Hahahahah daaah kwa hiyo Yale matokeo ya necta Ni kiini macho[emoji2][emoji2][emoji2]
Ila nyinyi mna matokeo halisi[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Daaah daah[emoji44][emoji44][emoji44][emoji119]
Yale huwa ni nakala ya matokeo kupitia vituo vya mitihani, yaani shule. Lakini huwa kuna orodha ya matokeo ya watahiniwa wote yaliyopangwa kwa ufaulu kuanzia mwanafunzi wa kwanza mpaka mwanafunzi wa mwisho kitaifa.
Pia huwa kuna orodha ya wanafunzi bora waliofanya vizuri kitaifa katika kila somo lililosajiriwa na NECTA.
Yaani kwenye masomo yote huwa kuna mwanafunzi aliyeongoza kitaifa na orodha zao huwa zipo, mwanafunzi wa kwanza mpaka mwanafunzi wa mwisho kitaifa katika kila somo.
Taarifa hizi huwezi kuzipata kwingine, tofauti au mbali na vitabu vya wahitimu. Huwa kuna vitabu vya wahitimu vinavyoonesha idadi yote ya wahitimu waliofanya mtihani wa taifa.
Hivi vitabu vya wahitimu ndio huwa vinavyotumika kujaza taarifa za wanafunzi kwenye faili la maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi husika.
NECTA huwa wanaonesha madaraja ya ufaulu tu, yaani DIVISION ONE, DIVISION TWO, DIVISION THREE, DIVISION FOUR na DIVISION ZERO. Lakini hivi vitabu vya wahitimu vinavyoonesha mambo yote kwa pamoja, yaani nafasi ya mwanafunzi kitaifa na daraja la ufaulu.
Na unatakiwa kufahamu kuwa kuandaa au kuchapisha cheti cha matokeo ya mwanafunzi huwa ni hatua ya mwisho kabisa, hapa ndio wanaachiwa baraza la mitihani kuchapisha vyeti vya wahitimu, yaani wanafunzi.
Lakini wanaosahisha mitihani ya wanafunzi huwa sio watu kutoka NECTA, huwa kuna tume maalum [ tume isiyo rasmi ] inayoteuliwa na ofisi ya rais kusahisha mitihani ya wanafunzi husika. Hii tume maalum anaweza kuchaguliwa mwalimu yoyote kutoka shule yoyote ya serikali au isiyo ya serikali pasipo hata NECTA kujua.
Na kila somo huwa linasahishwa katika mkoa ulioteuliwa kwa mwaka huo. Yaani hii tume maalum inaweza kuamua mwaka huu somo la Mathematics likasahishwa mkoa wa Iringa! Somo la Biology likasahishwa mkoa wa Kagera! Somo la Civics likasahishwa mkoa wa Tabora! Somo la Physics likasahishwa mkoa wa Dodoma! Somo la Chemistry likasahishwa mkoa wa Arusha! Yaani hakuna sehemu maalum au watu maalum wa kusahisha mitihani, huwa inabadilika kila mwaka ili kuondoa ubadilifu.
Baada ya kusahisha mitihani katika kila mkoa ulioteuliwa kwa mwaka huo, huwa wanajumuisha masomo yote ili kupata matokeo ya ujumla kwa kila mwanafunzi. Na hapo ndio huwa anapatikana mwanafunzi wa kwanza mpaka mwanafunzi wa mwisho kitaifa.
Lakini kuandaa au kuchapisha vyeti huwa wanaachiwa Baraza la Mitihani, yaani NECTA.
Hapa NECTA ndio huwa wanacheza na nakala za matokeo kwenye kuandaa vyeti tu na kuvituma kwenye vituo vya mitihani yaani shule baada ya kupokea matokeo halisi kutoka ile tume maalum ya usahishaji.
Sasa hii tume maalum huwa iko chini ya ofisi ya rais, na wajumbe wa hii tume huwa wanakula kiapo cha utii na kutunza siri za kitaaluma za wanafunzi waliofanya mtihani wa taifa.
Baraza la Mitihani yaani NECTA huwa wanaandaa au kuchapisha vyeti tu maana hata kutangaza wanafunzi bora waliofanya vizuri kitaifa lazima wapate idhini ya Rais, wanaita OPD au PDO [ PRESIDENTIAL DECREE ORDER ]. Ndio maana kuna miaka mingine unaona orodha ya wanafunzi bora na miaka mingine orodha ya wanafunzi bora huwa hakuna. Hapo Rais anakuwa hajatoa idhini ya kutangaza wanafunzi bora waliofanya vizuri kitaifa.
Nadhani tumeelewana sasa! Kwa hiyo, michezo yote michafu huwa inafanyika hatua ya mwisho ya kuandaa au kuchapisha vyeti vya wahitimu yaani wanafunzi. Lakini matokeo halisi baada ya kusahisha huwa yapo na haya ndio huwa yanatumika pia kuchapisha vitabu vya wahitimu.