Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Acha waipige tu hadi kitakapopatikana kizazi kinachojitambua,ndio utakuwa mwisho wao!!sasa ni MANYUMBU tuNaililia nchi yangu dah! Inapigwa na inapigika kisawa sawa.
Kama mada inavyojitabaisha, upande wa kaskazini mwa stendi ya ya mabasi ya mikoani hapo Msamvu Morogoro kuna kituo cha mafuta kinajengwa humo ndani ya uzio eneo ambalo lilitakiwa iwe vizimba vya wajasiriamali wadogo na mama lishe lakini limegawiwa kwa mtu ambaye inasemekana ana nguvu za kiuchumi na kisiasa!!!!
Je, serikali siku hizi inaendesha biashara ya kununua na kuuza mafuta ya magari?
Je, kwa mtindo huu ni kweli kwamba kituo hicho cha mabasi cha umma kiko mbioni kubinafisishwa kwa watu binafsi?
Je, baraza la madiwani wa manispaa ya Morogoro wameridhia kisha wananchi wakapewa mrejesho?
Je, serikali kuu inatambua kuhusu hili?
Ufafanuzi tafadhali
Siri inasema hivi temblea Chalinze ndo utajua ni nani anayesumbua hivi kwa ujasiri.................................inashangaza mpaka msitu wa Maseyu umeanza kufyekwa ili vituo vya mafuta vijengwe. Sio kwamba viongozi hawaoni hapana wanafahamu na wameridhia kwa kuwa mzizi mkuu umekitishwa kitako ukiwa umezungukwa na silaha tano za kingaSio hapo tuu hata hapa daresalamu pale stop over mataa mkono wa kushoto kama unaelekea mbezi kuna jamaa anaweka hapo sheli wakati pale kuna mtu kabomolewa nyumba zake kwa kigezo cha kusema ni sehemu ya barabara kinachonishangaza pale mbele usawa huo huo (kituo suka)kuna sheli pale imefungwa kwa kigezo cha kusema iko barabarani sasa hapo sijaelewa hii mchi kumbe ina watu ndio na watu sio
Labda GIPSA wakala wa serikali ila kama ni mtu binafsi vyombo vya serikali vifuatilie.Inajengwa ndani ya uzio wa stendi yenyewe huku imekingwa na vizimba vya kupoteza malengo kwa wapitaji barabarani
Unajua maana ya sheli au Mahaba ya usukuma gang yanakusumbua?Hata mimi nimeiona hiyo sheli ikijengwa karibu na geti la kuingia msamvu.
#MaendeleoHayanaChama
Kwani hujui Serikali inayo hisa kwenye PUMA.Kama mada inavyojitabaisha, upande wa kaskazini mwa stendi ya ya mabasi ya mikoani hapo Msamvu Morogoro kuna kituo cha mafuta kinajengwa humo ndani ya uzio eneo ambalo lilitakiwa iwe vizimba vya wajasiriamali wadogo na mama lishe lakini limegawiwa kwa mtu ambaye inasemekana ana nguvu za kiuchumi na kisiasa!!!!
Je, serikali siku hizi inaendesha biashara ya kununua na kuuza mafuta ya magari?
Je, kwa mtindo huu ni kweli kwamba kituo hicho cha mabasi cha umma kiko mbioni kubinafisishwa kwa watu binafsi?
Je, baraza la madiwani wa manispaa ya Morogoro wameridhia kisha wananchi wakapewa mrejesho?
Je, serikali kuu inatambua kuhusu hili?
Ufafanuzi tafadhali