TANZIA Mfanyabiashara Andrew Mollel afariki dunia (mmiliki wa Happy Sausages)

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mfanyabiashara maarufu mkoani Arusha, Andrew Mollel ambaye alikuwa mwanzilishi na Mkurugenzi wa kampuni mbalimbali mkoani Arusha amefariki dunia na kuibua simanzi kwa wakazi wengi wa jiji hilo.

Akizungumza na Mwananchi leo, Februari 28, Mbunge wa jimbo la Monduli , Fredrick Lowassa amesema kifo cha Mollel ni pigo kubwa katika jiji la Arusha kutokana na mchango wake.

Lowassa amesema taratibu za mazishi wa Mollel zinaendelea kufanywa na wanafamilia lakini, kubwa ambalo Arusha watamkumbuka ni kuandaa michoro ya mradi mkubwa wa nyumba za PPF zilizopo eneo la Kijenge jijini hapa ambalo lilikuwa ni eneo lake.

Mollel alikuwa pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Happy Sausages ,Kijenge Animal Products Limited, Georges Center Ltd na AGM Holding na pia mjumbe wa bodi mbali mbali hapa nchini.

Mollel pia alikuwa ni rafiki wa karibu wa Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa.

Kifo cha mfanyabiashara huyu ni mfululizo wa vifo vya wafanyabiahara kadhaa katika jiji la Arusha katika siku za karibuni.

Taarifa zaidi za kifo cha mfanyabiashara huyu zitaendelea kutolewa
 
Apumzike kwa amani bwana Mollel.

Ile mijamaa itadai siyo ule ugonjwa kama vile kuna aliyeiambia ni wenyewe.

Kwa kweri tuko vizuri:

Hivi wa Northern Electrical ndio huyu huyu au tofauti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…