Ngoja niwaambie jamani ,kitu wokovu sio mchezo,hasa kama ulikuwa mwanachama mzuri wa huyu anae itwa ibilisi bin sheitwan,mambo ya kidunia ukitaka kuyaacha kuna mtihani mkubwa zaidi ya vile unavyoweza kufikiri,nguzo zote ulizokuwa nazo zinaweza kuporomoka na ukajikuta unabaki peke yao,kumbuka kabisa kwamba umebadili mfumo wa maisha na unaingia kwenye mfumo mpywa ambao hapo mwanzo haukuwepo.
Sasa hapa ibilisi bin sheitwani huingia kazin baada ya kukuona umeanza kukenguuka ,hakupi nafasi ya kupumua ,anapika uchumi,familia na jamii yako inakuona kuwa wewe ni fala na umekosea kila kitu,kiufupi lazima ujione mpweke,na ukicheza unaweza kupoteza hata watoto kwa vifo na kufarakana na mkeo ndugu na jamaa.
Tatizo ni kwamba ukitangaza kuacha jambo fulani na likaonekana kutaka kuleta ukinzani kwa huyu bwana mkubwa wa hapa duniani jua wazi kwamba umefungulia vita za kiroho.Vita vya kiroho huwa havipiganwi ki mwili ila effects zake unaziona mwanana kwenye maisha yako.Ukitaka kuamini waulize watu wenye tabia chafu ambao huchoka natabia hizo na mwisho wa siku huamua ku declare kwamba wameacha ,watu hawa badala ya kuacha hujikuta wameanza safari upya na kujikuta wanafanya mara mbili yake zaidi.Waulize wanao jichua kinachowapata kila wakitaka kufanya maamuzi ya kuacha hutokewa na nini,walevi,wezi ,makahaba,tapeli,wazinzi nk.
Shetani huwa hana shida na mtenda dhambi mana anajua yeye hana kikwazo kwake,utapata tabu ipi na kuku aliye bandani mwako?,yeye anapigana vita na watu wanaotangaza vita juu yake na ni vita moto moto ,inahitaji ujiimalishe hasa, la sivyo utanyosha mikono juu na kusalim amri.
Huyu mzee anatakiwa ajipange vyema na achague wapi kunako mstahili ,akhera ipo kwa wale walio jitoa kweli kweli na haipatikani vyepesi hasa kwa mtu kama yeye aliyekuwa amezoea anasa na mambo mengine ya kidunia ,anatakiwa ajipange na ujue naweza kuharibu zaidi na ninavyoona ni heri angebaki tu huko alipo kua amepaamua kuwepo.Au aamue ubaya ubaya hadi kufa ,yeye na dunia kwa kwa mpya ,na sisi tunasema mbwa kayarudia matapishi yake mwenyewe na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugala gala matopeni.Msamaha wa mtu kama huyu huwa ni Mgumu sana kwa Mwenyezi Mungu japo kuwa yeye ni Mwingi wa rehema.Mungu atunusuru kwa kila hali maisha yetu ni ya shida sana hapa duniani mana kila kona shilingi inahitajika.
Sent using
Jamii Forums mobile app