Mfanyabiashara ahukumiwa kunyongwa Dar, alimuua mdai wake aliyempa hela amuagizie Fuso

Hpn muuaji ndie aliye mpa pesa jamaa amuagizie gari Aina ya fuso ikapita muda bila kuletewa gari ndipo muuaji akamuita jamaa na Kisha kuja kumuua nyumbni kwake aliko panga bean muuaji

Kutoka mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam:

Godoro,pazia vyapokewa kortini kielelezo ushahidi kesi ya mauaji

www.ippmedia.com › habari › godoropa...

16 Sept 2022 · MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepokea kielelezo cha godoro, pazia na nyavu ambavyo vinadaiwa kumfungia marehemu Farahani Maluni, ......



September 24, 2022 Udaku


MKEMIA Mwandamizi kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kaijunga Brassy ameiambia mahakama mabaki ya mwili wa marehemu Farihani Maluni, ikiwamo mifupa, hayakuonyesha majibu ya vinasaba kwa sababu ulikuwa na udhahiri mdogo.

Pia amedai mwili huo ambao ulifukiwa mbele ya nyumba iliyoko Ilala Sharif Shamba inawezekana ulichomwa moto kabla haujazikwa au ardhi aliyozikwa ilikuwa na chumvi, hivyo seli hazikuwa na muunganiko.

Brassy alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Joyce Minde wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati akitoa ushahidi wake dhidi ya Hemed Ally anayetuhumiwa kumuua Maluni na kumfukia.

Alidai kuwa vielelezo alivyovifanyia uchunguzi huo ni mifupa miwili ya paja, nguo ya ndani ya marehemu, plasta, mifupa ya kwenye kiuno, kamba na nguo yenye vifungo, meno, fuvu la nyuma la kichwa, mkanda, upindo wa suruali na kola ya shati.

Alidai barua ya kufanya uchunguzi wa vitu hivyo pia ilimtaka afanye uchunguzi wa vinasaba vya Abisalum Maluni ambaye ni baba wa marehemu, Faisal na Fahadi (watoto wa marehemu), ambapo aliwachukua mipanyuso mitatu ya kinywa.


Alidai kuwa uchunguzi huo wa vinasaba DNA ulikuwa na lengo la kufananisha mabaki ya marehemu na ndugu hao ili walinganishe vinasaba vyao kama Farihani ni ndugu yao.

Alidai vielelezo hivyo alivipa namba za usajili 115/2015 na baadaye alivihifadhi na akaja kuvifanyia kazi Julai 27/2018 na alibaini kuwa vielelezo namba moja hadi nane havikutoa majibu ya vinasaba.

Hata hivyo, kielelezo namba tisa - baba na watoto wa marehemu vilitoa majibu ya chembe halisi za urithi DNA , katika kulinganisha vilifanana vinasaba vya watoto na baba wa marehemu Farihani.

"Kielelezo namba moja hadi nane yakiwamo mabaki ya mwili wa Maluni havikutoa majibu kwa sababu havikuwa na udhahiri, inawezekana huo mwili ulichomwa moto kabla haujazikwa au ardhi aliyozikwa ilikuwa na chumvi, hivyo seli hazikuwa na muunganiko," alidai.

Awali Brassy alidai Februari 12, 2015 akiwa ofisini, alipokea vielelezo na barua kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dar es Salaam wakiomba uchunguzi wa vielelezo tisa.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Jumatatu saa tatu asubuhi. Inadaiwa Juni mwaka 2014, Hemed Ally alimuua Farihani Maluni eneo la Sharif Shamba ndani ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam

September 2022
Amedai kuwa haikuwa rahisi kujua chanzo cha kifo cha Maluni lakini kutokana na uwapo wa plasta eneo la fuvu, alihisi aliuawa kwa kuzibwa mdomo na kusababisha akose pumzi.

Dk. Mosha alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Joyce Minde wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati akitoa ushahidi katika kesi ya mauaji inayomkabili Hemed Ally.

Alidai kuwa Februari 9, 2015 akiwa katika eneo lake la kazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, alipelekewa taarifa na Ofisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa (RCO) wa Ilala, ikimtaka kwenda Sharif Shamba ndani ya Wilaya ya Ilala kuchunguza mwili wa binadamu unaohisiwa kufunikwa ndani ya ua wa nyumba.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Salome Asey, Dk.Mosha alidai alichukua vifaa vyote vya kazi na kuongozana na askari polisi hadi eneo la tukio.

Walipofika eneo hilo majira ya saa sita kasoro mchana, Dk. Mosha alidai kuwa alikuta vijana wakiwa wameishaanza kufukua eneo hilo na ndani ya shimo walikuta matofali mapya, mabaki ya mwili yaliyokuwa yamezungushiwa ndani ya godoro, huku mikono ikionekana kufungwa kwa katani na fuvu likiwa na plasta.

Shahidi huyo alidai baada ya mabaki ya mwili huo kuonekana, wananchi waliokuwapo katika eneo hilo walikumbwa na taharuki wakitaka kumpiga mtuhumiwa aliyekuwapo pale na kumfanya ashindwe kufanya uchunguzi, ikabidi wachukue mabaki na nguo hadi Muhimbili.

Alidai Februari 10, 2015 alifanya uchunguzi akiwa na askari pamoja na ndugu wa marehemu waliotambua mavazi ya marehemu ikiwamo fulana ya pinki.

Dk. Mosha alidai katika uchunguzi wake, alibaini kuwa yale yalikuwa mabaki kweli ya binadamu kwa kuangalia fuvu, mpangilio wa meno na mifupa michache iliyokuwapo.

Baada ya kutoa ushahidi, Dk. Mosha aliiomba mahakama kupokea ripoti ya uchunguzi kama kielelezo na mahakama ilipokea kama kielelezo.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi kesho kutwa, Septemba 28, 2022 itakapokuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.

Inadaiwa kuwa Juni, 2014 Hemed Ally alimuua Farahani Maluni eneo la Sharif Shamba, Ilala na kumzika mbele ya nyumba aliyokuwa akiishi.


Mfanyabiashara ahukumiwa kunyongwa hadi kufa Dar

www.mwananchi.co.tz › ... › Kitaifa

1 day ago · Hemed Ally akitoka Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya ... leo Jumatatu Oktoba 17, 2022 na Hakimu Mkazi Mkuu, Joyce Minde, ...
 
Acha tu, mimi nikihesabu hela nilizowasamehe naowadai zinafika m 5, kwangu ni kubwa ila ndio nilishazipotezea kwa kuogopa kifo, vitisho vilikuwa vingi, kikubwa uhai.
Pole sana. Mimi kikubwa kwangu amani. Kwa hiyo huwa sikopeshi. Na nikikopesha ni kama sijakopesha tu, nimetoa msaada.

Simuamini mtu kwenye hela maana hata mimi mwenyewe sijiamini
 
Huu mlolongo wa hiz kësi kutajwa Mahakama za chini unapoteza Muda sana, cjui ni Kwanini wadau wa Sheria watuelimishe why? Kwanini kësi kama hizi zisiende Mahakama kuu Moja Kwa Moja??
 
Duuh...kazi sana huu ubinadamu
 
Eti Mimi nilisikia jirani na hapo Kuna ghorofa Sasa Kuna mtoto aliona baada ya muda akamwambia mama yake
 
Ila ukiwa tayari kujiunga na Jeshi la polisi unatakiwa uwe na moyo wa ujasiri na ushujaa. Lazima tu utakutana na visa kama hivi. Polisi wakikusimulia kesi wanazokumbana nazo hapo ndo utamjua binadamu ni kiumbe hatariiii na utaishi kwa tahadhari ya kutomuamini yoyote yule.

mrangi
 
Mie mdau sana wa detectives stories yanj wanakwambia hakuna mauaji yanayokua perfect inatokea mara chache sana lazma kuna pahala muuaji akosee...


Kama huyu jamaa shimo lake hakufukia kwa kiwango pakaja kumuumbua
Wazee WA mbanga za FBI files na behind mansion walls detectives , hatari Sana , wazee wanatrack mpaka udongo ,unaambiwa kila kitu kibachokuwa involved kwenye crime lazima kuna signature inaachwa pale ,so suala la utaalamu Kwa kuzisoma hizo criminal signatures
 
Kitu pesa ni habari nyengine kinachotakiwa jenga mazoea ya kulipa kila anaekudai hata kama ni 10,000/= muite umpe ukiizoea hii hali hata anayekudai 5mill hakusumbui utatoa na huwezi kuwa na tamaa kiasi cha kuuwa na Tsh 30Mill ya wakati wa Kikwete haikuwa hela ya kumuuwa partner wa biashara maana kwa hao wauza magari walikuwa wanaingiza hela hiyo kwa sekunde tu.

Mf;ukiangalia hii case ktk angle tofauti na dhulma utakuta hii hela haikuwa pesa ya kuuwa mtu ilikuwa amyeyushe tu jamaa miaka isogee kama mahakamani wapelekane abishe bishe kidogo huyo mdai munkari upungue maisha yaendelee,hela ya mtu siyo ya kukaa nayo hasa ukiwa mtu wa kuzungusha cash sokoni maana itatokea siku mwenyewe anaitaka ukute kule ulikoitia imekwama na alternative nyengine huna.

Ukiwa mtu wa tamaa ikifikia hatua ya kutema bungo kama kazi uliyopewa haujaifanikisha utaona kama unampa mtu pesa zake bure na matokeo yake ndo haya unapoteza vyote.
 
Sasa nimekupata vzr mzee wa ilala shrif shamba
 
Acha tu, mimi nikihesabu hela nilizowasamehe naowadai zinafika m 5, kwangu ni kubwa ila ndio nilishazipotezea kwa kuogopa kifo, vitisho vilikuwa vingi, kikubwa uhai.
Acha kbsa dai Chako ni hatarinsana mm nilimdai mtu changu alichonifanya siyo POA kbsa acha tu
 
Kudhulumu udhulumu na kuua uuwee

Jamaa katili sana huyo

Ova
Mkuu kuna watu wanajuwa kudai Kwa maudhi sana,

Kama una roho ndogo unaweza either kujidhuru au umdhuru mtu.,
Inatakiwa uwe na uvumilivu sana.

Mtu unadaiwa hata kufikia hatua ya kuichukia simu yako mwenyewe ya mkononi.

Muda wote simu au sms ikiingia huna raha.

Kudaiwa kubaya sana,,
 
Mnakumbuka kisa cha uriah aluvyokuwa anadai chake mke wake kwa Daudi? Alikomaa hadi akakataa kwenda nyumbani. Daudi alimaindi kichiz akaamua tu kumpoteza.
.
Mkuu sina hakika na kitabu gani kitakatifu ulichotumia hapa, Lakini kama ni biblia basi umepotosha kidogo.

Huria alikuwa ni kati ya wapiganaji wa jeshi ambalo Daudi alikuwa Mfalme. Jeshi lilienda vitani na Huria kama mmoja wa wapiganaji alienda vitani pia.

Mfalme Daudi hakwenda vitani pamoja na jeshi, kama ilivyokawaida mke wa Huria alibaki nyumbani pia mmewe alipoenda vitani.

Ikatokea jioni Mfalme Daud katika kutembea uwandani akamuona mke wa Huria akioga! Akawaka tamaa akamtwaa akamjua. Mke wa Huria akapata ujauzito kabla haujaonekana kwa watu mfalme Daudi akajulishwa.

Mfalmw Daudi ili kufunika dhambi yake, akatuma ujumbe jeshini Huria aje Ikulu ampe mfalme maendeleo ya vita.

Huria baada ya kurejea akafanya mazungumzo mpaka jioni sana. Hivyo Mfalme akamshauri kwa kuwa ni usiku sasa hauwezi kurejea vitani nenda nyumbani kwako ulale kesho urejee vitani. Mfalme Daudi alilenga jamaa akienda tu nyumbani basi atalala na mkewe na hivyo mtoto itaobekna ni wa Huria.

Huria alikata offer ya Mfalme kwamba siwezi kwenda kulala ndani kitandani na mwanamke wakati jeshi liko vitani.

Akalala nje uwandani kwa Mfalme asubuhi arudi vitani.

Mfalme akatafuta option nyingine ya kufunika dhambi yake, ni kumuua Huria bila kujulikana alafu amuoe mkewe Huria hivyo mtoto akizaliwa pasiwe na shida watu kuuju uzinzi wa mflme na mtumishi wa Mungu.

Akamwandikia kamanda wa vita barua kwamba Huria awekwe mstari wa mbele afie vitani. Akampatia Huria aipeleke kwa kamanda. Huo ndo ukawa mwisho wa Huria mwaminifu.
 
Februari 9, 2015 Hamjat alipokea simu kutoka kwa polisi wakimtaka aende katika nyumba yake kuna tukio mshtakiwa alilifanya naye akaenda na baada ya kufukua walikuta mabaki ya mwili wa Farihani ukiwa umefungwa kamba mikononi na plasta maeneo ya fuvu(Daktari alihisi ilitumika kumziba mdomo na kumsababishia akose pumzi).[emoji24][emoji24][emoji24]
 
Inasikitisha!!!

Kwanini mamlaka za mtaa husika na polisi wasingeunga dots wakamuwajibisha huyo jamaa?tamaa gani hii ni kusema kama hiyo mission ingekubali angeuwa familia nzima.
 
Acha tu, mimi nikihesabu hela nilizowasamehe naowadai zinafika m 5, kwangu ni kubwa ila ndio nilishazipotezea kwa kuogopa kifo, vitisho vilikuwa vingi, kikubwa uhai.
Siwezi kufanya hiyo kitu, kama yangu ni lazima ulipe. Na kuniua uwezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…