Mfahanu Williams Shakespeare na utata wa kazi zake

Nilisoma vitano katika vitabu vyake nikiwa o-level,
Kipindi hicho sikuwa naingia darasani japo nipo shule kila siku, walimu watano walinifukuza sababu niliwajibu majibu yenye ukweli na ukakasi...
Nilipofika chuo nikasoma viwili tu, Hardley Chase akawa kaniathiri na riwaya zake
 
Ukisoma hivi vitabu, basi umesoma fani nyingi, na unakua na uelewa wa vitu vingi... Kiukweli hadi sasa kama ukivifuatilia msg zake ziko valid sana
 
Leonardo Da Vinci ni hatari sana ana secrets nyingi
 
Ni kweli kabisa.
Uwezo na umahiri wa kuandika fasihi/hadithi/riwaya hauna connection ya moja kwa moja na elimu kubwa.

Reference; Shabaan Robert
 
harafu wazungu wa zamani walikuwa tofauti na wasiku hizi. labda ndo revolution of man....?
 
Mkuu jama alikuwa anatumia misamiati mingi sana katika uandishi wake, pia alikuwa ana ufahamu mkubwa sana wa vitu vingi ambavyo mtu wa kawaida ni ngumu sana kujua hasa kipindi hicho 1500-1600 information access haikuwa rahisi kama sasa hivi ambapo unaweza zama google unaweza fanya research ukajua sehemu mbalimbali hata ambazo hujafika.
"Let me have men about me that are fat,
Sleek-headed men and such as sleep a-nights.
Yond Cassius has a lean and hungry look,
He thinks too much; such men are dangerous."
Huo mfano niliokuwekea ni Ceaser alikuwa anamwambia Antony, ukisoma juu juu utaona kama maneno tu.
Lakini hebu fikiria Ceaser anamwambia Antony kwamba anataka watu walioshina ndiyo wawe karibu naye siyo watu wembamba, watu wembamba ni watu wasioridhika, huwaza sana, wako ambitious na ukisoma psychology imekuwa proved to be true. Hivyo utagundua Shakespeare alikuwa anafahamu psychology.
Njoo kwenye sheria, ukisoma The Merchant of Venance utaona kuwa William alikuwa anajua sana sheria.
Matumizi na mpangilio wa misamiati na maneno.
Mzungumzaji wa kawaida wa Kingereza anajua misamiati 10,000-20,000 lakini yeye inakadiriwa alikuwa anajua misamiati 66,000+. Hivyo utaona jamaa hakuwa mwandishi wa kawaida na ndiyo maana wanazuoni wanashangaa iweje mtu wa kawaida kama yeye aandike vitu kama vile wakati hata hakuwahi kusafiri wala hakuwa na elimu kubwa.
Tofautisha wakati alioishi yeye na wakati tunaoishi sisi, mtu anaweza google mitaa ya London akakuandikia story kama vile aliwahi kufika kumbe wapi.
 
Ni kweli kabisa.
Uwezo na umahiri wa kuandika fasihi/hadithi/riwaya hauna connection ya moja kwa moja na elimu kubwa.

Reference; Shabaan Robert
Mkuu hebu kasome vitabu vyake, fanya research kidogo kuhusu jamaa mpaka wamempa number 1, na bado kuna mabishano kama ni kweli yeye ndiye kaandika hayo ujue kuna sababu.
Kuna waandishi wengi wa enzi zake na enzi za sasa lakini he stands among the rest
 
Bado naamini alikuwa mjuzi na mwenye kipaji. Si kila msomi aliyebobea angeweza kuandika. Lah tungekuwa na wanazuoni wengi wenye maelfu ya vitabu kama vya Shakespere.

Ndiyo maana nikandika kumhusu Shabaan Robert, angalia mtiririko wa fikra na uandishi. Soma Kusadikika na fikra alizotia humo.

Kwa Mtu kama yeye tena asiye na elimu kubwa Watu wangeshangaa sana kuandika namna ile.

Hili la Shakespere kujua maneno ya Kiingereza zaidi ya 66,000 linaelezeka. Kwa Mtu mwenye bongo pana tena kazaliwa katika mazingira ya lugha yenyewe si ajabu kuwa na uwezo huo.

Siwezi kushangaa Shabaan Robert, mzaliwa wa Pwani tena Pangani mwenye ujuzi wa kuandika akawa na uwezo wa kuweka maneno mapya na istalahi mpya za Kiswahili
 
Mkuu naomba kujua majina ya vtabu ivyo
 
Hardley nimesoma vitabu vyake kadhaa ni mkali sana halafu zile sio plays kama shakespeare.
Nimesoma No orchids for Mrs Blandish, A coffin from Hongkong, The vulture is patient, Strictly cash, I will burry my dead, Mission to venice, Like a hole in the head
 
Itafute mkuu Jhuyu alikua kachanganya rangi..
Kama hutajali weka Picha za Amelia..



Hii ndiyo picha ya Amelia Basso (Dark lady) mbayo nimekutana nayo mtandaoni na kwenye sources mbalimbali

Hii pia wale wanodai kuwa vitabu vyake viliktaliwa kuwa published kisa ni black wanatumia hii picha.
Ila wanachokubariana wote ni kwamba yeye ndiye mwandishi.
Kwamba familia yake ilihamia Uingereza kutokea Morocco ambapo wazazi wake wana origin ya Italy, Jews na morocco.
Swali la kujiuliza ni hili, je wazazi wenye origin ya hivyo wanaweza kuzaa mtoto mweusi hivyo?
Na Amelia alipofika Uingereza aliwahi kufanya kazi kwenye kitengo cha mahakama kitu ambacho kwa mtu mweusi ingekuqa ngumu.
Pia alishiriki katika michezo ya kuigiza jambo ambalo pia kwa mweusi ingekuqa ngumu.
Ila ni kweli Amelia alikuwa somehow dark na ndiyo maana ana a.k.a ya the dark lady.
Kuhusu uandishi wake wa hivyo vitabu hakuna mwenye hakika wa asilimia mia kwa maana hizo rumours ht hazijaanza siku nyingi, zimeanza mwaka 2015 bada ya mtu flani kupost kwenye mtandao akidai kuna ushahidi unaoonyesha kuwa yeye ndiye mwandishi.
Ila mpaka sasa kuna zaidi ya watu 66, ambao wanasemekana kuwa ni waandishi na kati yo hakuna mwenye ushahidi wa kujitoshereza, hivyo shakespeare bado anabaki kuchukuliwa ndiye mwandishi halisi mpaka sasa.
 
Kuna kitabu chake kimoja alisema "ukitaka maendeleo kwenye jamii uue kwanza wanasheria wote"
Kwenye Henry VI
The first thing we do, let's kill all the lawyers.
Ulisemwa na Dick the butcher.
Lakini lengo alikuwa anamaanisha waondoa watu ambao wanafikra huru mostly wana sheria ili waweza kufanikisha utawala wao.
Hivyo ndivyo nilielewa mimi
 
Kwenye Henry VI
The first thing we do, let's kill all the lawyers.
Ulisemwa na Dick the butcher.
Lakini lengo alikuwa anamaanisha waondoa watu ambao wanafikra huru mostly wana sheria ili waweza kufanikisha utawala wao.
Hivyo ndivyo nilielewa mimi
Absolutely...
 
Anakaa na wataalam wa hivyo vitu wanamsaidia mengi, umaarufu wake anapokuja kutaka ufafanuzi wa mambo kwa mtaalamu anapata tu.

Mkuu hivi Shaaban Robert kwa lugha naye unamfahamu vizuri? Mtu ambaye harudii maneno hovyo, ana misamiati migumu na ya ajabu hadi riwaya zake katia ukurasa wenye baadhi ya maneno yake kama vile ukurasa wa maneno magumu kwenye agano la kale. Naye unaweza kusoma riwaya yake usielewe baadhi ya sehemu.

Yote ya yote hakuwa na ujuzi wa kitaaluma, yule anachoandika analenga kitu kingine kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…