Mfamasia wa Wilaya apewe majukumu ya kusimamia pharmacy kwenye eneo lake. Tuache kubandika vyeti vya wafamasia kwenye maduka, siyo cctv camera

Mfamasia wa Wilaya apewe majukumu ya kusimamia pharmacy kwenye eneo lake. Tuache kubandika vyeti vya wafamasia kwenye maduka, siyo cctv camera

hospitali hatutafungua, tutaendelea kuwanyoosha wafamasia hadi mtia adabu.
Umnyooshe nani kwa mfano?Huoni we ndo umenyooshwa hadi unakuja kulia lia hapa!Fanyia biashara kazi uliyosomea kwani lazima ulazimishe biashara ya dawa?Tatizo mnaona maisha rahisi rahisi
 
Naomba kuuliza hivi hiyo Pharmacology anayosoma
1. Mfamasia
2. MD
3. Nurse
Zina utofauti yaani Pure na ingine Basic???
Mtujuze kwanza....
Kwa lugha rahisi, mfamasia ni mtaalamu wa madawa! kazi yake inahusisha kutengeneza, kuchanganya, kutunza na kufikisha dawa kwa wagonjwa zikiwa salama. Ndiye anayeweza kuya-handle madawa na anajua vizuri kwa undani mode of action ya madawa. Daktari/MD ni mtaalamu wa tiba! kazi yake ni kutibu watu , anajua ni dawa ipi inafaa mgonjwa yupi, lakini, si mtaalamu wa kui-handle na kuitunza hiyo dawa, na hata mode of action ya hiyo dawa si lazima aijue kwa undani!!. Nurse ni mtaalamu wa kuuguza! kazi yake ni kuuguza wagonjwa na kuwandle wagonjwa katika kipindi wanachokuwa wanatibiwa. Ndiye anayefuatilia hali ya mgonjwa jinsi anavyoendelea!

Utaona kuwa kila mtaalamu ana majukumu yake ya kumtosha yaliyomgharimu miaka isiyopungua 5 kuhitimu kwa ngazi ya shahada!! Kwenye masomo yao kuna baadhi ya kozi wanazisoma wote!! Kwa hiyo hakuna ambaye ni mshamba kabisa kwa eneo laa mwenzake na hapo ndipo tatizo linapoanzia!! Kwa kuwa kila mmoja anajua baadhi ya majukumu ya mwenzake anaweza kujaribiwa kuona kuwa anaweza kuyafanya mwenyewe!! Kwa mfano Daktari anaweza kuona anaweza kuendesha pharmacy kwa kuwa kuna vitu vingi tu anavijua kuhusu madawa wakati SI KWELI!! Hali kadhalika mfamasia kuna vitu vingi anavijua kuhusu tiba kwa mujibu wa masomo yake na kwa mujibu wa uzoefu na siku hizi kuna ku-google!!. Kwa hiyo naye anaweza kuona anaweza kumtibu mgonjwa wakati SI KWELI!! Pia Nurse yeye pia kwa mujibu wa masomo yake na uzoefu wake na ku-google naye pia anajua mambo mengi sana ya kifamasia na kidaktari. Kwa hiyo nurse naye anaweza kuona anaweza kufanya majukumu ya mfamasia au ya daktari wakati SI KWELI. Afya zetu ni jambo TAKATIFU, lazima zishugfhulikiwe na mtaalamu husika kwenye eneo husika!!

Wtaalamu wetu hawa waheshimiane, wasiingiliane na watimize majukumu nyao kwa mujibu wa Sheria na kwa mujibu wa taaluma zao!! Ni ukosefu wa maadili daktari kuingilia majukumu ya mfamasia, hali kadhalika ni ukosefu wa maadili mfamasia kuingilia majukumu ya daktari. Kwa bahati nzuri madaktari na wafamasia huwa hawaingilii majukumu ya NURSE!! nafikiri ni kwa sababu ni magumu sana na hayaambatani na maslahi wakiyaingilia. Ila nurses huweza kujaribiwa kuingilia majukumu ya daktari na ya mfamasia hasa akiwa kwenye pharmacy!!

PENDEKEZO: Kuwe na adhabu kubwa sana kwa mtaalamu atakayeingilia majukumu ya taaluma isiyo yake kwa kuwa kwa kufanya hivyo atakuwa anahatarisha afya zetu.
 
Kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.. mambo ya kuoneana wivu hayasaidii.. ukiona wafamasia wanafaidi sana kutokana na fani yake, kasome nawewe miaka minne..
 
Nataka kujua cheti cha mfamasia kinaruhusiwa kubandikwa kwenye pharmacy ngapi ndani ya wilaya anakoishi? Maana kama kinaweza kubandikwa ndani ya pharmacy zaidi ya moja basi haina maana kabisa. Kama kinaweza kubandikwa ndani ya pharmacy zaidi ya moja kwa maana ya kuzisimamia, kazi hii angepewa mfamasia wa wilaya kazi hii anaweza kuifanya kwa ufanisi zaidi.

Kubandika cheti dukani then unalipwa milioni moja daah. Hivi hii hela huwa inalipiwa kodi?
Nenda kasomee pharmacy na wewe.
Physics, chemistry,na biology ndivyo vigezo vikuu.
 
Unaelewa chochote kuhusu business of pharmacy?

Certificate kukaa hapo iko kisheria kwenye pharmacy act sio kuwa wamejiamulia.

Na upo utaratibu wa kufanya supervision sio kwamba cheti kinakuwepo kama hewa , na ukiona mtu hafanyi monthly supervision basi tatizo lipo kwake.

Kwa nchi nilizowahi kuishi na hata nilipo pharmacist anapaswa kuwepo full time.
Kwa Tanzania labda 10% ya Pharmacies ndiyo utamkuta Pharmacist yupo full time, otherwise wagonjwa wengi tuna interact na wahitimu wa ADDO, Technicians na Nurses. Ni vyeti tu wameweka na wanapita mara moja kwa mwezi kuja kuichukua Tsh 1,000,000 -1,500,000.

Nami naunga mkono hoja ya mtoa mada, District Pharmacist anatosha kufanya kazi hiyo badala ya kuning'iniza vyeti tu huku watu hawafanyi supervision
 
Kwa Tanzania labda 10% ya Pharmacies ndiyo utamkuta Pharmacist yupo full time, otherwise wagonjwa wengi tuna interact na wahitimu wa ADDO, Technicians na Nurses. Ni vyeti tu wameweka na wanapita mara moja kwa mwezi kuja kuichukua Tsh 1,000,000 -1,500,000.

Nami naunga mkono hoja ya mtoa mada, District Pharmacist anatosha kufanya kazi hiyo badala ya kuning'iniza vyeti tu huku watu hawafanyi supervision
Kama hawafanyi supervision ni kosa kubwa nadhani ni wakati wa kufanya mabadiliko wawepo hapo wakati wote kama kwa wenzetu.
 
Huu uzi unafurahisha sana.
Mfamasia akija kuwa superintendent wako huwa upo mkataba unaowafungamanisha baina ya mmiliki na mfamasia msimamizi., kama unaona mfamasia anakuonea, ule mkataba unawezwa kuvunjwa kutokana na vipengele vilivyopo chini ya mkataba huo.
Pesa unayomlipa mfamasia mmekubaliana ktk mkataba wenu, sasa ni kipi kinakuuma?

Hii ishu ilishafikishwa hadi wizara ya afya na kwa sababu ipo kisheria kabisa (pharmacy act 2012) watu huishia kupiga mapambio mitandaoni ila mwisho wa siku mnawalipa wafamasia (tena mnawapa hela za miezi 6 au mwaka kabisaa)

Tafuteni namna msome bachelor of Pharmacy, nanyi muanze kula keki hiyo.

Mkemia.
 
Kama hawafanyi supervision ni kosa kubwa nadhani ni wakati wa kufanya mabadiliko wawepo hapo wakati wote kama kwa wenzetu.
Ukiona haridhishi huduma anayokupa, unaweza kuvunja nae mkataba ukatafuta mwingine boss.
Wafamasia wamejaaa wengi mnoo
 
Back
Top Bottom