Mfamasia wa Wilaya apewe majukumu ya kusimamia pharmacy kwenye eneo lake. Tuache kubandika vyeti vya wafamasia kwenye maduka, siyo cctv camera

Mfamasia wa Wilaya apewe majukumu ya kusimamia pharmacy kwenye eneo lake. Tuache kubandika vyeti vya wafamasia kwenye maduka, siyo cctv camera

Naomba kuuliza hivi hiyo Pharmacology anayosoma
1. Mfamasia
2. MD
3. Nurse
Zina utofauti yaani Pure na ingine Basic???
Mtujuze kwanza....
 
Sheria zimetungwa ili zitekelezwe, zisinge kuwa ni sheria hata HKL, CBG,Pcm wangepelekwa kusomea MD naz wangefaulu vizuri. Mwisho wa siku mtasema lab technologist wawepo famasi

Wanasimamia famasi sbb wapo kisheria
 
Nataka kujua cheti cha mfamasia kinaruhusiwa kubandikwa kwenye pharmacy ngapi ndani ya wilaya anakoishi? Maana kama kinaweza kubandikwa ndani ya pharmacy zaidi ya moja basi haina maana kabisa. Kama kinaweza kubandikwa ndani ya pharmacy zaidi ya moja kwa maana ya kuzisimamia, kazi hii angepewa mfamasia wa wilaya kazi hii anaweza kuifanya kwa ufanisi zaidi.

Kubandika cheti dukani then unalipwa milioni moja daah. Hivi hii hela huwa inalipiwa kodi?
EeeeeenHeeee!

Huo ndio uozo wa kitaaluma!

Na siyo hao tu, kila mahala ukiangalia ni uozo tu; mpaka Bungeni!

Sasa itabidi tuwe na utaratibu wa kuibua uozo sehemu mbalimbali za utendaji na kuujadili humu JF, labda hiyo itasaidia. SIJUI.

Lakini lazima niseme hili, na wala siyo kusamehe huo uozo uliopo huko ndani ya utendaji wa fani hiyo ya Pharmacy.

Kubandika cheti siyo hoja. Palipo na UBUNIFU, inawezekana kabisa kwa mtaalam mmoja akahudumia sehemu kadhaa kwa wakati mmoja kama miundo mbinu ya teknologia inaruhusu.
Na huko ndiko tutakakoelekea miaka siyo mingi tokea sasa, na hili halitahusu fani hiyo pekee, bali muundo wote wa uhudumiaji wa wagonjwa na huduma za Afya kiujumla.
Tutafika mahali ambapo si kila mgonjwa ni lazima aende kumwona tibabu kila mara atakapohitaji huduma. Kama ni mgonjwa ambaye tayari hali ya ugonjwa wake inafahamika, na alishawekwa katika matibabu yanayofanya kazi, basi huyu anaweza kuwa ana'monitor' hali yake kila mara kwa kutumia teknolojia kuendelea na matibabu yanayofanya kazi bila ya lazima ya kwenda kutafuta huduma tena mara kwa mara. Hii inapunguza misongamano kwa watoa huduma.

Kutafika wakati ambapo mgonjwa kujihudumia itawezekana, hasa katika magonjwa yasiyokuwa hatarishi.

Tunaelekea huko, na miaka si mingi, huku kung'ang'ania taaluma kama raslimali itakuwa haina maana tena.
 
Naomba kuuliza hivi hiyo Pharmacology anayosoma
1. Mfamasia
2. MD
3. Nurse
Zina utofauti yaani Pure na ingine Basic???
Mtujuze kwanza....
Yeah, kwa izo carrier ulizozitaja hapo pharmacist yupo deep zaidi ya hao wote kwa upande wa pharmacology, ana semester nyingi zaidi za pharmacology na kaenda mbali zaidi kuliko hao wote uliowataja.

Ni course pana na ngumu na kwa nchi za wenzetu kama india wanabachelor yake inajitegemea, inaitwa B. Pharm in phatmacology, a 4 years degree.
 
imagine, wanaruhusiwa kusimamia maduka matatu. na kila duka huwa tunawalipa milioni moja kwa mwezi, and still wanajifanya miunguwatu. hizi takataka zinaitwa mfamasia zinatesa sana nafsi za watu mtaani huko. kuna siku tutawataja majina na mali mnazomiliki hapa.
We nae punguani tu.
Hamjui lolote kujiropokea kwenye sm
 
Naomba kuuliza hivi hiyo Pharmacology anayosoma
1. Mfamasia
2. MD
3. Nurse
Zina utofauti yaani Pure na ingine Basic???
Mtujuze kwanza....
Mkuu 'Papai'
Inaonyesha kama una nia ya kutaka kujua. Ngoja nijaribu kukuelimisha kidogo.

Pharmacology, kila mmoja wa hao watu anaisoma kwa kina tofauti kufuatana na taaluma za kila mmoja wao inavyohitaji.

Ngoja nitoe mfano, pengine itaeleweka zaidi: Medical Assistant (nadhani siku hizi huitwa Clinical Officers, sina uhakika na hili), anasoma karibu masomo yote anayosoma daktari, lakini si kwa kina kama kile anachopaswa kusoma daktari. Huyu anaposoma Anatomy, kwa mfano, haingii ndani hadi kufanya 'dissection' ya cadaver. Na hivyo hivyo na masomo mengine ya udaktari, na muda anaochukua kuyasoma haya ni mfupi zaidi ili kumwezesha tu kuweza kufanya kazi anayohitaji kufanya kwa kiwango chake.

Hali ipo hivyo hivyo, na katika hii 'Pharmacology' inayozungumziwa sana katika fani hizi tatu.

Pharmacology ni somo linalohusu jinsi dawa inavyofanya kazi mwilini kumtibu mgonjwa.

famasia, yeye anachosoma zaidi ni kuhusu dawa katika maeneo mbalimbali ya dawa hiyo, ikiwemo jinsi inavyofanya kazi mwilini.

Dawa, ni kemikali, kama kemikali zingine zozote, kwa hiyo kufanya kazi mwilini kwa dawa hiyo, maana yake ni jinsi kemikali hii inavyo'interact' na mwili au wadudu ili kumponyesha mgonjwa.

Kwa hiyo utaona wazi hapa kwamba, pamoja na kutakiwa kujua 'pharmacology', kuna ujuzi zaidi unaotakiwa juu ya kujua muundo wa kemikali hiyo, ambayo ni dawa.
Famasia anasoma kemikali ya dawa (Medicinal Chemistry), mbali ya kujua 'Pharmacology'ya dawa husika. Somo hili la Medicinal Chemistry halifundishwi katika fani nyingine yoyote bali fani ya Famasia pekee. Kwa hiyo utaona hapa wazi kwamba mfamasia ana la ziada katika kujua dawa kuliko hao wengine uliowataja.

Na siyo hivyo pekee. Kujua 'pharmacology' hakumfanyi mtu kuwa na uhakika wa jinsi dawa itakavyofanya kazi yake vizuri mwilini mwa mgonjwa.
Dawa, kama vidonge, sindano, za kupaka, n.k., zinatengenezwa kwa kuunganisha na vitu vingine ili hiyo dawa iweze kufanya kazi yake vizuri, au iweze kutumika kwa urahisi, au iweze kufanya kazi mwilini kwa muda mrefu zaidi ili mgonjwa asitakiwe kutumia mara kwa mara.

Kwa hiyo, unaposema dawa, kama kidonge, kidonge hicho siyo dawa pekee, kuna vitu vingi vingine humo vinavyoongezwa kwa sababu mbalimbali. Hivi vitu vinavyoongezwa humo, nazo ni kemikali, ambazo nazo zinaweza kusaidia au kuathiri matumizi ya dawa.

MFamasia, anasoma somo linaloitwa "Pharmaceutics", ambalo linahusu utengenezaji wa dawa hizo kama nilivyoeleza hapo juu. Yaani muunganiko wa kemikali mbalimbali, ili iweze kutokea kama kidonge au kapsulu, au dawa ya majimaji, n.k.
Hili nalo ni somo lisilofundishwa kwingine kokote katika hizo fani ulizotaja hapo, bali linafundishwa kwa Famasia pekee.

Si kawaida yangu kuandika gazeti, naona nishaandika vya kutosha kukupa mwanga kidogo, kati ya tofauti iliyopo kati ya fani hizo tatu.

Mifano niliyotoa hapa ni sehemu tu ya tofauti. Sijazungumzia "Pharmacokinetics", somo analosoma mfamasia, lakini wengine hawalisomi. Hili linahusu dawa itakavyoweza kutembea na kujisambaza mwilini mwa mgonjwa na kiasi cha chemmbechembe za dawa hiyo kitakachofikia eneo lenye matatizo ya ugonjwa. Kama ni sehemu pungufu, basi mgonjwa hawezi kufaidika na dawa hiyo, kama ni kiasi kikubwa zaidi, basi mgonjwa anaweza kudhurika badala ya kufaidika na dawa hiyo. Na wakati huo huo mwili wa mgonjwa nao unashughullika kuiondoa dawa hiyo mwilini, kwenye mkojo, na maeneo mengine. Ni lazima dawa hiyo aliyokunywa mgonjwa iweze kutengenezwa ili wakati ipo mwilini haipungui au kuongezeka zaidi ya kiasi kinachohitajika kutibu ugonjwa.

Kuna mengine mengi...

Nipe mrejesho kama umeelewa kidogo tofauti iliyopo kati ya hao watatu, mbali ya kuitazama tu 'Pharmacology' kuwa ndicho kitu pekee kinachowaunganisha.
 
imagine, wanaruhusiwa kusimamia maduka matatu. na kila duka huwa tunawalipa milioni moja kwa mwezi, and still wanajifanya miunguwatu. hizi takataka zinaitwa mfamasia zinatesa sana nafsi za watu mtaani huko. kuna siku tutawataja majina na mali mnazomiliki hapa.
Pole sana mkuu, hauko updated!

Hiyo ya kusimamia Famasi zaidi ya moja ilikuwa zamani ila sio sasa.
 
Naomba kuuliza hivi hiyo Pharmacology anayosoma
1. Mfamasia
2. MD
3. Nurse
Zina utofauti yaani Pure na ingine Basic???
Mtujuze kwanza....
Utofauti wake ni kama anayesoma Basic Applied Mathematics(BAM) na mwingine anasoma Advanced Mathematics(Pure Mathematics)

Kama umepita kidato cha tano na sita hasa mchepuo wa Sayansi, utakuwa umenielewa vizuri
 
Any pharmacy Act Caption au kanuni inayotaka uwepo wa hili?
 
Nataka kujua cheti cha mfamasia kinaruhusiwa kubandikwa kwenye pharmacy ngapi ndani ya wilaya anakoishi? Maana kama kinaweza kubandikwa ndani ya pharmacy zaidi ya moja basi haina maana kabisa. Kama kinaweza kubandikwa ndani ya pharmacy zaidi ya moja kwa maana ya kuzisimamia, kazi hii angepewa mfamasia wa wilaya kazi hii anaweza kuifanya kwa ufanisi zaidi.

Kubandika cheti dukani then unalipwa milioni moja daah. Hivi hii hela huwa inalipiwa kodi?
Njia yako bado sio suluhisho, serikali ukitaka namna bora wapo watu watawapa suluhu ,kuwa mikononi mwa wafamasia wa wilaya ni mwanzo wa rushwa
 
imagine, wanaruhusiwa kusimamia maduka matatu. na kila duka huwa tunawalipa milioni moja kwa mwezi, and still wanajifanya miunguwatu. hizi takataka zinaitwa mfamasia zinatesa sana nafsi za watu mtaani huko. kuna siku tutawataja majina na mali mnazomiliki hapa.
Tatizo ni kwamba watu ambao si wafamasia wanataka kufanya biashara ya pharmacy, hapo ni lazima utafute mfamasia mwenye utaalamu huo! Sasa unalaumu nini? Unataka uruhusiwe kufanya biashara inayogusa afya za watu bila usimamizi wa wataalamu husika? Ulitaka mfamasia aliyesoma shahada kwa miaka 5 na kulipia ada ya chuo mamilioni ya shilingi alipwe shilingi ngapi kwa kusimamia biashara hiyo inayokuingizia mamilioni ya kutisha kwa mwezi!! Kama huwezi kumlipa mfamasia kwa huduma yake nenda kauze nafaka!! Duniani kote pharmacy zinaendeshwa na kusimamiwa na wafamasia!! Kama unaona wanafaidi na wewe nenda kasomee pharmacy!! Wewe unataka ufanye kazi ambayo hujaisomea haiwezekani!! Mtu halali na kuamka halafu akawa mfamasia!!
 
Unaelewa chochote kuhusu business of pharmacy?

Certificate kukaa hapo iko kisheria kwenye pharmacy act sio kuwa wamejiamulia.

Na upo utaratibu wa kufanya supervision sio kwamba cheti kinakuwepo kama hewa , na ukiona mtu hafanyi monthly supervision basi tatizo lipo kwake.

Kwa nchi nilizowahi kuishi na hata nilipo pharmacist anapaswa kuwepo full time.
Huku Tanzania cheti ndo kinakuwepo full time, mfamasia mwenye hajawahi kuonekana. Huoni tatizo hapo?
 
Any pharmacy Act Caption au kanuni inayotaka uwepo wa hili?
Yote yanayolalamikiwa yapo kisheria!! Wanaolalamika hawajui sheria!! Na si Tanzania tu bali ni duniani kote!! Kimsingi maduka yote ya pharmacy yalitakiwa kusimamiwa na wafamasia tu. Lakini kwa sababu wafamasia ni wachache sana ndio maana serikali ikaja na mpango wa maduka ya dawa muhimu ambayo si lazima yasimamiwe na mfamasia japo ni lazima yawe yanakaguliwa na mfamasia wa halmashauri mara kwa mara!! Kwa nchi za ulaya hakuna kitu kama duka la dawa muhimu au dawa baridi. Maduka yote ya dawa ni pharmacy, na sisi huko ndiko tunakokwenda. Kwa kadri wafamasia wanavyozidi kuongezeka ndivyo maduka ya dawa muhimu yatakavyokuwa yanapungua na tukiwa na wafamasia wa kutosha maduka ya dawa muhimu yataondolewa na kubakiza pharmacy tu.
 
Huku Tanzania cheti ndo kinakuwepo full time, mfamasia mwenye hajawahi kuonekana. Huoni tatizo hapo?
Pia mfamasia anafanya majukumu yake yote hapo kwa mujibu wa sheria! kama kuna muuzaji mwenye sifa kama muuguzi si lazima mfamasia awepo muda wote ila ndiye anayemsimamia huyo muuzaji na ndiye anayetoa ripoti ya utendaji wa pharmacy kwenye mamlaka zinazohusika! Tatizo la jamii ni kuwa haijui majukumu ya mfamasia!
 
imagine, wanaruhusiwa kusimamia maduka matatu. na kila duka huwa tunawalipa milioni moja kwa mwezi, and still wanajifanya miunguwatu. hizi takataka zinaitwa mfamasia zinatesa sana nafsi za watu mtaani huko. kuna siku tutawataja majina na mali mnazomiliki hapa.
Tumesoma sana kuhusu dawa mkuu.. kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.
 
Tatizo ni kwamba watu ambao si wafamasia wanataka kufanya biashara ya pharmacy, hapo ni lazima utafute mfamasia mwenye utaalamu huo! Sasa unalaumu nini? Unataka uruhusiwe kufanya biashara inayogusa afya za watu bila usimamizi wa wataalamu husika? Ulitaka mfamasia aliyesoma shahada kwa miaka 5 na kulipia ada ya chuo mamilioni ya shilingi alipwe shilingi ngapi kwa kusimamia biashara hiyo inayokuingizia mamilioni ya kutisha kwa mwezi!! Kama huwezi kumlipa mfamasia kwa huduma yake nenda kauze nafaka!! Duniani kote pharmacy zinaendeshwa na kusimamiwa na wafamasia!! Kama unaona wanafaidi na wewe nenda kasomee pharmacy!! Wewe unataka ufanye kazi ambayo hujaisomea haiwezekani!! Mtu halali na kuamka halafu akawa mfamasia!!
Pharmacy is a business of Pharmacist!
 
cheti chabandikwa kwa pharmacy kwa kati ya shilingi 700,ooo hadi 1,500,ooo kwa mwezi ili hali na yeye ni mwajiriwa tena wa serikali ama wa taasisi binafsi na hela hizo hazilipiwi kodi.

TRA piteni nao waingie kwenye mfumo kwa kodi manake fedha hiyo haikatwi kodiii
Kasomee pharmacy uweke cheti chako hutaulizwa.Tatizo mnalazimisha kufanyia biashara fani za watu.Sheria iko clear
 
Back
Top Bottom