Naomba kuuliza hivi hiyo Pharmacology anayosoma
1. Mfamasia
2. MD
3. Nurse
Zina utofauti yaani Pure na ingine Basic???
Mtujuze kwanza....
Mkuu 'Papai'
Inaonyesha kama una nia ya kutaka kujua. Ngoja nijaribu kukuelimisha kidogo.
Pharmacology, kila mmoja wa hao watu anaisoma kwa kina tofauti kufuatana na taaluma za kila mmoja wao inavyohitaji.
Ngoja nitoe mfano, pengine itaeleweka zaidi: Medical Assistant (nadhani siku hizi huitwa Clinical Officers, sina uhakika na hili), anasoma karibu masomo yote anayosoma daktari, lakini si kwa kina kama kile anachopaswa kusoma daktari. Huyu anaposoma Anatomy, kwa mfano, haingii ndani hadi kufanya 'dissection' ya cadaver. Na hivyo hivyo na masomo mengine ya udaktari, na muda anaochukua kuyasoma haya ni mfupi zaidi ili kumwezesha tu kuweza kufanya kazi anayohitaji kufanya kwa kiwango chake.
Hali ipo hivyo hivyo, na katika hii 'Pharmacology' inayozungumziwa sana katika fani hizi tatu.
Pharmacology ni somo linalohusu jinsi dawa inavyofanya kazi mwilini kumtibu mgonjwa.
famasia, yeye anachosoma zaidi ni kuhusu dawa katika maeneo mbalimbali ya dawa hiyo, ikiwemo jinsi inavyofanya kazi mwilini.
Dawa, ni kemikali, kama kemikali zingine zozote, kwa hiyo kufanya kazi mwilini kwa dawa hiyo, maana yake ni jinsi kemikali hii inavyo'interact' na mwili au wadudu ili kumponyesha mgonjwa.
Kwa hiyo utaona wazi hapa kwamba, pamoja na kutakiwa kujua 'pharmacology', kuna ujuzi zaidi unaotakiwa juu ya kujua muundo wa kemikali hiyo, ambayo ni dawa.
Famasia anasoma kemikali ya dawa (Medicinal Chemistry), mbali ya kujua 'Pharmacology'ya dawa husika. Somo hili la Medicinal Chemistry halifundishwi katika fani nyingine yoyote bali fani ya Famasia pekee. Kwa hiyo utaona hapa wazi kwamba mfamasia ana la ziada katika kujua dawa kuliko hao wengine uliowataja.
Na siyo hivyo pekee. Kujua 'pharmacology' hakumfanyi mtu kuwa na uhakika wa jinsi dawa itakavyofanya kazi yake vizuri mwilini mwa mgonjwa.
Dawa, kama vidonge, sindano, za kupaka, n.k., zinatengenezwa kwa kuunganisha na vitu vingine ili hiyo dawa iweze kufanya kazi yake vizuri, au iweze kutumika kwa urahisi, au iweze kufanya kazi mwilini kwa muda mrefu zaidi ili mgonjwa asitakiwe kutumia mara kwa mara.
Kwa hiyo, unaposema dawa, kama kidonge, kidonge hicho siyo dawa pekee, kuna vitu vingi vingine humo vinavyoongezwa kwa sababu mbalimbali. Hivi vitu vinavyoongezwa humo, nazo ni kemikali, ambazo nazo zinaweza kusaidia au kuathiri matumizi ya dawa.
MFamasia, anasoma somo linaloitwa "Pharmaceutics", ambalo linahusu utengenezaji wa dawa hizo kama nilivyoeleza hapo juu. Yaani muunganiko wa kemikali mbalimbali, ili iweze kutokea kama kidonge au kapsulu, au dawa ya majimaji, n.k.
Hili nalo ni somo lisilofundishwa kwingine kokote katika hizo fani ulizotaja hapo, bali linafundishwa kwa Famasia pekee.
Si kawaida yangu kuandika gazeti, naona nishaandika vya kutosha kukupa mwanga kidogo, kati ya tofauti iliyopo kati ya fani hizo tatu.
Mifano niliyotoa hapa ni sehemu tu ya tofauti. Sijazungumzia "Pharmacokinetics", somo analosoma mfamasia, lakini wengine hawalisomi. Hili linahusu dawa itakavyoweza kutembea na kujisambaza mwilini mwa mgonjwa na kiasi cha chemmbechembe za dawa hiyo kitakachofikia eneo lenye matatizo ya ugonjwa. Kama ni sehemu pungufu, basi mgonjwa hawezi kufaidika na dawa hiyo, kama ni kiasi kikubwa zaidi, basi mgonjwa anaweza kudhurika badala ya kufaidika na dawa hiyo. Na wakati huo huo mwili wa mgonjwa nao unashughullika kuiondoa dawa hiyo mwilini, kwenye mkojo, na maeneo mengine. Ni lazima dawa hiyo aliyokunywa mgonjwa iweze kutengenezwa ili wakati ipo mwilini haipungui au kuongezeka zaidi ya kiasi kinachohitajika kutibu ugonjwa.
Kuna mengine mengi...
Nipe mrejesho kama umeelewa kidogo tofauti iliyopo kati ya hao watatu, mbali ya kuitazama tu 'Pharmacology' kuwa ndicho kitu pekee kinachowaunganisha.