Mfahamu T.O Kihombo 2006 aliyepata Degree yake ya Kwanza baada ya Miaka 11

Mfahamu T.O Kihombo 2006 aliyepata Degree yake ya Kwanza baada ya Miaka 11

Dah haya maisha Mungu tu anajua. Yaani jamaa na degree yake ya Petroleum anauza vitini wakati kuna washkaji nawafahamu wana vidiploma vya DIT wanapiga pesa ndefu kwenye makampuni ya PUMA Oryx nk. Full mikoko ya kutembelea mishahara ya hatari. Mungu ambariki aendelee kutengeneza vitini ndo wito wake alioitiwa na mwenyezi Mungu
Vidiploma ndio elimu gani
 
Huu uzi bhana!
Umejaa Watu hawa;
walioshindwa,
Wasiopenda mafanikio ya wengine,
Kutofautiana katika uelewa wa dhana ya mafanikio ni nini?
 
Imepita miaka takribani 12 sasa, tangia Tanzania ilipapata kumshuhudia mwanafunzi aliyeshindikana katika maswala ya Elimu hapa namzungumzia,Tanzania One (2006) Elias Kihombo katika matokeo ya Kidato cha Sita mwaka 2006 akitokea shule ya sekondari Tosamaganga wengi wanapenda kuiita Tosa Boy's

Mwaka 2006, Necta ilimtangaza mwanafunzi Elias Kihombo kutoka Tosamaganga Secondary School kuwa ndo kipanga wa mwaka huo akiwapita wanafunzi wenye akili zaidi waliovuma toka shule kongwe na special schools kama kibaha, ilboru, mzumbe, kilakala, Tabora boys etc ukweli ni kwamba Elias Kihombo hakuwa maarufu kwa kipindi hiko na wengi walisikia tu story zake haswa kwa wanafunzi wa Mzumbe Boys ambao Mara nyingi walipata kumuona katika mazingira yao.

Kumbuka kwamba Elias Kihombo hakupewa Priority kubwa sana ya kuwa T.O wa Advance Level kutokana pia na matokeo yake ya Kidato cha Nne (4) kuonekana kuwa ya kawaida sana, Kihombo alifanikiwa kupata Division One (1.14) akiwa na Physics-A Chemisrty-A Biology na Mathematics-B, Ndipo mwaka huo 2003 alipata kuchaguliwa Tanga Technical school iliyopo mkoa wa Tanga (tetesi), lakini baadae aliamua kurudi tena katika shule yake ya zamani yaani Tosamaganga secondary kuendelea na masomo yake ya Advance level. Alimaliza hapo hapo akifanikiwa kuwa mwanafunzi wa kwanza toka Tosamaganga kwa Advance Level kuwa mwanafunzi bora kitaifa, Alifanikiwa kupata maksi za juu sana na kupata Division One (1.3)
Physics-A
Chemistry-A
Advanced Mathematics-A

October 2006 Alichaguliwa kujiunga na University of Dar Es Salaam (UDSM) akiwa kama T.O kusoma Bachelor of Science In Telecommunication Engineering (4years) na tetesi zinasema alifanikiwa kupata ufadhili wa masomo yake chini ya kampuni ya Airtel.
Siku zilienda na alikuwa karibu kumaliza Elimu yake ya chuo kikuu, huku akipata madili mengi ya kufundisha Tuition maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar Es Salaam na shule nyingi za sekondari ndani ya Tanzania hasa shule za Advance.

Lakini baada ya Miaka 4 kupita ikiwa miezi michache tu imebaki ya kumaliza chuo Tanzania One Kihombo alidisco chuo na hivyo kumfanya asifanikiwe kupata degree yake ya kwanza mwaka huo 2010, lakini wengi wanasema hakupaswa kudisco chuo lakini ndivyo ambavyo Hatima yake ilipoishia hapo. (tetesi [emoji6] [emoji6]).

Moja kati ya maneno ambayo wengi wanamnukuu aliyopata kuyasema ndani ya Miaka hiyo, alisema "Duniani walionipita kwa akili ni watu wawili tuu wa kwanza Mola, wa pili ni Mzungu" hapa ndipo hatima yake inavyosemekana ikafungwa na wakuu wake lakini wengine wanasema vingine.

Elias hakutaka kwenda chuo chochote kile na ndani ya Miaka hiyo mitatu baada ya kudisco chuo, yaani 2011,2012 na 2013 alikuwa anazunguka shule mbalimbali za sekondari Tanzania kupiga mapindi ya Physics na Chemistry na kwelii huyu jamaa alikuwa ni Invisible katika masomo hayo mawili, Japo Pure Mathematics alikuwa hafundishi kabisa kwasababu alikuwa anasema "Siwezi kufundisha Somo rahisi duniani kama Pure Mathematics, Mimi nafundisha Physics na Chemistry tu"

Ndipo baada ya Miaka mitatu kupita (3) T.O aliyetukuka zaidi katika vinywa vingi vya wanafunzi wa Tanzania, kutokana na ufundishaji wake na kuwaita wanafunzi wake Nyumbu na kuwa na Jeuri zaidi ya Akili zaidi ya watu wengine, alifanikiwa kurudi tena ndani ya University of Dar Es Salaam safari hii akiwa ameamua na amezamilia kuchagua kozi nyingine Mpya kabisa iliyoanzishwa mwaka huo 2013 hapohapo Udsm iliyoitwa (Bachelor of Science In Petroleum Engineering). Hii kozi ilikuwa inachukua wanafunzi 20 pekee Tanzania nzima tena wale waliosoma PCM tu (Physics, Chemistry na Advanced Mathematics) na waliopata Marks za juu kabisaa.

Baada ya Miaka 4 kupita, ndipo July 2017, T.O Elias Kihombo alifanikiwa kumaliza Degree yake ya kwanza (Bachelor of Science In Petroleum Engineering) na mnamo November 2017 Elias Kihombo alifanikiwa kutunukiwa Degree yake ya kwanza akiwa ndani ya University of Dar Es salaam baada ya Miaka 11 kupita.

Hapa imepita Miaka mingi tangia, 2006 Engineer Elias Kihombo alivyotangazwa kuwa Tanzania One lakini ilimchukua Miaka mingine 11 mpaka kutunukiwa Degree yake ya kwanza. Huyu ndiye The Best Of The Best, Eng Elias Kihombo Mwanafunzi aliyepata kutokea Tanzania na kuwaonesha wengine uwezo wakee katika nyanja nzima ya Elimu.

Wapo wengi wanaojiuliza Eng Elias Kihombo yupo wapi kwasasa, Lakini mpaka sasa Kihombo yupo chini ya Himaya ya Mkoa wa Geita Nyumbani kwa Mheshimiwa Rais John Joseph Pombe Magufuri, huku akiendeleza harakati zake na akiwa na vitabu vyake vingi alivyoviandika kuwasaidia vijana wa Tanzania ikiwa pamoja na Physics Books na Chemistry Books.


Written by Eng EVANS RICHARD.

*We Always Live To Fight Another Day*




View attachment 818214View attachment 818215View attachment 818222
GPA please
 
kuna jamaa anaitwa Jamal aka Babu waliosoma Azania nahis story zake wanazifahamu
 
Huyu jamaa si masikhara ni kichwa balaa ila anadharau sana alitufundisha pale Tosamaganga physics na Chemistry na alitusaidia wengi ambao tulikuwa hatujacover baadhi ya topics , mzee wa vimangala na nyumbu dah ! basi ilikuwa tafrani tupu , kwa wale ambao mmesoma PCB na PCM mtaelewa ninachomaanisha , ugumu wa yale masomo halafu mtu anatembeza maswali bila kugusa kitabu asubuhi saa 1 hadi saa 5 usiku si utani

Ye alikuwa anaanza topic anafundisha theory zake na maswali mnamtajia nyie kutoka kwenye mavitabu yenu mnayoyajua halafu ananayasolve na mnaangalia na kujiridhisha kama majibu ni kweli , huyu mshikaji angekuwa mbali sana sema tatizo lake kubwa ndo hilo ni mkorofi sana
 
Back
Top Bottom