Kudo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2017
- 1,821
- 6,119
Hii nadharia umesema ndiyo yenye mashiko,sijaelewa ina mashiko kwa nani,kama ni kwako ni sawa...
Kwangu mimi nadharia hii naiona haina mashiko kabisa mkuu.Nasema hivi kwasababu zifuatazo..
1;Suala la yeye "kupewa kazi ya kuiangalia safina ili isigngane na mawe"ni nadharia ya kuchekesha sana maana unataka kumfanya Mungu kama asiyejiweza na kuelewa alilokuwa anafanya.Kwanza ni mawe gani hayo? Maana maji yalifunika milima yote,kuna jiwe kubwa zaidi ya mlima Kilimanjaro kwa mfano?Lakini unapaswa tu uelewe kwamba suala zima la gharika ni suala lilisimamiwa na Mungu,sijuwi kama unaelewa ni nini maana ya Mungu kwa ujumla wake.....
2;Unadaio kuwa "kwa akili ya kawaida dunia nzima izame halafu wewe pekee uwe kwenye boti,hivi waliokufa watakuacha kweli?",yaani hiki nacho ni kichekesho kingine mkuu. Kwanza safina siyo boti,pili safina ilijengwa kwa namna ya ajabu na kwa maelekezo ya Mungu mwenyewe unadhani unaweza ivunja? Kwa kutumia nini? Halafu ukiwa kwenye maji huku ukipigania uhai wako? Are you serious?
Mungu aliwajuwa hao majitu vizuri sana na kwakuwa yeye aliisimamia "shoo"haya unayofikiria ni kama kitu cha kuchekesha sana kwake...
Hii nadharia yako haina mashiko kabisa hata kiduchu....
Hii nadharia inajaribu kuelezea namna kizazi cha Wanefili kilivyokuja kupatikana baadaye,baada ya gharika.Inawezekana au isiwezekane ukizingatia sababu kuu ya gharika ni hao hao Wanefili na sidhani kama Mungu angeruhusu ikawa hivi japokuwa inaweza ikawezekana pia...
Hii nadhara nayo haifai kabisa.Hii nadharia inataka kumfanya Mungu asiwe Mungu kabisa maana kama tu mtu anaweza kupanda kwenye mlima halafu Mungu atake kumuua na ishindikane kwasababu kapanda kwenye mlima huyo siyo Mungu ni kitu kingine kabisa...
Inawezekana lakini swali kubwa ni namna ilivyowezekana....
Wanefili wa kabla ya gharika walifikia futi 30 hivyo huyu OGu unayemsema hapa sijaona uajabu wake.Ninachokielewa ni kwamba Wanefili wa baada ya gharika walikuwa na urefu wa futi 10 hadi 18 hivyo walikuwa wadogo kiumbo kuliko wale wa kipindi kile cha kabla ya gharika....
Majengo ya kustaajabisha hayapatikani mashariki ya kati pekee mkuu,yapo dunia nzima kuanzia Puma Punku kule Bolivia hadi Urusi mpaka kwenye kisiwa cha Sardinia kule Italy ambapo baadhi ya watafiti wanasema kwamba inawezekana ilikuwa ni moja ya ground Zero ya Wanefili wa kabla yagharika maana walishafukua mabaki makubwa sana ya hawa Wanefili.Moja ya fuvu lililowashangaza ni lile ambalo waliweza kuingiza kwenye eye socket ylile fuvu,ule upanga refu wenye makali kila upande,upanga maarufu wa vitani na ulizama wote na ulipogota kisogoni sehemu pekee iliyobakia nje ni ile sehemu ya kushikia tu...
Unaweza tu kufikiria lilikuwa ni fuvu kubwa kwa kiwango gani...
Mabaki ya majitu haya yenye urefu wa zaidi ya futi 25 yamefukuliwa maeneo mengi sana America ya kusini,kaskazini,Africa,Ulaya na Asia hivyo huyo unayemsema hakuwa peke yake labda baada ya gharika kama ulivyoelezea hapo juu kwasababu baada ya gharika Wanefili walikuwa wadogo kiumbo...
Sijaelewa ulichotaka kutuambia ila naamini ulitaka kutuambia kitu flani muhimu,lakini pia ungelijaribu kutupa na wew ushahidi wako ikibidi na baadhi ya nukuu ili twende sawa kuhusu kusalia kwa mtu huyo au kufa kwa mtu huyo wakati wa garika maana nukuu nyingi sana zinaonesha uwezekano wa Ogu kusalia na tayari watu wengi wamechangia hapa na nukuu zao kutoka vitabu tofauti tofauti
Lakini pia naomba nikuulize swali moja Hope utatusaidia
Nuhu aliwezaje kujenga safina ile kubwa peke yake? Na aliwezaje kupata mbao au miti mingi vile kujengea na aliitoa wapi ikiwa sehemu alikokuwa akiijengea kulikuwa ukanda wa jangwa?