora ardhi ya Wapalestina
 
Hii hii quran waraka wa kiarabu?
 
Umeeleweka mkuu
 
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Wana endelea kufuatilia kwa awamu,karibuni wanaingia awamu ya pili
 
bora hati iyo ina miaka 117 sasa biblia ina miaka 4000 na uchafu...ndan yake kuna uthibitisho wa ardhi iyo kuwa mali yao tena inasema hawajanunua bali wamepewa na MUNGU bure🤣😅😆😁😄
 
Kiuhalisia israel ni wavamizi,hilo eneo hata wakati ibrahimu anaoneshwa kuwa atakuja kupewa,tayari kulikua na watu wanaoishi(makabila mbalimbali ambayo yanaunda palestina),ilibidi Mungu awapatie eneo ambalo halina watu na sio kufanya uvamizi uliosababisha vita vya muda mrefu na mauaji ambayo ni tatizo hadi leo hii tunavoongea
 
Nimepata Jambo hapo kwenye hiyo nyaraka ambayo imenipa maswali mengi swali langu hiyo hati iliyolewa jurish ni wapi na jina Hilo Lina maana ipi.
Nini history ya jina Hilo jurish
 
wakipata yote kuna nchi zitajikuta ziko ndani ya mipaka ya israel. Kwenye zile vita israel ilitakiwa izipige zile nchi zilizounda umoja wa kupambana nayo ili iteke maeneo makubwa zaidi
Iliteka maeneo mengi tu makubwa kama Gaza, Sinai ila iliyarudisha kama njia ya kurudisha amani.
 
Israel hati zake za kumiliki hayo maeneo alikabidhiwa Ibrahim na Mwenyezi Mungu kwa hiyo huyo mzee asiwapotoshe
 
Ukianzia Kwa Sumerians ,Kisha Anunak,ni rahisi kutrack,lkn ukianzia kwenye Biblia na Quran, ni rahisi kupotea Kwan zimeandikwa Kwa mitindo ya Summary sana na hazianzii mbali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…