Mfalme Zumaridi ni nani haswa?

Wewe kati ya hayo lipi umeliamini katika harakati za kuaminishwa
 
Haya mafundisho ya hawa mitume na manabii wa siku hizi huwafanya wengi kuwa watumwa wao, na mbaya zaidI kwasababu wengi wa waumini wao hawana maarifa yoyote ya biblia hujikuta wanatumbukizwa kwenye mafundisho potofu huku wao wakiamini wako kwenye njia salama.

Njaa zao za kutafuta miujiza huwapofusha akili na macho yao wasione hatari iliyowazunguka au inayowakaribia kutoka kwa mafundisho ya hao manabii wa uongo.

Tumfuteni kwanza Yesu Kristu kupitia maandiko ya biblia, tusijidharau kwa kujiona tuna dhambi sana au vyovyote vile.

Tukishamjua Yesu yeye ndie atatutendea miujiza tunayoitafuta kwasababu yeye ndie mtenda miujiza, sio tunapoteza muda kuitafuta miujiza wakati Yesu Kristu mwenyewe hatumjui, tunajidanganya, na tutachezewa sana na hawa manabii wa uongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…