Kuhusu uandishi tuulize tunaoandika riwaya ndiyo tunaweza kukudadavulia.
Mtu kufikia kuandika asichokuwa na elimu nacho si tatizo, utafiti anaoufanya kwenye kazi yake ndiyo bumpelekea aonekane mjuzi upande huo.
Hivyo Shakespeare kujua mambo mengi ni kutokana na utafiti anaoufanya kabla ya kuandika, kuuliza watu na hata kusoma baadhi ya maandiko ya kitaaluma nayo ni njia nzuri kwake ya kuandaa kitu kilicho bora.
Hivyo sababu iliyotajwa hapo na wasomi haina mashiko kabisa, si kwamba hakutunga.
Uandishi wa aina hiyo unakuta mtu anatafiti kitu nusu mwaka, unategemea akija kukitoa kilingane na yule anayekiburuza tu kichwani
Mkuu jama alikuwa anatumia misamiati mingi sana katika uandishi wake, pia alikuwa ana ufahamu mkubwa sana wa vitu vingi ambavyo mtu wa kawaida ni ngumu sana kujua hasa kipindi hicho 1500-1600 information access haikuwa rahisi kama sasa hivi ambapo unaweza zama google unaweza fanya research ukajua sehemu mbalimbali hata ambazo hujafika.
"Let me have men about me that are fat,
Sleek-headed men and such as sleep a-nights.
Yond Cassius has a lean and hungry look,
He thinks too much; such men are dangerous."
Huo mfano niliokuwekea ni Ceaser alikuwa anamwambia Antony, ukisoma juu juu utaona kama maneno tu.
Lakini hebu fikiria Ceaser anamwambia Antony kwamba anataka watu walioshina ndiyo wawe karibu naye siyo watu wembamba, watu wembamba ni watu wasioridhika, huwaza sana, wako ambitious na ukisoma psychology imekuwa proved to be true. Hivyo utagundua Shakespeare alikuwa anafahamu psychology.
Njoo kwenye sheria, ukisoma The Merchant of Venance utaona kuwa William alikuwa anajua sana sheria.
Matumizi na mpangilio wa misamiati na maneno.
Mzungumzaji wa kawaida wa Kingereza anajua misamiati 10,000-20,000 lakini yeye inakadiriwa alikuwa anajua misamiati 66,000+. Hivyo utaona jamaa hakuwa mwandishi wa kawaida na ndiyo maana wanazuoni wanashangaa iweje mtu wa kawaida kama yeye aandike vitu kama vile wakati hata hakuwahi kusafiri wala hakuwa na elimu kubwa.
Tofautisha wakati alioishi yeye na wakati tunaoishi sisi, mtu anaweza google mitaa ya London akakuandikia story kama vile aliwahi kufika kumbe wapi.