Mfalme Ogu wa Bashani: Mnefili pekee aliyepona kwenye Gharika la Nuhu

Halafu msipende kuwafananisha malaika na majini jaman ni viumbe wawili tofauti kabisa jaman majini ni kama sisi tu wanadam baadhi ya sifa zao na zetu zinafanana
Majini ni malaika waovu, ni waasi walifukuzwa mbinguni wakatupwa hapa duniani
 
Mku nmekusoma pooooote lkn uliposema tu alikua tishio dunia nzima ndo ninapokataaga je alishawai kuja kupigana na wahehe, au akina Zwangendaba, mkuu siku utakapopata historia za nyumbani ndo utakapojua nasi tuna hadithi zetu
 
Possibility kuwa maji yalijaa mikono 15 zaidi ya mlima mrefu ikimaanisha huyu Ogu kma alikuwa na urefu wa zaidi ya futi 15 ina maana basi anaweza kuwa maji aliyazidi kimo kuendana na hoja hii ya MIKONO 15!!! Other factors remaining constant ingawa ni finyu kma unavyosema ila kwa msimamo huu wa biblia je haiwezekani??
 
Duu huyu ni abnormal imagine daraja la mkapa eti ndo maiti ilitumika kama daraja la MTO Nile,maajabu
 
Mku nmekusoma pooooote lkn uliposema tu alikua tishio dunia nzima ndo ninapokataaga je alishawai kuja kupigana na wahehe, au akina Zwangendaba, mkuu siku utakapopata historia za nyumbani ndo utakapojua nasi tuna hadithi zetu
Naposema Dunia kwa context ya agano la kale ni mashariki ya kati pekee ndio ilikuwa dunia..... Enzi hizo watu waliishi maeneo ya mesopotamia hadi eridu mpaka misri basi na walikuwa hawazidi hata million 5 dunia nzima!!

Enzi za mfalme ogu afrika ilikuwa inaishia libya na misri tu hivyo hakukuwa bado na matishio huku afrika ingawa najua baadae afrika ilikuja kupata watu mashujaa ila all in all huyu Ogu alikuwa ni MWEUSI sababu anatambuliwa kma muamori ambaye ni jamii ya HAMITES ngozi nyeusi kabisa walioishi canaan/palestina-israel ya sasa takriban miaka 6000 iliopita hivyo ni ''mwenzetu'' huyo!!
 
Nadhani huyu mfalme OGU ana undugu na UNJU bin UNUQ
Inasemekana mkuu ndio mtu mmoja ila wazungu wanamuita OGU ila alikuwa mweusi ndio maana hata kwenye biblia anatajwa kuwa yupo kwenye uzao wa HAM ambao watoto wake walikuwa weusi mf mizraim phut cush n.k hivyo kuna ukweli kuwa UJ BIN ANAQ ama OG OF BASHAN ndio UNJ BIN UNUQ !!
 
Asante mkuu ila naomba Critically hebu dhania kama Afrika hii ya kwetu enzi hizo kulikua hakuna watu au ilikuaje, saa ingine nadhan biblia iliandikwa kwa mujibu wa watu wa mashariki ya kati miksa Misri. Labda nasi tuna historia yetu nyingine kabisa labda na Nuhu wetu au Ogu wetu ila kwa vile hatuna namna ya utunzaji kumbukumbu nso maana tunasemaga tu alikua hatari dunia nzima au aliipiga dunia nzima au alitawala dunia nzima
 
Hawa wanefili ni matokeo ya malaika kuzaa na binadamu na inasemekana waliangamia na hawapo tena
Kwanini hawa malaika waliozaa na binadamu huwa hawashuki tena duniani na kuja kuzaa na mabinti wengine baada ya gharika hadi mpaka sasa?
Nini kimewazuia
Mie nadhani bado malaika huwa wanashuka aisee...rejea marehemu masogange...duuhhh...alikuwa kamili kila idara...sihaba malaika walitia nakshi kikatokea kitu kile....au hata shemela wetu kwa brother kiba...daah.
 
Wee mkuu nimekuelewa vizuri aisee...ujuwe manefili walikuwepo kitambo...sasa wakawa tishio kwa wanadamu...so mungu kutubust akili na maarifa akawatuma malaika wazae na mabinti zetu ndio wakatokea vizazi vyenye akili za kuwazidi manefil....good idea.
 
Unamaanisha nini kusema hivi?

Louis Seymour Bazett Leakey alituambia kua Mtu wa Zamani/Kale zaidi aliishi Tanzania, na aliigundua hii kitu baada ya kupata Fuvu la Binadamu huyo. Kama unaelewa issue za Zinjanthropus
 
kuna movie niliionaga zuku movies Nuhu anasaidiwa kujenga safina na THE WATCHERS ...majitu hayaeleweki eleweki kama yamejengwa na mawe halafu macho yao ni mwanga mkali...

Sikuielewa ,japo pia sielewi Watchers kwa kiswahili ni nini? wakuu tufafanulieni
 
mkuu assumptions hizo inabidi na Uhusika wa Mungu kwenye hilo zoezi hilo uwe neglected.
pia baadhi ya commentary zinasema kutumika kwa neno la kiebrania linaloendana na wanefili wa zamani sio lazima awe nefili aliyetoroka kichapo cha mafuriko, bali ni lugha kuwakilisha ufanano wa hilo jitu na majitu ya kale. maana ukiliita hivyo kwa waebrania wataelewa zaidi.

lkn kabla haijatajwa futi 15, fungu la nyuma linasema milima yote ilifunikwa (kufunikwa milima yote, assumption ilikuwa ni grobal flood hata everest yenye zaidi ya futi 20,000, yawezekana hiyo 15 foot ni kwa vimilima ambavyo vilikuwa karibu, ila lile fungu la nyuma lilipozungumzia milima yote sidhani kama huyo jamaa angeweza kusurvive).

Ikiwa ni futi 15 flat worldwide nadhani kuna sehemu zitakuwa hazijafunikwa na maji kama mlima kilimanjaro, kitu ambacho kitakanusha sentesi milima yote ilifunikwa.

Pia nawaza kwa assumption ya uwezekano wa kutoroka kwa huyo jamaa kutokana na umbo lake kuwa kubwa kuliko kimo chake.
mambo kadhaa yataibuka.
1: Mungu ataonekana ni unintelligent being kutoa adhabu ambayo kuimbe wake anaweza kuikwepa. kitu ambacho hakiungani na sifa za Mungu.
2:Mikono 15 ya watu wa enzi za nuhu ni tofauti na mikono ya kipindi hiki. kumbuka kabla ya mafuriko watu walikuwa ni wakubwa sana, na wenda ilichukuliwa reference ya mikono ya hayohayo manefili maana lengo la mafuriko pamoja na yote hao ndio walikuwa walengwa wakuu.
3:Gharika ilidumu juu ya nchi zaidi ya siku arobaini. huyo OG alitakiwa asimame kwenye maji yenye nguvu bila kula siku arobaini. Kumbuka kwao mvua ilkuwa ni mshtukizo japo nuhu alihubiri na kutoa tahadhari miaka 120. hivyo huyo jamaa hakujiandaa kisaikolijia, pia kusema alikula Mizoga kwa wigo wa bibilia watu walianza kula nyama baada ya gharika.
sidhani kama angepata stamina ya kusimama siku zote hizo. Kumbuka nguvu ya maji pia mkuu na huyo kiumbe hajawahi kukutana na hayo mazingira.

4:Mvua ilinyesha Siku 40, maji yakadumu siku 150 siku karibu 200 huyo mdau alikuwa yuko majini. na Mungu akimuangalia tu. Zaidi ya nusu mwaka. mkuu biologically kwa non-aquatic being kuwa hai majini hata kama ni maji ya kiuno?



najaribu kufikiri na kuvaa viatu vya OG napata shida inabidi assumptions nyingi sana ziongezeke, na constants nyingi sana ziondolewe na uwezo wa Mungu na nia yake udogoshwe kabisa awe kama nyampala flani tu ambaye alikiwa anaadhibu vijana wake na baadhi wakamchenga.


nawaza mkuu.
assumption kuu. Yale maji hayakuwa tulivu kama ya kwenye swimming pool hadi mdau apate kusimama raha mstarehe miezi sita, bali yalikuwa ni zaidi ya tsunami kwa maana ya nguvu na vurugu zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…