Mfahamu Nemanja Vidic

Mfahamu Nemanja Vidic

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,976
NEMANJA VIDIC NI JIWE AMBALO FERGUSON ALIJENGA KANISA JUU YAKE
.
Kwanza leo nipo ndotoni lakini ajabu sana naota Kilatini leo, 'Veni vidi vici' Came, saw and Conquered, ndio ni stori ya binadamu mmoja kutoka Kusini mwa Ulaya pale Serbia, ndio maskani ya Nemanja Vidic, aliemfanya Babu afanye Umafia kwa Florence ili kunasa saini yake.
.
Alimsaini ile siku ya Christmass ya 2005, mtoto huyu aliekuwa anaishi kwa kukimbia mabomu pale Yugoslavia, ndio huyu na wenzake waliwafanya Cristiano Ronaldo, Tevez, Giggs na wakina Rooney wacheze wanavyotaka, huyu alisimama kama Mwamba wa jengo hilo.
.
Walikuja kutengeneza ukuta pale Old Trafford, golini una Edwin Van Der Sar, mbavuni una Garry Neville na Patrice Evra, kwenye ulinzi wa kati una Rio Ferdinand na Nemanja Vidic, pacha bora kuwahi kutokea ukisahau ile ya Bruce na Pallister, once upon a time in Manchester, wallahy vile walikuwa wanyama[emoji119]
.
Rio akisimama kama Kiongozi, ila mbele yake alikua na Vidic aliyekuwa binadamu aliyezaliwa bila damu hakuwa muoga wala kujali, ukiweka mguu yeye ataweka kichwa, hakuwa anajali chochote, simply hakuwa binadamu bali chuma.
.
Majukwaa ya Old Trafford yalikuwa yanamtazama kama Chuck Norris, mitaani kwangu pale Kusini walikua wanamtazama kama Anorld The Terminator, hakuwa na style ya nywele[emoji23]hakuwa anaziwaza hata kidogo, kwenye 50-50 Challenge yeye alikua anakupa 150- Nil, atakaba kibabe na kuondoka na gozi la mnyama.
.
Nyuma ya jina lake kuna EPL tano, kombe la ligi tatu na UEFA yake, bila shaka unakumbuka usiku wa pale Moscow alivyotembea na Didier Drogba, alimuweka mfukoni na kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa, mnakumbuka header yake dhidi ya Sunderland 2009 kuhakikisha United wanabeba ndoo.
.
Ana rekodi kubwa ya clean sheet na kupora mipira, namuweka daraja moja na wakina Tony Adams, binadamu aliefanya kazi ya Ferdinand iwe rahisi sana, ila aliwahi kukiri Didier Drogba na Fernando Torres ni mastraika hatari kuwahi kucheza nao[emoji4].
.
Naanza kustuka usingizini, nasikia Vidic kazidiwa na VVD? Sina la kusema ila VVD na Vidic hawafanani kimchezo, VVD mlinganisheni na Ferdinand, hawa wote mabishoo[emoji23] Vidic ni mbwa wa kusaka mpira na beki halisi msimuweke sehemu ya hao Period!

NEMANJA VIDIC NI JIWE AMBALO FERGUSON ALIJENGA KANISA JUU YAKE.

Vidic.jpg
 
Uliangalia fainali ya UEFA ile waliyocheza Fc Barcelona na Man U? Nadhani ilikua 2009 kama sikosei. Ungewaonea huruma hao unaowataja Vidic na wenzake
 
Vidic na Rio walikua mabeki hodari kabisa katika kipindi walicho cheza pamoja. Goli la kichwa alilofunga Mess katika fainal ile ni jambo la kushangaza mbaka leo. Mpira ambao Rio ameruka juu kwa uwezo wake wote na ku ukosa, nyuma ya bega lake anaruka kichwa andunje Mess anaupiga kichwa na kufunga.
Nijambo ambalo atayeye Mess analishangaa mbaka leo. Mwisho wa siku mpira ndivyo ulivyo na mambo ya kushangaza, lakini hilo haliondoi ubora wa ile pair ya Vidic na Rio.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe umeandika Kama shabiki wa mpira sio hao wehu wengine huko juu hongera mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umesema kweli kabisa kuna pair tano nazikumbuka sana, combination bora kabisa kuwahi kutokea kwenye miongo miwili ya soka 2000-2020.

1; Vidic na Rio Ferdinand man u

2;Gerald Pique na Carlos Puyor Barcelona

3;Ramos na Pepe R. Madrid.

4; Jonh Terry na David Luis Chelsea.

5;Vicent Company na Michael Richard
Man City
 
Huyo Vidic na mwenzake Rio walikuwa kama mademu wa kirangi au Mbulu,beki hazikabi kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mabeki wa kati bora kabisa kuwahi kutokea mkuu.
Usiwasahau na wakina
Jonh Terry
Carlos Puyor
Pepe
Ramos
David Luis
Vicent Company
Vicent Colocheny( Kama sijalikosea jina lake) huyu alikuwa Newcastle United
Colo You're
Thiago silver
Fabio Canavarho
 
Umesema kweli kabisa kuna pair tano nazikumbuka sana, combination bora kabisa kuwahi kutokea kwenye miongo miwili ya soka 2000-2020.

1; Vidic na Rio Ferdinand man u

2;Gerald Pique na Carlos Puyor Barcelona

3;Ramos na Pepe R. Madrid.

4; Jonh Terry na David Luis Chelsea.

5;Vicent Company na Michael Richard
Man City

2000-2020 huwezi kuwa serious mzee.

Futa uvute kumbukumbu vizuri kisha uandike upya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umesema kweli kabisa kuna pair tano nazikumbuka sana, combination bora kabisa kuwahi kutokea kwenye miongo miwili ya soka 2000-2020.

1; Vidic na Rio Ferdinand man u

2;Gerald Pique na Carlos Puyor Barcelona

3;Ramos na Pepe R. Madrid.

4; Jonh Terry na David Luis Chelsea.

5;Vicent Company na Michael Richard
Man City

Hapana kwa chelsea mkuu nakataa

Safu kali ya ulinz kuwahi kuiona pale chelsea ni hii

John terry Na Ricardo Carvalho

Ashley cole Na william Gallasa

Huo ni moto.
 
Hapana kwa chelsea mkuu nakataa

Safu kali ya ulinz kuwahi kuiona pale chelsea ni hii

John terry Na Ricardo Carvalho

Ashley cole Na william Gallasa

Huo ni moto.
Ni kweli mkuu lkn unausahau vipi mchango wa David Luis mwamba alie simama imara hadi wanatwaa ndoo ya UEFA 2012 mbele ya Buryan ya Roben, Ribery, Muller na Gomez.

Mwamba alie simama kumzuia Messi asitambe kabisa kwenye nusu final
Mkuu mkumbuke kidogo tu.
 
Definitely mkuu lazima David Luiz apewe heshima yake though amekuwa uchochoro siku hizi lkn jamaa alikuwa mwamba kweli kweli no matter hata Kama walitatuliwa 7-0 na German machine kwenye world cup

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fernando Torres aliwahi kuwafunga Tella na Mwenzake Rio Ferdnand. Lakini ukweli Mwamba alikuwa nondo kweli kweli, kumtia mtama Mshambuliaji kwenye 18 kwake haikuwa issue.
 
Kuna ile beki moja kali sana ilikuwa Man U SAF akawauzia Arsenal kwa bei ya record ya Dunia ya kuitwa Silvester Mbona umeihau
 
Umesema kweli kabisa kuna pair tano nazikumbuka sana, combination bora kabisa kuwahi kutokea kwenye miongo miwili ya soka 2000-2020.

1; Vidic na Rio Ferdinand man u

2;Gerald Pique na Carlos Puyor Barcelona

3;Ramos na Pepe R. Madrid.

4; Jonh Terry na David Luis Chelsea.

5;Vicent Company na Michael Richard
Man City
Mkuu Na.4 happy naona humtendei haki mtu anaitwa Ricardo Cavalho alitengeneza pacha matata na John Terry.Pia pale AC Milan walikuwepo Jap Stam na Allesandro Nesta, huu nao ulikuwa ukuta zege kweli kweli!
 
Back
Top Bottom