Kuna Civil Engineer kutoka chuo kikuu cha Dar Es Salaam [UDSM] anachonga madirisha.
Na ukiangalia vyeti vyake ana matokeo mazuri tu ya kidato cha nne na kidato cha sita.
Matokeo ya kidato cha nne ana division one ya point 7 [2008] na matokeo ya kidato cha sita ana division one ya point 7 [2011].
Lakini TSM9 inagoma! Hii fomu ndio inayotoa taarifa sahihi za mwanafunzi husika.
TSM9 inasoma kidato cha nne alipata division one ya point 11 na kidato cha sita alipata division three ya point 13.
Kwahiyo inaonekana kuna udanganyifu ulifanyika katika kuwasilisha matokeo ya huyu mwanafunzi kwenye nakala za matokeo, yaani vyeti.
Hapa inaonekana ilitumika rushwa! Kama tunavyofahamu shule binafsi zinavyofanya ili kuvutia wateja.
Na matatizo kama haya ndio atapata muhitimu pale atakapohitimu masomo yake na kuanza kutafuta ajira.
Watahiniwa 1,059 wafutiwa matokeo, wakosa nafasi kurudia
Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) limewafutia mitihani watahiniwa 1,059 kutoka shule 38
zilizofanya udanganyifu katika mitihani hiyo.
Herieth Makwetta,
Mwananchi
hmakwetta@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam.
Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) limewafutia mitihani watahiniwa 1,059 kutoka shule 38 zilizofanya udanganyifu katika mitihani hiyo.
Akitangaza matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi (PSLE) leo Jumamosi, Novemba 21, 2020 Katibu Mtendaji wa Necta Dk Charles Msonde amesema watahiniwa hao hawatapata nafasi nyingine ya kurudia matokeo hayo.
Msonde alisema pamoja na kamati ya mitihani kutimiza wajibu wao vizuri, kulijitokeza matukio machache ya udanganyifu wa mitihani katika baadhi ya shule nchini.
“Jumla ya shule 38 sawa na asilimia 0.22 ya shule zote za msingi 17,329 zilizofanya mitihani, zimebainika kufanya udanganyifu wa mitihani kwa namna mbalimbali. Watahiniwa 1,059 sawa na asilimia 0.1 ya wote 1,023,950 waliofanya mitihani walibainika kudanganya,” alisema Dk Msonde.
Msonde alisema shule hizo zilifanya makosa mbalimbali ikiwamo kuiba mitihani, kugawa majibu kwa wanafunzi na kubadilisha watahiniwa kwa kuwaweka wasio halisi kuwafanyia mitihani wanafunzi watoto.
Shule zilizobainika kufanya udanganyifu huo ni pamoja na shule za msingi za Ngiloli, Nguyami, Ibuti, Ihenje, Bwawani, Mogohigwa, Chakwale, Msingisi zilizopo Halmashauri ya Gairo.
Zingine ni Mafiri, Kibogoji, Ng’wambe, Digalama, Dihinda kutoka Halmashauri ya Mvomero na shule za msingi za Nyawa A iliyopo Halmashauri ya Bariadi vijijini (Simiyu).
Shule zingine ni za Halmashauri ya Chabutwa, Sikonge Tabora ikiwemo shule yawmsingi Chabutwa, shule ya msingi Usagari, Uyui Tabora shule ya msingi Siashimbwe iliyopo Moshi Kilimanjaro, Dominion Arusha, Matogoro ya Tandahimba Mtwara, Ng’arita Bariadi vijijini Simiyu, Olkitikiti Kiteto iliyopo Manyara na Nyamimina Buchosa Mwanza