Lazima itakuwa ibapatika hio orodha[emoji2]
Hako la kitabu kenye jina lako ukiwa top ten ndio mzizi wa fitna ulipo
Kiweke hapa uwakate watu kisebengo.
Halafu unaseme necta inaonesha juu tu kwa division 1,2,3,4 huku kwenye kitabu wanagrade vipi ufaulu .
Unamkumbuka Nabii kibwetere [emoji44]
Yaani inabidi nikueleze hivi kwa ufupi, ijapokuwa hii inafahamika kwa wanataaluma wote na wale waliosoma elimu ya TANZANIA.
Huwa kuna taarifa za maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi na huanza kujazwa kwa kufuata ufaulu wa mwanafunzi husika.
Kwa elimu ya shule ya msingi, hii fomu ya maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi huitwa TSM9.
Kwa elimu ya shule ya sekondari, hii fomu ya maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi huitwa SELECTION FORM na kwa ufupi huitwa SELFORM.
Kwa elimu ya shule ya Chuo, hii fomu ya maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi huitwa COURSEWORK ASSESSMENT na kwa ufupi huitwa CA.
Na matumizi ya fomu ya maendeleo ya mwanafunzi huanza kutumika baada ya matokeo ya mtihani wa taifa wa darasa la nne.
Kwa mfano, kwa matokeo ya darasa la nne, hii fomu ya TSM9 huwa inajaza taarifa na matokeo ya mwanafunzi kidarasa, kiwilaya na kimkoa.
Hii fomu ya maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi [ TSM9 ] huwa inaendelea mpaka darasa la saba. Na huwa inajaza taarifa za maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi kidarasa, kiwilaya, kimkoa na kitaifa.
Kwa kujiunga na masomo ya sekondari, lazima kuwepo na taarifa za kitaaluma kutoka shule ya msingi ili kuweza kuendelea na masomo ya sekondari.
Na hii fomu ya maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi kwa upande wa sekondari huanza kujazwa na kutumika kidato cha pili baada ya mtihani wa taifa. Wote tunafahamu mtihani wa taifa wa kidato cha pili huwa ni kama mtihani wa taifa wa darasa la nne.
Matokeo ya kidato cha pili huwa yanapangwa kidarasa na kimkoa.
Kwa hiyo, kila mwanafunzi atakuwa na matokeo yake ya kidarasa na kimkoa. Na hii fomu ya maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi [ SELFORM ] hujaza taarifa za mwanafunzi kidarasa na kimkoa, pamoja na DARAJA LA UFAULU yaani division.
Baada ya mtihani wa kidato cha pili, huwa kuna mtihani wa kidato cha nne. Huu mtihani ndio huwa mtihani wa kuhitimu elimu ya kidato cha nne.
Kwa kidato cha nne, hii fomu ya SELFORM inajaza taarifa za matokeo ya mwanafunzi kidarasa, kimkoa na kitaifa pamoja na DARAJA LA UFAULU yaani division.
Baada ya matokeo ya kidato cha nne kutangazwa, huwa kuna wanafunzi wanaoendelea kidato cha tano na wengine wanajiunga na vyuo kwa ngazi ya astashahada, stashahada, shahada, uzamiri nakadhalika.
Hii fomu ya maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi huendelea kutumika kidato cha sita na wale wanaoendelea na vyuo.
Huu mtihani wa taifa wa kidato cha sita huwa unafanyika kwa pamoja na wanafunzi wa taifa zima na matokeo ya wanafunzi hupangwa kitaifa. Yaani huwa kuna orodha ya wahitimu wa kidato cha sita kuanzia mwanafunzi wa kwanza mpaka mwanafunzi wa mwisho kitaifa. Kama inavyofanyika kwa kidato cha nne.
Hapa tena, taarifa za maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi huendelea kujazwa kwa kufuata ufaulu wa mwanafunzi husika - kidarasa, kimkoa na kitaifa.
Na matumizi ya fomu ya maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi [ SELFORM ] huendelea kutumika baada ya matokeo ya mtihani wa kidato cha sita.
Mwanafunzi anayeendelea na Chuo, hii fomu ya maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi huendelea kutumika lakini Chuo Kikuu huwa wanaita COURSEWORK ASSESSMENT yaani CA.
Hii yote kwa ujumla wanaita ni faili la maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi na mara nyingi wanaita TSM9 kwa ujumla kwa sababu hauwezi kuwa na SELFORM pasipo kuwa na TSM9 na hauwezi kuwa na CA pasipo kuwa na SELFORM. Kwa hiyo faili la maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi kutoka shule ya msingi ndio huwa inabeba kila kitu ndio maana kwa ufupi wanaita TSM9.
Ngoja nikipata muda mzuri tutajadili kwa kirefu na kina jinsi elimu ya TANZANIA ilivyo lakini kwa leo naomba niishie hapa.