Matanga
JF-Expert Member
- Nov 13, 2019
- 2,281
- 3,976
NEMANJA VIDIC NI JIWE AMBALO FERGUSON ALIJENGA KANISA JUU YAKE
.Kwanza leo nipo ndotoni lakini ajabu sana naota Kilatini leo, 'Veni vidi vici' Came, saw and Conquered, ndio ni stori ya binadamu mmoja kutoka Kusini mwa Ulaya pale Serbia, ndio maskani ya Nemanja Vidic, aliemfanya Babu afanye Umafia kwa Florence ili kunasa saini yake.
.
Alimsaini ile siku ya Christmass ya 2005, mtoto huyu aliekuwa anaishi kwa kukimbia mabomu pale Yugoslavia, ndio huyu na wenzake waliwafanya Cristiano Ronaldo, Tevez, Giggs na wakina Rooney wacheze wanavyotaka, huyu alisimama kama Mwamba wa jengo hilo.
.
Walikuja kutengeneza ukuta pale Old Trafford, golini una Edwin Van Der Sar, mbavuni una Garry Neville na Patrice Evra, kwenye ulinzi wa kati una Rio Ferdinand na Nemanja Vidic, pacha bora kuwahi kutokea ukisahau ile ya Bruce na Pallister, once upon a time in Manchester, wallahy vile walikuwa wanyama[emoji119]
.
Rio akisimama kama Kiongozi, ila mbele yake alikua na Vidic aliyekuwa binadamu aliyezaliwa bila damu hakuwa muoga wala kujali, ukiweka mguu yeye ataweka kichwa, hakuwa anajali chochote, simply hakuwa binadamu bali chuma.
.
Majukwaa ya Old Trafford yalikuwa yanamtazama kama Chuck Norris, mitaani kwangu pale Kusini walikua wanamtazama kama Anorld The Terminator, hakuwa na style ya nywele[emoji23]hakuwa anaziwaza hata kidogo, kwenye 50-50 Challenge yeye alikua anakupa 150- Nil, atakaba kibabe na kuondoka na gozi la mnyama.
.
Nyuma ya jina lake kuna EPL tano, kombe la ligi tatu na UEFA yake, bila shaka unakumbuka usiku wa pale Moscow alivyotembea na Didier Drogba, alimuweka mfukoni na kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa, mnakumbuka header yake dhidi ya Sunderland 2009 kuhakikisha United wanabeba ndoo.
.
Ana rekodi kubwa ya clean sheet na kupora mipira, namuweka daraja moja na wakina Tony Adams, binadamu aliefanya kazi ya Ferdinand iwe rahisi sana, ila aliwahi kukiri Didier Drogba na Fernando Torres ni mastraika hatari kuwahi kucheza nao[emoji4].
.
Naanza kustuka usingizini, nasikia Vidic kazidiwa na VVD? Sina la kusema ila VVD na Vidic hawafanani kimchezo, VVD mlinganisheni na Ferdinand, hawa wote mabishoo[emoji23] Vidic ni mbwa wa kusaka mpira na beki halisi msimuweke sehemu ya hao Period!
NEMANJA VIDIC NI JIWE AMBALO FERGUSON ALIJENGA KANISA JUU YAKE.