Mfano mdogo wa jinsi Nyerere alivyoongoza kwa hisia zake na mawazo yake bila kufata Katiba ama kupenda kupingwa

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Baada ya kuhitimu sekondari, Sitta alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na kusomea Shahada ya Sheria (LLB) mwaka 1964.

Sitta alisoma shahada hiyo kwa miaka saba kati ya mwaka 1964 na 1971, baada ya kufukuzwa chuoni hapo mwaka 1966 alipokuwa mwaka wa pili; akiwa kiongozi wa wanafunzi chuoni hapo, wakati wanafunzi walipogoma na kuandamana kupinga kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na kukatwa mishahara yao baada ya mafunzo ya JKT.

Samuel Sitta, Wilfred Mwabulambo na wengine kadhaa waliokuwa mstari wa mbele kutetea walichokiita haki zao, waliishutumu Serikali ya wakati huo wakisema; “…ni heri wakati wa Ukoloni kuliko utawala wa Mwalimu Nyerere.”

Kutokana na kauli hiyo, Rais wa Tanzania wakati huo, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, alikasirishwa na kuwafukuza chuo wanafunzi wote 400 kwa kile alichokiita “kwenda kufunzwa adabu majumbani mwao.”

Hata hivyo, baada ya mgomo na shinikizo hilo la wanafunzi, Mwalimu Nyerere alikubali kupunguza mshahara wake wa Sh. 4,000 bila kodi akaagiza pia mishahara ya mawaziri ipunguzwe kwa asilimia mbili.

Miezi miwili baadaye, akatangaza Azimio la Arusha (Februari 5, 1967) kuyapa uzito malalamiko ya wanafunzi hao waliopinga kukatwa mishahara yao wakati mawaziri wakiwa na mishahara mikubwa.

Miezi kumi baadaye, baada ya Mwalimu Nyerere kushawishiwa na hasira kutulia aliamua kuwarudisha chuoni wanafunzi 392, lakini Sitta na wenzake saba hawakurejeshwa chuoni.

Hata hivyo, viongozi wa chuo hicho walitumia busara kuandikiwa barua mbili maalumu mwaka 1967 kwa Mwalimu Nyerere, kumuomba awarejeshe chuoni wanafunzi hao.

Kuchapwa viboko na Nyerere

Baada ya barua hizo, hatimaye, Mwalimu Nyerere aliwarejesha chuoni Sitta na wenzake saba kwa sharti, yeye mwenyewe awatandike viboko Sitta na Mwabulambo, ambapo walitii adhabu hiyo na kurejea chuoni kuendelea na masomo hadi walipohitimu mwaka 1971.
 
Wakati Nyerere anaongoza nchi kwa kichwa Babu yako yeye alikuwa wapi, pengine angeongoza vizuri kuliko Nyerere.
 
Kwaiyo unataka tumchukie nyerere?? we unavo bwabwaja hivi unaweza fanya hata robo ya aliyofanya?
 
Baada ya kuhitimu sekondari, Sitta alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na kusomea Shahada ya Sheria (LLB) mwaka 1964.

Sitta alisoma shahada hiyo kwa miaka saba kati ya mwaka 1964 na 1971, baada ya kufukuzwa chuoni hapo mwaka 1966 alipokuwa mwaka wa pili; akiwa kiongozi wa wanafunzi chuoni hapo, wakati wanafunzi walipogoma na kuandamana kupinga kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na kukatwa mishahara yao baada ya mafunzo ya JKT.

Samuel Sitta, Wilfred Mwabulambo na wengine kadhaa waliokuwa mstari wa mbele kutetea walichokiita haki zao, waliishutumu Serikali ya wakati huo wakisema; “…ni heri wakati wa Ukoloni kuliko utawala wa Mwalimu Nyerere.”

Kutokana na kauli hiyo, Rais wa Tanzania wakati huo, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, alikasirishwa na kuwafukuza chuo wanafunzi wote 400 kwa kile alichokiita “kwenda kufunzwa adabu majumbani mwao.”

Hata hivyo, baada ya mgomo na shinikizo hilo la wanafunzi, Mwalimu Nyerere alikubali kupunguza mshahara wake wa Sh. 4,000 bila kodi akaagiza pia mishahara ya mawaziri ipunguzwe kwa asilimia mbili.

Miezi miwili baadaye, akatangaza Azimio la Arusha (Februari 5, 1967) kuyapa uzito malalamiko ya wanafunzi hao waliopinga kukatwa mishahara yao wakati mawaziri wakiwa na mishahara mikubwa.

Miezi kumi baadaye, baada ya Mwalimu Nyerere kushawishiwa na hasira kutulia aliamua kuwarudisha chuoni wanafunzi 392, lakini Sitta na wenzake saba hawakurejeshwa chuoni.

Hata hivyo, viongozi wa chuo hicho walitumia busara kuandikiwa barua mbili maalumu mwaka 1967 kwa Mwalimu Nyerere, kumuomba awarejeshe chuoni wanafunzi hao.

Kuchapwa viboko na Nyerere

Baada ya barua hizo, hatimaye, Mwalimu Nyerere aliwarejesha chuoni Sitta na wenzake saba kwa sharti, yeye mwenyewe awatandike viboko Sitta na Mwabulambo, ambapo walitii adhabu hiyo na kurejea chuoni kuendelea na masomo hadi walipohitimu mwaka 1971.
Sasa wewe ulitakaje?

Kwanza usifanye ionekane kuwa hisia binafsi za kiongozi wakati ikiwa ni maamuzi yaliyofanyika kwa taratibu serikalini kuhusu uamzi wa kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa.
Ulitaka serikali ikajadili na wanafunzi juu ya maamuzi hayo?
 
Back
Top Bottom