Mfalme Ogu wa Bashani: Mnefili pekee aliyepona kwenye Gharika la Nuhu

1.Ahsante mkuu, ila tatizo ninaloliona tukikataa kuwa wale sio wana wa Mungu, inabidi tuseme wanadamu duniani hawapo (really)?.
2. Endapo netamuki alipona na gharika vipi uzao wake nao uliangamizwa baadae?, maana kama wapo wana wa wanadamu wangeendelea kuwepo vilevile majitu
Maoni yako mkuu
1. Ikiwa tutafuata definition hiyo basi itabidi tukubaliane kuwa wanadamu hawapo tena duniani waliobaki ni wana wa Mungu!!! Sounds funny i know..... Ila kwa tafsiri ya kibiblia itabidi tukubali hivyo kuwa hakuna tena wanadamu au kama wapo basi ni wale wasiofuata mapenzi ya Mungu nf wazinzi wauaji nk

2. Inaelezwa Neitamuk alikuwa na watoto wengi tu mkuu na ndipo uzao wa watu weusi ulipotokea yaani Ham alikuwa mweupe tu kma baba yake (book of enoch inaeleza hili) hivyo kwa kuoa mwanamke mweusi akapata watoto kma phut (libya) cush (ethiopia) na mizraim (misri) ambao kupitia hao ndio makabila mengi sana ya waafrika yametokea hapo hivyo twaweza kusema WAAFRIKA wote ni zao la neitamuk
 
Mkuu nimekuelewa point#1
#2 inaelekea waafrika ndo wanadamu waliobaki je, mbona hatuzai ma giant tuki interbreed na wana wa Mungu (other race).
 
Mbona walizaliwa giants soma vizuri biblia.... Watoto wa Ham 90% walikuwa giants kuanzia canaan watoto wake woote walikuwa giants gibeoni,hivi,amori,amon,aruba,anaki,yebusi n.k wote walikuwa majitu makubwa hata biblia inasema hivo pia kwenye uzao wa mizraim tunakutana na baba wa wapalestina wote alieitwa caphtor huyu alikuwa JITU kubwa sana na hta uzao wake ndio anatokea goliath so bado tunaona wanefili wakirudi baada ya gharika sababu ya damu ya neitamuk

Ila cha kujiuliza hicho kizazi kiliishia wapi?? Ingawa kina Eiyer na Mchawi Mkuu wamedai wanefili bado wapo ingawa sio kwa miili kma zamani ila akili zao ni za kinefili na wameenda mbali na kusema kuna viongozi wakubwa wa sasa wa dunia hii ni damu hiyo ya wanefili so bado ni mjadala hawa wanefili waliishia wapi ila kibiblia hatuelezwi sababu tunaona mpaka agano la kale linaisha bado wanatajwa tu uwepo wao sielewi walipotelea wapi baadae na kwanni sahvi hawaziliwi tena

Subject of debate
 
Ila navyoelewa ka kadri ya ufahamu wangu mdogo juu ya Biblia inaposemwa Ulimwengu inamaanisha Mashariki ya Kati ina maana hata gharika lilipiga maeneo hayo tu haikuwa dunia nzima huenda Ogu wakati mvua inaanza alihama huko na kwenda maeneo mengine ambako hapakuwa na mvua hivyo biblia inazungumza Ulimwengu/Dunia kwa maana ya maeneo hayo ya Mashariki ya kati tu hivyo Ogu aliishi hata baada ya Gharika na kubaki pekee yake huko Mashariki ya kati lkn sehemu zingine huenda Wanefili waliendelea kuishi ila kwa sababu hawajazungumzwa kwe biblia hatuwezi kujua,ni hayo tu wadau!!
 
1.Kuendana na hoja ya kwamba wana wa Mungu ni watoto wa Seth na wanadamu ni watoto wa cain hivyo tunaweza kusema kizazi cha wanadamu yaani cain kilimalizwa kwenye gharika ila kizazi cha seth ndio alipotokea Nuhu hivyo wanadamu wote baada ya gharika baba yetu ni SETH ukimtoa mke wa ham aliyeitwa neitamuk anayesadikiwa kuwa ukoo wa cain

2. Kuhusu kwanini majitu hayazaliwi..... Kama bado unasimamia hoja kuwa wana wa Mungu ni seth na wanadamu ni cain basi jibu ni hayazaliwi majitu sababu ukoo wa cain haupo maana kama hao watoto wa seth walikuwa watu wa kawaida ila walipooa watoto wa cain ndio ikatokea viumbe wa ajabu basi ina maana shida ilikuwa kwa ukoo wa cain huenda baada ya laana walikuwa na ukuaji wa miili tofauti na yetu ndio ikapelekea kuzaa wanefili so jibu ni KWAKUWA UZAO WA CAIN HAUPO

Ila tukifuata hoja ya kuwa malaika walioanguka ndio walizalisha wanadamu jibu lipo kwenye kitabu cha YUDA kuwa malaika hao wamefungwa kuzimu wakisubiri hukumu na moto wa milele hiyo inaweza kueleza kwanni hawazai tena na wanadamu

3.Kwa tafsiri ya Yesu kizazi cha Nyoka kinakuwa kile kinachofuata matendo ya shetani mfano wazinzi wauaji wezi n.k ila wana wa Mungu wanakuwa wale wote wanaofuata na kutenda mafundisho ya Mungu

NB:Kuna mjadala upo kama Kulikuwa na kizazi cha nyoka (shamael) kihalisia.... yaani Eva alizalishwa na Nyoka (kabla hajabadilishwa mwili na kuwa hivi alivo) ndio mtoto akawa Cain na ndio inaeleza kwanini wana wa seth walipooana nao wakazaliwa watoto wa ajabu na wanefili n.k nafkiri hii hoja inaweza elezewa vizuri na kina Mshana Jr

Ni hayo tu
Jamaa inaonekana unasoma sana vitabu na unajitahidi sana kuelewa na kulinganisha na uhalisia wa maisha yetu ya kawaida tunayoishi kila siku, vizuri sana mkuu
 
Ila navyoelewa ka kadri ya ufahamu wangu mdogo juu ya Biblia inaposemwa Ulimwengu inamaanisha Mashariki ya Kati ina maana hata gharika lilipiga maeneo hayo tu haikuwa dunia nzima huenda Ogu wakati mvua inaanza alihama huko na kwenda maeneo mengine ambako hapakuwa na mvua hivyo biblia inazungumza Ulimwengu/Dunia kwa maana ya maeneo hayo ya Mashariki ya kati tu hivyo Ogu aliishi hata baada ya Gharika na kubaki pekee yake huko Mashariki ya kati lkn sehemu zingine huenda Wanefili waliendelea kuishi ila kwa sababu hawajazungumzwa kwe biblia hatuwezi kujua,ni hayo tu wadau!!
Hii hoja yako imenifikirisha sana mkuu ntatafiti zaidi uhalisia wake
 
Ila navyoelewa ka kadri ya ufahamu wangu mdogo juu ya Biblia inaposemwa Ulimwengu inamaanisha Mashariki ya Kati ina maana hata gharika lilipiga maeneo hayo tu haikuwa dunia nzima huenda Ogu wakati mvua inaanza alihama huko na kwenda maeneo mengine ambako hapakuwa na mvua hivyo biblia inazungumza Ulimwengu/Dunia kwa maana ya maeneo hayo ya Mashariki ya kati tu hivyo Ogu aliishi hata baada ya Gharika na kubaki pekee yake huko Mashariki ya kati lkn sehemu zingine huenda Wanefili waliendelea kuishi ila kwa sababu hawajazungumzwa kwe biblia hatuwezi kujua,ni hayo tu wadau!!
Fuatilia upanue mawazo zaidi..
New Evidence Suggests Biblical Great Flood Happened
 
Vipi kuhusu mali kale za baharini kukutwa juu ya milima kma alps na mengineyo je bado haiwezekani ikaprove kuwa maji ya baharini yaliwahi kufurika hadi kwenye ardhi ikafunikwa??

Tuanzie hapo
Ukiona hivo soma formation za mlima husika, sjuwi ni physical geography ya darasa la ngapi!
 
Biblia gani mpya mbona vitabu vya dini vinavyotumika kwenye masynagogue ya waisraeli/wayahudi wanasema ogu alikuwepo kabla ya gharika na alipona gharika sasa why sisi weusi ndio tunashupaza shingo ilihali wenye nchi yao ambapo maandiko yalizaliwa wanakubali simulizi hii

Kingine hapa hatuongezi kitu tunajaribu kupata tu story nzima ya huyu mtu kutoka source mbalimbali ndio maana nikahoji yafuatayo na ningeomba tusaidiane kujibu ili tujue ukweli wa mambo

1. Je kwanini biblia inasema Og alikuwa mnefili aliyebakia?? Je alibakiaje ilihali wote waliangamizwa na gharika tusaidie alitoka wapi??

2. Je kama hakupona kwenye gharika hiyo damu ya wanefili ilivukaje gharika hadi wakazaana na kuishi nchi ya canaan mfano waamori wahivi wahiti annaki caphtori na wengineo

Tuanzie hapo kwanza
Labda ungeandika kifungu kabisa kurahisisha halafu nikujibu
 
Kuna kilicho salia zaidi ya hapa nipeni mstari wa Bible nisome tena
IMG_20180504_155547_602.jpg
IMG_20180504_155637_520.jpg
 
Conclusion:..
Mfalme OG alikuwepo
Hakuangamizwa for reasons.
Wanefili walikuwepo
Uzao wao unatokana Na malaika waasi Na kuzaa Na wanadamu!..

Wana wa Mungu hapo Bible imetafsiri kama malaika waasi Na Wala siyo Wana wa set!..

Hitimisho
Bible msomeni kwa uangalizi Na roho Mt!..
 
Kuna kilicho salia zaidi ya hapa nipeni mstari wa Bible nisome tena View attachment 765637View attachment 765638

Mkuu ukiwa msomaji wa biblia utaelewa hoja yangu kivipi Mungu anaweza toa hukumu ila akaruhusu masalia wabaki na amefanya hivyo hata kwa wanefili wa baada ya gharika (Waamori)ambayo ni familia ya mfalme Ogu

Twende taratibu

1. Mungu anamuamuru waisraeli waue wakaanani WOTE wasibakize kitu

Kumbukumbu la torati 20
16 Lakini katika miji ya mataifa haya akupayo BWANA, Mungu wako, kuwa urithi, usihifadhi kuwa hai kitu cho chote kipumzikacho;
17 lakini uwaangamize kabisa, Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, kama alivyokuamuru BWANA, Mungu wako
;

2.Tukisoma kwenye joshua baada ya kuwa wameikamata canaani waliweka makubaliano na hawa wanefili ya kuwaacha hai!!

Joshua 9:15
15 Naye Yoshua akafanya amani pamoja nao, na kufanya agano nao, ili kwamba waachwe hai; na wakuu wa mkutano wakawaapia

3.Kinyume kabisa na maagizo ya Mungu ya kwanza tunaona wagibeoni wakiachwa hai na waliingia agano ambalo Mungu alisupport

Kumbukumbu 7
1 BWANA, Mungu wako, atakapokutia katika nchi uendayo kuimiliki, atakapoyang?oa mataifa mengi watoke mbele yako, Mhiti, na Mgirgashi, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, mataifa saba makubwa yenye nguvu kukupita wewe;
2 wakati BWANA, Mungu wako, atakapowatoa mbele yako, nawe utawapiga; wakati huo ndipo uwaondoe kabisa; usifanye agano nao, wala kuwahurumia; wala usioane nao

4.mpaka hapa unaweza kufikiri waliamua wenyewe waisrael lahasha..... Huko mbeleni tutaona MUNGU akiwaadhibu waisraeli kwa kuvunja agano hilo la kuwaacha waamori/wagieboni hai

2 samuel 21
1 Kulikuwa na njaa siku za Daudi muda wa miaka mitatu, mwaka kwa mwaka; naye Daudi akautafuta uso wa BWANA. BWANA akasema, Ni kwa ajili ya Sauli, na kwa nyumba yake yenye damu, kwa kuwa aliwaua hao Wagibeoni.

Je unataka kusema Mungu ni kigeugeu au utakubaliana na mimi kuwa Mungu aliamua kuwaacha hao wagibeoni kwa kusudi lake???

Na je kama tunaona hapa Mungu aliamrisha waue waamori WOTE ila baadae Mungu alitaka wengine wabakizwe je huoni hoja ya kusema Ogu kuwa mnefili pekee kuachwa kwenye gharika kuwa ina mashiko maana tumeona kumbe Mungu akitoa hukumu ya WOTE huwa anaacha exceptions!!!

Karibu tuelimishane mkuu wangu
Cc Mchawi Mkuu
 
Kiongozi usijaribu kubishana Na watu!.
Mbona hapo juu nishatoa hitimisho!.
Mpango wa Mungu Huwa Na kusudi maalumu!.
Nimesema hapo juu kuwa Mungu alimwacha OG Na waamor for reasons!...
 
Back
Top Bottom