Salamu wana jamvi, corona ipo na inaua ,nyungu inapandisha mapepo tu.
Moja kwa moja niende kwenye mada
Anaitwa Diana Richard Bundala,au waumini wake wanapenda kumuita mungu chini ya jua,mfalme wa dunia.
Juzi kanisa lake lenye waumini zaidi ya elfu mbili lililopo maeneo ya Iseni Mwanza,lilifungiwa na serikali kutoa huduma za kiroho kwa kwenda kinyume na misingi ya kiimani.
Diana anadai kwamba yeye ni mungu chini ya jua,na pia ni mfalme wa dunia yote.
Diana anadai kuwa yeye ametumwa na Mungu kuja kuukomboa ulimwengu baaada ya Yesu kristu.
Yaani Mungu baada ya kumtuma Yesu hapa duniani na kuona bado matendo maovu yanaendelea,ndio akaamua eti sasa amtume yeye
Diana anadai yeye kapewa mamlaka ya kimungu hapa duniani,hivyo kila akionekana inabidi asujudiwe(na waumini wake wamekuwa wakimsujudia kila anapoonekana)
Diana bundala anadai kuwa na yeye hapa duniani anasurubiwa kwa dhambi za wanadamu kama alivyosurubiwa Yesu kristo.
Anasema yeye anasurubiwa kwa kusemwa vibaya, kutukanwa na hata kufungiwa huduma yake na serikali.yote hayo ni kwa sababu ya dhambi za wanadamu.
Diana anadai kuwa kwakuwa yeye ndiye mungu wa hapa duniani,basi yeye ndiye anasamehe dhambi...hivyo wanadamu wote waende kwake kusamehewa dhambi.
Diana Bundala anadai kuwa marehemu wengi wenye majina makubwa waliofariki wapo kwake.
Anadai Marehemu Kanumba yupo kwake,marehemu Ruge yupo kwake na wengine wengi!!!anadai siku akiamua kuwatoa basi atawatoa.
View attachment 1709595