Mfahamu T.O Kihombo 2006 aliyepata Degree yake ya Kwanza baada ya Miaka 11

Mi naomba nione orodha ya wewe ukiwemo katika top ten.

Nikiona tu nitakuwa mfuasi wako [emoji2]

La sivyo utakuwa kibwetere[emoji2][emoji119]
Unataka kuniweka mtegoni wewe na nitiwe nyavuni 🤣🤣🤣

Hizo orodha za wanafunzi bora waliofanya vizuri kitaifa huwa hazitangazwi bila idhini ya Rais.

Ofisi ya Rais ndio inatoa idhini ya NECTA kutangaza wanafunzi bora waliofanya vizuri kitaifa.

Ikitokea umejitangaza wewe bila ya kufuata utaratibu unaweza kuchukuliwa hatua kali ya kisheria au ukaonekana ni muongo au tapeli.

Ndio maana tunataka idhini ya Rais kupitia NECTA watangaze wanafunzi bora waliofanya vizuri kitaifa hata kwa miaka ya nyuma kama inavyofanyika sasa hivi ili kuondoa sintofahamu na kutovunja sheria.
 
Unataka kuniweka mtegoni wewe na nitiwe nyavuni [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Hizo orodha za wanafunzi bora waliofanya vizuri kitaifa huwa hazitangazwi bila idhini ya Rais.

Ofisi ya Rais ndio inatoa idhini ya NECTA kutangaza wanafunzi bora waliofanya vizuri kitaifa.

Ikitokea umejitangaza wewe bila ya kufuata utaratibu unaweza kuchukuliwa hatua ya kali ya kisheria au ukaonekana ni muongo au tapeli.

Ndio maana tunataka idhini ya Rais kupitia NECTA watangaze wanafunzi bora waliofanya vizuri kitaifa hata kwa miaka ya nyuma kama inavyofanyika sasa hivi ili kuondoa sintofahamu na kutovunja sheria.
Lazima itakuwa ibapatika hio orodha[emoji2]

Hako la kitabu kenye jina lako ukiwa top ten ndio mzizi wa fitna ulipo

Kiweke hapa uwakate watu kisebengo.

Halafu unaseme necta inaonesha juu tu kwa division 1,2,3,4 huku kwenye kitabu wanagrade vipi ufaulu .

Unamkumbuka Nabii kibwetere [emoji44]
 
Hizo orodha hazikutangazwa lakini zinapatikana Wizara ya TAMISEMI, Wizara ya Muungano, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na pia pale Utumishi wa Umma - Dodoma zinapatikana.

Kuna orodha mpaka za wanafunzi waliofanya vizuri kitaifa kwenye kila somo, hizi orodha hata Utawala wa Magufuli wenyewe bado haujafikiria kuanza kutangaza. Lakini ni muhimu kwa wanafunzi kufahamu matokeo yao ya kitaifa katika kila somo na sio orodha za wanafunzi bora tu.

Maana ubadilifu na udanganyifu ni mkubwa sana, unakuta mwanafunzi ameongoza somo fulani kitaifa lakini kwenye cheti ameandikiwa alama ya ufaulu "D" na mfano halisi upo kabisa. Kwa mfano, mwanafunzi aliyeongoza kitaifa somo la Physics kidato cha sita, mwaka 2010 ameandikiwa alama ya ufaulu "E" badala ya "A". Huyu alikuwa ni mwanafunzi wa Moshi Secondary High School. Hii ni hasara kwa mwanafunzi husika na kituo chake cha mtihani, yaani shule.

Mambo ni mengi ya kueleza, lakini NECTA ni JIPU na ikiwezekana litumbuliwe hata kesho [😂😂😂] maana sisi wengine tumeshafahamu hata baada ya katibu mtendaji CHARLES MSONDE tunafahamu atakeyefuatia ni nani? Inabidi hiyo NECTA ifumuliwe yote kwa masilahi ya Umma na watumishi wote wa hapo wapangiwe shughuli nyingine za kufanya.

Hizi shule binafsi na shule za seminari huwa hazifaulu kama zinavyotangazwa, huwa wanapika matokeo ndio maana hata wanafunzi wao wanahangaika kupata ajira na wengine kukosa ajira kabisa.

Na mifano iko mingi kabisa, kuna mwanafunzi wa kidato cha nne alipata division I ya point 8 kutoka shule ya St Francis Girls na baadae alifanikiwa kupata shahada yake kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini lakini sasa hivi anatengeza na kuuza juisi ya matunda huko kwao, Forest - Mbeya.

Ukiangalia matokeo halisi ya huyu binti yanayosoma kwenye vitabu vya wahitimu yanasoma alipata division III ya point 23! Can't imagine! Yaani ni madudu tupu 😂😂😂

Sasa tatizo sio la mwanafunzi [ binti mwenyewe ni mzuri kweli kweli 😋], tatizo ni NECTA na kituo cha mtihani yaani shule. Mambo ni mengi, tukiyaeleza yote hapa hawa NECTA watafukuzwa kazi na baadhi ya shule zitakosa wateja. Ngoja tuishie hapa au unasemaje mshikaji wangu!.
Sijakuelewa..kwamba huku matokeo ya necta mtu ana division 1.8..kwenye kitabu cha wahitimu ana division 3..inawezekana vipi hii?ina maana kwa mantiki hiyo kuna watu necta iliwawekea division 4 lkn kwenye kitabu cha wahitimu wana division one?
 
Ndio maana yake! Haya mambo yanawezekana kwa zile shule zilizotoa wanafunzi bora kitaifa halafu matokeo yao hayakutangazwa.

Kwa mfano, shule iliyotoa mwanafunzi bora kitaifa kidato cha nne mwaka 2006 ilikuwa ni shule ya sekondari ya UHURU iliyopo Shinyanga. Lakini huyu mwanafunzi bora aliandikiwa division one ya point 11 badala ya division one ya point 7.

Sasa basi, wakichakachua matokeo ya mwanafunzi aliyeshika nafasi ya kwanza huwa inaleta mabadiliko kwa matokeo ya wanafunzi wa darasa zima ili isionekane tofauti yoyote.

Kwa hiyo, kitabuni inaonesha shule ya UHURU ilikuwa na division I mpaka division III tu na kutoa wanafunzi bora kitaifa lakini baada ya uchakachuaji, matokeo ya darasa zima yalibadilika mpaka division 0 ilikuwepo.
 
Wizara ya elimu wanayajua hayo?
 
Wizara ya elimu wanayajua hayo?
Ndio maana nasema hivi, siku NECTA wakiamua kutangaza wanafunzi bora waliofanya vizuri kitaifa hata kwa miaka ya nyuma.

Shule zilizotoa wanafunzi bora kitaifa, matokeo yote ya darasa zima yatabadilika kwa zile shule zilizotoa wanafunzi bora tu.
 
Lazima itakuwa ibapatika hio orodha[emoji2]

Hako la kitabu kenye jina lako ukiwa top ten ndio mzizi wa fitna ulipo

Kiweke hapa uwakate watu kisebengo.

Halafu unaseme necta inaonesha juu tu kwa division 1,2,3,4 huku kwenye kitabu wanagrade vipi ufaulu .

Unamkumbuka Nabii kibwetere [emoji44]
Yaani inabidi nikueleze hivi kwa ufupi, ijapokuwa hii inafahamika kwa wanataaluma wote na wale waliosoma elimu ya TANZANIA.

Huwa kuna taarifa za maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi na huanza kujazwa kwa kufuata ufaulu wa mwanafunzi husika.

Kwa elimu ya shule ya msingi, hii fomu ya maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi huitwa TSM9.

Kwa elimu ya shule ya sekondari, hii fomu ya maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi huitwa SELECTION FORM na kwa ufupi huitwa SELFORM.

Kwa elimu ya shule ya Chuo, hii fomu ya maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi huitwa COURSEWORK ASSESSMENT na kwa ufupi huitwa CA.

Na matumizi ya fomu ya maendeleo ya mwanafunzi huanza kutumika baada ya matokeo ya mtihani wa taifa wa darasa la nne.

Kwa mfano, kwa matokeo ya darasa la nne, hii fomu ya TSM9 huwa inajaza taarifa na matokeo ya mwanafunzi kidarasa, kiwilaya na kimkoa.

Hii fomu ya maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi [ TSM9 ] huwa inaendelea mpaka darasa la saba. Na huwa inajaza taarifa za maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi kidarasa, kiwilaya, kimkoa na kitaifa.

Kwa kujiunga na masomo ya sekondari, lazima kuwepo na taarifa za kitaaluma kutoka shule ya msingi ili kuweza kuendelea na masomo ya sekondari.

Na hii fomu ya maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi kwa upande wa sekondari huanza kujazwa na kutumika kidato cha pili baada ya mtihani wa taifa. Wote tunafahamu mtihani wa taifa wa kidato cha pili huwa ni kama mtihani wa taifa wa darasa la nne.

Matokeo ya kidato cha pili huwa yanapangwa kidarasa na kimkoa.

Kwa hiyo, kila mwanafunzi atakuwa na matokeo yake ya kidarasa na kimkoa. Na hii fomu ya maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi [ SELFORM ] hujaza taarifa za mwanafunzi kidarasa na kimkoa, pamoja na DARAJA LA UFAULU yaani division.

Baada ya mtihani wa kidato cha pili, huwa kuna mtihani wa kidato cha nne. Huu mtihani ndio huwa mtihani wa kuhitimu elimu ya kidato cha nne.

Kwa kidato cha nne, hii fomu ya SELFORM inajaza taarifa za matokeo ya mwanafunzi kidarasa, kimkoa na kitaifa pamoja na DARAJA LA UFAULU yaani division.

Baada ya matokeo ya kidato cha nne kutangazwa, huwa kuna wanafunzi wanaoendelea kidato cha tano na wengine wanajiunga na vyuo kwa ngazi ya astashahada, stashahada, shahada, uzamiri nakadhalika.

Hii fomu ya maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi huendelea kutumika kidato cha sita na wale wanaoendelea na vyuo.

Huu mtihani wa taifa wa kidato cha sita huwa unafanyika kwa pamoja na wanafunzi wa taifa zima na matokeo ya wanafunzi hupangwa kitaifa. Yaani huwa kuna orodha ya wahitimu wa kidato cha sita kuanzia mwanafunzi wa kwanza mpaka mwanafunzi wa mwisho kitaifa. Kama inavyofanyika kwa kidato cha nne.

Hapa tena, taarifa za maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi huendelea kujazwa kwa kufuata ufaulu wa mwanafunzi husika - kidarasa, kimkoa na kitaifa.

Na matumizi ya fomu ya maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi [ SELFORM ] huendelea kutumika baada ya matokeo ya mtihani wa kidato cha sita.

Mwanafunzi anayeendelea na Chuo, hii fomu ya maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi huendelea kutumika lakini Chuo Kikuu huwa wanaita COURSEWORK ASSESSMENT yaani CA.

Hii yote kwa ujumla wanaita ni faili la maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi na mara nyingi wanaita TSM9 kwa ujumla kwa sababu hauwezi kuwa na SELFORM pasipo kuwa na TSM9 na hauwezi kuwa na CA pasipo kuwa na SELFORM. Kwa hiyo faili la maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi kutoka shule ya msingi ndio huwa inabeba kila kitu ndio maana kwa ufupi wanaita TSM9.

Ngoja nikipata muda mzuri tutajadili kwa kirefu na kina jinsi elimu ya TANZANIA ilivyo lakini kwa leo naomba niishie hapa.
 
Asante
 
Engineer anafundisha??..... hii kweli tz ya vi-wonder.....poor utilization of scare resources
Kuwa daktari lazima ufundishwe na daktari.
Kuwa engineer lazima ufundishwe na engineer.
Kuwa vyovyote vile lazima ufundishwe na mwenye elemu ya unavyotaka kuwa.
 
Jamaa boya sana. Angekomaa na hiyo taaluma ya kwanza sasa hivi angekuwa katika mojawapo ya makampuni ya simu au ISP wanamlipa above 5 milioni per month plus marupurupu kibao.....

Sasa yeye anakalia ufahari wa kufaulu amekuja kuwaimpress watu hapa duniani au kuishi maisha yake.... Nonsense kabisa.... Bongo sio sehemu ya kuleta hisia za kutaka kuwa nani ukipata upenyo ni hapo hapo unachukua fursa ukizubaa mambo hubadilika.

Maboya wenzake tunawaona kitaa huko wanatoa toa macho tu.....
 
Yaani inabidi nikueleze hivi kwa ufupi, ijapokuwa hii inafahamika kwa wanataaluma wote na wale waliosoma elimu ya TANZANIA.

Huwa kuna taarifa za maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi na huanza kujazwa kwa kufuata ufaulu wa mwanafunzi husika.

Kwa elimu ya shule ya msingi, hii fomu ya maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi huitwa TSM9.

Kwa elimu ya shule ya sekondari, hii fomu ya maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi huitwa SELECTION FORM na kwa ufupi huitwa SELFORM.

Kwa elimu ya shule ya Chuo, hii fomu ya maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi huitwa COURSEWORK ASSESSMENT na kwa ufupi huitwa CA.

Na matumizi ya fomu ya maendeleo ya mwanafunzi huanza kutumika baada ya matokeo ya mtihani wa taifa wa darasa la nne.

Kwa mfano, kwa matokeo ya darasa la nne, hii fomu ya TSM9 huwa inajaza taarifa na matokeo ya mwanafunzi kidarasa, kiwilaya na kimkoa.

Hii fomu ya maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi [ TSM9 ] huwa inaendelea mpaka darasa la saba. Na huwa inajaza taarifa za maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi kidarasa, kiwilaya, kimkoa na kitaifa.

Kwa kujiunga na masomo ya sekondari, lazima kuwepo na taarifa za kitaaluma kutoka shule ya msingi ili kuweza kuendelea na masomo ya sekondari.

Na hii fomu ya maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi kwa upande wa sekondari huanza kujazwa na kutumika kidato cha pili baada ya mtihani wa taifa. Wote tunafahamu mtihani wa taifa wa kidato cha pili huwa ni kama mtihani wa taifa wa darasa la nne.

Matokeo ya kidato cha pili huwa yanapangwa kidarasa na kimkoa.

Kwa hiyo, kila mwanafunzi atakuwa na matokeo yake ya kidarasa na kimkoa. Na hii fomu ya maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi [ SELFORM ] hujaza taarifa za mwanafunzi kidarasa na kimkoa, pamoja na DARAJA LA UFAULU yaani division.

Baada ya mtihani wa kidato cha pili, huwa kuna mtihani wa kidato cha nne. Huu mtihani ndio huwa mtihani wa kuhitimu elimu ya kidato cha nne.

Kwa kidato cha nne, hii fomu ya SELFORM inajaza taarifa za matokeo ya mwanafunzi kidarasa, kimkoa na kitaifa pamoja na DARAJA LA UFAULU yaani division.

Baada ya matokeo ya kidato cha nne kutangazwa, huwa kuna wanafunzi wanaoendelea kidato cha tano na wengine wanajiunga na vyuo kwa ngazi ya astashahada, stashahada, shahada, uzamiri nakadhalika.

Hii fomu ya maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi huendelea kutumika kidato cha sita na wale wanaoendelea na vyuo.

Huu mtihani wa taifa wa kidato cha sita huwa unafanyika kwa pamoja na wanafunzi wa taifa zima na matokeo ya wanafunzi hupangwa kitaifa. Yaani huwa kuna orodha ya wahitimu wa kidato cha sita kuanzia mwanafunzi wa kwanza mpaka mwanafunzi wa mwisho kitaifa. Kama inavyofanyika kwa kidato cha nne.

Hapa tena, taarifa za maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi huendelea kujazwa kwa kufuata ufaulu wa mwanafunzi husika - kidarasa, kimkoa na kitaifa.

Na matumizi ya fomu ya maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi [ SELFORM ] huendelea kutumika baada ya matokeo ya mtihani wa kidato cha sita.

Mwanafunzi anayeendelea na Chuo, hii fomu ya maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi huendelea kutumika lakini Chuo Kikuu huwa wanaita COURSEWORK ASSESSMENT yaani CA.

Hii yote kwa ujumla wanaita ni faili la maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi na mara nyingi wanaita TSM9 kwa ujumla kwa sababu hauwezi kuwa na SELFORM pasipo kuwa na TSM9 na hauwezi kuwa na CA pasipo kuwa na SELFORM. Kwa hiyo faili la maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi kutoka shule ya msingi ndio huwa inabeba kila kitu ndio maana kwa ufupi wanaita TSM9.

Ngoja nikipata muda mzuri tutajadili kwa kirefu na kina jinsi elimu ya TANZANIA ilivyo lakini kwa leo naomba niishie hapa.
Nahitaji kukufuata pembeni unieleweshe vyema
 
Wizara ya elimu wanayajua hayo?
Ndio! Wizara ya Elimu wanafahamu vizuri sana!

Yaani pale Baraza la Mitihani [ NECTA ] wanapaita machinjioni, pale ndio ACADEMIC SUICIDAL inafanyika.

Kupika matokeo ya kitaaluma kwa lugha ya kiingereza wanaita ni "REPRESSION AND FALSIFICATION OF ACADEMIC RESULTS".

Kwa mfano, matokeo ya mwanafunzi kwenye cheti yakisoma "DIVISION ONE" halafu kwenye kitabu cha wahitimu au TSM9, matokeo ya mwanafunzi huyo huyo yakisoma "DIVISION THREE" au "DIVISION TWO". Hapa wanaita REPRESSION yaani ubadilifu umefanyika.

Kwa mfano tena, matokeo ya mwanafunzi kwenye cheti yakisoma "DIVISION FOUR" halafu kwenye kitabu cha wahitimu au TSM9, matokeo ya mwanafunzi huyo huyo yakisoma "DIVISION ONE" au "DIVISION TWO". Hapa wanaita FALSIFICATION yaani udanganyifu umefanyika.

Hii yote wanaita ni ACADEMIC SUICIDAL na hakuna aliye na nafuu, wote ni wahangaa.

Lakini yule mwanafunzi ambaye matokeo yake ya kitaaluma yameshushwa anaweza akafikiriwa mara mbili kutokana na SOCIAL CONSTRAINTS na yule mwanafunzi ambaye matokeo yake ya kitaaluma yamepandishwa anaonekana hafai kabisa kwa sababu ya rushwa na ubadilifu wa matokeo.

Na hapa kwenye FALSIFICATION [ udanganyifu ] huwa kuna kitu ambacho kinachangia matokeo ya mwanafunzi husika au shule kwa ujumla kushushwa, huwa kuna kitu wanaita SOCIAL CONSTRAINTS.

Kama unakumbuka huwa kuna fomu ambazo mwanafunzi anatakiwa azijaze kama ni yatima au ana wazazi wote wawili au ana mzazi mmoja, majina ya wazazi au walezi wake, kazi za wazazi au walezi wake, dini za wazazi au walezi wake, kabila za wazazi au walezi wake. Hizi taarifa ndio wanaziita SOCIAL CONSTRAINTS.

Na hizi taarifa zote huwa zinajumuishwa kwenye faili la kitaaluma la mwanafunzi husika.

Kwa hiyo hizi taarifa binafsi huwa zina nafasi yake katika kuchangia ufaulu wa mwanafunzi husika.

Ndio maana unakuta mwanafunzi amepata DIVISION ONE kwenye faili lake na kwenye kitabu cha wahitimu lakini kwenye cheti chake cha matokeo kinasoma amepata DIVISION FOUR au DIVISION ZERO kabisa.

Au mwanafunzi unakuta kwenye cheti chake cha matokeo kinasoma amepata DIVISION ONE lakini kwenye faili la kitaaluma la mwanafunzi husika na kitabu cha wahitimu matokeo yanasoma amepata DIVISION THREE au DIVISION FOUR.

Hii ndio TANZANIA! Na mtindo huu ulikuwa na unaendelea kufanyika mpaka leo, tangu ulipoasisiwa na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kwa hiyo, kama taifa tunahitaji mabadiliko katika sekta ya Elimu. Tunahitaji kuwe na uwazi, hata hivi vitabu vya wahitimu vikiwa vinapatikana kwa urahisi itasaidia sana kuondoa sintofahamu na ubadilifu mkubwa uliopo katika sekta ya Elimu.

Ukiziangalia nchi za Kenya, Zambia na Uganda utagundua kuwa wametupita mbali sana kitaaluma. Na hii yote inatokana na uwazi uliopo katika hizi nchi za Kenya, Zambia na Uganda.

Tunahitaji mabadiliko! Tena mabadiliko ni muhimu sana hasa katika kipindi hiki cha utandawazi, ukizingatia serikali ya TANZANIA imekuwa ikijinadi kuwa ina UCHUMI WA KATI.

Sasa itakuwa ni vichekesho ikiwa nchi ipo UCHUMI WA KATI halafu matokeo ya wanafunzi yanapikwa na wala hakuna uwazi!

Hata hao wataalum wa sekta mbalimbali wanaohitajika watapatikana vipi?

Ndio maana hata madaktari wa binadamu waliopaswa kuwepo kazini bado hawajapata ajira. Hii yote inatokana na ACADEMIC SUICIDAL inayofanyika pale Baraza la Mitihani [ NECTA ].

Inabidi ifike mahala tuelezane ukweli! Mabadiliko ni lazima na wala sio ombi!
 
Halafu hii tabia ya kujikweza kitaaluma ipo sana Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam [ UDSM ] mpaka wengine wanadiriki kusema uongo!

Kama huyu Martin Chegere hakuwahi kuongoza mara tatu na wala hayupo kwa wale wanafunzi waliowahi kufanya vizuri NECTA.

Ngoja niwape siri nyingine - "Majina ya wanafunzi waliofanya vizuri kitaifa - kuanzia darasa la nne, darasa la saba, kidato cha pili, kidato cha nne na kidato cha sita huwa yanahifadhiwa IKULU na kuandikwa kwa wino wa dhahabu.

Huwa wanayaita Golden Ink Personnel [ GIP ] au wengine huwa wanaita VIP.

Sasa huyu Martin Chegere sio GIP wala VIP, ni muhuni muhuni tu. Hawa ndio wajanja wajanja, wale walionufaika kwa madhaifu ya NECTA 😂😂😂

Inabidi mfungue uzi unaomuhusu huyu Martin Chegere maana inaonekana hata Elias Kihombo ana nafuu Lol!

Duuuhh!

"Ngoja niwape siri nyingine - "Majina ya wanafunzi waliofanya vizuri kitaifa - kuanzia darasa la nne, darasa la saba, kidato cha pili, kidato cha nne na kidato cha sita huwa yanahifadhiwa IKULU na kuandikwa kwa wino wa dhahabu
."

Hawa basi ndio wameyaweza maisha au vipi ?
Kaaazi kweli kweli
 
Duuuhh!

"Ngoja niwape siri nyingine - "Majina ya wanafunzi waliofanya vizuri kitaifa - kuanzia darasa la nne, darasa la saba, kidato cha pili, kidato cha nne na kidato cha sita huwa yanahifadhiwa IKULU na kuandikwa kwa wino wa dhahabu."

Wote wako hoi hamna mwenye afadhali maana kwa miaka ya nyuma, wanafunzi waliokuwa wakifanya vizuri kwenye mitihani yao walikuwa hawatangazwi na wengine walikuwa wakipewa madaraja ya ufaulu tofauti kabisa na uwezo wao.

Kwa hiyo wanafunzi hawa hawajitambui mpaka muda huu lakini majina yao yamehifadhiwa IKULU na kuandikwa kwa wino wa dhahabu yaani Golden Ink Personnel [ GIP ].

Tofauti na kipindi hiki cha Magufuli, wanafunzi bora waliofanya vizuri kitaifa wamekuwa wakitangazwa na kuna baadhi ya makampuni au taasisi zimekuwa zikitoa ahadi za ajira kwa wanafunzi bora endapo tu watamaliza masomo yao ya Chuo Kikuu.

Halafu kuna kitu kingine ambacho watu wengi hawajakifahamu au kukitambua mapema. Sekta ya uandishi wa vitabu ya Tanzania yaani Tanzania Publishing Industry tayari imeshakufaa. Watanzania wengi kama sio wote wanatumia vitabu vilivyoandikwa na waandishi kutoka nje.

Imekufaa kutokana na ACADEMIC SUICIDAL inayofanyika pale NECTA, matokeo yake wale waliopaswa kuandika vitabu vya masomo mbali mbali hawajitambui na wale wanaoandika vitabu vya masomo mbali mbali hata fasihi tu ni waandishi wasio na sifa za kitaaluma.

Kwa mfano, ukitizama majirani zetu wa nchi ya Kenya. Sekta ya uandishi wa vitabu yaani Kenya Publishing Industry iko juu sana kuliko Tanzania kwa sababu elimu yao iko vizuri na imejaa uwazi.

Wanafunzi bora waliofanya vizuri kitaifa nchini Kenya hawasubiri ajira, wamekuwa ni chachu katika uandishi wa vitabu. Nchini Kenya, hata yule mwanafunzi aliyeongoza kitaifa katika somo la Kiswahili anatangazwa, ndio maana Kenya wako vizuri sana kwenye sekta ya uandishi wa vitabu na elimu yao imekuwa ikijinadi kimataifa.

Hata kazi za wasanii wa Kenya na Uganda ni tofauti sana na kazi za wasanii wa Tanzania. Hii inatokana na elimu yao! Kenya ni kawaida kabisa kukuta msanii wa nyimbo za Sanaa ana shahada, lakini Tanzania imekuwa hali ni tofauti.
 
Duuuhh!

"Ngoja niwape siri nyingine - "Majina ya wanafunzi waliofanya vizuri kitaifa - kuanzia darasa la nne, darasa la saba, kidato cha pili, kidato cha nne na kidato cha sita huwa yanahifadhiwa IKULU na kuandikwa kwa wino wa dhahabu."

Hawa basi ndio wameyaweza maisha au vipi ?
Kaaazi kweli kweli
Na kama una uwezo wa kifedha, TANZANIA sio sehemu salama kwa mtoto kusoma elimu ya msingi wala elimu ya sekondari labda elimu ya Chuo Kikuu.

Maana unaweza kumlaumu mtoto kwa kutofanya vizuri kwenye mtihani, kumbe tatizo sio hata la mtoto. Na hii inawatokea wazazi au walezi wengi sana. Tatizo ni Elimu ya Tanzania.

Maana kufanya vizuri au kutofanya vizuri kwenye mtihani inategemea sana taarifa binafsi za kitaaluma za mwanafunzi husika. Unaweza kukuta mwanafunzi ameandikiwa DIVISION FOUR au DIVISION ZERO kwenye cheti chake lakini kwenye orodha ya matokeo ya wahitimu kwa ujumla ana DIVISION ONE au DIVISION TWO.
 
Nakukubali Mkuu, sio mchezo
Huo upuuzi mimi niliushtukia long time
Mimi nilichagua A level shule ninazotaka nikijua sikosi hata Div 2 lakini wakanipa Div3 nikapangiwa mkoani, nikaahirisha nikaenda zangu VETA
Yaani sio hivyo pia nilipigwa bao mwenyewe kusoma Electronics na hii ni VETA tu kwa waliomaliza one year Electrical Changombe ukipiga vizuri wanafunzi 4 wanapelekwa VETA Moshi kusoma Electronic au Industrial Elictrical ,
hiki kilikuwa ni chuo kipya kimejengwa na Serikali ya Sweden,
Nafasi akapewa shemeji, mbele ya macho yangu hivi hivi na alikuwa mweupe kwenye Theory na Practical yaani we acha tu, wakanipa Industrial Electrical ambayo kwa kweli sijui sasa VETA Moshi ikoje lakini miaka ya tisini hii kozi ilikuwa bora sana na workshop na laboratory zilikuwa zinapendeza na vifaa kuliko hata UDSM kwa Electrical Engineering.
Lakini poa tu nilisha achana na huo mfumo wa kibongobongo ages ago.
Na sasa nina BEng ya wazungu wa malkia , lakini wafia NECTA, watasema nimeunga unga.
 
Back
Top Bottom