Kwani kutaja mapato ndio kutoa code?
Au unadhani CocaCola na PepsiCo huwa hawatangazi mapato na matumizi yao kila mwaka. Na wakati huo formula ya syrup na concentrate hawatoi.
Kutaja mapato ni kujiropokea tu. Alafu hiyo kiasi ni ghafi, faida yake baada ya gharama ni ipi. Na mchakato wa kupata faida na kuendesha ni upi.
Usipokuwa makini utakurupuka umuulize muuzaji maarufu wa bangi mtaani kwako, akwambie mauzo ya debe labda ni 800,000 alafu ukurupuke kuagiza madebe nawewe. Kumbe yeye kwenye hiyo laki 8 kuna mgawo wa afisa wa polisi wa mtaa na mwenyekiti, na vilevile huyo jamaa ana ndugu yake fisadi la CCM Halmashauri au kaka yake idara ya polisi huo mkoa analindwa. Wewe unakurupuka na madebe yako unaenda jela unahonga mtaji mzima.
Unarudi unajiuliza wanafanyaje, sasa unataka akwambie ana kaka yake afisa wa polisi makao makuu ya mkoa, anawapa mgawo viongozi wa mtaa na anahonga polisi ili kuwatuliza? Ukitoka hapo si unamtangaza?