Mfanyabiashara ahukumiwa kunyongwa Dar, alimuua mdai wake aliyempa hela amuagizie Fuso

Kwa hiyo, marehemu aliuwawa kwa sababu alidai chake?

Na kwamba hela aliyokuwa anadai marehemu ilinunulia nyumba Magomeni badala ya kununulia Fuso kama marehemu alivyokubaliana na mshtakiwa/muuaj...
Tatizo kuna watu wanadaigi kwa jazba kejeli na matusi tena hadharani. Sasa hii inapelekea kumpa nafasi shetani atawale nafsi na akili ya mdaiwa nakusababisha sintomfaham kupelekea kufanya mauaji bila kujijua.

Mnakumbuka kisa cha uriah aluvyokuwa anadai chake mke wake kwa Daudi? Alikomaa hadi akakataa kwenda nyumbani. Daudi alimaindi kichiz akaamua tu kumpoteza.

Dawa ya deni ni kulipa. Tusiwe wachoyo na tamaa zembe. Dhulma ni mbaya inasababisha mdaiwa kuwa na hasira za kijinga akidaiwa nakupelekea kuua nafsi isiyokuwa na hatia.

Saa zingine ukimdai mtu anakukwepa na kukudhulumu muachie Mungu tu. Jamaa angemuachia Mungu asingeuwawa.

Acha anyongwe tu.
 
Uzuri bongo hakunaga kunyongwa.

Tangu enzi za Nyerere hakuna Raisi aliyewahi kutia saini ya 'hanging penalty'
Si nasikia Nyerere na Mwinyi walinyonga? Mama pia inabidi afanye hivyo. Watu wamezidi sana ukatili. Aanze na waliohukumiwa kunyongwa miaka ya sabini na themanini huko. Wapigwe kitanzi hadi tena live streaming.
 
Inasemekana japo niliipata miaka mingi huko nyuma.

Aliyeuliwa (baba feisari) alikuwa anafanya kazi ubungo kwenye mabus ya muuaji.

Wakachanga na muuaji ili wanunue gari lao.

Marehemu siku hiyo ameenda job na alikuwa na tabia ya kumpigia mke wake cm kila saa nne au saa kumi, cm hakupiga siku hiyo.

Hapo ndugu wakaanza kutafuta.

Baadae sana inasemekana aliyepanga pale alipofukiwa marehemu, akipaki gari nje usiku anasikia linawashwa, mwisho mpangaji kafanya kisomo.

Ndo ikawa mwanzo wa marehemu kujulikana, ni mengi mno,

Ila ninayo hii strory full, nawahi job.
 
Hpn muuaji ndie aliye mpa pesa jamaa amuagizie gari Aina ya fuso ikapita muda bila kuletewa gari ndipo muuaji akamuita jamaa na Kisha kuja kumuua nyumbni kwake aliko panga bean muuaji
 
Mimi nakumbuka mke wa Marehemu alienda kuripoti polisi kupotea Kwa Mumewe na kuulizwa NI Nani anaemshuku ndio akamtaja mtuhumiwa Kwa sababu alipoondoka aliaga anaenda Kwa Mtuhumiwa kuchukua gari yake.
Ndipo polisi wakamshika Mtuhumiwa baada msago kidogo akakiri na kuwapeleka polisi alipofanya tukio
 
Wabongo wana Roho mbaya sana aisee duuh yaani kamuua mtu kamfukia na inawezekana kafukia wengi ajaanza kwa huyo tuu...daah huyo inatakiwa anyongwe haraka asipewe hata nafasi ya kuvuta sigara..yaani ilikua akitoka mahakani ni kwenye kitanzi sio mambo ya kusubiri rufaa kwa makatili..
 
Kama ushahidi umetimia na hakuna rushwa iliyotolewa auliwe na kusiwe na watetezi wa haki za binadamu.
 
Ama kweli waarabu wa pemba hujuana kwa vilemba vyao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…