Kamwene kamwene
JF-Expert Member
- Jul 7, 2019
- 1,159
- 2,601
Ukisoma comments za humu hasira zinaishia kula kambwa tu..
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yes Ni kweli hiyoKwa wachache Hesabu ni rahisi lakini kwa walio wengi Hesabu ni Janga sio mchezo kabsa kabsa.[emoji22] [emoji22]
ZNilimuona kihombo mwaka 2014 nikiwa mwaka wa NNE pale COET. Nilimfahamu kabla hasa baada ya sifa zake kuvuma sana mwaka 2006. Nijuavyo Mimi, kihombo ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kukariri na kufundisha tu. Si innovative kabisa
Huyo Jamaa kasaidia wAtu wengi , ww humtaki !! Walimu wengine wapo lakini wachovu tuNimeuona mswada wa Tanzania Teachers Board of Professional Act 2018. Unakataa haya mambo. Tuombe upite salama hawa sio walimu hawa ni wale wanaosimama tu mbele ya wanafunzi haphazardly
Inalinda fani bila ya kuangalia maslahi ya walaji ? Walaji Ni wanafunzi ambao wanaridhika na inputs za watu hao , au unataka watu wafuate vyeti tu vya ualimu bila ya uwezo ? Maana kuwa na cheti Cha ualimu haina maana kuwa una uwezo wa kufundishaNa hii imeongeza ukosefu wa ajira kwa watu wenye sifa stahiki za taaluma husika.
Setikali lazima inapotengeneza fani iilinde fani yenyewe pamoja na maslahi husika.
Sent using Jamii Forums mobile app
Watu wengi Wana roho ya kwann na husdaHuyo mwalimu wa tuition anauwezo wa kuwa pita katika ufundishaj hata walimu waliosomea ualimu mara 1000 halafu kwenye hizo tuition zake anaingiza pesa nyingi kuliko mfanya kazi yeyote hapa tanzania. Kifupi ukimsikia Elias kihombo unatakiwa kusema 👉 He is anaother person in this education sector
-----Appreciate uwezo wa mtu bro yani elias ni mtu
Wenzake na ONTARIO nadhani walikua batch moja si ndio!Ila kiukweli MA TO wa Tz hawafiki mbali kuliko vichwa vyao..... Mi mshkaji wangu aliyemaliza na TO Elias PETROLEUM yupo kitaa, wkt alikuwa nae To 2013
Uko sahihiHuu uzi bhana!
Umejaa Watu hawa;
walioshindwa,
Wasiopenda mafanikio ya wengine,
Kutofautiana katika uelewa wa dhana ya mafanikio ni nini?
Mwaka gani hiyo kaka? mechanics uliipiga kisawasanmekumbuka maisha ya fizikia [emoji23]
namaliza mtihani wa taifa paper one ndani ya saa moja na nusu wasimamizi wanahisi nmeibia wanafungua na calculator [emoji28]
that life was awesome
Sent using Jamii Forums mobile app
zamani sana mechanics nlimaliza kabla ya kuanza form fiveMwaka gani hiyo kaka? mechanics uliipiga kisawasa
Upo sahihi kabsa brother.Huu uzi bhana!
Umejaa Watu hawa;
walioshindwa,
Wasiopenda mafanikio ya wengine,
Kutofautiana katika uelewa wa dhana ya mafanikio ni nini?
Daah mkuu hili umeongea point sana, madaktari wameacha kazi za kutibu wagonjwa hospitali kama Dk Hamisi Kigwangala ameenda kwenda siasa. Na wengne wapo vyuoni wanafundisha wanafunzi. Wanasheria wameacha Nazi zao wanafundisha wanafunzi vyuoni na wengne wapo kwenye mambo yao binafaiiKwani MAENGINEER WANAFUNDISHWA NA NANI VYUO VIKUU KAMA SIO WENZAO? MADAKTARI JE? TUMUUNGE MKONO KWA KUSAIDIA WANAOKUJA CHINI
Sijajua alipata GPA ya ngapi, ila nitakupa mrejesho soon nikipata detailsGPA please
Amewasaidia wengii hasa alivyodisco chuo mwaka 2010 mpka 2013 alivyokuwa kitaa. Mwaka 2012-13 alikuwa pale TOSAMAGANGA BOY'S HIGH SCHOOL chini ya utawala wa Headmaster wa shule aliyeitwa J.J SHULLA kabla ya mwezi January 2013 kupelekwa uhamishoni Kuwa Headmaster wa ILBORU HIGH SCHOOL (ARUSHA)Huyu jamaa si masikhara ni kichwa balaa ila anadharau sana alitufundisha pale Tosamaganga physics na Chemistry na alitusaidia wengi ambao tulikuwa hatujacover baadhi ya topics , mzee wa vimangala na nyumbu dah ! basi ilikuwa tafrani tupu , kwa wale ambao mmesoma PCB na PCM mtaelewa ninachomaanisha , ugumu wa yale masomo halafu mtu anatembeza maswali bila kugusa kitabu asubuhi saa 1 hadi saa 5 usiku si utani
Ye alikuwa anaanza topic anafundisha theory zake na maswali mnamtajia nyie kutoka kwenye mavitabu yenu mnayoyajua halafu ananayasolve na mnaangalia na kujiridhisha kama majibu ni kweli , huyu mshikaji angekuwa mbali sana sema tatizo lake kubwa ndo hilo ni mkorofi sana
Hivi kuna orodha yoyote inayoonesha huyu mwanafunzi aliongoza kidato cha sita mwaka 2006? Kama ipo, naomba utuoneshe?Imepita miaka takribani 12 sasa, tangia Tanzania ilipapata kumshuhudia mwanafunzi aliyeshindikana katika maswala ya Elimu hapa namzungumzia,Tanzania One (2006) Elias Kihombo katika matokeo ya Kidato cha Sita mwaka 2006 akitokea shule ya sekondari Tosamaganga wengi wanapenda kuiita Tosa Boy's
Mwaka 2006, Necta ilimtangaza mwanafunzi Elias Kihombo kutoka Tosamaganga Secondary School kuwa ndo kipanga wa mwaka huo akiwapita wanafunzi wenye akili zaidi waliovuma toka shule kongwe na special schools kama kibaha, ilboru, mzumbe, kilakala, Tabora boys etc ukweli ni kwamba Elias Kihombo hakuwa maarufu kwa kipindi hiko na wengi walisikia tu story zake haswa kwa wanafunzi wa Mzumbe Boys ambao Mara nyingi walipata kumuona katika mazingira yao.
Kumbuka kwamba Elias Kihombo hakupewa Priority kubwa sana ya kuwa T.O wa Advance Level kutokana pia na matokeo yake ya Kidato cha Nne (4) kuonekana kuwa ya kawaida sana, Kihombo alifanikiwa kupata Division One (1.14) akiwa na Physics-A Chemisrty-A Biology na Mathematics-B, Ndipo mwaka huo 2003 alipata kuchaguliwa Tanga Technical school iliyopo mkoa wa Tanga (tetesi), lakini baadae aliamua kurudi tena katika shule yake ya zamani yaani Tosamaganga secondary kuendelea na masomo yake ya Advance level. Alimaliza hapo hapo akifanikiwa kuwa mwanafunzi wa kwanza toka Tosamaganga kwa Advance Level kuwa mwanafunzi bora kitaifa, Alifanikiwa kupata maksi za juu sana na kupata Division One (1.3)
Physics-A
Chemistry-A
Advanced Mathematics-A
October 2006 Alichaguliwa kujiunga na University of Dar Es Salaam (UDSM) akiwa kama T.O kusoma Bachelor of Science In Telecommunication Engineering (4years) na tetesi zinasema alifanikiwa kupata ufadhili wa masomo yake chini ya kampuni ya Airtel.
Siku zilienda na alikuwa karibu kumaliza Elimu yake ya chuo kikuu, huku akipata madili mengi ya kufundisha Tuition maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar Es Salaam na shule nyingi za sekondari ndani ya Tanzania hasa shule za Advance.
Lakini baada ya Miaka 4 kupita ikiwa miezi michache tu imebaki ya kumaliza chuo Tanzania One Kihombo alidisco chuo na hivyo kumfanya asifanikiwe kupata degree yake ya kwanza mwaka huo 2010, lakini wengi wanasema hakupaswa kudisco chuo lakini ndivyo ambavyo Hatima yake ilipoishia hapo. (tetesi [emoji6] [emoji6]).
Moja kati ya maneno ambayo wengi wanamnukuu aliyopata kuyasema ndani ya Miaka hiyo, alisema "Duniani walionipita kwa akili ni watu wawili tuu wa kwanza Mola, wa pili ni Mzungu" hapa ndipo hatima yake inavyosemekana ikafungwa na wakuu wake lakini wengine wanasema vingine.
Elias hakutaka kwenda chuo chochote kile na ndani ya Miaka hiyo mitatu baada ya kudisco chuo, yaani 2011,2012 na 2013 alikuwa anazunguka shule mbalimbali za sekondari Tanzania kupiga mapindi ya Physics na Chemistry na kwelii huyu jamaa alikuwa ni Invisible katika masomo hayo mawili, Japo Pure Mathematics alikuwa hafundishi kabisa kwasababu alikuwa anasema "Siwezi kufundisha Somo rahisi duniani kama Pure Mathematics, Mimi nafundisha Physics na Chemistry tu"
Ndipo baada ya Miaka mitatu kupita (3) T.O aliyetukuka zaidi katika vinywa vingi vya wanafunzi wa Tanzania, kutokana na ufundishaji wake na kuwaita wanafunzi wake Nyumbu na kuwa na Jeuri zaidi ya Akili zaidi ya watu wengine, alifanikiwa kurudi tena ndani ya University of Dar Es Salaam safari hii akiwa ameamua na amezamilia kuchagua kozi nyingine Mpya kabisa iliyoanzishwa mwaka huo 2013 hapohapo Udsm iliyoitwa (Bachelor of Science In Petroleum Engineering). Hii kozi ilikuwa inachukua wanafunzi 20 pekee Tanzania nzima tena wale waliosoma PCM tu (Physics, Chemistry na Advanced Mathematics) na waliopata Marks za juu kabisaa.
Baada ya Miaka 4 kupita, ndipo July 2017, T.O Elias Kihombo alifanikiwa kumaliza Degree yake ya kwanza (Bachelor of Science In Petroleum Engineering) na mnamo November 2017 Elias Kihombo alifanikiwa kutunukiwa Degree yake ya kwanza akiwa ndani ya University of Dar Es salaam baada ya Miaka 11 kupita.
Hapa imepita Miaka mingi tangia, 2006 Engineer Elias Kihombo alivyotangazwa kuwa Tanzania One lakini ilimchukua Miaka mingine 11 mpaka kutunukiwa Degree yake ya kwanza. Huyu ndiye The Best Of The Best, Eng Elias Kihombo Mwanafunzi aliyepata kutokea Tanzania na kuwaonesha wengine uwezo wakee katika nyanja nzima ya Elimu.
Wapo wengi wanaojiuliza Eng Elias Kihombo yupo wapi kwasasa, Lakini mpaka sasa Kihombo yupo chini ya Himaya ya Mkoa wa Geita Nyumbani kwa Mheshimiwa Rais John Joseph Pombe Magufuri, huku akiendeleza harakati zake na akiwa na vitabu vyake vingi alivyoviandika kuwasaidia vijana wa Tanzania ikiwa pamoja na Physics Books na Chemistry Books.
Written by Eng EVANS RICHARD.
*We Always Live To Fight Another Day*
View attachment 818214View attachment 818215View attachment 818222
Una miaka mingapi?Huyu mwanafunzi hakuwahi kuongoza matokeo ya kidato cha sita, mwaka 2006.
Hata huu wastani wa kupata 98 sio kweli na alipaswa kuchukuliwa hatua na serikali kwa KUPOTOSHA umma.
Na isitoshe hakuna orodha yoyote ya wanafunzi bora iliyokuwa ikitolewa na serikali miaka ya nyuma.
Orodha ya wanafunzi bora kuanzia darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita imeanza kutolewa mwaka 2016, kipindi cha rais Magufuli.