Mkuu ukiwa msomaji wa biblia utaelewa hoja yangu kivipi Mungu anaweza toa hukumu ila akaruhusu masalia wabaki na amefanya hivyo hata kwa wanefili wa baada ya gharika (Waamori)ambayo ni familia ya mfalme Ogu
Twende taratibu
1. Mungu anamuamuru waisraeli waue wakaanani WOTE wasibakize kitu
Kumbukumbu la torati 20
16
Lakini katika miji ya mataifa haya akupayo BWANA, Mungu wako, kuwa urithi, usihifadhi kuwa hai kitu cho chote kipumzikacho;
17 lakini uwaangamize kabisa, Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, kama alivyokuamuru BWANA, Mungu wako;
2.Tukisoma kwenye joshua baada ya kuwa wameikamata canaani waliweka makubaliano na hawa wanefili ya kuwaacha hai!!
Joshua 9:15
15
Naye Yoshua akafanya amani pamoja nao, na kufanya agano nao, ili kwamba waachwe hai; na wakuu wa mkutano wakawaapia
3.Kinyume kabisa na maagizo ya Mungu ya kwanza tunaona wagibeoni wakiachwa hai na waliingia agano ambalo Mungu alisupport
Kumbukumbu 7
1
BWANA, Mungu wako, atakapokutia katika nchi uendayo kuimiliki, atakapoyang?oa mataifa mengi watoke mbele yako, Mhiti, na Mgirgashi, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, mataifa saba makubwa yenye nguvu kukupita wewe;
2 wakati BWANA, Mungu wako, atakapowatoa mbele yako, nawe utawapiga; wakati huo ndipo uwaondoe kabisa; usifanye agano nao, wala kuwahurumia; wala usioane nao
4.mpaka hapa unaweza kufikiri waliamua wenyewe waisrael lahasha..... Huko mbeleni tutaona MUNGU akiwaadhibu waisraeli kwa kuvunja agano hilo la kuwaacha waamori/wagieboni hai
2 samuel 21
1
Kulikuwa na njaa siku za Daudi muda wa miaka mitatu, mwaka kwa mwaka; naye Daudi akautafuta uso wa BWANA. BWANA akasema, Ni kwa ajili ya Sauli, na kwa nyumba yake yenye damu, kwa kuwa aliwaua hao Wagibeoni.
Je unataka kusema Mungu ni kigeugeu au utakubaliana na mimi kuwa Mungu aliamua kuwaacha hao wagibeoni kwa kusudi lake???
Na je kama tunaona hapa Mungu aliamrisha waue waamori WOTE ila baadae Mungu alitaka wengine wabakizwe je huoni hoja ya kusema Ogu kuwa mnefili pekee kuachwa kwenye gharika kuwa ina mashiko maana tumeona kumbe Mungu akitoa hukumu ya WOTE huwa anaacha exceptions!!!
Karibu tuelimishane mkuu wangu
Cc
Mchawi Mkuu