TANZIA Mfanyabiashara Emilian Woiso afariki dunia

Vitu vyote ni ubatili mtupu isipokuwa kumcha MUNGU.

Unajitaabisha kwa dhiki nyingi mwisho wa siku vyote ulivyovitafuta kwa hadaa na dhuluma vinakusaliti.

Tutafute pesa kwa bidii zote lakini ziwe pesa za haki na halali huku tukiishi maisha mema yenye upendo, kufarijiana na kusaidiana huku tukimtanguliza MUNGU kwa kila jambo.

Maisha ya mwanadamu ni kama ua, huchanua na kupendeza mwisho husinyaa na kunyauka.

CHIEF PRIEST na Stuxnet mlifanikiwa kuuga mwili wa marehemu?.
 
Ndiyo mkuu pamoja na mikasa yake bado alikuwa mshikaji japokuwa sikuwahi kushiriki maovu yake
 
Ndiyo mkuu pamoja na mikasa yake bado alikuwa mshikaji japokuwa sikuwahi kushiriki maovu yake
Hapo sawa, ila story yake inatufunza mengi.

Pamoja na ukwasi aliojikusanyia kwa njia za kimafia na halali, bado maisha yake yaliandamwa na laana, maafa na fadhaa kuu kuliko furaha na amani.

Ni heri kula mhogo mbichi na ndimu kivulini kuliko nyama choma na kinywaji baridi vitani.
 
Mimi sikufanikiwa, nilikuwa na msiba mwingine.

Ila maisha yake ni fundisho kwa tuliobaki
 
"Ni heri kula mhogo mbichi na ndimu kivulini kuliko nyama choma na kinywaji baridi vitani."

Hiyo sentensi ya mwisho iwekewe lamination
 
Umenena vema. Jamaa rekodi yake mbaya imemuandama hadi kaburini.
 
"Ni heri kula mhogo mbichi na ndimu kivulini kuliko nyama choma na kinyaji baridi vitani."

Hiyo sentensi ya mwisho iwekewe lamination
Hakika, tutafute pesa kwa bidii na nguvu zote lakini tusiwadhuru wengine.

Vipi alifanikiwa kupata watoto wengine aliozaa na huyo house girl aliyegeuzwa mke baada ya kuondokewa na mke wake?.
 
Hakika, tutafute pesa kwa bidii na nguvu zote lakini tusiwadhuru wengine.

Vipi alifanikiwa kupata watoto wengine aliozaa na huyo house girl aliyegeuzwa mke baada ya kuondokewa na mke wake?.
Hakupata watoto na huyo house girl. Ila siku za mwisho alipoona hali yake mbaya alimjengea nyumba. Pia alimruhusu akaolewe akipata mume wa kumuoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…